Je, wajua kuwa hatma ya CHADEMA ipo mikononi kwa Lwakatare? Baada ya CHADEMA kumwaga ugali, Lwaka akiamua kumwaga mboga, CHADEMA kwishney!

pascal kabla jogoo hajawika bwana mkubwa atakuwa ameshasoma hili bandiko...(labda asilisome)

na amin amin nakuambia utapewa unachokitamani;

sio kwa hii alikasusu uliyoikoroga!
 
Serikali na Chama wameshindwa, Lwakatale ataweza? How? Huna namna nyingine ya kutafuta ukubalike machoni kwa Bwana?
CHADEMA wanapata umaarufu na nguvu kwa sababu Wananchi wengi wapo nyuma yao. Kiu ya Mabadiliko iliyopo Tanzania, ndio mtaji wa CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani. Leo CCM hata tukisema tuifute CHADEMA kwenye uso wa siasa za Tanzania, kitazaliwa Chama kingine chenye nguvu zaidi ya CHADEMA na CCM.
Kuondoa upinzani Tanzania ni Sawa na kusema unawaondoa Watanzania wasiwepo Tanzania.
Chama kinachoishi kwa kutegemea nguvu ya Umma, hakiwezi kuondolewa kwa hila na vitisho vya dola ama mtu mmoja mmoja.. ilikuwa hivyo hata wakati wa harakati za Mwalimu na TANU yake.
Njia rahisi ya kukabiliana na Upinzani wa Tanzania sio kuua vyama, sio kubambikia watu kesi, sio kuzuia shughuli za kisiasa, sio kuwabana wanahabari, sio kuwanunua wanasiasa...Bali ni kuwapa watumishi stahiki zao sahihi. Kuwapa wakulima masoko ya mazao yao kwa uhakika. Kuwapa wanafunzi mikopo isiyo na ubaguzi. Kuondoa Sheria kandamizi kwa Umma. Kuwapa Watanzania fursa ya kuwaona wawakilishi wao wakifanya kazi za uwakilishi kwa uwazi, uhuru na mshikamano wa vyama vyote. Serikali kutekeleza miradi inayopendekezwa na kukubaliwa na Wananchi kupitia Bunge na sio Watawala. Kuua upinzani ni kuhakikisha Umeme, Maji, huduma za Afya, Elimu vinakuwa ni mahitaji ya lazima kupelekwa kwa Watanzania sio kusubiri fadhira za Watawala. Kuua upinzani ni kuhakikisha wanaoongoza Nchi wanatenda kwa mujibu wa matakwa ya Katiba na Sheria na sio mawazo ya Watawala... Tofauti na hayo, sio Dola wala Lwakatale wanaoweza kuwa mwiba wa wapinzani.
Unaweza kufanikisha yote hayo lkn upinzani ukaishi na kuendelea kuwa na nguvu.. Hii ni kwa sababu ni vigumu wote kuwa na mawazo na fikra mfanano.. Siku ikitokea wote tukawaza sawa, bila shaka Taifa litakuwa kituko. Haiwezekani. Tujifunze kuishi na Upinzani. Wakoloni weupe wameweza, wakoloni weusi mtashindwa vipi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Paskali meko pamoja na kuipa cdm kesi za kitoto kaishindwa,sembuse huyo mjinga mwenye kisukari sugu.
Aendelee kula senene tu cdm ni kubwa kuliko mlangira huyo.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukweli mchungu lazima huyo mpiga debe wa ccm,atapike supu ya mapupu,alipigwa pini na bunge kabaki kua vuvuzela na kijakazi wa meko humu jf

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu umeandika vizuri sana,Japokuwa kwa upande wangu nilivyoelewa ni kuwa Chadema kilitakiwa kifutwe na Msajili kwa sababu ya ile video yao,lakini aliyekinusuru Chama kisifutwe alikuwa Lwakatare ambaye huenda kuna ukweli aliuficha wakati ule ili kukilinda Chama kisifutwe. Atakapoamua kuuanika ukweli huo (kama upo) ndiyo Paskal akasema Chadema itakuwa kwishney,kwamba itafutiliwa mbali.
 
Trust me hakuna kitu kama hicho, tukianza kuonyeshana video mbona kuna watu wataomba dunia ipasuke?
 
