Je, Waislam mtakubali kupandikiziwa figo ya nguruwe?

Je, Waislam mtakubali kupandikiziwa figo ya nguruwe?

Nahisi kuna kutoelewana kwa taarifa na mapokeo ya kale (mafunzo ya dini )

Huyu mdudu sijaona kosa (uharamu) lake
[emoji41]
Kwako wewe hujaona uharamu wake lakini Mungu akishasema kitu ni haramu basi haina haja ya binadamu kubisha mna yy ndo alokuumba.
 
[emoji2960][emoji2960][emoji2960] watasema "kila mtu atakufa tu" ila ukiumwa wewe hakuna wingi.

Nasikia Qur'an inaruhusu kula [emoji200] ukiwa kwenye hali ya kufa ili kuyaokoa maisha yako.

FaizaFoxy Bwana Utam STRUGGLE MAN
Ufafanuzi tafadhali
Ndio dini ya kiislamu inaruhusu kula nguruwe kwa ajili ya kuokoa maisha ya m.damu endapo hakuna chakula kwa wakati ule lkn asile kwa kushiba bali ale kwa kiasi tu ili asijepatwa na mauti
 
Tatizo kuna watu wanamwona kama adui na kama ameumbwa na shetani hata kumeona tuu wanataka kumshambulia
Hao wanofanya ivo wanafanya kwa utashi wao tuu mana uislamu haujasema ivo na umekataza pia dharau ata kama ni huyo nguruwe
 
Mi huwa kila nikipata dhalula ya njaa ya kufa siku za weekend huwa nakula nyama ya Nguruwe kilo moja tu (sio ya kushiba) na najisikia nafuu hapo hapo.
Kwali kila kiumbe cha Mwenyezi Mungu kina umuhimu wake.
Uislamu umeruhusu kula nguruwe endapo hakuna chakula chengine iyo sehemu ulokuepo lkn sio kama unavofanya wewe
 
Muislamu si sahihi kutumia kitu chochote kitokanacho na nguruwe, si nyama yake wala viungo vyake wala huduma yake. Huo ndiyo mtihani tuliyopewa watu wa vitabu.
Huko nyuma mayahudi waliambiwa siku ya Sabato wasifanye kazi iwe ni siku maalum ya ibada, kuna baadhi yao wakapewa mtihani wa kujiwa na samaki wengi siku ya Sabato, wakaamua kutega nyavu usiku wa Ijumaa na kwenda kuzitoa siku ya Jumapili asubuhi, hivyo Mungu akawakasirikia na kuwageuza nyani na nguruwe. Sasa huwenda hizi tafiti ni confirmation ya kuwa hao nguruwe wana vitu vyenye kuingiliana na binadamu (maghdhubi alayhim) waliyoghadhibikiwa na Mungu kwa ukaidi wao. Sasa wale wenye kula nguruwe huenda wakawa wanakula nyama za kizazi cha wanadamu waliyogeuzwa nguruwe.
 
Back
Top Bottom