Je, Viongozi wa Idara ambao ni Wachagga waachie ngazi!??

Je, Viongozi wa Idara ambao ni Wachagga waachie ngazi!??

Status
Not open for further replies.
Mbona huoni unbalance ya maendeleo kati ya mikoa ya kusini na kaskazini?
Wachagga wameiba wakaweka maendeleo kwao mkoa wa Kilimanjaro angalia miundo mbinu ya Mtwara,Lindi,Ruvuma,Rukwa,Tabora,Kigoma je hao wachagga ambao wapo kwenye system za uongozi wameitendea nini mikoa hiyo?Zaidi ya kupora mabilioni na kuinemeesha mikoa ya kaskazini kwenu huko.
Ili nchi hii iendelee inabidi wachagga wakae kando kwenye system kwani kila idara ukienda wameenea.

You must be kidding!
 
.....u need to get your facts straight before u spew your ignorance!
 
[
".. Generalizing ndio cheche za wenye kuleta hoja na majibu yenye mtazamo huo huo ndio yametufikisha hapa tulipo.."

Mkandara,nimenukuu maneno yako hapo juu,
Kama hii topic ilikuwa inahusu chama fulani,basi ingeandikwa specific based on that party na sio general as it was.Kama wachagga wanaotakiwa kuachia ngazi ni wa Chadema basi iwe specific lakini mnapoweka post with such a general message, i guess you are definitely ready for the general comments as well. BTW some of us are not into Chadema or any other political party in TZ, so kama mtu ana bifu na watu fulani katika mambo ya kichama basi napendekeza awe specific kwenye title. Hakuna kabila pumbavu ila pia hakuna kabila ambalo litajisikia vyema kama kila kukicha kuna jambo linasemwa kuhusu wao. It's a human nature no one likes to have fingers pointed on them for things which are not necessarily true.
 
Tonga.. unachokiona hapa na mawazo ambayo yanatolewa dhidi ya Wachagga yapo na kuna watu wanaamini kabisa wanachosema. Nina uhakika siyo tu umeshtushwa na baadhi ya maneno lakini pia umehuzunishwa kuwepo kwa maneno hayo.

Haya mambo tumekuwa tukiyakwepa kuyazungumzia au kuyacknowledge kuwa yapo. Mada hii siyo tu imeendelea kunithibitishia kuwa kuna watu wana chuki kali kweli na isiyo na msingi dhidi ya Wachagga lakini pia imenifanya nielewe kwa namna fulani sentiments zinazoweza kuwa zimechangia hisia hizo.

Kama jamii ni lazima tupinge kwa nguvu zetu zote wale wanaoeneza sumu ya ukabila, udini, urangi kwa ajili ya kupata manufaa ya kisiasa au ya kinamna yoyote ile. Wakati huo huo tusije kufanya mambo yetu bila kuangalia jinsi gani mambo hayo yanaweza kutafsirika vibaya.

Ndio maana kwa upande wangu linapokuja suala la Chadema kwa mfano, tatizo ninaloliona lilitokea katika suala la wagombea wa viti maalumu ni suala la utaratibu na mchakato wa jinsi gani hao wanapatikana. Jambo hilo nasikia hata wao wanafahamu ndio maana baada ya mabadiliko ya Katiba yao ya 2006 waliamua kubadili jinsi wanavyofanya uteuzi wa wabunge wa viti maalumu.

Hili pia linatokea katika nafasi mbalimbali za uongozi au utumishi ambapo ninachokiona kama tatizo kubwa si ukabila bali undugunization uliokithiri kutokana na utaratibu mbaya wa kupata ajira na madaraka nchini. Ni kwa sababu hiyo utaona mngoni aliyepata nafasi atahakikisha watoto wake na wenyewe wanaingia kwenye eneo hilo, au akawapa habari za ndani zenye faida watu wa "kwao" na wakapata unfair advantage ya mambo fulani. Hili linatokea kwa karibu makabila yote.

Tatizo kubwa wakati mwingine ni suala la taratibu zilizowazi, huru, na fair kwa mtu yeyote. Endapo, inatangazwa nafasi, kwa uwazi, na huru na nafasi hiyo ikatokewa kugombewa na na watu kadhaa basi lazima tujifunze kukubali matokeo yake hata kama hatupendi yawe hivyo.

