Kungurumweupe,
..nilifanya makosa ktk posting yangu ya kwanza na nimekuja hapa na kuyarekebisha na nimeridhika kwamba nilichofanya ni uungwana.
..kama hukuridhika na umepoteza imani na yale ninayoandika hilo haliko ndani ya uwezo wake. pamoja na hayo unaweza kusoma makala niliyokuwa niki-refer kwa kubofya hapa kwenye :
Historia ya Mangi Marealle
..umeleta maneno ya mitaani kuhusu relation kati ya wachaga/ujambazi/maisha na mali za wananchi zilizopotea. pia umeeleza kwamba huamini kama madai hayo ni ya kweli. hata mimi naona ni madai ya kipuuzi, kama ulivyoyaona wewe, kwa hiyo nitayaacha kama yalivyo.
Mizizi,WildCard,
..mradi wa barabara ktk jimbo la Mramba ulianza wakati wa waziri John Magufuli. Basil Mramba aliukuta mradi huo ukiwa ktk hatua ya ujenzi.
..miradi hii ya barabara hupitia hatua za upembuzi yakinifu, design, na kuitishwa tenda, na mwisho ndiyo ujenzi huanza. katika kila hatua huwa kuna fedha zinatengwa.
..hatua ya mwisho ya ujenzi ndiyo hutumia fedha nyingi kuliko hizo za awali. katika miradi yenye wafadhili, mara nyingine huwa kunakuwa na makubaliano ya serikali kuchangia kiwango fulani. serikali ikikiuka makubaliano hayo mradi unaweza kusimama.
..Mbunge Selelli alipiga kelele kwamba mradi wa barabara jimboni kwake ulipewa fedha chache na fedha zote zikapelekwa jimboni kwa Mramba. Mbunge Selelli alifanya kosa la "kiufundi." Mbunge hakueleza kwamba mradi wake ulikuwa ktk hatua ya upembuzi yakinifu, au design, na ndiyo maana ukatengewa fedha ambazo zilionekana ni kidogo.
..hata katika mazungumzo yale utaona kwamba ili kumpoza Mramba alimhakikishia kwamba atahangaika kumtafutia WAFADHILI watakaosaidia kutoa fedha za UJENZI.
..lakini pamoja na hayo Basil Mramba amekuwa waziri wa Ujenzi na miundo mbinu kwa kipindi cha kisichozidi miaka 3. pia sina kumbukumbu za karibuni za waziri wa ujenzi/miundo mbinu anayetokea Uchagani. sasa kwanini hizi lawama zinaelekezwa kwa Wachaga?
..kuna barabara ya Dodoma-Singida-Mwanza ambayo fedha zake zilifujwa na Nalaila Kiula na George Mlingwa. nashangaa hawa hawalaumiwi anakuja kulaumiwa Mramba.
..serikali ya Japan ilitoa msaada wa vifaa kujenga barabara ya kusini. iliamuliwa jeshi ndiyo wangefanya kazi hiyo baada ya kujenga kipande cha barabara ya makambako. Kawawa[mtu wa kusini] kama waziri wa ulinzi did not take action na vifaa vikaharibika. leo hii tunamjengea Kawawa makumbusho kwa utumishi wake uliotukuka. wakati huohuo -tunamlaumu Mramba na Wachaga kwamba ndiyo waliodhulumu mpaka mikoa ya kusini ikakosa barabara.