Je, wajua kuwa hatma ya CHADEMA ipo mikononi kwa Lwakatare? Baada ya CHADEMA kumwaga ugali, Lwaka akiamua kumwaga mboga, CHADEMA kwishney!

Pasco vijana wanakutukana sio kwamba hawakuheshimu ni kwa sababu hawakuelewa Nyoosha maelezo mze Mwaka wa uchaguzi
Paskal mayala leo hapati usingizi hukutarajia kunyukwa hivi alijiamini akaandika makala ndefu akazani Naibu Rais Daud Bashite ataisoma kisha asuke mipango ya uteuzi lakini matokeo yamekuwa kinyume wengi wanasoma kidogo wanaamua kumshambulia na asipokuwa makini chadema watampora mke abakie kuwa single mzee kama Lipumba.
 

[emoji1241]NASIMAMA NA UKWELI,CHADEMA INAKUFA TARATIBU.

Hivi kufa kwa chadema mnatarajia ife kama binadamu au?

Watu maarufu wote wanaikimbia.

Walioibeba tangu mwanzo wanaondoka.

Warombo wanabaguliwa na wamachame.

Mmetoka kuwa chadema ya watu makini hadi kina mdude nyangali wavuta bangi na watukanaji ovyo.

Mmefikia mahali wabunge nusu hawatii au wamekaidi maagizo ya mwenyekiti.

Chama kimepoteza dira rasmi ya sera, ilikuwa ufisadi lakini sasa ndio kinawatetea walioko jela kwa ufisadi.

Wabunge wamekuwa watoro majimboni badala yake wamehamishia majimbo mitandaoni.

Watu maarufu kwa matusi kina kigogo na fyatu karume,mange kimamboo ndio wamegeuka makamanda.

Bado mnasema ooh chadema ipo ok

Itakuwepo lakini inaelekea kuwa kama TLP.....


Time will tell!........



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Paschal nadhani hauko sahihi! Ikumbukwe pia haya mambo ya kuwafutia uanachama hufanywa na vyama vyote hasa pale inapotokea kuna utovu wa nidham hivyo kwa CDM si jambo geni kumtimua kada wake muhim km Rwakatale( Zitto alikua muhim zaidi). Hata chama tawala CCM wamepata kuwatimua makada wao mahili sana km Membe lakini bado hayo unayoyatabiri hayakutokea! TUJIFUNZE KUFANYA MAAMZI SAHIHI NA KUWA TAYARI KWA IMPACT YA MAAMZI YETU
 
Ndungai hutumii Sheria na katiba ya Tanzania kuongoza Bunge bali anatumia Sheria za kijijini kwake kongwa
 
Ndoto za ALINACHA hizi. Utasubiri sana kwa Chadema kufa.
kulikua na kina thomaso kama ninyi walipokua wanaambiwa NCCR itaondoka kama chama kikuu cha Upinzani, kulikua na kina Thomaso kama ninyi wakati wanaambiwa CUF itasambaratishwa sioni ajabu kama bado wapo hata leo. Hiki chama kikirudisha Wabunge 10 itakua ushindi mkubwa sana kwa CHADEMA. Zitto kama si ujinga wake angeweza kuvuna baadhi na kuwa KUB lakini naiona NCCR inaturudi tena upya itasheheni watu wa maana siyo wa kuburuzwa maana sasa hivi CCM wanaburuzwa na CDM nao Mbiwe anawaburuza udikteta CCM udikteta CDM
 
Kwa msaada wa dola sawa, kama mnaua watu na kuteka mtashindwa kutumia dola kuifuta cdm, si mnapeleka mswada bungeni tu.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndungai hutumii Sheria na katiba ya Tanzania kuongoza Bunge bali anatumia Sheria za kijijini kwake kongwa
Katiba ya CDM inasemaje katika kuwafukuza watu uanachama? Wafuasi wa CDM waacha waitwe wakazi wa Serengeti juzi juzi tu hapa mlikua mnaishambulia CCM kumfukuza Membe japo wenzenu hata kama walimuonea lakini walipitia ngazi kumfukuza mtu aliitwa na kuhojiwa na akapewa nafasi ya kujitetea lao mmesahau mmekua kama akili ya Bata vile. Poleni sana
 
Pasco umekuja kua mpuuzi mmoja wa ajabu.
CHATA, bila shaka unaufahamu usemi huu wa kikulacho ki nguoni mwako na amini usiamini kinacholitafuna hili jamvi letu ki nguoni mwetu. Kuna siku ukweli huu utakuja kudhihirika na wana JF wasishangae siku watakapozinduka na alaa, kumbe mtu mwenyewe ndiye huyu? Kweli umdhaniye siye, ndiye.

Mimi si Chadema lakini nimewaunga mkono kwa mengi hadi baadhi ya wenzetu humu kunituhumu kuwa mwana Chadema. Ukweli ni kwamba naamini kwa dhati kuwa adui mkubwa wa taifa hili ni CCM na siku Watanzania watakapolitambua hili kwa ujumla wao watakuwa wamekata minyororo ya utumwa kwa hili zimwi.

Ninavyofahamu Lwakatare awali alikuwa mbunge kutoka kutoka chama cha CUF na Chadema ilimpa hifadhi kama ilivyowapa wahamiaji wengi tu kama Dr. Slaa pamoja na Lowassa. Hili swala la Chadema kufa au hatma yake kuwa mikononi mwa mtu kwa kuwa tu ametimuliwa humo ni utabiri wa kijinga.

Hata hivyo ukweli mchungu ni kwamba hatma ya wana Chadema iko mikononi mwa hilo zimwi, CCM. Wanaweza wakawaua wana Chadema, wanaweza wakawateka, kuwatesa na hata kuwamiminia risasi, wanaweza wakawafunga gerezani, wanaweza wakawanunua kwa nguvu wana Chadema, naam yote hayo wanaweza.

Lakini ambacho hawawezi na katu hawataweza ni kulazimisha wapendwe, hawataweza kufuta upinzani...siku hadi siku wataendelea kuchukiwa zaidi na zaidi kwa dhulma na maovu dhidi ya Watanzania. Najua kwa uovu wao wanaamini kuwa watakuwa viongozi milele, hiyo ni ndoto waliyo nayo wadhulumiaji siku zote.
 
Hakutamalaki
wanamsikiliza yule Prof wa jalalani kama Kabudi Lwaitama. Tanzania tuna matatizo sana na wasomi wetu wakiingia katika Siasa wakua kama mapimbi. Kabudi Lwaitama Mwakyembe Baregu Mvungi peke yake labda ndiyo maana aliuawa
 
unajuaje kama hawapendwi? Mkuu mimi siyo CCM wala Chadema japo nilikua mwanamageuzi huko nyuma. Na niliachana na kuwa mfuasi wa chama chochote sababu niliona napoteza muda wangu kufuatilia siasa za Tanzania za chama kimoja. Kama wapinzani wasingekua wajinga wa kukimbilia Ikulu wakidhani watawaondoa CCM ule mwaka 1995 wangeng'ang'ania kudai katiba kama tulivyokubaliana mwaka 1990/91 wakati tukiwa na NCCR kama daraja la kutuvusha kupata katiba mpya basi labda sasa hivi CCM ndiyo wangekua wapinzani. Tatizo la vijana wengi hapa Jamii siasa mmeanza kuzifuatilia mwaka 2010 na wengine mwaka 2015 hivyo nawonea huruma saana mnapopata taabu ya kulumbana humu.

CCM haiwezi kuondolewa na kina Mbowe wala Mbatia mlishachezea shilingi kwenye shimo la choo imendoka kama mngekua na akili mngeacha siasa za maji taka labda hisani ya ccm ingewasaidia. Na kama mlichezea bahati ya katiba wakati wa kikwete na mkaona labda alitaka kujiongezea muda basi mmeula wa chuya. Kulikua na ubaya gani Kikwete abaki hata miaka miwili halafu tuanze upya na katiba mpya??? na Tume huru.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…