Je, Viongozi wa Idara ambao ni Wachagga waachie ngazi!??

Je, Viongozi wa Idara ambao ni Wachagga waachie ngazi!??

Status
Not open for further replies.
Mzee,
Daraja lile lilianza kujengwa wakati wa Mwinyi na nadhani ndiye alienda kuomba fedha kwa wafadhili wa Kiarabu na wengine. Magufuli alifanya "kujipendekeza" kwa Mkapa kwa kulipa daraja lile JINA la Mkapa.

Wildcard.. unaona ulichofanya? Umeenda kuonesha mchakato wa ujenzi wa kitu fulani na hukukubali madai yangu kuwa Mkapa kajipendelea... Je ni barabara ngapi za huko Kilimanjaro zilizoanza kuingizwa katika mipango ya bajeti ya serikali kabla ya Mramba kuwa waziri wa Miundo Mbinu?
 
Kungurumweupe,

..nilifanya makosa ktk posting yangu ya kwanza na nimekuja hapa na kuyarekebisha na nimeridhika kwamba nilichofanya ni uungwana.

..kama hukuridhika na umepoteza imani na yale ninayoandika hilo haliko ndani ya uwezo wake. pamoja na hayo unaweza kusoma makala niliyokuwa niki-refer kwa kubofya hapa kwenye : Historia ya Mangi Marealle

..umeleta maneno ya mitaani kuhusu relation kati ya wachaga/ujambazi/maisha na mali za wananchi zilizopotea. pia umeeleza kwamba huamini kama madai hayo ni ya kweli. hata mimi naona ni madai ya kipuuzi, kama ulivyoyaona wewe, kwa hiyo nitayaacha kama yalivyo.

mizizi said:
.. Juzi mramba alipokuwa anatoa mchango wake bungeni, alizema ili tanzania tuweze kuendelea tunatakiwa tuwe na miundombinu ya barabara ambayo itaunganisha vijiji, kata, wilaya, mikoa na mwisho nchi nzima. hutu akitolea mfano kwa madoido kwamba, jimboni kwake wamefanikiwa hilo, kwani wanabarabara nzuri. zaidi ya hapo alionyesha hata sehemu ya kupata fedha kujengea barabara hizo. huku akisahau kwamba, alipokuwa akijenga barabara za kwake, huku akiwa waziri katika nchi hii, akiacha sehemu nyingine. je huu sio ubaguzi ambao anaouzungumzia mwanakjj? hatuwezi kuzungumzi hili, kwani bila usawa hakuna haki.

Mizizi,WildCard,

..mradi wa barabara ktk jimbo la Mramba ulianza wakati wa waziri John Magufuli. Basil Mramba aliukuta mradi huo ukiwa ktk hatua ya ujenzi.

..miradi hii ya barabara hupitia hatua za upembuzi yakinifu, design, na kuitishwa tenda, na mwisho ndiyo ujenzi huanza. katika kila hatua huwa kuna fedha zinatengwa.

..hatua ya mwisho ya ujenzi ndiyo hutumia fedha nyingi kuliko hizo za awali. katika miradi yenye wafadhili, mara nyingine huwa kunakuwa na makubaliano ya serikali kuchangia kiwango fulani. serikali ikikiuka makubaliano hayo mradi unaweza kusimama.

..Mbunge Selelli alipiga kelele kwamba mradi wa barabara jimboni kwake ulipewa fedha chache na fedha zote zikapelekwa jimboni kwa Mramba. Mbunge Selelli alifanya kosa la "kiufundi." Mbunge hakueleza kwamba mradi wake ulikuwa ktk hatua ya upembuzi yakinifu, au design, na ndiyo maana ukatengewa fedha ambazo zilionekana ni kidogo.

..hata katika mazungumzo yale utaona kwamba ili kumpoza Mramba alimhakikishia kwamba atahangaika kumtafutia WAFADHILI watakaosaidia kutoa fedha za UJENZI.

..lakini pamoja na hayo Basil Mramba amekuwa waziri wa Ujenzi na miundo mbinu kwa kipindi cha kisichozidi miaka 3. pia sina kumbukumbu za karibuni za waziri wa ujenzi/miundo mbinu anayetokea Uchagani. sasa kwanini hizi lawama zinaelekezwa kwa Wachaga?

