Je, Wabunge Viti Maalum ni wa kubebwa? Mnaonaje iwe ni awamu moja tuu kisha waendeni jimboni, kupisha wengine, au waendelee kubebwa tu?

Je, Wabunge Viti Maalum ni wa kubebwa? Mnaonaje iwe ni awamu moja tuu kisha waendeni jimboni, kupisha wengine, au waendelee kubebwa tu?

Pascal Mayalla,
Sofia simba alianzisha movement kama hii yako ila yeye alisema mwisho awamu mbili, alipigwa vita na wenzie hadi alijuta sasa wewe sijui watakuacha salama.
 
wakagombee majimboni, na hao walioko majimboni waende wapi? majimbo yako machache, kwanza wabunge wa viti maalum ni wachache inafaa waongezwe, kila jimbo inafaa liwe na mbunge wa viti maalum idadi iwe sawa
Nahis gender equality kama wangekua 50%___50%....au mwanaume akiwa na nguvu ni faulo AF mwanamke akiwa Nazo
ni superior
 
Nyakageni,
Uchaguzi na kuongoza nchi siyo masuala ya kufanyia majaribio hata kidogo. Sawa, mtabeba hivyo vyama 3 ulivyotaja halafu vitaanzishwa vipya vingine. Nchi itaendeshwa kwa mtindo wa kubebana hivyo mpaka lini?

Kila uchaguzi mnabeba chama kipya! Mbona dunia yote itacheka kwa sauti ya dharau na kebehi? Kwenye masuala ya msingi ya nchi tusifanye michezo michezo ya kubebana kwa majaribio.
 
wakagombee majimboni, na hao walioko majimboni waende wapi? majimbo yako machache, kwanza wabunge wa viti maalum ni wachache inafaa waongezwe, kila jimbo inafaa liwe na mbunge wa viti maalum idadi iwe sawa
Na iwapo mbunge wakuchaguliwa ni wa kike, hapo inakuwaje? au ndio wanakuwapo wanawake wabunge wawili?
 
comte,
Wanawake watatakuwa wabunge peke yao? Hahaaa hiki kichekesho, hawa wanawake ambao kutwa nzima wanashinda wakipiga umbea wa nani katoka na nani? hawa wanawake ambao wamepata hata exposure kidogo hiyo exposure yenyewe bado wanaitumia kwenye umbeya, wana simu zenye intaneti, wanaishi mjini, wana elimu, lakini cha maana wanachofanya na hizo simu ni kutembelea instagram kucheki umbea wa Zari na Diamond?

Nimesoma na wanawake, nimeishi na wanawake, nimefanya kazi na wanawake, wanawake hawawezi siasa wala utawala, ni mambo magumu sana kwao, tazama hata hapa JF kwa mfano, ni nadra sana kuwakuta jukwaa la siasa au hata habari na hoja, utawakuta kwenye MMU na Chit Chat wakijadili umbeya na mapenzi, sasa hawa kwa nini ilazimishwe kuwapa nafasi za kisiasa za upendeleo wakati hawawezi siasa?
 
Pascal Mayalla,
Dawa ilikuwa ndani ya katiba ya Warioba. Ilikuwa haina viti maalum lakini ililazimisha uchaguzi wa wabunge wanawake na wanaume kwa lazima, kwa pamoja. Sitta aliyejidai kuwa ni samaki aliyerudi majini akajikuta hana muelekeo na Bunge lake. Aibu tupu!

Hata wakijaa Bungeni haisaidii kueleza gender equality maana vijijini bado wanawake wanahangaika. Bahati mbaya hili akina Pompeo hawalioni na badala yake wanahangaika na mambo ya mashoga,
haya mabo ya gender equality si yamekuwa initoated na hao hao wazungu? kama sio wao hata viti maalumu visingekuwepo,japo havisaidii
 
Johnny Sack,
Johnny Sack, unajua wanawake ndio wapiga kura wengi- hivi wakiamua kujipigia wewe mwanaume na hoja zake utafika bungeni? Maelezo yako yanaunga mkono mpango wa viti maalumu- ASANTE
 
Johnny Sack, unajua wanawake ndio wapiga kura wengi- hivi wakiamua kujipigia wewe mwanaume na hoja zake utafika bungeni? Maelezo yako yanaunga mkono mpango wa viti maalumu- ASANTE
Wanawake na wanaume ni kama wanalingana kwa idadi tu ni kama 51 kwa 49 tukiwaganywa kwa asilimia, kacheki takwimu za sensa uhakiki mwenyewe, na hata hivyo wanawake hawafuatilii sana na siasa hata wanaopiga kura wanakuwa wachache kuliko wanaume
 
Wanawake na wanaume ni kama wanalingana kwa idadi tu ni kama 51 kwa 49 tukiwaganywa kwa asilimia, kacheki takwimu za sensa uhakiki mwenyewe, na hata hivyo wanawake hawafuatilii sana na siasa hata wanaopiga kura wanakuwa wachache kuliko wanaume
Johnny Sack, SO wakijipa 51 nyinyi mna 49 mnaingiaje bungeni?
 