Tusikubali kuongozwa na hisia kinyume (negative emotions) kwa sababu hatuoni tunachotaka kuona. Tusilazimishwe kuona kitu ambacho hakipo kama alivyofanya Wangwe hivi karibuni.

Lakini ukweli utaendelea kubakia Watanzania siyo binadamu tofauti na wengine kiasi kwamba hawana mawazo ya kibaguzi ati tu kwa vile ni wa Tanzania. Mawazo haya yapo, yanachochewa na wakati mwingine yanatukuzwa. Ni jukumu la kila mtanzania kuhakikisha siyo tu anapinga mawazo ya kuchochea ukabila, lakini pia kupinga dalili zozote za ukabila zinapojitokeza hata kama zinahusu kabila lake au watu wa jamii yake.

Ni tutakapofanya hivyo ndipo tutakuwa kweli tunajenga Taifa la watu "walio huru, sawa, na wenye kufurahia haki zote za msingi sawasawa katika Taifa lao".
 
Hao wanaosema kuwa wachaga waachie ngazi katika nyasifa walizonazo serikalini wanachuki binafsi. Nakumbuka kipindi cha nyuma watu walikuwa wanawashambulia watu wa kabila la wahaya kuwa wanapeana nafasi kazi kwenye maofisi, lakini ukumbuke kuwa wakati huo kabila ambalo lilikuwa limeenda shule hapo nyuma ni kabila la wahaya. Kwa kuwa walikuwa wamesoma basi walikuwa na sifa za kuwa kwenye maofisi, waliajiriwa kwenye maofisi kwa kuwa ni watu walioenda shule. Wachaga hapo nyuma walikuwa hapendi shule, walikuwa wanapenda kufanya biashara, mtoto akimaliza elimu ya msingi anafunguliwa duka aanze kufanya biashara ndio maana wachaga wanaongoza kwa kuwa na maduka hapa nchini.

Sasa hivi wachaga wamejua umuhimu wa elimu ndio maana shule nyingi za A level na O level zipo uchagani. Wazee wengi ambao ni wasomi hapa nchni ni wahaya, ambao hapo awali walienda shule. na vijana wengi ambao ni wasomi hapa nchini ni wachaga. Watu wa mikoa ya kaskazini wameenda shule kuliko watu wa mikoa ya kati na kusini. Na ukiangalia shule nyingi zapo mikoa ya kaskazini. Watu wa mikoa ya kusini ambao wameenda shule ni wachache sana kiasi kwamba hata walioko maofisini sasa hv ni wachache. Wanyakyusa nao wamesoma na ni moja kati ya kabila ambalo ni wachapa kazi hapa nchini.

Mahali ambapo umechemsha zaidi ni hapa, "Ushauri wangu ni kuwa, kwa vile Wachagga wameshasoma sana na kuendelea katika biashara karibu mikoa mingi nchini. Na kwa vile wanaendelea kufanikiwa pia katika nafasi mbalimbali za uongozi nchini, basi itakuwa vizuri kama watajitolea kuachilia nafasi hizo ili kuwapa nafasi watu wa makabila mengine." Ningefurahi kama ungewapa ushauri makabila mengine waongeze bidii katika kuwapeleka wanao shule na kujenga shule nyingi kwao ili nao waje washike nafasi katika maofisi.

Kama unataka wachaga waachie ngazi kwenye maofisi basi na watu wa mkoa ya musoma nao waachie ngazi katika kugombea kazi jeshini ili wawapishe makabila mengine katika hiyo nafasi, kwani wao ndio wamejaa sana jeshini.

Kuna kaparagraph iliandika hivi " Ubaguzi huo msingi wake mkubwa ni idadi ya wachagga katika nafasi mbalimbali za uongozi na hasa kuhusiana na elimu yao. Kuanzia mara tu baada ya uhuru jamii ya wachagga mojawapo ya jamii ambayo watu wake wengi wamesoma sana na kufanikiwa kielimu na kiuchumi imekuwa ikinyoshewa kidole cha kupendelewa." Jamani kama wamesoma kwanini wanyooshewe vidole? wamesoma ndio maana wamepewa hizo nafasi kwenye maofisi.

Endapo itatangazwa nafasi yoyote ya kitaalamu usishangazwe ukiona kuwa waombaji wengi wana majina ya "Kichagga". Yeah utakuta majina mengi ya kichaga kwa kuwa wao wanaona wanasifa za hiyo kazi ndio maana wangi wametuma maombi.