..kuna barabara ya Dodoma-Singida-Mwanza ambayo fedha zake zilifujwa na Nalaila Kiula na George Mlingwa. nashangaa hawa hawalaumiwi anakuja kulaumiwa Mramba.

..serikali ya Japan ilitoa msaada wa vifaa kujenga barabara ya kusini. iliamuliwa jeshi ndiyo wangefanya kazi hiyo baada ya kujenga kipande cha barabara ya makambako. Kawawa[mtu wa kusini] kama waziri wa ulinzi did not take action na vifaa vikaharibika. leo hii tunamjengea Kawawa makumbusho kwa utumishi wake uliotukuka. wakati huohuo -tunamlaumu Mramba na Wachaga kwamba ndiyo waliodhulumu mpaka mikoa ya kusini ikakosa barabara.
 
nilikuwa na imani kubwa sana kwako mkuu M.M.M
sasa naanza kuipoteza.Tukumbuke kuna baadhi ya wanaforum na wale guest wanatutegemea sana kwa maoni na ushauri wetu kwa matatizo tunayopambana nayo kama taifa.And when you come will such post mzee....! naishiwa maneno ya kusema zaidi ya kusisitiza kuwa KILA MMOJA WETU AELEWE NAFASI YAKE KATIKA KULIJENGA NA KULIBOMOA TAIFA HILI.Kama huna cha kupost mzee......... siku nyingine uwe msomaji tu.

Well said Bonnie. Maintain well that good brain.
 
Here's what y'all Chagga haters should do, stop being tribalistic and start working your butts off!!
PS Do not translate this as meaning I am a Chagga, just don't like seeing an obviously hardworking people being dissed for their achievements
 
Kuna baadhi ya wachaga wanaogopa kutumia majina yao ya ukoo kwa kuhofia kutopata kazi kwenye ofisi anayoomba kazi. kwani kwenye hiyo ofisi wachaga wamejaa na wanaogopa kuajiri wachaga wengine. Kama mtu anaitwa Diana Boniface Mushi, anaandika Diana Boniface. usishnagae ukiona mchaga anaukana uchaga kwenye interview.

Ni hayo tu mtu wangu.

Huo ni ukweli. Sio kwa sababu wako Wachaga wengi kwenye hiyo ofisi bali Wachaga wanajua rohoni mwao kuwa hawapendwi simply kwa sababu ni Wachaga.
Wengi wameacha majina halisi ya ukoo ili kuwafix wasiojua.

Ajabu ni kuwa nilikutana na Mhindi mmoja Director wa Kampuni kubwa, ya magari akaniambia anatafuta kijana wa Kichaga katika nafasi fulani. Nilishangaa kweli maana ni nadra kwa Msukuma au Mnyamwezi kufanya hivyo. Kuna sababu maalumu nadhani ,japo alikataa kuniambia kwa nini preference yake ni Mchaga. Nikisoma na hapa JF watu walioonyesha chuki za wazi na hili la Mhindi nabaki mtupu. Labda wahindi tu ndio hawawachukii Wachaga .Do'nt know.....
 
Kungurumweupe,

..nilifanya makosa ktk posting yangu ya kwanza na nimekuja hapa na kuyarekebisha na nimeridhika kwamba nilichofanya ni uungwana.

..kama hukuridhika na umepoteza imani na yale ninayoandika hilo haliko ndani ya uwezo wake. pamoja na hayo unaweza kusoma makala niliyokuwa niki-refer kwa kubofya hapa kwenye : Historia ya Mangi Marealle

..umeleta maneno ya mitaani kuhusu relation kati ya wachaga/ujambazi/maisha na mali za wananchi zilizopotea. pia umeeleza kwamba huamini kama madai hayo ni ya kweli. hata mimi naona ni madai ya kipuuzi, kama ulivyoyaona wewe, kwa hiyo nitayaacha kama yalivyo.

Mizizi,WildCard,

..mradi wa barabara ktk jimbo la Mramba ulianza wakati wa waziri John Magufuli. Basil Mramba aliukuta mradi huo ukiwa ktk hatua ya ujenzi.

..miradi hii ya barabara hupitia hatua za upembuzi yakinifu, design, na kuitishwa tenda, na mwisho ndiyo ujenzi huanza. katika kila hatua huwa kuna fedha zinatengwa.

