Je, Waislamu tunaitendea haki Qur'an?

Je, Waislamu tunaitendea haki Qur'an?

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
6,514
Reaction score
15,247
Hakika Mtume Muhammad (rehma na Amani ziwe juu yake) ametuachia vitu viwili ambavyo ndio Muongozo wetu Sisi Waislamu ambavyo ni Qur'an na Sunna, ndio vituongoze siku zote katika Maisha yetu.

Lakini Kwa Masikitiko makubwa kabisa hakika tumeitupa Qur'an ambao ndio msingi mama WA kuwaongoza wanadamu katika njia iliyoonyoka,tunaisoma Qur'an katika swala Tu na baada ya hapo hatuna habari nayo kabisa,je Kwa staili hii umma huu utafaidikaje na Qur'an ?

Na hata hao wachache wanaosoma pia hawayafikii malengo ya Qur'an kwasababu wanasoma pasina kujua maana yake pia. Ndugu zangu katika Imani kama ilivyokuwa makusudio ya kuletwa Mitume ili watuonye tuache mabaya na kufanya mema na kutubashiria yajayo mbele yetu ima mwisho mwema WA kuingia peponi Kwa watu wema wenye kufanya vitendo vizuri hapa duniani na mwisho mbaya Kwa watu wabaya wataingia Motoni.

Na ndo hivyo hivyo Qur'an nzima mafundisho yake kusudio lake ni kumfahamisha mwanadamu njia sahihi ya kufuata Kwa kutenda mambo mema na kumkanya kuepukana na njia mbaya ambayo itampelekea kuingia Motoni, Qur'an imeeleza ujumbe wake Kwa wanadamu kumtambua Mola wao na kumwabudu yeye Peke yake pasina kumshirikisha na chochote,pamoja na kufanya matendo yote mema anayoridhia Allah azza WA jallah na kujiepusha na makatazo yake,ni hiyo ndiyo njia sahihi itakayo mfanya mwanadamu awe salama dawamu.
Sasa wengi wetu tunaisoma Qur'an pasina mazingatio yaliyo kusudiwa,ebu tuangalie Aya moja ya Qur'an inasemaje juu ya hili;

((Na hakika tumekuteremshieni Kitabu ambacho ndani yake yamo makumbusho yenu. Je! Hamzingatii?))
21:10

Hapo tunaona kuwa Qur'an ni ukumbusho Kwa wanadamu ni ujumbe maalum ambao kusudio lake ni kumkumbusha mwanadamu juu ya dhumuni la uwepo wake duniani,je mwanadamu huyu atazingatiaje endapo hajui maana ya Hicho anachokisoma?

Tumekuwa tukihimizwa Sana kusoma Qur'an na Masheikh wetu lakini bahati mbaya Sana hatuhimizwi tusome Kwa kujua maana yake,je tutapataje ibrah au hiyo elimu ndani ya Qur'an itafahamika vipi? Matokeo yake unakuta watu wanasoma Qur'an lakini huoni Athari yoyote ambayo inapatikana katika nyoyo zao.

Ndio unakuta hao hao wasoma Qur'an ni wazinifu,wezi,wachawi,wapiga ramli na mambo kadha WA kadha ,yote hayo ni kwasababu hawasomi Qur'an Kwa mazingatio,Lau kwamba mtu akasoma Qur'an Kwa mazingatio na kujua maana yake wallah tusingekuwa na kizazi kibovu kama ambacho tunacho Leo hii.

Alhamdulillah Leo hii Misahafu ya tafsiri iko tele Mashallah je tunakwama Wapi? Na kuna kasumba ambayo naiona miongoni mwetu,tunaona Qur'an ni Ile iliyoandika Kwa lugha ya kiarabu Tu, laa tunakosea Sana. Qur'an ilishushwa Kwanza Kwa lugha ya kiarabu Kwa kuwa Mtume alikuwa muarabu na umma wake kipindi kile ulikuwa unazungumza lugha ya kiarabu,je ingekuwaje yeye ni mwarabu halafu Qur'an ije Kwa kizigua au kifaransa?

Vitabu vyote vya Mwenyezi Mungu vilishushwa Kwa Mitume kupitia ulimi WA lugha zao ili ujumbe upate kuwafikia,na baadae kutafsiriwa katika lugha mbali mbali ili uwafikie watu wote popote pale duniani,na kubwa zaidi na la kufurahisha Qur'an hata ikitafsiriwa katika lugha yoyote Ile lazima original yake iwepo pembeni ili kuzuia upotofu usitokee.

