Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Kawaida Benki Kuu Duniani huwa zinamilikiwa na Serikali za nchi husika zikiratibu sera mbalimbali za kifedha ikiwemo kudhibiti kiwango cha fedha kinachoingia kwenye mzunguko na kuzisimamia benki binafsi zilizopo kwenye nchi husika. Benki kuu huwa zina nafasi ya kipekee kuimarisha uchumi wa nchi.
Benki kuu ya Afrika Kusini ilianzishwa mwaka 1921 na kuwa benki kuu ya nne kuanzishwa nje ya bara Ulaya na ni benki yenye umri mkubwa zaidi barani Afrika. Benki hiyo inazo hisa milioni 2 huku kila mwanahisa hawezi kuzidisha umiliki wa hisa 10,000 na kwasasa benki hiyo ina wanahisa 696.
Nchi nyingine zenye benki za aina hiyo ni Ubelgiji, Ugiriki, Italia, Japan, Switzerland, Uturuki na Marekani.
Mwaka 2017 chama tawala cha ANC kiliazimia kutaifisha benki hiyo, azimio ambalo utekelezaji wake umekwama hadi sasa.
Rais wa sasa wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa akiwa kwenye kongamano la sera siku tatu zilizopita amethibisha kuendelea kwa azimio hilo huku wajumbe wakitaka utekelezaji wa kasi ikizingatia gharama kwa hazina ya Taifa hilo ambayo tayari imetumika.