..hatua ya mwisho ya ujenzi ndiyo hutumia fedha nyingi kuliko hizo za awali. katika miradi yenye wafadhili, mara nyingine huwa kunakuwa na makubaliano ya serikali kuchangia kiwango fulani. serikali ikikiuka makubaliano hayo mradi unaweza kusimama.

..Mbunge Selelli alipiga kelele kwamba mradi wa barabara jimboni kwake ulipewa fedha chache na fedha zote zikapelekwa jimboni kwa Mramba. Mbunge Selelli alifanya kosa la "kiufundi." Mbunge hakueleza kwamba mradi wake ulikuwa ktk hatua ya upembuzi yakinifu, au design, na ndiyo maana ukatengewa fedha ambazo zilionekana ni kidogo.

..hata katika mazungumzo yale utaona kwamba ili kumpoza Mramba alimhakikishia kwamba atahangaika kumtafutia WAFADHILI watakaosaidia kutoa fedha za UJENZI.

..lakini pamoja na hayo Basil Mramba amekuwa waziri wa Ujenzi na miundo mbinu kwa kipindi cha kisichozidi miaka 3. pia sina kumbukumbu za karibuni za waziri wa ujenzi/miundo mbinu anayetokea Uchagani. sasa kwanini hizi lawama zinaelekezwa kwa Wachaga?

..kuna barabara ya Dodoma-Singida-Mwanza ambayo fedha zake zilifujwa na Nalaila Kiula na George Mlingwa. nashangaa hawa hawalaumiwi anakuja kulaumiwa Mramba.

..serikali ya Japan ilitoa msaada wa vifaa kujenga barabara ya kusini. iliamuliwa jeshi ndiyo wangefanya kazi hiyo baada ya kujenga kipande cha barabara ya makambako. Kawawa[mtu wa kusini] kama waziri wa ulinzi did not take action na vifaa vikaharibika. leo hii tunamjengea Kawawa makumbusho kwa utumishi wake uliotukuka. wakati huohuo -tunamlaumu Mramba na Wachaga kwamba ndiyo waliodhulumu mpaka mikoa ya kusini ikakosa barabara.

Mkuu Joka Kuu,

Naishangaa akili yako jinsi ilivoshindwa kuelewa umuhimu wa maneno ya mtaani! Kwa kukusaidia tu ni kwamba maneno ya mtaani ni maneno ya watanzania. Au kwa kukufafanulia zaidi ni kwamba, huko mtaani wamechanganyikana watu wa aina mbalimbali ukianzia wamachinga hadi wasomi wa nchi hii wakiwemo baadhi ya wana JF. Watu hawa hukutana katika vikao mbalimbali vikiwemo vile vya harusi, bar na vinginevyo, bila kujali tofauti za kiwango cha elimu yao katika familiya zao na za marafiki zao.

Pia nakushauri uelewe kwamba, hata hizo habari za kwenye magazeti mashuhuri ya tz unazoziamini wewe, chanzo chake ni huko huko mtaani kwani huko ndiko wanakokaa watu ambao hufanya kazi kwenye makampuni mbalimbali ya tz. Hata zile habari za EPA hawa watu wa huko mtaani ndio wamesaidia kupatikana kwa urahisi, kwani ni wao haohao wanaofanya kazi huko BOT na sehemu zingine nyeti katika nafasi mbalimbali na kisha jioni hurudi mtaani kwao kujipumuzisha wakijichanganya na watu wa mtaani kwao.

Please Think Big! Elewa kwa upana nini maana ya mtaani!
 
Kungurumweupe,

..lakini hayo maneno ya mtaani uliyoyaleta kuhusu ujambazi/maisha yaliyopotea/mali zilizopotea/na chuki dhidi ya uchaga, ni maneno ambayo umesema huyaamini. sasa labda ungetueleza kwanini huyaamini.

..zaidi nashukuru kwa ufafanuzi wako mzuri na msisitizo kuhusu umuhimu wa habari za mitaani.
 
mizizi.. ili tulinganishe hebu tuoneshe rekodi za Mawaziri wengine walifanya nini kuhusu maeneo ya kwao? Mkapa si amejenga daraja kwenda kwao ambalo linaitwa na jina lake na hadi leo hawajajenga daraja la kuvuka Kigamboni, au kujenga daraja la kisasa kupita Kamanga, pale Mwanza? Je huo ni ubaguzi wa Wamakonde wote? (kama unaweza kuita ubaguzi).