Kwahiyo ndugu zangu tunazinduana tuisome Qur'an Kwa kuielewa na kuizingatia,kwani Qur'an sio kusudio lake kukaririwa Tu na kusomwa Kwa sauti nzuri pasina kujua maana yake,na hakika asomaye Qur'an mara Kwa mara Kwa kuielewa hakika anapata mawaidha mazuri na hubadili hata mwenendo wake wa Maisha na kuwa Mcha Mungu,na hata kama atateleza kama mwanadamu lakini ni rahisi kukumbuka neno la Allah na akarejea katika mstari.

Bi Aisha (r.a) alipo ulizwa vipi kuhusu matendo/Maisha ya Mtume (s.a.w)
Alisema hakika Maisha yake ni Qur'an Kwa maana aliishi Kwa kufuata misingi ya Qur'an,je vipi Sisi umati wake? Tunaishi kama Qur'an inavyotutaka tuishi?

Leo hii nenda misikitini si rahisi kukuta Misahafu yenye tafsiri ya Qur'an, hata hao wanao nunua Misahafu na kuipeleka misikitini kama waqfu nao wanapeleka yenye lugha ya kiarabu Tu,je Kwa namna hii tutafikia kweli lengo la kusoma Qur'an ?

Tubadilike sasa tusisome Tu Qur'an Kwa kupata thawabu Bali tusome ili itutoe katika Giza na kutepeleka katika mwanga Kwa idhini yake Allah azza WA jallah

Ijumaa Mubarak!
 
Mimi kwa mtazamo wangu haya mambo ya kutafsiri tafsiri ndio yatatokea yale ya kwenye biblia utatafsiri kwa lugha ambayo haijitoshelezi kwa maneno je kipi kitatokea? Quran iachwe tu kwa lugha yake ya asili,halafu mwanadamu ni mbishi tu kwa asili kumbuka kisa cha wana wa israeli ambao walikuwa wanauona utukufu na nguvu za Mungu live kabisa kwa macho yao ila kwamakusudi kabisa walikuwa wanampinga Mungu sembuse sisi ?mimi binafsi ni mkristo kwasababu baba yangu ni mkristo ila ndugu zangu wote kwa upande wa mama yangu ni waislamu tena wamesoma sana akiwemo na mama yangu mzazi nae kasoma,sasa hebu nikupe kisa cha mjomba wangu yeye kasoma sana tena sana ila kwamakusudi kabisa ni mganga ambae anatumia aya za Quran kuwaroga watu,kuwaua nk ni mtu maarufu mno na anaogopeka sana na kwasasa ni mwenyekiti wa halmashauri moja huku kusini,huwa nakaa nae huwa ananiambia mjomba mimi naenda msikitini kama ushahidi tu ila mimi sistahili kabisa yaani nikifa moja kwa moja motoni, sasa watu wa aina hii wapo wengi mno ambao wamechagua kuyaishi maisha hayo hata kama wana elimu kubwa mno ya dini ila ni makusudi yao tu..........NB mwanamke mzuri yeyote anaeenda kwake kufuata tiba lazima amle,je mtoa mada nalo hili linahitaji mtu kama huyu aambiwe kuwa kuzini ni dhambi?
 
Sababu hii imepelekea kufeli pakubwa kwa waislamu wengi wa zama hizi za karibuni, mfano mwepesi nimepata historia ya wasanii wetu hawa wa bongo fleva wa kiislamu wamepitia madrassa tena wengine nimewashuhudia walisoma Qu'ran kwa hakika wana visomo vizuri.

Ila ukija huku kwenye miziki yao ndio wachochezi wakubwa wa Uzinzi ,Pombe na mambo ya maasi mengine dah inasikitisha sana laiti wangejua maana au kuzingatia Qur'an wasingefanya kabisa wanachofanya.

Kadhia hii ya watu kuipuuza Qu'ran imezungumzwa sana kwenye hadithi na Qu'ran yenyewe .Tena Qu'ran ni rahisi kujua maana yake hata kama mtu haelewi kiarabu anaweza kuchukua misahafu ya tafsiri na vitabu vya wanachuoni tena vipi kwa lugha mbalimbali...
tadabbur-quran-800x800.jpeg
 
Sababu hii imepelekea kufeli pakubwa kwa waislamu wengi wa zama hizi za karibuni, mfano mwepesi nimepata historia ya wasanii wetu hawa wa bongo fleva wa kiislamu wamepitia madrassa tena wengine nimewashuhudia walisoma Qu'ran kwa hakika wana visomo vizuri.

Ila ukija huku kwenye miziki yao ndio wachochezi wakubwa wa Uzinzi ,Pombe na mambo ya maasi mengine dah inasikitisha sana laiti wangejua maana au kuzingatia Qur'an wasingefanya kabisa wanachofanya.

Kadhia hii ya watu kuipuuza Qu'ran imezungumzwa sana kwenye hadithi na Qu'ran yenyewe .Tena Qu'ran ni rahisi kujua maana yake hata kama mtu haelewi kiarabu anaweza kuchukua misahafu ya tafsiri na vitabu vya wanachuoni tena vipi kwa lugha mbalimbali...View attachment 2433627
Hapo ndipo watu wanafeli wanadhani kusoma dini ndio kuishika nikuambie kitu kimoja hofu juu ya Mungu inaanzia nafsini mwako,hivi masheikh wangapi ambao wana elimu kubwa mno na wamefundisha watu ila maisha yao nyuma ya pazia ni hatari sana? Sembuse haji manara na alikiba
 
Mimi kwa mtazamo wangu haya mambo ya kutafsiri tafsiri ndio yatatokea yale ya kwenye biblia utatafsiri kwa lugha ambayo haijitoshelezi kwa maneno je kipi kitatokea? Quran iachwe tu kwa lugha yake ya asili,halafu mwanadamu ni mbishi tu kwa asili kumbuka kisa cha wana wa israeli ambao walikuwa wanauona utukufu na nguvu za Mungu live kabisa kwa macho yao ila kwamakusudi kabisa walikuwa wanampinga Mungu sembuse sisi ?mimi binafsi ni mkristo kwasababu baba yangu ni mkristo ila ndugu zangu wote kwa upande wa mama yangu ni waislamu tena wamesoma sana akiwemo na mama yangu mzazi nae kasoma,sasa hebu nikupe kisa cha mjomba wangu yeye kasoma sana tena sana ila kwamakusudi kabisa ni mganga ambae anatumia aya za Quran kuwaroga watu,kuwaua nk ni mtu maarufu mno na anaogopeka sana na kwasasa ni mwenyekiti wa halmashauri moja huku kusini,huwa nakaa nae huwa ananiambia mjomba mimi naenda msikitini kama ushahidi tu ila mimi sistahili kabisa yaani nikifa moja kwa moja motoni, sasa watu wa aina hii wapo wengi mno ambao wamechagua kuyaishi maisha hayo hata kama wana elimu kubwa mno ya dini ila ni makusudi yao tu..........NB mwanamke mzuri yeyote anaeenda kwake kufuata tiba lazima amle,je mtoa mada nalo hili linahitaji mtu kama huyu aambiwe kuwa kuzini ni dhambi?
Kutafsiri haimaanishi kwamba ile OG inatupwa au kupuuzwa kama alivyotaka Rais wa kwanza Ataturk kuwa Qu'ran isomwe kituruki na sio kiarabu hapana, bali Qu'ran Og ipo na imehifadhiwa hakuna namna yeyote ile kupotea isipokuwa atake Mwenyezi Mungu.

Msisitizo unaotakiwa watu wanatakiwa wajifunze na kiarabu chake ili wajue maana ya Aya kwa undani pamoja na kukaa katika vikao ya darasa za tafsiri na uchambuzi wake , na ikishindikana vyote kujua kiarabu chini kabisa mtu awe na misahafu yenye kiarabu na tafsiri ile hata kwa uchache apate mawili matatu na kuelewa na kumfanyia Kazi hayo ndio malengo makuu ya kuletwa Qu'ran na siyo watu wasome tu.
 
Hapo ndipo watu wanafeli wanadhani kusoma dini ndio kuishika nikuambie kitu kimoja hofu juu ya Mungu inaanzia nafsini mwako,hivi masheikh wangapi ambao wana elimu kubwa mno na wamefundisha watu ila maisha yao nyuma ya pazia ni hatari sana? Sembuse haji manara na alikiba
Mashekhe wa namna hiyo wapo kibao wengine wazinzi ,tapeli, wachawi nk hata mimi baadhi nawajua cha muhimu ubaya ni ubaya na dhambi ni dhambi haijalishi nani amefanya.

Muhimu watu kusoma misingi ya dini kwa usahihi kwani mambo mengi yaliyo katazwa kwenye vitabu yanafanyika kutokana na uchache wa elimu na mtu mwenye kuamua kufuata matamanio yake haliyakuwa elimu anayo na hoja za wazi zimembainikia..
 
Hapo ndipo watu wanafeli wanadhani kusoma dini ndio kuishika nikuambie kitu kimoja hofu juu ya Mungu inaanzia nafsini mwako,hivi masheikh wangapi ambao wana elimu kubwa mno na wamefundisha watu ila maisha yao nyuma ya pazia ni hatari sana? Sembuse haji manara na alikiba
Hao watu ndio hatari sana ,aya hiyo chini imekemea watu ambao Wana elimu lakini haiakisi matendo yao..
1bd469133d5f1022d7923d1e688c35ba(1).jpg

0f597388de3c21efb47520a24aaecea6.png
 
Ahsantee hii Quran imenitendea na inanitendea miujiza mnoo
Kwangu ni tiba tosha kwa Kila kitu
 
Kufikiri kuwa Mungu hajui lugha yako ya asili aliyokuwa kwa mawasiliano na badala yake kufanya Sala la maombi kwa lugha za kigeni linafikirisha
 
Kufikiri kuwa Mungu hajui lugha yako ya asili aliyokuwa kwa mawasiliano na badala yake kufanya Sala la maombi kwa lugha za kigeni linafikirisha
Naomba nikusaidie kitu kimoja,sio kwamba tunafikiri kuwa Mungu asikii sala Kwa lugha nyingine laa,Bali katika hiyo sala kuna matendo ambayo yanaendana na Maneno maalum ambayo yanamtakasa Mwenyezi Mungu ,hivyo ikaamuliwa yabakie hivyo ili yabakie na maana yake ya asili,Kwa mfano kuna maneno yenye kumaanisha "ametakasika Mwenyezi Mungu na machafu yote " huo ni mfano tu

Kwahiyo ni utaratibu ambao tumefundishwa na kuachiwa na Mtume wetu..

Vile vile sala ya kiislamu ni universal Kwa maana Leo muislamu akienda popote pale duniani ataswali Bila tabu yoyote kwakuwa utaratibu WA sala ni mmoja Tu,tofauti na Dini nyingine ,Leo mkristo hawezi kwenda China au ufilipino akaingia kanisani na kusali Kwa lugha zao,kwakuwa kuna tofauti kubwa ya lugha
 
U
Mimi kwa mtazamo wangu haya mambo ya kutafsiri tafsiri ndio yatatokea yale ya kwenye biblia utatafsiri kwa lugha ambayo haijitoshelezi kwa maneno je kipi kitatokea? Quran iachwe tu kwa lugha yake ya asili,halafu mwanadamu ni mbishi tu kwa asili kumbuka kisa cha wana wa israeli ambao walikuwa wanauona utukufu na nguvu za Mungu live kabisa kwa macho yao ila kwamakusudi kabisa walikuwa wanampinga Mungu sembuse sisi ?mimi binafsi ni mkristo kwasababu baba yangu ni mkristo ila ndugu zangu wote kwa upande wa mama yangu ni waislamu tena wamesoma sana akiwemo na mama yangu mzazi nae kasoma,sasa hebu nikupe kisa cha mjomba wangu yeye kasoma sana tena sana ila kwamakusudi kabisa ni mganga ambae anatumia aya za Quran kuwaroga watu,kuwaua nk ni mtu maarufu mno na anaogopeka sana na kwasasa ni mwenyekiti wa halmashauri moja huku kusini,huwa nakaa nae huwa ananiambia mjomba mimi naenda msikitini kama ushahidi tu ila mimi sistahili kabisa yaani nikifa moja kwa moja motoni, sasa watu wa aina hii wapo wengi mno ambao wamechagua kuyaishi maisha hayo hata kama wana elimu kubwa mno ya dini ila ni makusudi yao tu..........NB mwanamke mzuri yeyote anaeenda kwake kufuata tiba lazima amle,je mtoa mada nalo hili linahitaji mtu kama huyu aambiwe kuwa kuzini ni dhambi?
Kuhusu tafsir ya Qur'an haiwezi kubadilisha au kupotosha maana halisi ya Qur'an kwasababu nakala halisi IPO na itaendelea kuwepo mpaka mwisho wa dunia hii, na hapa ndipo waislamu walipofanikiwa katika kuhifadhi Qur'an ibakie vile vile Kama ilivyo.

Kuhusu Mjomba wako kutumia Qur'an kuroga watu hapo napata ukakasi kidogo kwasababu Mwenyezi Mungu amesema Qur'an ni ponyo na Tiba pia ,sasa iweje iwe INA madhara Kwa watu.

Watu wengi wakiona maandishi ya kiarabu au yanayofanana na kiarabu wanadhani ni Qur'an kitu ambacho si kweli

Kujua elimu ya Dini ni kitu kimoja na kuifuata ni kitu kingine,kwahiyo kuna watu Wana elimu nzuri ya Dini lakini Kwa ukaidi Tu wanaamua kwenda kinyume na mafundisho ya dini,hiyo ni hasara Yao na watawajibika Kwa Hilo,mfano mzuri Mjomba wako kama ulivyosema anajua kabisa anachofanya sio kizuri lakini anafanya Tu na mwisho wake anaujua kuwa utakuwaje.

Lakini Kwa ukubwa wake watu wengine wanafanya maovu Kwa kukosa elimu sahihi ya Dini,hawajui mafundisho ya dini zao,na hawa wakipata elimu sahihi ya Dini hubadilika na kuwa watu wema kabisa.

Mengi kuhusu urahisi WA tafsir ya Qur'an amezungumza tayar ndugu yangu adriz
 
Back
Top Bottom