Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Paskal mayala leo hapati usingizi hukutarajia kunyukwa hivi alijiamini akaandika makala ndefu akazani Naibu Rais Daud Bashite ataisoma kisha asuke mipango ya uteuzi lakini matokeo yamekuwa kinyume wengi wanasoma kidogo wanaamua kumshambulia na asipokuwa makini chadema watampora mke abakie kuwa single mzee kama Lipumba.Pasco vijana wanakutukana sio kwamba hawakuheshimu ni kwa sababu hawakuelewa Nyoosha maelezo mze Mwaka wa uchaguzi
Paskal mayala yeye ni Msukuma anawatetea wasukuma ni mwendekeza ukabila anayesaka uteuzi kwa njia zotepaskali simtofautishi na wapiga debe
Hakuna kitu hapo bali propaganda kutafuta huruma kwa watawala. Kama CHADEMA haijafa baada ya Dk Slaa na haijafa miaka 5 bila siasa na haijafa kwa bunduki na mabomu na jela na mapanga na jela, ni nani wa kuipoteza CHADEMA? Lwakatare sisimizi ndo aipoteze CHADEMA? Kweli ww njaa imekupanda kichwani kama lilivo jina lako.
Chadema ni imani, chadema sio majengo...chadema iko sisiemu...chadema iko kwenye utawala.
Paschal nadhani hauko sahihi! Ikumbukwe pia haya mambo ya kuwafutia uanachama hufanywa na vyama vyote hasa pale inapotokea kuna utovu wa nidham hivyo kwa CDM si jambo geni kumtimua kada wake muhim km Rwakatale( Zitto alikua muhim zaidi). Hata chama tawala CCM wamepata kuwatimua makada wao mahili sana km Membe lakini bado hayo unayoyatabiri hayakutokea! TUJIFUNZE KUFANYA MAAMZI SAHIHI NA KUWA TAYARI KWA IMPACT YA MAAMZI YETUWanabodi,
Kuna vitu mimi huwa navisema humu na watu wanavichukulia poa, ila vikija kutokea ndipo wenye uelewa wanaanza kuelewa nilikuwa nazungumzia nini.
Hivi ni baadhi ya vitu nilivyovisema na kweli vikaja kutokea
Sasa ninachokisema leo ni kuwa sio wengi wanajua kuwa hatma ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Chadema, iko mikononi mwa Mhe. Wilfred Lwakatare?. Chadema imepakua ugali kwa kila mtu kupewa ugali kwenye sahani yake, Kamati Kuu ya Chadema, wakaamua kuipindua sahani ya ugali wa Lakwatare, na kuumwaga ugali ili Lwakatare asile, huku wengine wote wakiwa na ugali wao kwenye sahani zao, wakisubiri bakuli la mboga litetwe, huku haku mwenye kumbukumbu ni nani aliyetumwa jikoni kwenda kuleta bakuli ya mboga, watu wapakuliwe ndipo wale!.
- Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli - JamiiForums
- Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam - JamiiForums
- Dr. Shein Mfute Kazi Haraka, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Kabla Hajamwaga Sumu Hii - JamiiForums
- Je, Wajua Bunge linaweza kutoa azimio batili? CAG yuko kikatiba. Je, Bunge lina uwezo kutopokea ripoti ya CAG? - JamiiForums
- Je, Wajua Bunge linaweza kuvunjwa Siku 7 Zijazo?. lisipopokea ripoti ya CAG, Bunge linavunjwa kwa mujibu wa Katiba - JamiiForums
Mara aliyeibuka jikoni na bakuli ya mboga ni Mhe. Wilfred Lwakatare!, Amelishika bakuli la mboga za moto kwa mikono yake, huku mikono yake inaungua lakini amestahimili na kuvumilia huku akitokwa machozi, jasho na damu, kwa ajili ya Chadema!. Kabla hajalitua bakuli la mboga ili watu watu wapakue wote wale, akandua kuwa ugali wake umemwagwa!.