Je Mawaziri wengine wamefanya nini in relation to their areas, ukisema Mkapa tu angalau tuwekee data za kulinganisha. Halafu, iweje vitendo vya waziri mmoja alivyofanya (aidha kwa upendeleo au vinginevyo) vibebeshwe Kabila zima au jumuiya nzima ya watu?

Kikwete hivi sasa ni Rais je kuna miradi yoyote inayofanyika Pwani ambayo ingeweza kufanyika mahali pengine na tunaweza kuiita upendeleo? Kuna Uwanja wa Kimataifa unatarajiwa kujengwa huko, kwanini usijengwe Morogoro au Tanga, au Lindi au Dar yenyewe? Hivi sasa Kuna uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mbeya ambao nadhani umefikia mwisho, je mradi ulianza lini na aliyekuwa waziri wa Ujenzi Mwandosya alihusika vipi? Je kila kiongozi ambaye anapeleka mradi kwenye maeneo ya kwao anafanya hivyo? au kila kiongozi anayetoka eneo fulani asiwajibike kuleta maendeleo jimboni mwake kwa hofu ya kuitwa mkabila?

MMJJ,
Your deep love for Mbowe/CHADEMA is unfortunately now making you stupid.

Though this is totaly out of your perceived idea of bringing this thread, i.e. defending Mbowe against Wangwe, but how on earth can you compare a heavily funded Rombo-Tarakea road to a bridge connecting southern regions just because Mkapa comes some 1000km along the brigde roadway?? Do you think this was a fair comparison? How important is the road to Tarakea or even Marangu - Rombo Mkuu in comparison to the connection of Lindi, Mtwara, Songea and even Mozambique to the rest of the country?? Were you out of your mind?

Stop this BS of overdefending anything related to Mbowe, as it now makes you a totaly zombie. Wake up and be a man with brains.
 
Kungurumweupe,

..lakini hayo maneno ya mtaani uliyoyaleta kuhusu ujambazi/maisha yaliyopotea/mali zilizopotea/na chuki dhidi ya uchaga, ni maneno ambayo umesema huyaamini. sasa labda ungetueleza kwanini huyaamini.

..zaidi nashukuru kwa ufafanuzi wako mzuri na msisitizo kuhusu umuhimu wa habari za mitaani.

Nilichokisema mimi ni kwamba siyaamini na wala sikusema kwamba ni maneno ya kipuuzi! Siwezi kusema kwamba ni ya kipuuzi kwani sijafanya research yoyote.
 
Kusema kweli MMJJ anaonekana amefumba macho kabisa as if ni kipofu.
Wakati ukweli wa mambo anaujua kabisa kuwa ukabila na undugunisation kwa hawa jamaa zetu umestawi mno.

Big up KUBWAJINGA KWA COMMENTS ZAKO,
naamini MMJJ amekupata vilivyo, kama akiifanya shingo yake ngumu hiyo ni shauri yake lakini ujumbe umemfikia.
 
Kungurumweupe said:
Nilichokisema mimi ni kwamba siyaamini na wala sikusema kwamba ni maneno ya kipuuzi! Siwezi kusema kwamba ni ya kipuuzi kwani sijafanya research yoyote.

Kungurumweupe,

..nashukuru tena kwa ufafanuzi wako kuhusu haya madai ya ujambazi yanayohusisha Wachaga.

..je, habari za mitaani zinahusisha ujambazi na jamii nyingine yoyote Tanzania, au ni Wachaga peke yao?

..sasa labda huo ni upande mmoja wa shilingi, kwa upande mwingine kuna habari za mitaani zinazohusisha sifa yeyote nzuri na Wachaga?

Kubwajinga,

..ujenzi wa barabara ya kusini umeanza wakati wa Raisi Mwinyi, na Waziri Kiula.

..off course kilio cha barabara ya kusini ni cha muda mrefu na ndiyo maana ujenzi wake ukaanza kabla ya ujenzi wa barabara za Tarakea,Marangu,Rombo.

..ninavyoelewa mimi barabara ya kusini siyo ndefu kama hizi nyingine isipokuwa ujenzi wake ni mgumu na wa gharama kubwa kutokana na nature of the terrain it is passing thr'.