Wanabodi,

Kwanza angalieni hii picha
More than 60% of Rwanda’s parliamentarians are women. Photo: Sam Ngendahimana
More than 60% of Rwanda’s parliamentarians are women. Photo: Sam Ngendahimana

Nimesoma kwenye Ripoti ya WB, Bunge la Rwanda ndilo Bunge linaloongoza Dunia kwa gender equality baada ya kuwa na asilimia kubwa ya wabunge wanawake kuliko wanaume, wakati Bara la Africa likiongoza duniani kwa kuwa na maspika wengi wanawake kuliko mabara yote.

Hii maana yake ni gender equality is possible ila pia nafasi za upendeleo kwa wanawake vikiwemo viti maalum, dhumuni lake sio kuongeza tuu idadi ya wanawake bungeni, bali ni kuwajengea uwezo wabunge wanawake walioteuliwa, yaani empowerment, kuwa empower.

Hilo kwa Rwanda limewezekana kwasababu ubunge wa viti maalum kule ni kwa awamu moja tuu, awamu ya pili wanakwenda majimboni na kupisha wengine.

Mnaonaje na sisi Tanzania tukafuata mfumo huo?.

Japo sio neno zuri kulitumia lakini ndio ukweli wenyewe, Ubunge wa Viti Maalum ni ubunge wa kubebwa. Sasa kama wewe Mbunge mwanamke umebahatika kubebwa, ukaukwaa ubunge wa Viti Maalum, na ukakaa Bungeni miaka 5, maana yake umeisha kuwa empowered, huhitaji kubebwa tena kumendea ubunge kupitia Viti Maalum, sasa unakuwa umeiva kustahili kwenda kugombea jimboni.

Kama umekuwa Mbunge Viti Maalum miaka mitano na bado huwezi kwenda jimboni, then wewe utakuwa hufai, hata ukirudi Bungeni utakuwa huna jipya!, hivyo ni bora upumzishwe, wapewe nafasi wengine wenye uwezo wa kujiongeza kwasababu kiukweli kabisa kuna baadhi ya hawa wabunge wa viti maalum huwasikii wakichangia mjadala wowote zaidi ya kuupara na kutokelezea, hadi watu humu kuwabatiza jina la Wabunge wa "Vitu Maalum".

Ukibebwa, bebeka, haiwezekani mtu ubebwe mara ya kwanza, uvushwe mto mpaka ng'ambo ya pili, halafu baada ya kufika upande wa pili, badala ya kushuka na kutembea mwenyewe, wewe bado unang'ang'ania mgongoni uendelee kubebwa!. Kitakacho fuata hapo ni wewe kubwaga tuu chini puu!, unless huyo anayekubeba, naye anapata uroda fulani kukubeba,maana kiukweli ukibeba chochote nimzigo kwako,ila kama mzigo huo unafaida kwako, japo ni mateso kuendelea kuubeba, utaendelea kuubeba tuu.

Mnaonaje wanabodi, hawa wabunge wa kubebwa kupitia Viti Maalum, wawekewe ukomo wa miaka 5 tuu au kwa sababu kubebwa ni raha, na kula uroda hivyo wabebaji wanapenda kuendelea tuu kubeba na wabebwaji wanaona uroda kubebwa?.

Ukibebwa bebeka, na next time jibebe, usibwete, na kupenda kuendelea kubebwa tuu, oneni aibu!. Tuweni kama Rwanda!.

Vipi wajameni, wa kubebwa waendelee kubebwa tuu au wajibebe, na wasipojibeba wabwagwe?

Paskali
Pascal....Kama ni 60 per cent in favour of one gender then there is no gender equality....teheteh just an argument Pascal....Sina Nia ya ubishi
 
Pascal....Kama ni 60 per cent in favour of one gender then there is no gender equality....teheteh just an argument Pascal....Sina Nia ya ubishi
Naunga mkono hoja, gender balance is not 50/50, but promotional representation, kama kwa Rwanda wanawake wako 60% na wanaume ni 40%, then hiyo 60% ya wabunge wanawake Rwanda ni gender balance. Hata sisi Tanzania, kwenye matokeo ya sensa yetu ya watu na makazi, wanawake wako wengi kupita wanaume, hivyo wanapaswa kuwa wengi zaidi ya wanaume kwenye kila sekta zisizo hitaji muscle powers.
P
 
Back
Top Bottom