Huu Ujenzi upo sawa kabisa kama pesa iliyokuwepo ni ndogo.
Kitaalam hapo hawajajenga Septic Tank wala hamna Soak Away Pit na hakuna haja ya kutumia vizuizi vya hewa Chafu kama S, P na U Traps ambazo hubaki na majimaji muda wote kuzuia hewa kurudi.
Kama sijakosea, Naona hii ni Modified Pit Latrine yaani Choo Cha Shimo Cha kisasa. Kitaalam kinaitwa REED ODOURLESS EARTH CLOSET
View attachment 1962440
Hairuhusu hewa kurudi ndani ya Choo kama wengi tunavyosema.
It's provided with Vent Pipe and is extremely a Satisfactory Toilet.
Faida zake 2 kwa aina hii ya Choo ni hizi;
1. Sakafu yake inabebwa na Udongo tu na hakuna Shimo chini yake kwa hiyo choo hakiwezi kushuka kwa kuporomoka kipindi Udongo ukizidiwa uwezo
2. Shimo lake linakaa pembeni ni rahisi kutapisha Uchafu na kuendelea kulitumia Tena Shimo hilohilo. Kwa hiyo kinadumu sana. Ni tofauti na hiki hapa chini kinachoweza kutumbukia
View attachment 1962441
Wasiwasi labda ni hizo Bomba kuwa za Plastic zinaweza zisidumu. Licha ya kuwa zitafukiwa vizuri maana pia zimewekwa karibu sana na Usawa wa ardhi na mbali kidogo kutoka kwenye Mashimo yenyewe ya Choo. Zingekuwa Rigid Pipes au Flexible Pipes na sio hizo BRITTLE choo safi saana