..ugumu wa ujenzi wa barabara ya kusini na ukubwa wa gharama ndiyo umesababisha wafadhili wengi wasite kutusaidia. serikali ilibidi ifanye kazi ya ziada mpaka kuwapata Saudi na Kuwait Fund, lakini hawa "wafadhili tuliowazoea" walikuwa wagumu kuwashawishi kutoa msaada.
 
Kama jamii ni lazima tupinge kwa nguvu zetu zote wale wanaoeneza sumu ya ukabila, udini, urangi kwa ajili ya kupata manufaa ya kisiasa au ya kinamna yoyote ile. Wakati huo huo tusije kufanya mambo yetu bila kuangalia jinsi gani mambo hayo yanaweza kutafsirika vibaya.

Ndio maana kwa upande wangu linapokuja suala la Chadema kwa mfano, tatizo ninaloliona lilitokea katika suala la wagombea wa viti maalumu ni suala la utaratibu na mchakato wa jinsi gani hao wanapatikana. Jambo hilo nasikia hata wao wanafahamu ndio maana baada ya mabadiliko ya Katiba yao ya 2006 waliamua kubadili jinsi wanavyofanya uteuzi wa wabunge wa viti maalumu.

Hili bila shaka umemuelekezea Wangwe, which might be true or can as well be your opinions on him.

Ukweli ni kuwa, wako wengi zaidi ya Wangwe wanaoafikiana na mawazo yake. Kama utaratibu wa uteuzi ulikuwa na walaakini;
  1. Kwa nini tokea malalamiko yalipotokea uteuzi usingefanyika upya??
  2. Kwa nini kila mtu anaambiwa asubiri tu mpaka 2010 wakati mabadiliko yanawezekana leo hii hii???
Hili pia linatokea katika nafasi mbalimbali za uongozi au utumishi ambapo ninachokiona kama tatizo kubwa si ukabila bali undugunization uliokithiri kutokana na utaratibu mbaya wa kupata ajira na madaraka nchini. Ni kwa sababu hiyo utaona mngoni aliyepata nafasi atahakikisha watoto wake na wenyewe wanaingia kwenye eneo hilo, au akawapa habari za ndani zenye faida watu wa "kwao" na wakapata unfair advantage ya mambo fulani. Hili linatokea kwa karibu makabila yote.

Kwa kweli MMJJ umependa, sasa unaita chongo kuwa ni kengeza?? Is it undugunization NOT EQUAL to Ukabila or Ukabila NOT Equal to undugunization?? Was it a coincidence or just unfortunate that only one group of people had ndugus who are capable of being drivers and secretaries?

I think you have invested too much in Mbowe or Mbowe have invested too much in you that you'll go as far as it take to defend him. Very unfortunate.

Tusikubali kuongozwa na hisia kinyume (negative emotions) kwa sababu hatuoni tunachotaka kuona. Tusilazimishwe kuona kitu ambacho hakipo kama alivyofanya Wangwe hivi karibuni.

Sijui hapa ni nani anayelazimisha watu wasione wanachoona?? Kengeza ni kengeza tu na chongo ni chongo. If you call it otherwise it should be at your own peril. Kipambe utakavyo kwa vile umekipenda lakini lazima ujue kuwa hakitabadilika unless umekibadili.

Lakini ukweli utaendelea kubakia Watanzania siyo binadamu tofauti na wengine kiasi kwamba hawana mawazo ya kibaguzi ati tu kwa vile ni wa Tanzania. Mawazo haya yapo, yanachochewa na wakati mwingine yanatukuzwa. Ni jukumu la kila mtanzania kuhakikisha siyo tu anapinga mawazo ya kuchochea ukabila, lakini pia kupinga dalili zozote za ukabila zinapojitokeza hata kama zinahusu kabila lake au watu wa jamii yake.

Ni tutakapofanya hivyo ndipo tutakuwa kweli tunajenga Taifa la watu "walio huru, sawa, na wenye kufurahia haki zote za msingi sawasawa katika Taifa lao".

Utakapoondoa hilo banzi kwenye macho yako, hapo ndio utakapokuwa na uwezo wa kuona anayoona Wangwe. Hapo ndio hayo maandiko yako hapo juu yatakapokuwa na nafasi kwako binafsi.
 
