Pre GE2025 Je, wabunge watakaoshinda kupitia CHADEMA 2025 watagomea mshahara wa Milioni 18 kwa mwezi?

Pre GE2025 Je, wabunge watakaoshinda kupitia CHADEMA 2025 watagomea mshahara wa Milioni 18 kwa mwezi?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Umebadili swali tena aisee chadema bana, pale ni kuwa wanaoona inafaa watahamia bandari nyungine,ikishindikana wataacha walipwe mafao au waajiriwe na waliopewa kuendesha bandari
Mliwaahidi hakuna atakayekosa ajira,

Uzuri uchaguzi u karibu,

Hakuna RANGI hamtaona 2024&2025.
 
Unaona maneno anayotumia yule bilionea wenu Jacob dhidi ya ACT? Kama mnaona ACT inakufa achaneni nayo tuu ijifie si kutumia maneno kama yale,nyie jengeni chama mbona mlipofika CHADEMA ni pakubwa tuu
Kama anatukana Si vizuri, anatakiwa ajirekebishe.
 
Kwa mtazamo wangu concept yake ilikuwa inalenga ni kwa namna gani viongozi wabinafsi, wanajiongezea wao mishahara ili hali watumishi wa umma kama walimu, madoctor, askari n.k kilio chao cha muda mrefu hakifanyiwi kazi
Mbowe amewahi kuwa mbunge na walikuwa wakilipwa 12ml,

Hawakuwahi kugomea mishahara hiyo Ili kuipunguzia serikali Mzigo Ili pesa hizo zisaidie kulipa angalau posho za walimu.

Na hicho ndio Hasa kiini Cha thread hii, tunataka kujua ikiwa sasa ametamka Kwa kudhamiria au ni kauli ya kisiasa tu!!
 
Muulize mleta mada, hii inchi ni yetu sote, Kila mtu anayeumizwa na tatizo hili ni jukumu lake kutafuta namna ya kulitatua. Kwa kuwa ameliona tatizo na anafikiri wa kulitatua ni chadema, basi naye ajiunge na chadema, agombee ubunge, apambane na kukataa wizi huu.
Shukran mkuu. Huyu mdau hazungumzii suala la CHADEMA kutatua tatizo hilo la ufujaji wa fedha za umma. Yeye anachotaka ni CHADEMA waseme mapema kwamba 2025 wakipata ubunge, hawatachukua hayo malipo ili kuonyesha msimamo kuwa hawakubaliani nayo. Basi.

Yaani hata kama malipo yanaendelea kutolewa, wabunge wa CCM ambao ni wengi zaidi na wengineo wakiendelea kulipwa, mradi wabunge wa CHADEMA peke yao hawayachukui yeye roho yake itakuwa na amani!

Tuseme anataka kuona msimamo wa CHADEMA kwa vitendo. Basi. Hana shida na wengine wakiendelea kujinufaisha na hayo malipo. Tuseme haoni tatizo katika hayo malipo bali hakufurahia kauli ya Mbowe kuyapinga.

Kwangu mimi huyu ni ama mgonjwa wa kisaikolojia au mnafiki wa hali ya chini sana asiyeelewa suala ni lipi hasa hapa.
 
Salaam, Shalom!

Mimi ni MMOJA wa wananchi anayepinga wabunge kulipwa zaidi ya milioni 3 tatu, Kwa mwezi kutokana na Pato kiduchu linalokusanywa maana ubunge ni KAZI ya kujitolea, ni seasonal job!!

Inakadiriwa, makusanyo ya Serikali kupitia Kodi na vyanzo vingine vya mapato havizidi bil 900 Kwa mwezi, Kwa mshahara wa wabunge 399 kulipwa ml 18 Kwa mwezi, Serikali italipa Billion takriban 7 Kwa mwezi, hao ni wabunge pekee,

Tukilipa watumishi wote wa Serikali mishahara na stahiki zao Kwa mwezi, ni dhahiri kulingana na makusanyo madogo, italazimika Serikali kukopa pesa Ili kujazia ulipaji wa watumishi wa Serikali,pesa za ndani haxitatosha kulipa mishahara.

CHADEMA ilikuwa na wabunge wengi tu tangu 2000, 2005,2010, 2015 na wakapungua Hadi mbunge mmoja 2020.

