Uchaguzi 2020 Je, Vyombo vya Habari hapa nchini vimeripoti "press conference" aliyoifanya mgombea Urais kupitia Chadema, Tundu Lissu?

Kwani Tanzania kuna vyombo vya habari? Au kuna vyombo vya ccm?
 
N
Ndiyo mimi nimeiona TBC.
 
Kwanza huu ni upuuzi.TBC ipi mnataka iripoti mambo yenu ? Kiburi na jeuri yenu mkiongozwa na Mwenyekiti wenu Kuidhalilisha TBC mlidhani hata mkiomba msamaha wananchi tutawaelewa ?
TBC ndiyo shirika mama.Mmewadhalilisha kiasi kile sasa hivi vyombo vingine si mtawavunjiavunjia kila kitu?Nawashauri kwa sababu mmeshakosa adabu muende kwenye hayo mashirika yenu BBC n.k wawatangazie mambo yenu yatawafikia wananchi wote wa Tanzania mpaka vijijini.
 
Baba yako jiwe ameanza figisu figisu kwa Lissu, leo serikali yake ya WATEKA NYARA imekataa kutoa kibali cha chopa. CCM wenzangu tunakwama wapi?

si ndo maaana ya siasa we unataka mpinzani wako akupige kete ama? pointi apa sio chopa
 
Kuna hofu kubwa.Hofu ni kubwa kuliko maelezo
 
Huwa unaangalia taarifa ya habari saa ngapi??
Jana hiyo taarifa ya Lisuruwali lirushwa Jamii Forum na TBC kwnye taarifa ya habari niliiona so wewe ulikuwa unazungumzia vyombo gani?????????
 
Kwanza wewe nakuonea huruma sana...................

Kwa kuwa huelewi mwanzo wa mgogoro na TBC ni nini?

Hivi wewe hujui kuwa TBC, ambapo ni ya Umma, inayogharimiwa na sisi sote walipa kodi wa nchi hii, bila kujali itikadi zetu za siasa, hivi sasa inaendeshwa kama chombo cha propaganda cha CCM?

Na hilo alilikiri mwenyewe, Mkurugenzi wa TBC, kwa kuiomba radhi Chadema na kukiri madhaifu yaliyotokea siku hiyo ya kukata kata matangazo ya moja kwa moja, siku ya ufunguzi wa kampeni
 
Vyombo vya habari mnafukuza na airtime mnataka nyambafu
 
Jambo la kushangaza ni kuona kuwa hata chombo cha habari cha Umma, Televisheni ya TBC, ambayo gharama za uendeshaji wake tunaibeba walipa kodi wa nchi hii, bila kujali itikadi zetu za kisiasa, nacho hakitaki kumripoti mgombea huyo wa kiti cha Urais!

**********

Brother acha kujidhalilisha verify information zako kabla ya kuzileta humu
 
Haitawasaidia chochote, mwisho wa siku watakuja kuaibika tu. Hakuna Dikteta anayedumu MILELE.
Bravo. Hata Saddam, Gaddafi, Mubarak, Al Bashir na Mugabe hawapo tena, siku inayokucha moja moja imewazidi kimo.
 
Mliwafukiza TBC sasa laana inawaandama. Hata hivyo msitupotezee muda maana hamshindi uchaguzi
 
Kinachotakiwa na vyombo vya habari hapa nchini ni kuondoa hofu ambayo imetanda miongoni mwa
hofu itaondoka vipi kila siku mnawatukana mara kuwafukuza mara muwaambie wamenunuliwa
mtakula jeuri yenu safari hii
 
Uliangalia taarifa ya habari TBC jana ukaona hawakutangaza?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…