Kubwajinga,

..ujenzi wa barabara ya kusini umeanza wakati wa Raisi Mwinyi, na Waziri Kiula.

..off course kilio cha barabara ya kusini ni cha muda mrefu na ndiyo maana ujenzi wake ukaanza kabla ya ujenzi wa barabara za Tarakea,Marangu,Rombo.

JokaK,
Hili sidhani kuwa linahusiana na hii thread ingawa tunalijadilia hapa.

Sidhani kama ni vema kutetea yasiyofichika. Ujenzi wa barabara ya Marangu-Rombo-Tarakea, umewezekana kutokana na influence ya Mramba. Yaliyofanyika pale ni vioja kwani hata kabla bajeti haijapitishwa, tayari contractor alishakuwa site akifanya kazi muda mrefu, ikiwa ni pamoja na ulipaji fidia wa nyumba zilizobomolewa.

Tusichanganye watu kuwa barabara ya Mtwara ilianza siku nyingi, that doesn't matter. It is the amont of funds alocated to the project that makes it viable. Ndio maana mpaka leo hatujui ni lini tutaweza kuendesha kwenda Mtwara bila shida.

Kwa TZ yenye shida kibao, barabara ya Marangu-Rombo-Tarakea haikutakiwa kupewa kipaumbele kabisa wakati huu. After all tayari ilikuwa ni nzuri sana kwenye gravel level kuliko ile ya kwenda kwa akina Zitto Kigoma. Ukiwa na VW beatle inakufikisha bila shida Rombo, lakini leo hii hata Landcruser inapata shida kwenda Kigoma au Mtwara.

Ulegevu uliopo ndani ya Bunge letu, ndio unaowapa hawa mawaziri wabinafsi kufanya mamboa watakavyo hata pale isipolisaidia taifa.

..ninavyoelewa mimi barabara ya kusini siyo ndefu kama hizi nyingine isipokuwa ujenzi wake ni mgumu na wa gharama kubwa kutokana na nature of the terrain it is passing thr'.

..ugumu wa ujenzi wa barabara ya kusini na ukubwa wa gharama ndiyo umesababisha wafadhili wengi wasite kutusaidia. serikali ilibidi ifanye kazi ya ziada mpaka kuwapata Saudi na Kuwait Fund, lakini hawa "wafadhili tuliowazoea" walikuwa wagumu kuwashawishi kutoa msaada.

JokaK,
Huku ndio kutokuwa na nia ya kujua yanayotokea sehemu nyingine za nchi yako kwa vile tu kwako tayari kuko poa. Nenda hata kwenye Google map ukaangalie urefu wa barabara unaohitajika kusini mwa TZ, maana huko barabara means direction in the bush. Ndio maana watu wengi wa kusini wakija Dar hufia huko huko na hata kuzikiwa huko, kwani wengi wameshakata tamaa kama inawezekana kwao kuwa na mawasiliano mazuri siku moja.

Northeastern TZ, kuna barabara nzuri nyingi zilizojengwa kwa kodi za waTZ wote, ingawa population yake ni ndogo, na hivi sasa hakuna vitega uchumi vipya vikubwa zaidi ya Utalii na Kahawa. Kusini na Magharibi mwa TZ kuna maeneo kibao ya kilimo yaliyoko wazi na hivi sasa kuna hata prospects za gesi na mafuta huko Mtwara, lakini ni vigumu kwa waTZ kujitajirisha na hayo yote kwa vile hakufikiki. Uliza waTZ wangapi wanaojua nini kinachoendelea na akina Artumas?? Hata mkuu wa wilaya ni vigumu kuwatembelea mara kwa mara.

Tanzania will never move forward by just lumping the little resources we have in the Northeast. We need to realise this and rectify our development plans. Ujenzi wa barabara hauchukui muda mrefu kama contractor ni reputable na kuna pesa za ujenzi. Mfano mzuri ni barabara ya Chalinze-Segerea au hata hii ya Rombo.
 
Kubwajinga,

..hatua zote mpaka kufikia kuanza ujenzi zilifanyika kabla Mramba hajafika miundombinu.

..kuna hatua nyingi zinaweza kuendelea bila kusubiri bajeti kupitishwa.