CHADEMA ilipokuwa bungeni tangu awali, hawakuwahi hata siku moja kugomea posho na mishahara ya wabunge wao bungeni zaidi ya kusema mishahara na marupurupu hayo ni kiduchu kulingana na hadhi ya mbunge.

Sasa Kwa kuwa Mwenyekiti Mbowe ameamka Kutoka usingizini na kuonyesha kukerwa na wabunge kuongezewa posho na marupurupu Yao Kutoka ml 13 Hadi ml 18 Kwa mwezi, naungana naye kupinga ubadilifu mkubwa wa Kodi za wananchi,

Na Kwa kuwa CHADEMA imetoa kauli kuwa itashiriki uchaguzi 2025, na Kwa kuwa itasimamisha wagombea ubunge Nchi nzima,

Na Kwa kuwa CHADEMA Ina uwezekano wa kushinda ubunge katika majimbo kadhaa nchini,

Je, wabunge watakaoshinda ubunge kupitia tiketi ya CHADEMA 2025 watagomea kupokea posho na marupurupu yanayofikia 18 ml Kwa mwezi?

NB: Vyama, viwekwe pembeni, walipakodi tujadili kwanza maslah ya nchi, Hasa matumizi mazuri ya Kodi zetu,

Swali: Upi Hasa uwe mshahara na marupurupu ya mbunge Kwa mwezi kulingana na makusanyo yetu kupitia Kodi?

ANGALIZO: Ni muhimu wananchi Kwa UMOJA wetu tupambanie KATIBA mpya na Tume huru ya Uchaguzi kabla ya Uchaguzi wowote, vyama vya siasa na wanasiasa hawaaminiki.

Karibuni🙏

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Mungu ibariki CHADEMA.

Amen
Kifup ni kwamba watapokea hiyo hela na hizi kelele huto zisikia kamwe
 
Shukran mkuu. Huyu mdau hazungumzii suala la CHADEMA kutatua tatizo hilo la ufujaji wa fedha za umma. Yeye anachotaka ni CHADEMA waseme mapema kwamba 2025 wakipata ubunge, hawatachukua hayo malipo ili kuonyesha msimamo kuwa hawakubaliani nayo. Basi.

Yaani hata kama malipo yanaendelea kutolewa, wabunge wa CCM ambao ni wengi zaidi na wengineo wakiendelea kulipwa, mradi wabunge wa CHADEMA peke yao hawayachukui yeye roho yake itakuwa na amani!

Tuseme anataka kuona msimamo wa CHADEMA kwa vitendo. Basi. Hana shida na wengine wakiendelea kujinufaisha na hayo malipo. Tuseme haoni tatizo katika hayo malipo bali hakufurahia kauli ya Mbowe kuyapinga.

Kwangu mimi huyu ni ama mgonjwa wa kisaikolojia au mnafiki wa hali ya chini sana asiyeelewa suala ni lipi hasa hapa.
CCM inaondolewa madarakani,

Chama mbadala ni CHADEMA,

Na ndio Hasa msingi wa HOJA ya thread hii.

Mbona swali ni Rahisi tu, Vaa viatu vya Mbowe na CHADEMA, jibu je wabunge wa CHADEMA 2025 watapokea 18 ml au watazikataa Kwa maelekezo ya chama?

Mimi Hasa ndiye nayeisaidia CHADEMA ktk uso wa umma kuliko wewe unayeamini CHADEMA haikosei.

Karibu.
 
Kugomea Mishahara wala si utatuzi wa shida tulizo nazo kuna ubadhirifu mkubwa serikalini kuliko hiyo mishahara na posho za wabunge. Kikubwa serikali iangalie vipaumbele vya wananchi na kuvitimiza, wananchi wanashida na Bima ya Afya, Umeme, Darasa moja la msingi linawanafuzi 200,Mikopo elimu ya juu inatolewa kidogo na kwa wanafunzi wachache. Serikali inatakiwa izibe mianya ya ubadhirifu.
 
Tukubali uwezo wa watanzania ni mdogo sana
Mtu anailaumu chadema ambayo haina mbunge huku ccm wakiendelea kuitafuna nchi
Acha uongo, Uwezo wa watanzania ni "chini ya normal" yaani upo negatice, wewe unaona kama upo chini lakini ni zaidi ya chini.
Hvi vyuo vyetu vya mlimani city , udom na mzumbe kuanzia 1990 imezalisha takataka kabisa, chawa , walafi, wasio na uzalendo na wafia dini huku wakila wenzao!
 