Wakati wanamwaga ugali wake, hakuna aliyekumbuka kuwa anayesubiriwa kuleta mboga watu wale ni Lwakatare, hivyo sasa wote wamenyamaza kimya kusubiria Lwakatare, atafanya nini baada ya kubaini Chadema wamemwaga ugali wake, huku mwenye bakuli ya mboga ni yeye!, sasa hatima ya kama Chadema watakula ama hawali, ikomikononi mwa Lwakatare, baada ya wao kumwaga ugali, Lwakarare akiamua kumwaga mboga, then wanakosa wote!, Chadema ndio inakuwa kwishney!.
Ili uelewa mimi nazungumza nini, ni lazima kwanza ukijue kisa, ambacho ndio bakuli ya mboga.
Ngoma ilianzia Star TV tarehe 30 Dec, 2012
On Star TV: Zitto, Nchemba na Mtatiro ktk mjadala wa kutathmini ya Siasa Tanzania 2012 - JamiiForums
Ndipo hatimaye movie ikapandishwa you tube na hapa ukazungumzia mwanzo mwisho
Chadema wafichua mtandao wa ugaidi - JamiiForums
Mwigulu Nchemba amekiri kuhusika na movie ya Lwekatare - ashikwe na kuunganishwa kesi hiyo - JamiiForums
Kisa chenyewe ni hiki.
Kasoro kubwa katika video ya Lwakatare - JamiiForums
Chadema ni chama cha ajabu sana!, kuna watu unaweza kuwatimua lakini sio Lwakatare, na sababu ni moja tuu, ameipigania Chadema kwa machozi, jasho na damu!.
Chadema inapaswa kumyenyekea Lawakatare na kwasababu aliishatangaza kustaafu, Chadema walipaswa kumuacha tuu astaafu kwa amani, haswa kwa kuzingatia wamemfukuza wakati ambao Bunge hili limebakiza wiki3 tuu limalizike rasmi.
Umuhimu wa Lwakatare kuachwa tuu hata afanye nini au aseme nini, ni kumzuia asije kufungua mdomo wake!.
Ikitokea Lwakatare akaamua kufungua mdomo wake na kuyataja madudu ya ajabu Chadema inayoyafanya nyuma ya pazia, ikiwemo ile video mimi niliyoita hapo kuwa "bonafide genuine", Chadema Watakuwa mgeni wa nani?.
Mtu kama Lwakatare anafukuzwaje?.
Kufuatia hiyo video niliyoitaja kule juu, nilipokuta na Msajili wa vyama alisema
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, Kufutwa Kwa Mujibu wa Katiba!... Endapo ...! - JamiiForums
Sasa hiyo endapo katika bandiko hilo, ndilo bakuli la mboga, Lwakatare amelishikilia, licha ya yeye kunwagiwa ugali wake, anaweza kuamua yeye ndio akose na kulala njaa, hivyo atalitua tuu hilo bakuli la mboga na wengine wote wale, na yeye tuu ndio akafie mbele, ila akiamua kuonyesheana ubabe, na mambo yanakuwa ni ubabe ubabe tuu, maadamu wamemwaka ugali, na yeye anamwaga mboga...
yatakuwa mengine!.
Lets keep watching tukisubiria Lwakatare ataamua nini, ila amini usiamini, hatima ya Chadema, iko mikononi mwa Mhe. Lwakatare!, kubali, kataa!.
Paskali
P.
Ni umri wa le mutuz miaka 57
Ndungai sasa kajitoa fahamu kasahau kuwa wabunge wa CUF aliwavua yeye ubunge kwa Sheria hizo hizo lakini wabunge wa chadema kaamua kuwamiliki kwa utaratibu wa kienyeji kwa Sheria za kishetani
kulikua na kina thomaso kama ninyi walipokua wanaambiwa NCCR itaondoka kama chama kikuu cha Upinzani, kulikua na kina Thomaso kama ninyi wakati wanaambiwa CUF itasambaratishwa sioni ajabu kama bado wapo hata leo. Hiki chama kikirudisha Wabunge 10 itakua ushindi mkubwa sana kwa CHADEMA. Zitto kama si ujinga wake angeweza kuvuna baadhi na kuwa KUB lakini naiona NCCR inaturudi tena upya itasheheni watu wa maana siyo wa kuburuzwa maana sasa hivi CCM wanaburuzwa na CDM nao Mbiwe anawaburuza udikteta CCM udikteta CDMNdoto za ALINACHA hizi. Utasubiri sana kwa Chadema kufa.