Sasa hivi kila ofisi wachaga wapo na wapo kwa kuwa wameenda shule. Kuna baadhi ya wachaga wanaogopa kutumia majina yao ya ukoo kwa kuhofia kutopata kazi kwenye ofisi anayoomba kazi. kwani kwenye hiyo ofisi wachaga wamejaa na wanaogopa kuajiri wachaga wengine. Kama mtu anaitwa Diana Boniface Mushi, anaandika Diana Boniface. usishnagae ukiona mchaga anaukana uchaga kwenye interview.

Ni hayo tu mtu wangu.
 
Mwanakijiji,Tonga,

..kwanza inabidi umjue Mwanakijiji na maandiko yake hapa Jamii Forums ndipo uweze kufahamu kwamba hajawahi kuwa na hizi hisia za chuki-chuki dhidi ya Wachaga.

..tumekuwa naye kwa muda mrefu haswa ktk mjadala wa TRA na ukabila. naomba urejee michango yake kule ili then utaelewa kwanini sasa hivi ameamua kutumia njia aliyotumia kuanzisha mjadala huu.

..in short ktk mjadala wa TRA ilifika mahali mchangiaji mmoja akaleta orodha ya watumishi wa TRA. lakini wachangiaji walimpinga kwasababu ungeiamini basi madai ya ukabila TRA yangekuwa hayana msingi tena. hata management ya TRA na bodi yake haikujazwa wachaga kama habari zilivyozagaa mitaani.

Kunguru-mweupe,

..naomba nirekebishe kauli niliyoitoa hapo mwanzo. nimerejea makala niliyoisoma kuhusu Mangi Marealle na nasikitika kwamba nilifanya makosa ktk kuelezea habari hiyo.

..chuo cha maofisa wa polisi kipo Moshi. alichofanya Mangi Marealle ni kuwezesha kwa vijana wa Kitanganyika/Native bila kujali makabila yao kujiunga na mafunzo ya Uafisa Polisi.

..kati ya vijana waliojiunga na Polisi kutokana na juhudi za Mangi Marealle walikuwa ni Elangwa Shaidi[IGP wa kwanza], Hamza Azizi[IGP wa pili], na Geofrey Sawaya[Mkurugenzi CID].

..kuhusu ujambazi na mambo mengine naweza kusema kuna bad apples ktk kila kabila la Tanzania. hatuwezi ku-generalize jamii nzima kutokana na vitendo vibaya vya wachache.

..zaidi kuna wananchi wengi tu toka Uchagani ambao mchango wao ktk jamii[elimu,uchumi,jeshi,polisi,afya,ufundi...] ni wa kupigiwa mfano. sina haja ya kuwataja hapa maana kuna wengine watakereka na kuja na hoja kwamba Wachaga wana superiority complex.

..naamini kabisa tukirejea kwenye historia ya nchi yetu tutaweza kujifunza mengi na zaidi kuelewa kwanini nchi iko hapa ilipo.

..mfano mdogo ni haya malalamiko ya wananchi wa mikoa ya kusini kwamba maendeleo yote yamepelekwa Kilimanjaro na viongozi Wachaga.

..ninavyoelewa mimi mikoa ya kusini na pwani ilikuwa inasonga mbele kwasababu ya umaarufu wa zao la korosho miaka ya 1960. zoezi la vijiji vya ujamaa ndiyo lililoua zao la korosho na uchumi mzima wa mikoa ya kusini na pwani. tena wananchi walitafunwa hata na wanyama wakali.

..it is 40 yrs since then, na zao la korosho na mikoa ya kusini haija-recover. sasa sijui kwanini watu waelekeze lawama zao kwa Wachaga badala ya vijiji vya ujamaa?

..wananchi wanapumbazwa, badala ya viongozi kuchapa kazi wanatoa visingizio visivyokuwa na msingi. hivi Chacha Wangwe anafikiri Chadema inashindwa uchaguzi kwasababu kuna maderava na matarishi wa Kichagaa? zaidi hao matarishi na madereva wako wangapi mpaka azungumze kwa kichefu-chefu namna ile?
 
huu ni mzaa kwa kweli mwanakijiji .do u think this is a solution for ufisadi? unasema wachaga wote ndio mafisadi nchini?
 
wasukuma si wakabila na hawajipendelei kama wachagga.