Sasa wajibu wako kama raia ni nini, ikiwa kila jambo 'eti' fulani akufanyie. AMKA!
 
Mliwaahidi hakuna atakayekosa ajira,

Uzuri uchaguzi u karibu,

Hakuna RANGI hamtaona 2024&2025.
Thubutu,sisi tunaijua siasa wewe ngoja uone tutakavyowapiga kwa hoja hadi mtapoteana,CCM NDIO CCM MZEE ngoja utajionea.
 
Hakuna mtu timamu anagomea Hela ila tunagomea sera.
Sera ya kulipana kupitiliza huku nchi ikiwa hoi Kila idara ni sera ya kupingwa na Kila mtu timamu
 
Hakuna mtu timamu anagomea Hela ila tunagomea sera.
Sera ya kulipana kupitiliza huku nchi ikiwa hoi Kila idara ni sera ya kupingwa na Kila mtu timamu
Kwahiyo unachukua ml 18 Kwa mwezi.

U mbunge Jimbo Gani au umewahi kuwa mbunge?
 
Tukiachana na hayo je limi tulisimama kwa ujumla wetu kuonyesha kukerwa na malipo ya ziada kwa wenza wa mabosi wa nchi hiii
 
Salaam, Shalom!

Mimi ni MMOJA wa wananchi anayepinga wabunge kulipwa zaidi ya milioni 5 tano kwa mwezi kutokana na Pato kiduchu linalokusanywa ,maana ubunge ni KAZI ya kujitolea, ni seasonal job!!

Inakadiriwa, makusanyo ya Serikali kupitia Kodi na vyanzo vingine vya mapato havizidi bil 900 Kwa mwezi, Kwa mshahara wa wabunge 399 kulipwa ml 18 Kwa mwezi, Serikali italipa Billion takriban 7 Kwa mwezi, hao ni wabunge pekee,

Tukilipa watumishi wote wa Serikali mishahara na stahiki zao Kwa mwezi, ni dhahiri kulingana na makusanyo madogo, italazimika Serikali kukopa pesa Ili kujazia ulipaji wa watumishi wa Serikali,pesa za ndani haxitatosha kulipa mishahara.

CHADEMA ilikuwa na wabunge wengi tu tangu 2000, 2005,2010, 2015 na wakapungua Hadi mbunge mmoja 2020.

CHADEMA ilipokuwa bungeni tangu awali, hawakuwahi hata siku moja kugomea posho na mishahara ya wabunge wao bungeni zaidi ya kusema mishahara na marupurupu hayo ni kiduchu kulingana na hadhi ya mbunge.

Sasa Kwa kuwa Mwenyekiti Mbowe ameamka Kutoka usingizini na kuonyesha kukerwa na wabunge kuongezewa posho na marupurupu Yao Kutoka ml 13 Hadi ml 18 Kwa mwezi, naungana naye kupinga ubadilifu mkubwa wa Kodi za wananchi,

Na Kwa kuwa CHADEMA imetoa kauli kuwa itashiriki uchaguzi 2025, na Kwa kuwa itasimamisha wagombea ubunge Nchi nzima,

Na Kwa kuwa CHADEMA Ina uwezekano wa kushinda ubunge katika majimbo kadhaa nchini,

Je, wabunge watakaoshinda ubunge kupitia tiketi ya CHADEMA 2025 watagomea kupokea posho na marupurupu yanayofikia 18 ml Kwa mwezi?

NB: Vyama, viwekwe pembeni, walipakodi tujadili kwanza maslah ya nchi, Hasa matumizi mazuri ya Kodi zetu,

Swali: Upi Hasa uwe mshahara na marupurupu ya mbunge Kwa mwezi kulingana na makusanyo yetu kupitia Kodi?

ANGALIZO: Ni muhimu wananchi Kwa UMOJA wetu tupambanie KATIBA mpya na Tume huru ya Uchaguzi kabla ya Uchaguzi wowote, vyama vya siasa na wanasiasa hawaaminiki.

Karibuni🙏

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Mungu ibariki CHADEMA.

Amen
Simple answer; wakiwa wengi zaidi ya wabunge 50% watapinga kwa kanuni kupungua kwa mishahara

Wananchi Tulazimishe Mazingira ya kupata wabunge wa upinzani above 50% n
Mambo yakuwa mazuri
 
Back
Top Bottom