Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Kuna vitu vinafikirisha na kuzaa maswali yaliyokosa majibu kwa haya yanayoendelea hapa nchini kwa sasa yakihusisha kupotea ovyo kwa watu, kamata kamata ya wapinzani, wanaharakati na waandishi wa habari.
Taifa linalazimishwa kwa nguvu kubwa mnoo kuingizwa kwenye taharuki isiyo ya lazima. Vyombo mbalimbali vya habari duniani vinaripoti matukio haya huku vikijenga taswira mbaya ya ubovu wa utawala wa mama katika kusimamia haki za binadamu, demokrasia na utawala bora.
Heka heka hizi zinaendeshwa na nani, kwa malengo gani ikiwa ziko kinyume na mtazamo wa mama?
Kauli za kukinzana baina ya wanausalama wao kwa wao na baina ya watawala kuhusu haya yanayoendelea nchini zinazidisha hofu na mashaka kuwa huenda ni matukio ya njama za kimakusudi kumchafulia mama kisiasa.
Hakuna jambo linaloweza kutendeka kwa bahati mbaya ikiwa linafanywa na mfumo rasmi tena kwa mtindo wa kujirudia rudia.
Huenda yatakayofuata yatakuwa mabaya zaidi ikiwa hatua za kimakusudi kuzuia kuendelea kwa mambo haya hazitachukuliwa sasa. Hakuna aliye salama.
PIA SOMA
- Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe akamatwa uwanja wa Ndege Songwe
- Lissu, Mnyika na Sugu wakamatwa na Polisi usiku huu. Baadhi ya Waandishi wa habari pia wakamatwa
- Kuelekea 2025 - Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Nchimbi aiagiza Serikali kuwaachia Viongozi wa CHADEMA