..sasa ina maana Mramba alikuwa na influence kwa Magufuli na Makongoro Mahanga?

..pia naomba ufahamu kwamba contractor huwa anatumia fedha zake kabla hajaanza kulipwa na serikali. kwa hivyo hoja yako ya contractor kuwa site na kuanza kazi inabidi uirekebishe.

..mara nyingine pia hufikia contractor akakopwa na serikali ikiwa haina fedha.

..barabara ya kusini ina historia ndefu sana tangu wakati wa Mbunge Maalim Nabahan.

..tena ukitaka niko tayari kukufahamisha ni juhudi zipi zilifanyika na serikali. kuzorota kwa mradi huo hakutokani na kina Basili Mramba.

..kuna barabara[chalinze-segera,songea-makambako, dsm municipal,mwanza municipal...] nyingi tu zimejengwa kabla ya barabara za kusini. kwanini unahoji barabara ya Tarakea,Rombo, peke yake?

..labda nikuulize swali hili: hizi sentiments dhidi ya Wachaga ziko deep rooted, hata serikalini kuna watu wenye usongo kama wewe. je, ni kitu gani kinachowazuia kuwashughulikia kwa namna ambayo umependekeza hapa?

..naomba ikiwezekana utuletee makadirio ya matumizi ya wizara ya ujenzi na miundombinu tuone kama kweli serikali inaipunja mikoa mingine na kuipendelea Kilimanjaro.
 
Kubwajinga,

..hatua zote mpaka kufikia kuanza ujenzi zilifanyika kabla Mramba hajafika miundombinu.

..kuna hatua nyingi zinaweza kuendelea bila kusubiri bajeti kupitishwa.

..sasa ina maana Mramba alikuwa na influence kwa Magufuli na Makongoro Mahanga?

JokaK,
Kwa taarifa tu ni kuwa barabara nyingi tayari zimeshafanyiwa upembuzi yakinifu. Pesa ndio tu hazitoshi kupelekwa kila mahali. Lakini hii ambayo ilikuwa haina uharaka wala umuhimu, ilipatiwa pesa za kujenga mpaka vituo vya mabasi. Kama sio Mramba, basi mwenzetu tufahamishe jinsi huu upendeleo wa wazi ulivyowezekana.

..pia naomba ufahamu kwamba contractor huwa anatumia fedha zake kabla hajaanza kulipwa na serikali. kwa hivyo hoja yako ya contractor kuwa site na kuanza kazi inabidi uirekebishe.

Nafikiri hufahamu masuala ya ujenzi. Contractor anaanza kazi mkataba unapokamilika. Sasa sijui hawa walianzaje kazi kama pesa ilikuwa bado haijapitishwa bungeni kwenye bajeti?? Contractors huhitaji kupewa advance kwa ajili ya Mobilization n.k. Sijaona contractor, labda awe fake, wa miradi mikubwa hasa kwa nchi kama TZ anayekubali kutumia tu pesa yake bila kujua kama bajeti itapitishwa au la.

..mara nyingine pia hufikia contractor akakopwa na serikali ikiwa haina fedha.

Contractor sio kuwa anakopwa, yeye anafanya kazi kulingana na pesa anayoweza kupatiwa na benki anapowakilisha makabrasha ya mradi alionao. Mteja(Serikali) anapochelewa kulipa, au kushindwa, insuarance yake inam-cover kwenye pesa ya benk, na sio kuwa anatumia pesa yake. Haya yote yanawezekana tu kama mkataba umesainiwa kihalali, kitu ambacho nina wasiwasi hakikufuata taratibu kwenye Rombo project.

..barabara ya kusini ina historia ndefu sana tangu wakati wa Mbunge Maalim Nabahan.

..tena ukitaka niko tayari kukufahamisha ni juhudi zipi zilifanyika na serikali. kuzorota kwa mradi huo hakutokani na kina Basili Mramba.

..kuna barabara[chalinze-segera,songea-makambako, dsm municipal,mwanza municipal...] nyingi tu zimejengwa kabla ya barabara za kusini. kwanini unahoji barabara ya Tarakea,Rombo, peke yake?

