Je, Waislamu tunaitendea haki Qur'an?

Je, Waislamu tunaitendea haki Qur'an?

[emoji29]
FB_IMG_16700613057243055.jpg
 
Mimi kwa mtazamo wangu haya mambo ya kutafsiri tafsiri ndio yatatokea yale ya kwenye biblia utatafsiri kwa lugha ambayo haijitoshelezi kwa maneno je kipi kitatokea? Quran iachwe tu kwa lugha yake ya asili,halafu mwanadamu ni mbishi tu kwa asili kumbuka kisa cha wana wa israeli ambao walikuwa wanauona utukufu na nguvu za Mungu live kabisa kwa macho yao ila kwamakusudi kabisa walikuwa wanampinga Mungu sembuse sisi ?mimi binafsi ni mkristo kwasababu baba yangu ni mkristo ila ndugu zangu wote kwa upande wa mama yangu ni waislamu tena wamesoma sana akiwemo na mama yangu mzazi nae kasoma,sasa hebu nikupe kisa cha mjomba wangu yeye kasoma sana tena sana ila kwamakusudi kabisa ni mganga ambae anatumia aya za Quran kuwaroga watu,kuwaua nk ni mtu maarufu mno na anaogopeka sana na kwasasa ni mwenyekiti wa halmashauri moja huku kusini,huwa nakaa nae huwa ananiambia mjomba mimi naenda msikitini kama ushahidi tu ila mimi sistahili kabisa yaani nikifa moja kwa moja motoni, sasa watu wa aina hii wapo wengi mno ambao wamechagua kuyaishi maisha hayo hata kama wana elimu kubwa mno ya dini ila ni makusudi yao tu..........NB mwanamke mzuri yeyote anaeenda kwake kufuata tiba lazima amle,je mtoa mada nalo hili linahitaji mtu kama huyu aambiwe kuwa kuzini ni dhambi?
Hii kali naomba namba ako mkuu
 
Hakika Mtume Muhammad (rehma na Amani ziwe juu yake) ametuachia vitu viwili ambavyo ndio Muongozo wetu Sisi Waislamu ambavyo ni Qur'an na Sunna, ndio vituongoze siku zote katika Maisha yetu.

Lakini Kwa Masikitiko makubwa kabisa hakika tumeitupa Qur'an ambao ndio msingi mama WA kuwaongoza wanadamu katika njia iliyoonyoka,tunaisoma Qur'an katika swala Tu na baada ya hapo hatuna habari nayo kabisa,je Kwa staili hii umma huu utafaidikaje na Qur'an ?

Na hata hao wachache wanaosoma pia hawayafikii malengo ya Qur'an kwasababu wanasoma pasina kujua maana yake pia. Ndugu zangu katika Imani kama ilivyokuwa makusudio ya kuletwa Mitume ili watuonye tuache mabaya na kufanya mema na kutubashiria yajayo mbele yetu ima mwisho mwema WA kuingia peponi Kwa watu wema wenye kufanya vitendo vizuri hapa duniani na mwisho mbaya Kwa watu wabaya wataingia Motoni.

Na ndo hivyo hivyo Qur'an nzima mafundisho yake kusudio lake ni kumfahamisha mwanadamu njia sahihi ya kufuata Kwa kutenda mambo mema na kumkanya kuepukana na njia mbaya ambayo itampelekea kuingia Motoni, Qur'an imeeleza ujumbe wake Kwa wanadamu kumtambua Mola wao na kumwabudu yeye Peke yake pasina kumshirikisha na chochote,pamoja na kufanya matendo yote mema anayoridhia Allah azza WA jallah na kujiepusha na makatazo yake,ni hiyo ndiyo njia sahihi itakayo mfanya mwanadamu awe salama dawamu.
Sasa wengi wetu tunaisoma Qur'an pasina mazingatio yaliyo kusudiwa,ebu tuangalie Aya moja ya Qur'an inasemaje juu ya hili;

((Na hakika tumekuteremshieni Kitabu ambacho ndani yake yamo makumbusho yenu. Je! Hamzingatii?))
21:10

Hapo tunaona kuwa Qur'an ni ukumbusho Kwa wanadamu ni ujumbe maalum ambao kusudio lake ni kumkumbusha mwanadamu juu ya dhumuni la uwepo wake duniani,je mwanadamu huyu atazingatiaje endapo hajui maana ya Hicho anachokisoma?

Tumekuwa tukihimizwa Sana kusoma Qur'an na Masheikh wetu lakini bahati mbaya Sana hatuhimizwi tusome Kwa kujua maana yake,je tutapataje ibrah au hiyo elimu ndani ya Qur'an itafahamika vipi? Matokeo yake unakuta watu wanasoma Qur'an lakini huoni Athari yoyote ambayo inapatikana katika nyoyo zao.

Ndio unakuta hao hao wasoma Qur'an ni wazinifu,wezi,wachawi,wapiga ramli na mambo kadha WA kadha ,yote hayo ni kwasababu hawasomi Qur'an Kwa mazingatio,Lau kwamba mtu akasoma Qur'an Kwa mazingatio na kujua maana yake wallah tusingekuwa na kizazi kibovu kama ambacho tunacho Leo hii.

Alhamdulillah Leo hii Misahafu ya tafsiri iko tele Mashallah je tunakwama Wapi? Na kuna kasumba ambayo naiona miongoni mwetu,tunaona Qur'an ni Ile iliyoandika Kwa lugha ya kiarabu Tu, laa tunakosea Sana. Qur'an ilishushwa Kwanza Kwa lugha ya kiarabu Kwa kuwa Mtume alikuwa muarabu na umma wake kipindi kile ulikuwa unazungumza lugha ya kiarabu,je ingekuwaje yeye ni mwarabu halafu Qur'an ije Kwa kizigua au kifaransa?

Vitabu vyote vya Mwenyezi Mungu vilishushwa Kwa Mitume kupitia ulimi WA lugha zao ili ujumbe upate kuwafikia,na baadae kutafsiriwa katika lugha mbali mbali ili uwafikie watu wote popote pale duniani,na kubwa zaidi na la kufurahisha Qur'an hata ikitafsiriwa katika lugha yoyote Ile lazima original yake iwepo pembeni ili kuzuia upotofu usitokee.

Kwahiyo ndugu zangu tunazinduana tuisome Qur'an Kwa kuielewa na kuizingatia,kwani Qur'an sio kusudio lake kukaririwa Tu na kusomwa Kwa sauti nzuri pasina kujua maana yake,na hakika asomaye Qur'an mara Kwa mara Kwa kuielewa hakika anapata mawaidha mazuri na hubadili hata mwenendo wake wa Maisha na kuwa Mcha Mungu,na hata kama atateleza kama mwanadamu lakini ni rahisi kukumbuka neno la Allah na akarejea katika mstari.

Bi Aisha (r.a) alipo ulizwa vipi kuhusu matendo/Maisha ya Mtume (s.a.w)
Alisema hakika Maisha yake ni Qur'an Kwa maana aliishi Kwa kufuata misingi ya Qur'an,je vipi Sisi umati wake? Tunaishi kama Qur'an inavyotutaka tuishi?

Leo hii nenda misikitini si rahisi kukuta Misahafu yenye tafsiri ya Qur'an, hata hao wanao nunua Misahafu na kuipeleka misikitini kama waqfu nao wanapeleka yenye lugha ya kiarabu Tu,je Kwa namna hii tutafikia kweli lengo la kusoma Qur'an ?

Tubadilike sasa tusisome Tu Qur'an Kwa kupata thawabu Bali tusome ili itutoe katika Giza na kutepeleka katika mwanga Kwa idhini yake Allah azza WA jallah

Ijumaa Mubarak!
Hicho kitabu siyo Chenu, ni cha waAsia. nyie weusi tengenezeni kitabu Chenu na nyumba zenu za ibada.
 
Naomba nikusaidie kitu kimoja,sio kwamba tunafikiri kuwa Mungu asikii sala Kwa lugha nyingine laa,Bali katika hiyo sala kuna matendo ambayo yanaendana na Maneno maalum ambayo yanamtakasa Mwenyezi Mungu ,hivyo ikaamuliwa yabakie hivyo ili yabakie na maana yake ya asili,Kwa mfano kuna maneno yenye kumaanisha "ametakasika Mwenyezi Mungu na machafu yote " huo ni mfano tu

Kwahiyo ni utaratibu ambao tumefundishwa na kuachiwa na Mtume wetu..

Vile vile sala ya kiislamu ni universal Kwa maana Leo muislamu akienda popote pale duniani ataswali Bila tabu yoyote kwakuwa utaratibu WA sala ni mmoja Tu,tofauti na Dini nyingine ,Leo mkristo hawezi kwenda China au ufilipino akaingia kanisani na kusali Kwa lugha zao,kwakuwa kuna tofauti kubwa ya lugha
ni utaratibu emu rudia. Utumwa wa fikra unatusumbua. Lugha yako inafaa sana ndo maana dua zinakwama kozi kitu kinachoombwa kila siku sio kinachotakiwa. Sio kila muislamu anajua kiarabu.

Afu kuna katabia ka kuomba dua ya pamoja hii sio nzuri maana kuna watu kiarabu kinapiga chenga shekhe akiojiombea mke wa pili we unaitikia amen ☝️😁 ni ujinga mambo ya utaratibu.
 
Chief

Naona unachanganya mafaili

Kuna Sala na Dua, ingawa Sala vile vile inamaanisha dua

Lkn Sala inafunguliwa na takbira tul ihram na kufungwa na Salaam,Sala hii ndio inatakiwa iswaliwe kutokana na utaratibu kama ambao tumeupokea toka Kwa Mtume

Ila

Dua waeza omba Kwa lugha yoyote Ile,na ni Bora zaidi kuomba Kwa lugha unayo ifahamu kwakuwa utakuwa unajua unaomba nini Kwa Allah
 
Shukhuran 🙏 Allha Akbar
 
uislamu ndo njia ya haki pasina masaka na mtume Mohammad ndo mtume wa mwisho kabisa. Chamsingi waislamu tutafute Elimu. Ila uislamu ndo dini ya haki ndo dini pekee iliyokuwepo tangia Dunia inaumbwa.
 
Mimi kwa mtazamo wangu haya mambo ya kutafsiri tafsiri ndio yatatokea yale ya kwenye biblia utatafsiri kwa lugha ambayo haijitoshelezi kwa maneno je kipi kitatokea? Quran iachwe tu kwa lugha yake ya asili,halafu mwanadamu ni mbishi tu kwa asili kumbuka kisa cha wana wa israeli ambao walikuwa wanauona utukufu na nguvu za Mungu live kabisa kwa macho yao ila kwamakusudi kabisa walikuwa wanampinga Mungu sembuse sisi ?mimi binafsi ni mkristo kwasababu baba yangu ni mkristo ila ndugu zangu wote kwa upande wa mama yangu ni waislamu tena wamesoma sana akiwemo na mama yangu mzazi nae kasoma,sasa hebu nikupe kisa cha mjomba wangu yeye kasoma sana tena sana ila kwamakusudi kabisa ni mganga ambae anatumia aya za Quran kuwaroga watu,kuwaua nk ni mtu maarufu mno na anaogopeka sana na kwasasa ni mwenyekiti wa halmashauri moja huku kusini,huwa nakaa nae huwa ananiambia mjomba mimi naenda msikitini kama ushahidi tu ila mimi sistahili kabisa yaani nikifa moja kwa moja motoni, sasa watu wa aina hii wapo wengi mno ambao wamechagua kuyaishi maisha hayo hata kama wana elimu kubwa mno ya dini ila ni makusudi yao tu..........NB mwanamke mzuri yeyote anaeenda kwake kufuata tiba lazima amle,je mtoa mada nalo hili linahitaji mtu kama huyu aambiwe kuwa kuzini ni dhambi?
Hilo ni kweli kwani naamni hata tafsiri za Kiarabu kuna mengi hayapo sawa.
 
Nenda zako huko, toka lini wewe umekuwa Muislam?
 
Mungu ni MMOJA na YESU ndilo JINA lake.

Aamen
 
Back
Top Bottom