..tutaongea yote tuyamalize,wakati nchi inaendelea kurudishwa nyuma au kusimamishwa kimaendeleo.

..tutaendelea kujadili non-issues wakati tabaka la masikini linakuwa kwa kasi kubwa na halina elimu wala msaada wowote wa kujikwamua toka kwenye janga hilo.

..na tuone tutafaidi nini juu ya huu mjadala,zaidi ya kuwasifia wachagga,bila kujua.

..tuendelee kusahaulishana kuhusu epa na kiwira.

..tuendelee kuzunguka kwenye vicious circle.
 
.. Juzi mramba alipokuwa anatoa mchango wake bungeni, alizema ili tanzania tuweze kuendelea tunatakiwa tuwe na miundombinu ya barabara ambayo itaunganisha vijiji, kata, wilaya, mikoa na mwisho nchi nzima. hutu akitolea mfano kwa madoido kwamba, jimboni kwake wamefanikiwa hilo, kwani wanabarabara nzuri. zaidi ya hapo alionyesha hata sehemu ya kupata fedha kujengea barabara hizo. huku akisahau kwamba, alipokuwa akijenga barabara za kwake, huku akiwa waziri katika nchi hii, akiacha sehemu nyingine. je huu sio ubaguzi ambao anaouzungumzia mwanakjj? hatuwezi kuzungumzi hili, kwani bila usawa hakuna haki.
 
Huyo mramba hatuelezi kitu alipokuwa ktk power hakufanya chochote cha maana zaidi ya maneno yake yaliyojaa kiburi na kuwamo ktk magenge ya kifisadi
 
.. Juzi mramba alipokuwa anatoa mchango wake bungeni, alizema ili tanzania tuweze kuendelea tunatakiwa tuwe na miundombinu ya barabara ambayo itaunganisha vijiji, kata, wilaya, mikoa na mwisho nchi nzima. hutu akitolea mfano kwa madoido kwamba, jimboni kwake wamefanikiwa hilo, kwani wanabarabara nzuri. zaidi ya hapo alionyesha hata sehemu ya kupata fedha kujengea barabara hizo. huku akisahau kwamba, alipokuwa akijenga barabara za kwake, huku akiwa waziri katika nchi hii, akiacha sehemu nyingine. je huu sio ubaguzi ambao anaouzungumzia mwanakjj? hatuwezi kuzungumzi hili, kwani bila usawa hakuna haki.

mizizi.. ili tulinganishe hebu tuoneshe rekodi za Mawaziri wengine walifanya nini kuhusu maeneo ya kwao? Mkapa si amejenga daraja kwenda kwao ambalo linaitwa na jina lake na hadi leo hawajajenga daraja la kuvuka Kigamboni, au kujenga daraja la kisasa kupita Kamanga, pale Mwanza? Je huo ni ubaguzi wa Wamakonde wote? (kama unaweza kuita ubaguzi).

Je Mawaziri wengine wamefanya nini in relation to their areas, ukisema Mkapa tu angalau tuwekee data za kulinganisha. Halafu, iweje vitendo vya waziri mmoja alivyofanya (aidha kwa upendeleo au vinginevyo) vibebeshwe Kabila zima au jumuiya nzima ya watu?

Kikwete hivi sasa ni Rais je kuna miradi yoyote inayofanyika Pwani ambayo ingeweza kufanyika mahali pengine na tunaweza kuiita upendeleo? Kuna Uwanja wa Kimataifa unatarajiwa kujengwa huko, kwanini usijengwe Morogoro au Tanga, au Lindi au Dar yenyewe? Hivi sasa Kuna uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mbeya ambao nadhani umefikia mwisho, je mradi ulianza lini na aliyekuwa waziri wa Ujenzi Mwandosya alihusika vipi? Je kila kiongozi ambaye anapeleka mradi kwenye maeneo ya kwao anafanya hivyo? au kila kiongozi anayetoka eneo fulani asiwajibike kuleta maendeleo jimboni mwake kwa hofu ya kuitwa mkabila?
 
Mzee,
Daraja lile lilianza kujengwa wakati wa Mwinyi na nadhani ndiye alienda kuomba fedha kwa wafadhili wa Kiarabu na wengine. Magufuli alifanya "kujipendekeza" kwa Mkapa kwa kulipa daraja lile JINA la Mkapa.
 