JokaK,
Hebu funga macho uache hisia za kiupendeleo. Fananisha hizo barabra ulizotaja umuhimu wake, nini kinapitia humo, nani watumiaji wake n.k., halafu linganisha na Rombo-Tarakea au hata Marangu-Rombo, wapi kwa wapi?? Ukweli tuuseme viongozi wetu wanapokosea, hata kama ni wa kabila letu.

..labda nikuulize swali hili: hizi sentiments dhidi ya Wachaga ziko deep rooted, hata serikalini kuna watu wenye usongo kama wewe. je, ni kitu gani kinachowazuia kuwashughulikia kwa namna ambayo umependekeza hapa?

JokaK,
Kwanza kabisa sijapendekeza kumshughulikia mtu yeyote, tatizo ni kuwa wewe unajadili hapa kama Mchaga na kudefend anything no matter what. Facts are not important to you. Mimi hapa naongelea kama mtanzania. Hii ndio tofauti yetu.

Let's all be true Tanzanians and strive for what is best for us all and our country, and not our uncles and our mere village.
 
kubwajinga,

..mradi unaozungumzia umeanza wakati wa Magufuli, haukuanza na Mramba.

..mkandarasi huanza kazi na baadaye kulipwa kama consultant ameidhinisha alipwe.

..nimekuonyesha barabara zote ambazo vw bettle ingeweza kupita. ni sikuona kama una shida nazo ila hiyo iliyoko rombo tu.

..kuna suala la maintenance vilevile na kuna barabara nyingi tu zinafanyiwa maintanance wakati kuna maeneo mengine hayana hata barabara.

..hii mantiki yako kwamba kwasababu barabara inaweza kupitisha vw bettle basi haipaswi kutengewa fedha ktk mazingira yoyote yale ina walakini.

..mimi naomba utusaidie kwa kutuonyesha kwamba serikali ktk miradi ya barabara imekuwa ikidhulumu mikoa ya kusini.

..Kenya is one of our biggest trading partner na hata investor, kwa hiyo ndiyo barabara ya zinazoelekea huko zina umuhimu wake. na kuna hili suala la Afrika Mashariki.
 
Kubwa Jinga.. ni kwa kiasi gani Waziri ana nguvu ya kuamua fedha ya maendeleo iende kwenye jimbo lake au jimbo lolote lile? Na inawezekana vipi mtu mmoja (Mramba) kuwa na nguvu ya kuamua kupeleka fedha hiyo yote kwenye Bunge ambalo lina watu wa makabila mbalimbali, lenye Rais kutoka mikoa isiyo na barabara nzuri, na Waziri Mkuu ambaye kwake pia si kuzuri? Unataka tuamini kuwa aidha Mramba is the most convincing and conning politician in Tanzania au tuna mawaziri na Rais mbumbumbu kuliko yeyote aliyewahi kutawala!

Hii nguvu mnayompa Mramba ndiyo inasema mengi kuhusu watu wengine kuliko yeye. Lakini kwanza, jibu hilo la Waziri ana nguvu gani za kisheria na kiutendaji zinazoweza kumfanya aamue peke yake kufanya maamuzi ya kupeleka fedha kwenye jimbo lake? Maana kama ni fedha, ziliombwa Bungeni na Bunge la watu wa makabila mengi tu zikapitisha! why blame Mramba?
 
"kuna suali niliuliza mwanzo na sikujibiwa na mtu yeyote..... ni kuwa ukiachilia mbali serikalini au mashirika ya umma..ambako huenda kuna possibility ya kupendeleana.. je how do you explain dominance ya hawa wenzetu kwenye international orgs kama UN, bilateral agencies, private companies... je huko pia kuna ndugu zao wanawavuta? mimi nimekuwa nashangaa ni kwanini wamejaa huko kuliko makabila mengine na inajulikana wazi kuwa kazi hizo zinapatikana through a due process na ni meritocrity ndiyo inayoamua upate au ukose kazi.[/COLOR]....im still waiting to get people's views on this".[/QUOTE]

Yeap, there you go hapa umenena (am refering to the above paragraph), kama hao wachagga wanapendeleana katika mashirika ya umma na serikalini, hebu Mkjj na supporter wengine mjibu swali lililoulizwa hapo juu, nanukuu sehemu hii "how do you explain dominance ya hawa wenzetu kwenye international orgs kama UN etc...." ninasubiri majibu ya wakereketwa ili nijue siri ya hawa wachagga.
All the best.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom