*ANASIMULIA WILFRED LWAKATARE*
******************
#Hivi nyie mnafikiri madongo mnayonipiga mnakuwa mnanipulizia perfume? (La hasha). Mkiruhusu midomo yenu kuninyea mimi nitaarisha kabisa.
#Wengi wenu hamnijui, ulizeni wanaonijua. Nimekulia Kariakoo nikasoma Tambaza, jeshini nikaenda Ruvu kwa mwaka mmoja. Chuo Kikuu niliskma UDSM ambako huko maandamano na migomo ilikuwa kifungua kinywa nilichoshiriki kukiandaa.
#Ulizeni mzee "punch" alikuwa anakaa wapi, nikaajiriwa TUMETAA Lumumba kisha nikahamishiwa Iringa DC, baadaye Bukoba MC, tena Urambo Dc kisha nikarejeshwa Bukoba MC. Manispaa kote huko nikiwa kama Afisa utumishi mkuu (nikipata na marupurupu kibao)
#Nimepiga muziki kama DJ (Coffee Tree Inn Hotel) Nikajiuzulu kazi kwa notice ya masaa 24 kwa kuilipa serikali mishahara ya miezi mitatu.
#Niliingia CUF nikawa Naibu Katibu mkuu, nikawa mbunge,nikawa KUB. Nikiwa KUB nilimteua Mbowe kuwa waziri kivuli wangu wa wizara ya Biashara na viwanda, Dr. Wilibroad Slaa akiwa kama waziri wangu wa katiba na sheria na marehemu Ndesambulo akiwa waziri wangu maliasili na utalii na wengineo.
#Baadaye Cuf (maalim Seif na "walinizingua", nikajiuzuli nafasi zote ndani ya Chama. Nikakaa kwangu kijijini Kibeta kwa miezi mitatu huku vyama mbalimbali vikininyatia kunisajili, mwishowe tenda ya rafiki yangu Mbowe ikashinda japo sehemu kubwa ya ushawishi alioutoa kwangu haujawa kweli hadi leo hata yeye anafahamu, lakini akanishawishi kugombea nafasi ya kuwa KUB kumwondoa mbabe Dr Wallid Kabouru ( ambaye pia alikuwa katibu mkuu wa CDM, Mbowe akawa kampeini meneja na mpanga mikakati mkuu wa kumwondoa Kabouru) na kama amesahau naweza kumkumbusha..
#Mbowe kwa kunijua makali yangu nikiwa CUF hasa mambo ya kiulinzi na ki Intelligensia akaniomba kushikilia Kurugenzi ya Ulinzi na Usalama, yeye akiwa Mkt wa kamati ya ulinzi na usalama mimi nikiwa katibu wa kamati. Tukapanga mambo yakapangika, nikatengeneza miundo ya kiulinzi na programme mbalimbali ( ikiwemo ile iliyofahamika kama FTP 200) iliyoperekea kusajili vijana 97453 wa kukihami na kukitetea *chama na maslahi yake.*
# Matunda ya kazi yetu ilionekana bayana kwa kila mwana Chadema; CDM ikaheshimika,/ikaogopwa na wanachadema wakawa hawatishwi. Tukawa sehemu ya kusaidia Chama kushinda chaguzi mbalimbali au kutoshindwa kwa kura za haibu. RED BRIGADE ikawa chombo muhimu cha kukilinda na kukijenga chama. Tishio lake likaperekea mimi kukamatwa na vyombo vya dola na kufunguliwa kesi ya kwanza nchini tangu tupate uhuru KESI YA UGAIDI, nikawekwa gerezani Keko na baadaye Segerea kwa siku 118 na za Kituo kikuu cha polisi Dsm (kulala sakafuni) siku 9, kesi ikaendeshwa, Mh Zitto akiwa naibu katibu Mkuu CDM akawasilisha barua kwa katibu mkuu Dr Slaa akipinga chama(CDM) kutumia hata sh 100 kwenye kesi hiyo akidai hiyo kesi ni mambo yangu binafsi -- Eti CDM sio chama cha ugaidi.
#Mbowe akalisimamia swala la kesi yangu kwa nguvu zake zote kusimamiwa na chama. Nikawekewa mawakili shupavu; Lissu, Marando, prof Safari, Kibatara, Nyoronyo, n,k kunitetea. Wakafanikisha kufutwa kwa vifungu vyote vilivyokuwa vikinituhumu kuwa mimi ni Gaidi, nikabakiwa na kesi moja ya Kisutu inayodhaminika, nikadhaminiwa. Kesi zote zikakatiwa rufaa ili niendelee kukaa Segerea mpaka rufaa zisikilizwe. Mahakama ikanipa haki ya kukaa nje. Baada ya kutoka na kesi kuendelea kusikilizwa mawakili niliowekewa na Chama wakajitoa kwa mfumo wa chama kuwalipa kuharibika. Nikaanza kuiendesha kesi kwa nguvu zangu chini ya mawakili wasomi Rweyongeza na wakili msomi Dr Julius Lugazia mpaka kesi zote zilipoisha baada ya miaka minne. Chama kilipata matokeo kupitia magazetini na baadhi ya wanachama kushangaa kwa kutojua wala kujulishwa kama hizo kesi zilikuwa zikiendelea.(hii sio hadithi ni movie ya tukio halisi.)
#kwa leo yaweza kuwa chapter I ya utumishi wangu na matukio dhidi yangu ndani ya mageuzi tangu 1991 hadi juzi tarehe 14 lilipotolewa tamko la mimi Wilfred Muganyizi Lwakatare kufutiwa uanachama na KAMATI KUU ya CDM.
#Ukweli maamuzi hayo yameniacha na taharuki kubwa, mawazo na msongo wa mawazo. Uamuzi umenichinjia baharini bila kunipa haki yangu kikatiba ya kujieleza/kujitetea. Kazi niliyoifanya kwa moyo wangu wote, kazi niliyoruka vihunzi kibao vya hatari, kazi niliyoiingia kwa utashi wangu mwenyewe na kuacha kazi iliyokuwa ikinilipa vizuri na marupurupu tele, kazi niliyokuwa nikiifanya kwa kujitolea zaidi kuliko malipo.
#Yaani Mbowe amewaridhisha wajumbe kwa mtu kama mimi mwenye historia niliyoieleza kuchinjwa bila kusikilizwa?
# Hata Saddam alipewa nafasi ya kujitetea japo naamini ni kama walikuwa wanaigiza. Mbowe na wajumbe wake kweli hawakutanguliza roho na fikra zenye busara, hekima, utu, uzalendo na huruma kwa mtu aliyekwisha tangaza tena kwa kutoa taarifa ya kutogombea miaka mitatu iliyopita kuanzia ngazi ya msingi pale kwetu kibeta kwenye msingi wangu wa Omukituli, kisha kata, Wilaya, mkoa, kanda,Taifa na hata Bungeni,. Yaani nikiwa nimebakiza siku zisizozidi wiki tatu nipate "kahela" kangu ka kumaliza kazi ya utume niliyotumikia na kutumika kipindi chote cha kazi za kisiasa!
#Ukweli maamuzi hayo ya kuingia bungeni na kuupinga uamuzi wa Kamati kuu ya kutokwenda niliyafanya nikiwa na akili kamili, nikiwa na fikra kamilifu, bila shinikizo na wala bila kujutia maamuzi ambayo chama kingeliyafanya.
#Hayo maamuzi yalikuwa ya kuniweka kwenye majaribu, na mimi kwa principle zangu kuna mambo ambayo huwa siruhusu nijaribiwe ambayo kamwe ni kama haya.
#Najiheshimu, nawaheshimu waliokuwa viongozi wangu lakini siko tayari kufanyiwa tendo walilofanyiwa waumini wa Kibwetere huko Uganda ya kuwateketeza wauumini wote kwa petrol wakiwa wamefungiwa na kufuli ili wakauone vizuri ufalme wa mbinguni walioahidiwa na Kibwetere. Kibwetere hadi leo anatafutwa na vyombo vyote vya dola nchini Uganda ili atiwe nguvuni lakini hajapatikana hadi leo.
#Niliyoyaeleza ni Chapter ya kwanza, bado zipo chapter zaidi ya arobaini endapo kutatokea huitaji kutokea kwenu wafuatiliaji wa sakata hili. Kwa wenye vyombo vyao vya habari wako huru kunitembelea kwangu au kuniita popote mkizingatia kuwa mimi ni mtu huru nisiye na chama chochote ( BALI "MBUNGE ANAYETOKANA NA VITI VYA MH SPIKA) Linavyotokana na rungu lake lililoko mezani kwake BUNGENI) ili kuendeleza TAMTHILIA yetu. MBARIKIWE NA BWANA.
Sent using
Jamii Forums mobile app