Tonga.. unachokiona hapa na mawazo ambayo yanatolewa dhidi ya Wachagga yapo na kuna watu wanaamini kabisa wanachosema. Nina uhakika siyo tu umeshtushwa na baadhi ya maneno lakini pia umehuzunishwa kuwepo kwa maneno hayo.

Haya mambo tumekuwa tukiyakwepa kuyazungumzia au kuyacknowledge kuwa yapo. Mada hii siyo tu imeendelea kunithibitishia kuwa kuna watu wana chuki kali kweli na isiyo na msingi dhidi ya Wachagga lakini pia imenifanya nielewe kwa namna fulani sentiments zinazoweza kuwa zimechangia hisia hizo.

Kama jamii ni lazima tupinge kwa nguvu zetu zote wale wanaoeneza sumu ya ukabila, udini, urangi kwa ajili ya kupata manufaa ya kisiasa au ya kinamna yoyote ile. Wakati huo huo tusije kufanya mambo yetu bila kuangalia jinsi gani mambo hayo yanaweza kutafsirika vibaya.

Ndio maana kwa upande wangu linapokuja suala la Chadema kwa mfano, tatizo ninaloliona lilitokea katika suala la wagombea wa viti maalumu ni suala la utaratibu na mchakato wa jinsi gani hao wanapatikana. Jambo hilo nasikia hata wao wanafahamu ndio maana baada ya mabadiliko ya Katiba yao ya 2006 waliamua kubadili jinsi wanavyofanya uteuzi wa wabunge wa viti maalumu.

Hili pia linatokea katika nafasi mbalimbali za uongozi au utumishi ambapo ninachokiona kama tatizo kubwa si ukabila bali undugunization uliokithiri kutokana na utaratibu mbaya wa kupata ajira na madaraka nchini. Ni kwa sababu hiyo utaona mngoni aliyepata nafasi atahakikisha watoto wake na wenyewe wanaingia kwenye eneo hilo, au akawapa habari za ndani zenye faida watu wa "kwao" na wakapata unfair advantage ya mambo fulani. Hili linatokea kwa karibu makabila yote.

Tatizo kubwa wakati mwingine ni suala la taratibu zilizowazi, huru, na fair kwa mtu yeyote. Endapo, inatangazwa nafasi, kwa uwazi, na huru na nafasi hiyo ikatokewa kugombewa na na watu kadhaa basi lazima tujifunze kukubali matokeo yake hata kama hatupendi yawe hivyo.

Tusikubali kuongozwa na hisia kinyume (negative emotions) kwa sababu hatuoni tunachotaka kuona. Tusilazimishwe kuona kitu ambacho hakipo kama alivyofanya Wangwe hivi karibuni.

Lakini ukweli utaendelea kubakia Watanzania siyo binadamu tofauti na wengine kiasi kwamba hawana mawazo ya kibaguzi ati tu kwa vile ni wa Tanzania. Mawazo haya yapo, yanachochewa na wakati mwingine yanatukuzwa. Ni jukumu la kila mtanzania kuhakikisha siyo tu anapinga mawazo ya kuchochea ukabila, lakini pia kupinga dalili zozote za ukabila zinapojitokeza hata kama zinahusu kabila lake au watu wa jamii yake.

Ni tutakapofanya hivyo ndipo tutakuwa kweli tunajenga Taifa la watu "walio huru, sawa, na wenye kufurahia haki zote za msingi sawasawa katika Taifa lao".

MKJJ,
I salute you!..
1. Mwanzoni sikukuelewa una maana gani...I think im begining to understand you know. kama nimekuelewa vizuri nadhani you are trying to play the devil's advocate to provoke a discussion that would bring out people's feelings/attitudes and perceptions towards this particular tribe.Je, if you were to do the same with another tribe what would be the reaction? do you think it will be different? do you thing it is only chaggas that are not liked?

