Je, Vyama vya wafanyakazi vimeshawahi kuzungumzia Usalama mahala pa kazi

Je, Vyama vya wafanyakazi vimeshawahi kuzungumzia Usalama mahala pa kazi

OLS

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2019
Posts
457
Reaction score
773
Ni kweli kwamba mishahara huongeza ufanisi wa kazi, lakini usalama wa kazi huongeza vitu vingine ikiwamo kuepusha majanga ambayo yangepelekea mtu kulazwa hospitali kwa muda mrefu ambayo kwenye long run inapunguza utendaji kazi.

Tunaweza sana kuheshimu mishahara lakini nikitazama mazingira ambayo watu hufanyia kazi naona kuna haja ya OSHA kutoa elimu katika hili.

Mafundi mwashi, seremala, wahunzi nk wana risk kubwa ya kupata ajali kazini na kuumia vibaya(unaweza kutaja makundi mengine yenye risks) sijawahi kusikia wakiangaliwa kwa namna ya kuboresha mazingira yao.

Wengi ukiangalia mikoni na miguu imeharibiwa na cement au chokaa.

Usalama wa kazi unakwenda kwenye aina zote za kazi. Je ni kweli watumishi wote wana usalama wa kutosha maeneo yao ya kazi, au mshahara ndio kitu pekee ambacho vyama vya wafanyakazi wanahaki ya kupigania.

Polisi wamekuwa mstari wa mbele kuangalia usalama wa madereva na abiria barabarani kiasi cha kuwatuza faini. Lakini hakuna anayesisitiza fire extinguishers kwenye maofisi, helmets kwa wajenzi na mafundi umeme ambao tunakutana nao mtaani

Angalia hii video halafu fikiria ukuta ungeanguka kwa nje.


Signed

OEDIPUS
 
Back
Top Bottom