Unachekesha kweli,,hiyo mboga mnayozungumzia kama ina sura ya jinai maana yake ni kwamba inamhusu yeye moja kwa moja.Kwahiyo akimwaga mboga kama mnavyosema yeye ndo mhanga nambari mmoja,,ni sawasawa na mtu kukata tawi ulilokalia,je inawezekana?
Kumbuka mahakama zetu haziko kihaki asilimia mia, anaweza kujitoa mhanga na akaahidiwa baadhi ya mambo ila athari itakuwa kubwa zaidi kwa Chama kama taasisi kuliko yeye mtu binafsi
 
*ANASIMULIA WILFRED LWAKATARE*

******************

#Hivi nyie mnafikiri madongo mnayonipiga mnakuwa mnanipulizia perfume? (La hasha). Mkiruhusu midomo yenu kuninyea mimi nitaarisha kabisa.

#Wengi wenu hamnijui, ulizeni wanaonijua. Nimekulia Kariakoo nikasoma Tambaza, jeshini nikaenda Ruvu kwa mwaka mmoja. Chuo Kikuu niliskma UDSM ambako huko maandamano na migomo ilikuwa kifungua kinywa nilichoshiriki kukiandaa.

#Ulizeni mzee "punch" alikuwa anakaa wapi, nikaajiriwa TUMETAA Lumumba kisha nikahamishiwa Iringa DC, baadaye Bukoba MC, tena Urambo Dc kisha nikarejeshwa Bukoba MC. Manispaa kote huko nikiwa kama Afisa utumishi mkuu (nikipata na marupurupu kibao)

#Nimepiga muziki kama DJ (Coffee Tree Inn Hotel) Nikajiuzulu kazi kwa notice ya masaa 24 kwa kuilipa serikali mishahara ya miezi mitatu.

#Niliingia CUF nikawa Naibu Katibu mkuu, nikawa mbunge,nikawa KUB. Nikiwa KUB nilimteua Mbowe kuwa waziri kivuli wangu wa wizara ya Biashara na viwanda, Dr. Wilibroad Slaa akiwa kama waziri wangu wa katiba na sheria na marehemu Ndesambulo akiwa waziri wangu maliasili na utalii na wengineo.

#Baadaye Cuf (maalim Seif na "walinizingua", nikajiuzuli nafasi zote ndani ya Chama. Nikakaa kwangu kijijini Kibeta kwa miezi mitatu huku vyama mbalimbali vikininyatia kunisajili, mwishowe tenda ya rafiki yangu Mbowe ikashinda japo sehemu kubwa ya ushawishi alioutoa kwangu haujawa kweli hadi leo hata yeye anafahamu, lakini akanishawishi kugombea nafasi ya kuwa KUB kumwondoa mbabe Dr Wallid Kabouru ( ambaye pia alikuwa katibu mkuu wa CDM, Mbowe akawa kampeini meneja na mpanga mikakati mkuu wa kumwondoa Kabouru) na kama amesahau naweza kumkumbusha..

#Mbowe kwa kunijua makali yangu nikiwa CUF hasa mambo ya kiulinzi na ki Intelligensia akaniomba kushikilia Kurugenzi ya Ulinzi na Usalama, yeye akiwa Mkt wa kamati ya ulinzi na usalama mimi nikiwa katibu wa kamati. Tukapanga mambo yakapangika, nikatengeneza miundo ya kiulinzi na programme mbalimbali ( ikiwemo ile iliyofahamika kama FTP 200) iliyoperekea kusajili vijana 97453 wa kukihami na kukitetea *chama na maslahi yake.*

# Matunda ya kazi yetu ilionekana bayana kwa kila mwana Chadema; CDM ikaheshimika,/ikaogopwa na wanachadema wakawa hawatishwi. Tukawa sehemu ya kusaidia Chama kushinda chaguzi mbalimbali au kutoshindwa kwa kura za haibu. RED BRIGADE ikawa chombo muhimu cha kukilinda na kukijenga chama. Tishio lake likaperekea mimi kukamatwa na vyombo vya dola na kufunguliwa kesi ya kwanza nchini tangu tupate uhuru KESI YA UGAIDI, nikawekwa gerezani Keko na baadaye Segerea kwa siku 118 na za Kituo kikuu cha polisi Dsm (kulala sakafuni) siku 9, kesi ikaendeshwa, Mh Zitto akiwa naibu katibu Mkuu CDM akawasilisha barua kwa katibu mkuu Dr Slaa akipinga chama(CDM) kutumia hata sh 100 kwenye kesi hiyo akidai hiyo kesi ni mambo yangu binafsi -- Eti CDM sio chama cha ugaidi.

#Mbowe akalisimamia swala la kesi yangu kwa nguvu zake zote kusimamiwa na chama. Nikawekewa mawakili shupavu; Lissu, Marando, prof Safari, Kibatara, Nyoronyo, n,k kunitetea. Wakafanikisha kufutwa kwa vifungu vyote vilivyokuwa vikinituhumu kuwa mimi ni Gaidi, nikabakiwa na kesi moja ya Kisutu inayodhaminika, nikadhaminiwa. Kesi zote zikakatiwa rufaa ili niendelee kukaa Segerea mpaka rufaa zisikilizwe. Mahakama ikanipa haki ya kukaa nje. Baada ya kutoka na kesi kuendelea kusikilizwa mawakili niliowekewa na Chama wakajitoa kwa mfumo wa chama kuwalipa kuharibika. Nikaanza kuiendesha kesi kwa nguvu zangu chini ya mawakili wasomi Rweyongeza na wakili msomi Dr Julius Lugazia mpaka kesi zote zilipoisha baada ya miaka minne. Chama kilipata matokeo kupitia magazetini na baadhi ya wanachama kushangaa kwa kutojua wala kujulishwa kama hizo kesi zilikuwa zikiendelea.(hii sio hadithi ni movie ya tukio halisi.)

#kwa leo yaweza kuwa chapter I ya utumishi wangu na matukio dhidi yangu ndani ya mageuzi tangu 1991 hadi juzi tarehe 14 lilipotolewa tamko la mimi Wilfred Muganyizi Lwakatare kufutiwa uanachama na KAMATI KUU ya CDM.

#Ukweli maamuzi hayo yameniacha na taharuki kubwa, mawazo na msongo wa mawazo. Uamuzi umenichinjia baharini bila kunipa haki yangu kikatiba ya kujieleza/kujitetea. Kazi niliyoifanya kwa moyo wangu wote, kazi niliyoruka vihunzi kibao vya hatari, kazi niliyoiingia kwa utashi wangu mwenyewe na kuacha kazi iliyokuwa ikinilipa vizuri na marupurupu tele, kazi niliyokuwa nikiifanya kwa kujitolea zaidi kuliko malipo.

#Yaani Mbowe amewaridhisha wajumbe kwa mtu kama mimi mwenye historia niliyoieleza kuchinjwa bila kusikilizwa?

# Hata Saddam alipewa nafasi ya kujitetea japo naamini ni kama walikuwa wanaigiza. Mbowe na wajumbe wake kweli hawakutanguliza roho na fikra zenye busara, hekima, utu, uzalendo na huruma kwa mtu aliyekwisha tangaza tena kwa kutoa taarifa ya kutogombea miaka mitatu iliyopita kuanzia ngazi ya msingi pale kwetu kibeta kwenye msingi wangu wa Omukituli, kisha kata, Wilaya, mkoa, kanda,Taifa na hata Bungeni,. Yaani nikiwa nimebakiza siku zisizozidi wiki tatu nipate "kahela" kangu ka kumaliza kazi ya utume niliyotumikia na kutumika kipindi chote cha kazi za kisiasa!

#Ukweli maamuzi hayo ya kuingia bungeni na kuupinga uamuzi wa Kamati kuu ya kutokwenda niliyafanya nikiwa na akili kamili, nikiwa na fikra kamilifu, bila shinikizo na wala bila kujutia maamuzi ambayo chama kingeliyafanya.

#Hayo maamuzi yalikuwa ya kuniweka kwenye majaribu, na mimi kwa principle zangu kuna mambo ambayo huwa siruhusu nijaribiwe ambayo kamwe ni kama haya.

#Najiheshimu, nawaheshimu waliokuwa viongozi wangu lakini siko tayari kufanyiwa tendo walilofanyiwa waumini wa Kibwetere huko Uganda ya kuwateketeza wauumini wote kwa petrol wakiwa wamefungiwa na kufuli ili wakauone vizuri ufalme wa mbinguni walioahidiwa na Kibwetere. Kibwetere hadi leo anatafutwa na vyombo vyote vya dola nchini Uganda ili atiwe nguvuni lakini hajapatikana hadi leo.

#Niliyoyaeleza ni Chapter ya kwanza, bado zipo chapter zaidi ya arobaini endapo kutatokea huitaji kutokea kwenu wafuatiliaji wa sakata hili. Kwa wenye vyombo vyao vya habari wako huru kunitembelea kwangu au kuniita popote mkizingatia kuwa mimi ni mtu huru nisiye na chama chochote ( BALI "MBUNGE ANAYETOKANA NA VITI VYA MH SPIKA) Linavyotokana na rungu lake lililoko mezani kwake BUNGENI) ili kuendeleza TAMTHILIA yetu. MBARIKIWE NA BWANA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpaka uka tabiri could be magufuli , embu ngoja tuweke na hii kuwa MBOGA ZITAMWAGIKA , (IKIWEMO NA WALE WALIYOMSHAMBULIA LISSU AMBAO WAMO HUMO HUMO CHADEMA )
 

Mkuu uko sahihi sana, ila cdm sio kikundi cha kigaidi useme kuna siri za kutisha. Ni kweli huenda kuna uhuni wa hapa na pale, lakini sio siri kwa maana ya siri zaidi ya siasa na propaganda mfu. Hakuna lolote jipya atalitoa huyo Lwakatare useme eti ndio litapoteza imani ya wale wanaoiamini cdm. Ni jambo gani halijafanywa na dola dhidi ya cdm mpaka uone eti huyo Lwakatare ndio ameficha hizo siri? Hizo siri hata Lwakatare na yoyote waziweke hadharani, bado ccm hawatakuwa radhi kukubali tume huru ya uchaguzi, maana wanajua watu wengi wana upande tayari bila kujali hizo siri za Lakwatare.

Hebu fanyeni juu chini huyo Lwakatare amwage siri zote kisha cdm ifutwe uone kama hao wanapokubali cdm wataiunga mkono ccm. Hiyo dunia za vitisho sijui siri ilikuwa na nguvu enzi za NCCR ya kina Mrema watu wakiwa wamelala sio sasa.
 
Kama Mbowe anajua imekuwaje kakubali afukuzwe?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao wabunge walioondoka ni wangapi? Hebu wataje hapa tujue idadi yao na sio porojo tu.
Kama CDM imekufa,mbona mnahangaika nayo kila siku? Hata press ya chadema tu inawatisha
Nani ajitafakari: #CHADEMA AU Wabunge wake?
.
.
Mei 1 2020, #Chadema waliweka hadharani barua ya Mwenyekiti wao Freeman Mbowe kuwataka wabunge wa #Chadema kutohudhuria vikao vya Bunge. Lakini hadi Mbowe atoe maelekezo hayo hadi leo, wabunge 20 wa Chadema wamekwenda Bungeni. Wabunge hao ni: .
1.Mh Latifah Chande
2.Mh David Silinde
3.Mh Peter Lijulikali
4.Mh Mariam Msabaha
5.Mh Joyce Sokombi
6.Mh Jafari Michael
7.Mh. Susaane Maselle
8.Mh Mganyizi Lwakatare
9.Mh Anthony Komu
10.Mh Joseph Selasini
11.Mh William Qambalo
12.Mh Cecilia Paresso
13.Mh Sware Semesi
14.Mh Susan Lyimo
15.Mh Lucia Mlowe
16.Mh Saed Kubenea
17.Mh Anna Gideria
18.Mh Rose Kamili
19.Mh Lucy Magereli
20.Mh Salome Makamba
.
.
Unadhani nani anapaswa kujitafakari : Wabunge hao kwa kukiuka amri ya mwenyekiti Mbowe na #Chadema, au Mwenyekiti Mbowe anapaswa kujitafakari kwa kitendo cha wabunge hao (Wanachama wa chama anachoongoza) kukiuka maelekezo yake?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chadema ile ya 2015 kabla ya kuondoka Dr Slaa unaweza kuifananisha na hii ya 2020 au unaandika kwa ubishi tu?

Huwezi kufananisha kisa mazingira ya wakati huo ni tofauti na sasa. Huenda umetekwa na hizi propaganda mfu na uonevu wa kisiasa wanaofanyiwa cdm, ila ukweli tunaujua vizurina wananchi tuliowengi tulishaamka miaka kibao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…