Umeweka vema kuwa "Tatizo kubwa wakati mwingine ni suala la taratibu zilizowazi, huru, na fair kwa mtu yeyote. Endapo, inatangazwa nafasi, kwa uwazi, na huru na nafasi hiyo ikatokewa kugombewa na na watu kadhaa basi lazima tujifunze kukubali matokeo yake hata kama hatupendi yawe hivyo."...

kuna suali niliuliza mwanzo na sikujibiwa na mtu yeyote..... ni kuwa ukiachilia mbali serikalini au mashirika ya umma..ambako huenda kuna possibility ya kupendeleana.. je how do you explain dominance ya hawa wenzetu kwenye international orgs kama UN, bilateral agencies, private companies... je huko pia kuna ndugu zao wanawavuta? mimi nimekuwa nashangaa ni kwanini wamejaa huko kuliko makabila mengine na inajulikana wazi kuwa kazi hizo zinapatikana through a due process na ni meritocrity ndiyo inayoamua upate au ukose kazi.
....im still waiting to get people's views on this.
 
Mkuu JokaKuu,

Kwanza naomba nikufahamishe kwamba, sina tatizo na editing yako yoyote yenye lengo la kuifanya original post yako ibaki na MAANA ILE ILE YA MWANZO. But my VERY BIG PROBLEM comes when the same editing is intended to negate or distort the whole meaning of your original post. Hebu soma maneno yako mwenyewe hapa chini kisha fikiria mara mbili:

..naomba nirekebishe kauli niliyoitoa hapo mwanzo. nimerejea makala niliyoisoma kuhusu Mangi Marealle na nasikitika kwamba nilifanya makosa ktk kuelezea habari hiyo.

Kwa mantiki hii nalazimika kusema kwamba sina imani na post zako zote kuhusiana na hii mada kwa sababu, nalazimika vile vile kuamini kwamba, chochote ulicho-post hapa hakina ukweli wowote bali kimesukumwa na ushabiki wako wa KIKABILA au na mapenzi yako kwa KABILA unalolitetea, liwe la wadigo au WACHAGG.

Jipange upya mzee kisha ufanye tathimini juu ya uhusiano baina ya jambo zima la ujambawazi na utajiri wa wachagoa na umasikini wa makabila mengine ambayo yanadai kupotelewa si tu na mali yao bali ni pamoja na upotevu wa maisha ya ndugu zao wengi waliopoteza maisha katika matukio mengi ya ujambawazi katika sehemu mbalimbali za hapo nchin. Hili nalo wanasema ni sababu mojawapo ya chuki zao juu ya kabila la wachegga wa kili. Binafsi sijui na siamini kama madai haya ni ya kweli kwani nawakilisha maneno niliyoyasikia mitaani.
 
Duu huu Mjadala,
Niliukimbia lakini nakuta bado upo. Ntaomba niandike kwa kifupi saana.
Pana wakati Mengi alisema kuwa "kama jirani yako ni MASIKINI, basi ujuwe kuwa wewe si salama.." Sikumbuki neno kwa neno. Sasa mengi yaliyosemwa humu ndani yana ukweli kwa asilimia fulani. Inabidi WACHAGA mkubali na Wanachuki mkubali kuwa "SIKU ZOTE UKWELI UKO KATIKATI." Tusio Wachaga tuseme kuwa "Wachaga ni HARD WORKER na wanafanya kila liwezekanalo ili kubadilisha maisha yao .." Huu uwe mfano wa kuigwa kwa Makabila mengine. Wachaga pia mkubali kuwa "mnaka-UKABILA nyie watu na mkumbuke maneno ya Mengi na muanze kuwa msaada kwa makabila mengine..." Najua mna USHIRIKA wenu. Jaribuni kwenda katika USHIRIKA wa makabila mengine na kuwapa MWANGA kidogo wengine nini wafanye ili wabadili maisha ya KWAO. You have nothing to loose for this. Hii itafanya hata makabila mengine yaanze kuwaona nyie ni WATU na SI WACHAGA. Hii ni jambo muhimu sana kwa usalama wenu na TAIFA kwa ujumla.
Ila na makabila mengine si kuwa na NYINYI hamna ukabila. Na nyinyi pia huko huko muanze kuongelea hili maana wakiisha Wachaga mtafuata nyinyi.

NB:- Walikuwepo jamaa wawili Wanyamwezi. Mmoja akitwa Matata (Mwalimu). Huyu jamaa miaka hiyo akiendesha VW Kobe alipata nafasi kwenda kusome India na akirudi awe mkuu wa SIDO Tanzania. Boss wake aliyekuwa ampe makaratasi akasome alikuwa Ni NDUGU wa mbali na Mnyamwezi. Jamaa aliamua kwenda Mtembelea NYUMBANI jamaa yake na kujadili hiyo SAFARI na nafasi ya BOSS WA SIDO kwa ujumla. Alipofika, ALIFUKUZWA kwa matusi mazito kuwa amekuja msumbua NYUMBANI yeye na Wanae wakati akiwa kapumzika. Maswala ya OFISINI si aje OFISINI? Ndugu hawa walikosana hadi leo na leo hii wote wanasote KIJIJINI Tabora. Huwezi amini ukiambiwa kuwa jamaa kakaa USA miaka ya sitini, miaka zaidi ya 7 na nchi nyingine kibao na wakati namuona mara ya mwisho miaka ya 90 alikuwa hana kitu. Sasa hapa wangelikuwa Wachaga!! Wakiendelea tunasema WACHAGA ila sisi twafanya nini? Ndiyo maana nasema Wengine TWAHITAJI VIBOKO, tena hasa vya mti wa MKWAJU maana haukatiki mapema. OPPSS, nimeandika GAZETI 🙂
 
mi ntaunga hoja iwapo hao wachaga elimu yao haiendani na nafasi walizopata na pili ni kwamba kama nafasi zilitangazwa wakaomba na wengine aidha hawakuomba au waliomba wakakosa sasa kosa kwanini liwe la wachaga?? kuna mtu anayeweza kuachia ngazi kwa nafasi aliyoomba na kuipata kihalali na anatimiza wajibu wake?? mi ninachojua ni kwamba ukiona mafanikio ya jirani yako ni changamoto kwako ujitahidi ili uwezi kuyafikia na siyo kuombea afilisike. kama wachaga wameonekana wamefanikiwa bac makabila mengine wajitahidi kusoma na kugombea nafasi mbalimbali zinazotangazwa kama kuna upendeleo waseme ili tujue kwamba wachaga wanapendelewa. kwenye ufisadi sijaona mchaga anayeongoza kama Balali, Chenge, Lowasa, Karamagi,Mkapa na wengineo. Mimi siyo mchaga ila tuangalie jamii kwa ujumla kuliko kuangalia makabila tunaweza kufika pabaya.
 
Duh!! Hii kali!!
MKJJ sikuwahi kutegemea utaandika UPUUZI kama huu!! Totallly and completely BS!
Kwani hujui hata siku zinavyozidi kuenda ni watu wachache sana wanaweza kusema kuwa ni "purely" kabila fulani?
Kama waChagga wanafanya kazi, wamesoma nk kwa nini wasifanikiwe katika kila ngazi? Basi na waMaasai watolewe ktk kazi za ulinzi!!
 
A MODEST PROPOSAL

Na. M. M. Mwanakijiji

Kuna vumbi la chuki, fitina, wivu, kisasi, na hisia za kibaguzi dhidi ya jamii ya Wachagga nchini. Kuna kila dalili kuwa jamii ya Wachagga nchini siyo tu inaanza kutengwa lakini uwepo wake katika nafasi mbalimbali za uongozi inazua hoja ya ukabila kwa haraka zaidi yawezekana kuliko kabila jingine lolote nchini. Katika Tanzania yetu, wachagga wameanza kunyoshewa kidole siyo kwa siri tena bali kwa wazi kabisa tena na watu ambao wakati mwingine hawapati hata kigugumizi.

Ubaguzi huo msingi wake mkubwa ni idadi ya wachagga katika nafasi mbalimbali za uongozi na hasa kuhusiana na elimu yao. Kuanzia mara tu baada ya uhuru jamii ya wachagga mojawapo ya jamii ambayo watu wake wengi wamesoma sana na kufanikiwa kielimu na kiuchumi imekuwa ikinyoshewa kidole cha kupendelewa.

Mtu yeyote ambaye anaweza akafanya uchambuzi yakinifu hatoshangaa kukuta wataalamu wa kichagga katika nafasi mbalimbali za uongozi au taaluma nchini. Kwenye vyuo vikuu, kwenye idara za serikali na hata kwenye taasisi binafsi kumejaa watu wenye asili ya mkoa wa Kilimanjaro na hususan watu wa jamii ya Kichagga.

Endapo itatangazwa nafasi yoyote ya kitaalamu usishangazwe ukiona kuwa waombaji wengi wana majina ya "Kichagga".

Ni kwa sababu hiyo basi kuna kila dalili kuwa kutokana na wingi wao katika nafasi muhimu na vyeo mbalimbali (hata ndani ya Jeshi la Polisi) Wachagga siyo tu ni wengi lakini wanaonekana kufanikiwa zaidi. Hili ni tishio kwa baadhi ya watu. Ni tishio kwa watu ambao hawako tayari kuangalia jitihada za watu katika kufanikiwa kwao na matokeo yake kushutumu ukabila kila idadi ya Wachagga kwenye kitengo fulani inazidi mmoja.

Ushauri wangu ni kuwa, kwa vile Wachagga wameshasoma sana na kuendelea katika biashara karibu mikoa mingi nchini. Na kwa vile wanaendelea kufanikiwa pia katika nafasi mbalimbali za uongozi nchini, basi itakuwa vizuri kama watajitolea kuachilia nafasi hizo ili kuwapa nafasi watu wa makabila mengine.

Kwa vile ni wao wanaonekana kulalamikiwa kutokana na mambo ya kifisadi aidha kwa moja kwa moja au kwa kuashiria basi ni vizuri wawape watu wengine nafasi hizo hata kama watu hao hawajasoma sana. Hii yote itakuwa ni katika kudumisha mshikamano, umoja na udugu wa Taifa letu.

Endapo Wachagga wataachilia nafasi mbalimbali kama UCEO, Ukurugenzi, Ukuu wa Idara n.k watasababisha watu wawapende na kuwakubali kuwa ni wazalendo wa kweli. Sitoshangaa kuwa ndugu zetu wa Jamii ya Kichagga wakikaa pembeni, basi ufisadi utakoma serikalini, idara zitaongozwa na watu wazuri, na mara moja na daima Tanzania itaanza kukua katika uongozi.

Kwa kupendekeza nashauri wabunge wote ambao ni Wachagga au wana asili ya mkoa wa Kilimanjaro kuachia ngazi mara moja ili watu wa makabila mengine wapewe nafasi hizo. Siyo wao tu bali pia wabunge ambao wameoa au kuolewa uchagani vile vile wafuate nyazo hizo.

Wakishamaliza hao, wakuu wote wa idara za serikali ambao wana asili ya mkoa wa Kilimanjaro na hasa wa jamii ya kichagga (wamarangu, wamachame, wa Rombo, na wa Kibosho) na wao waamue kuachilia nafasi hizo kwa ndugu zao Wamakua, Wamwera, Wa Ndali, Wadigo n.k Katika hili Wapare hawahusishwi.

Tukishamaliza wakuu hao wa idara za serikali ningependekeza madaktari wote wenye kumiliki hospitali binafsi ambao ni wachagga au wameoa/kuolewa uchagani na wenyewe waamue kuingia ubia na watu wa makabila mengine kama wangengereko, wambuu, na wanjiro ili hayo makabila madogo na wenyewe wapate nafasi ya kujifunza fani hizi muhimu.

Zaidi ya yote, majaji na mahakimu wote ambao wana asili ya Uchaggani na wenyewe waamue kujitoa katika nafasi hizo kwani wingi wao pia unaonekana sana na hivyo kuwa kikwako kwa watu wa makabila mengine kufanikiwa zaidi katika nyanja ya sheria. Kwanza kabisa wale majaji wa Kichagga wa mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuu wawe wa kwanza kuweka manyanga chini.

Katika kufanya hivyo jamii ya Watanzania ambao inaona ukabila wa wachagga katika sehemu nyingi itaridhika kwani kwa mara ya kwanza tutakuwa tumeshughulikia chanzo cha matatizo yetu mengi.
nilikuwa na imani kubwa sana kwako mkuu M.M.M
sasa naanza kuipoteza.Tukumbuke kuna baadhi ya wanaforum na wale guest wanatutegemea sana kwa maoni na ushauri wetu kwa matatizo tunayopambana nayo kama taifa.And when you come will such post mzee....! naishiwa maneno ya kusema zaidi ya kusisitiza kuwa KILA MMOJA WETU AELEWE NAFASI YAKE KATIKA KULIJENGA NA KULIBOMOA TAIFA HILI.Kama huna cha kupost mzee......... siku nyingine uwe msomaji tu.
 
Bonnie na Injia.. msireact kutoka kwenye visima vya hisia zenu; someni pole pole mada hii you'll get the meaning.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom