Je Wajua Iran unaweza kuuza viungo vyako vya miili?

Je Wajua Iran unaweza kuuza viungo vyako vya miili?

Nilikua na mpango nimcheki ayatollah ili tuyajenge,
Ila nimekaa nikawaza waarabu walivyo wabaguzi wa rangi, watazitaka kweli figo zangu nyeusi hizi?
 
😃 😀 😄 😁 🤣 😂 😃 😀 wewe ndio huelewi. Yaani bei ya serikali ni dola 1300. Now fikirisha akili zako kidogo tu, achana na ngumalu yangu. Nchi ambayo wananchi wake wana uchumi mzuri, toa Iran weka nchi nyingine ya Kiarabu, yeyote tu unayo ijua wewe, halafu wananchi wake kama wanaweza kukubali kutoa figo kwa bei elekezi. Taja nchi moja tu. Hiyo bei elekezi (achana na hizo za back market ) na watu wanatoa, tafsiri yake ni 2 tu, is either Wairan wana huruma sana or ni mafukara mno, wanaona better kuuza kiungo kwa bei ya Tsh 3M. Bongo hapa, utawapata wachache mno
Kwani bongo damu mnauza sh ngap?

Hiyo Dola 1300 ni pesa ambayo serikali inatoka kama Asante yake ni kama vile wewe unavyopewa soda ukienda kujitolea damu. Lakin unaweza kukutana na mtu mwenye uhitaj wa dam mkakubaliana MALIPO
 
Daa, we jamaa; unafananisha damu na figo? Damu si inajitengeneza yenyewe kwa kutumia chakula unacho kula? Hili nalo la kuweka mjadara? Figo unatakiwa ufanye nini ili irudi nyingine baada ya ku donate? 💖 Interesting. Sitajibu tena naishia hapa.
 
Kwahyo we unataka wauze shingap ndo ujue matajiri? Na ukisema maskini unawafananisha na wakina Nan? Maana sizan kama Kuna nchi Africa hata Moja inaifikia Iran Kwa uchumi mkubwa na Pato la mtu Mmoja Mmoja
 
Iran si nchi maskini kwa viwango vya kimataifa, lakini inakabiliwa na changamoto kubwa za kiuchumi kutokana na vikwazo vya kimataifa, usimamizi mbaya wa uchumi, na mfumuko wa bei. Hali hii imeathiri maendeleo yake ya kiuchumi na ustawi wa wananchi.

📊 Takwimu za Kiuchumi za Iran (2024)

- Pato la Taifa (GDP) la Iran: Takriban dola za Kimarekani bilioni 434.24 [1] .

- Pato la Taifa kwa Mtu (GDP per capita): Dola za Kimarekani 5,013 [1] .

- Pato la Taifa kwa Mtu kwa PPP: Dola za Kimarekani 19,607 [1] .

🌍 Ulinganisho na Afrika

- Pato la Taifa la Afrika (2025): Takriban dola za Kimarekani trilioni 2.82 [2] .

- Pato la Taifa kwa Mtu Afrika (2025): Dola za Kimarekani 1,927 [2] .

- Nchi ya Afrika yenye GDP ya juu zaidi: Afrika Kusini, ikiwa na GDP ya dola za Kimarekani bilioni 403.05 [2] .

🔍 Ulinganisho wa Moja kwa Moja

- Iran vs Afrika Kusini: Iran ina GDP ya juu kidogo kuliko Afrika Kusini, lakini tofauti si kubwa sana.

- Iran vs Afrika nzima: GDP ya Iran ni chini sana ikilinganishwa na jumla ya GDP ya Afrika, ambayo ni zaidi ya mara sita ya Iran.

- GDP per capita: Iran ina GDP per capita ya dola 5,013, ambayo ni zaidi ya mara mbili ya wastani wa Afrika wa dola 1,927.

📉 Changamoto za Kiuchumi za Iran
Licha ya takwimu hizi, Iran inakabiliwa na matatizo makubwa ya kiuchumi:

- Mfumuko wa bei: Bei za bidhaa zimepanda sana, na kusababisha ugumu kwa wananchi kumudu maisha.

- Ukosefu wa ajira: Viwango vya ukosefu wa ajira vimeongezeka, hasa miongoni mwa vijana.

- Vikwazo vya kimataifa: Vikwazo vya kiuchumi kutoka nchi za Magharibi vimeathiri biashara na uwekezaji.
Hitimisho

Iran si nchi maskini kabisa, lakini inakabiliwa na changamoto kubwa za kiuchumi zinazopunguza ustawi wa wananchi wake. Ikilinganishwa na nchi nyingi za Afrika, Iran ina GDP na GDP per capita ya juu zaidi, lakini changamoto za ndani zinaathiri maendeleo yake.
 
Hapana, Israel si nchi maskini. Ni taifa lenye uchumi wa juu linaloainishwa kama "uchumi wa hali ya juu" na Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD). Licha ya changamoto za kiusalama na migogoro ya kijeshi, Israel inaendelea kuwa na uchumi thabiti unaoongozwa na sekta ya teknolojia ya juu na huduma.

📊 Takwimu za Uchumi wa Israel (2024–2025)

- Pato la Taifa (GDP) la Israel (2024): Takriban dola za Kimarekani bilioni 517. [1]

- Pato la Taifa (GDP) la Israel (2025): Inakadiriwa kufikia dola za Kimarekani bilioni 531.2. [1]

- Pato la Taifa kwa Mtu (GDP per capita) (2025): Dola za Kimarekani 57,379. [2]

- Pato la Taifa kwa Mtu kwa PPP (2025): Dola za Kimarekani 55,850. [2]

🌍 Ulinganisho na Afrika

- Pato la Taifa la Afrika (2025): Takriban dola za Kimarekani trilioni 2.82. [2]

- Pato la Taifa kwa Mtu Afrika (2025): Dola za Kimarekani 1,927. [2]

- Nchi ya Afrika yenye GDP ya juu zaidi: Afrika Kusini, ikiwa na GDP ya dola za Kimarekani bilioni 403.05. [2]

🔍 Ulinganisho wa Moja kwa Moja

- Israel vs Afrika Kusini: Israel ina GDP ya juu zaidi kuliko Afrika Kusini.

- Israel vs Afrika nzima: GDP ya Israel ni ndogo ikilinganishwa na jumla ya GDP ya Afrika, ambayo ni zaidi ya mara tano ya Israel.
: - GDP per capita: Israel ina GDP per capita ya dola 57,379, ambayo ni zaidi ya mara 29 ya wastani wa Afrika wa dola 1,927.

📉 Changamoto za Kiuchumi za Israel

Licha ya mafanikio haya ya kiuchumi, Israel inakabiliwa na changamoto kadhaa:

- Migogoro ya Kijeshi: Migogoro inayoendelea katika Ukanda wa Gaza na maeneo mengine imeathiri uchumi, ikisababisha kupungua kwa uwekezaji na matumizi ya walaji. [3]

- Mfumuko wa Bei: Inflation imeongezeka hadi 3.8% mnamo Januari 2025, ikichochewa na ongezeko la kodi na gharama za vita. [4]

- Gharama za Kijeshi: Matumizi ya kijeshi yameongezeka sana, kutoka dola bilioni 1.8 hadi 4.7 kwa mwezi, na kufikia jumla ya dola bilioni 27.5 mwaka uliopita. [5]

- Upungufu wa Wafanyakazi: Kusimamishwa kwa vibali vya kazi kwa Wapalestina kumesababisha upungufu wa wafanyakazi, hasa katika sekta ya ujenzi. [6]

✅ Hitimisho

Israel ni nchi yenye uchumi wa juu na maendeleo makubwa katika sekta ya teknolojia na huduma. Hata hivyo, changamoto za kiusalama na migogoro ya kijeshi zinaathiri ukuaji wake wa kiuchumi. Ikilinganishwa na nchi za Afrika, Israel ina GDP na GDP per capita ya juu zaidi, lakini changamoto za ndani zinaweza kuathiri maendeleo yake ya baadaye.
 
Hii taarifa umeiuliza huko chatGPT, Nimeona ulivyohitimisha hapo chini kwa mtindo wa swali
 
Serikali ya Iran sio ya kiislamu ni serikali inayoongozwa kishia, na ushia umeelekea kwenye uyahudi zaidi ni dini tofauti na uislamu.
Mkuu Shia ni dhehebu la kiislam
Linatumia Quran wanayotumia Sunni
Ushia haufanani kwa namna yoyote ile na Uyahudi

Tofauti ya Ushia na Usuni ni HADITHI tu ambazo kiasi kikubwa tofauti zao zilianzia baada ya Mwamedi kufa, kwamba ni nani alikua mrithi wa mikoba ya Mwamedi

I stand to be corrected
 
Turudi kwenye msingi wa HOJA yetu. Iran inakuzwa sana, kama figo raia wanauza kwa dola 1300 kiasi ambacho siamini kama kuna nchi nyingine ya Kiarabu raia wake wanaweza kufanya hivo; Iran ni masikini sana. Dola 1300 ni Tsh 3.25M. Hawa na Waafrica tu walio changamka. Same as North Korea; uwekezaji mwingi unafanywa kwenye security and intelligence badala ya mambo ya maendeleo kama viwanda, biashara na uwekezaji wenye tija.
Iran sio nchi ya kiarabu; na sio nchi masikini kama TZ; HDi yake very high, literacy rate very high na miundombinu very high na watu very educated. Sanctions ndo zimecripple uchumi ila miundombinu sio km ya TZ au nchi za Africa usijidanganye
 
mimi naona wale wanaofariki au kupata ajali wakafa viungo vyao ndo.vingeuzwa na watu wao wa karibu
 
Iran sio nchi ya kiarabu; na sio nchi masikini kama TZ; HDi yake very high, literacy rate very high na miundombinu very high na watu very educated. Sanctions ndo zimecripple uchumi ila miundombinu sio km ya TZ au nchi za Africa usijidanganye
Wewe umejadiri nchi, mimi nimejadiri financial capacity ya raia; wewe pia umejadiri chanzo cha UKATA wao (sanctions ) mimi sikutaka kwenda huko, kuhusu miundombinu, elimu nk hivo wala sio jambo lisilojulikana, wamewahi kununua ndege za Boeing kwa cash kama ndege 50 hivi at once, while pia kuna Airbus kibao from either France or USA, yote hayo ni serikali. Nazungumzia kipato cha mtu mmoja mmoja. Bro, hakuna nchi nyingine pale mashariki ya kati yenye inaweza kuruhusu mtu wake auze figo yake kwa dola 1300/= bongo tu yenyewe I doubt, unless awe ndugu yako ambaye of course unaweza hata kutoa bure, lakini sio Mnyakyusa wa Mbeya auze figo kwa Mgido wa Tanga kwa Tsh 3M; kataa ukubali, hili linafikirisha
 
Serikali ya Iran sio ya kiislamu ni serikali inayoongozwa kishia, na ushia umeelekea kwenye uyahudi zaidi ni dini tofauti na uislamu.
Muasisi wa shia ni Aliy ibn Abitwalib na mwanae husain mtoto wa fatma bint Muhamad unasaje sio uislam ni uyahudi?
 
Mbona hilo liko wazi mashia wana swala zao tofauti na zetu, na shahada na adhana kila kitu ni tofauti kubwa zaidi itikadi yetu na wao ni tofauti kabisa.
Wanaswali swala 5,wanafunga ramadhan, wanahiji makka,dini za kiyahudi hamna hii
 
Wewe umejadiri nchi, mimi nimejadiri financial capacity ya raia; wewe pia umejadiri chanzo cha UKATA wao (sanctions ) mimi sikutaka kwenda huko, kuhusu miundombinu, elimu nk hivo wala sio jambo lisilojulikana, wamewahi kununua ndege za Boeing kwa cash kama ndege 50 hivi at once, while pia kuna Airbus kibao from either France or USA, yote hayo ni serikali. Nazungumzia kipato cha mtu mmoja mmoja. Bro, hakuna nchi nyingine pale mashariki ya kati yenye inaweza kuruhusu mtu wake auze figo yake kwa dola 1300/= bongo tu yenyewe I doubt, unless awe ndugu yako ambaye of course unaweza hata kutoa bure, lakini sio Mnyakyusa wa Mbeya auze figo kwa Mgido wa Tanga kwa Tsh 3M; kataa ukubali, hili linafikirisha
Kipato Cha mtu mmoja mmoja Irani ni kidogo kulinganisha na kina nan
 
Kipato Cha mtu mmoja mmoja Irani ni kidogo kulinganisha na kina nan
Soma nyuzi zangu za nyuma huko, wewe hukawii kutukana as if mimi na wewe tuna interest na Iran.
Nimesema several times huko ju, linganisha vipato vya raia wa Iran na nchi zingine za Kiarabu pale Middle east. Weka Saudia, Kuwait, Qatar, Israel etc. Siwataji Jordan na Lebanon cause sijawahi kuwasikia kwenye biashara ya mafuta, not sure kama wanayo
 
Duh sawa niishie hapa upeo wako mdogo Sana, kwanza hao sio waarabu pia wanauza mafuta na ndo tegemeo lao tatu vikwazo ndo vnawakwamisha, NNE hyo hela ni Bei ya serikali kukupa ww unaetoa Figo kama posho lkn jua Figo n biashara ya WATU wawili mwnye uhitaji na muuzaji hvo uko serikali haingillii, Tano ungekua mtu wa kujiongeza na upeo mkubwa ungetambua kuwa hata maskini wa uku bongo hawezi uza Figo Kwa milioni 3 itawezekanaje Kwa waajemi hivo kwasabab hivo zote inaonesha ww n mtu usie na uwezo mkubwa wa kuchakata taarifa na upendi kuelekezwa pia
 
Back
Top Bottom