HakutamalakiKwa sasa chadema inaendeshwa na Mdee, Bulaya, na Lema, usitegemee akili kutumika hapo. Prof. Safari na Prof. Baregu sijui hawapo tena, mtanisaidia kujua.
Sent using Jamii Forums mobile app
kulikua na kina thomaso kama ninyi walipokua wanaambiwa NCCR itaondoka kama chama kikuu cha Upinzani, kulikua na kina Thomaso kama ninyi wakati wanaambiwa CUF itasambaratishwa sioni ajabu kama bado wapo hata leo. Hiki chama kikirudisha Wabunge 10 itakua ushindi mkubwa sana kwa CHADEMA. Zitto kama si ujinga wake angeweza kuvuna baadhi na kuwa KUB lakini naiona NCCR inaturudi tena upya itasheheni watu wa maana siyo wa kuburuzwa maana sasa hivi CCM wanaburuzwa na CDM nao Mbiwe anawaburuza udikteta CCM udikteta CDM
Katiba ya CDM inasemaje katika kuwafukuza watu uanachama? Wafuasi wa CDM waacha waitwe wakazi wa Serengeti juzi juzi tu hapa mlikua mnaishambulia CCM kumfukuza Membe japo wenzenu hata kama walimuonea lakini walipitia ngazi kumfukuza mtu aliitwa na kuhojiwa na akapewa nafasi ya kujitetea lao mmesahau mmekua kama akili ya Bata vile. Poleni sanaNdungai hutumii Sheria na katiba ya Tanzania kuongoza Bunge bali anatumia Sheria za kijijini kwake kongwa
CHATA, bila shaka unaufahamu usemi huu wa kikulacho ki nguoni mwako na amini usiamini kinacholitafuna hili jamvi letu ki nguoni mwetu. Kuna siku ukweli huu utakuja kudhihirika na wana JF wasishangae siku watakapozinduka na alaa, kumbe mtu mwenyewe ndiye huyu? Kweli umdhaniye siye, ndiye.Pasco umekuja kua mpuuzi mmoja wa ajabu.
wanamsikiliza yule Prof wa jalalani kama Kabudi Lwaitama. Tanzania tuna matatizo sana na wasomi wetu wakiingia katika Siasa wakua kama mapimbi. Kabudi Lwaitama Mwakyembe Baregu Mvungi peke yake labda ndiyo maana aliuawaHakutamalaki
unajuaje kama hawapendwi? Mkuu mimi siyo CCM wala Chadema japo nilikua mwanamageuzi huko nyuma. Na niliachana na kuwa mfuasi wa chama chochote sababu niliona napoteza muda wangu kufuatilia siasa za Tanzania za chama kimoja. Kama wapinzani wasingekua wajinga wa kukimbilia Ikulu wakidhani watawaondoa CCM ule mwaka 1995 wangeng'ang'ania kudai katiba kama tulivyokubaliana mwaka 1990/91 wakati tukiwa na NCCR kama daraja la kutuvusha kupata katiba mpya basi labda sasa hivi CCM ndiyo wangekua wapinzani. Tatizo la vijana wengi hapa Jamii siasa mmeanza kuzifuatilia mwaka 2010 na wengine mwaka 2015 hivyo nawonea huruma saana mnapopata taabu ya kulumbana humu.CHATA, bila shaka unaufahamu usemi huu wa kikulacho ki nguoni mwako na amini usiamini kinacholitafuna hili jamvi letu ki nguoni mwetu. Kuna siku ukweli huu utakuja kudhihirika na wana JF wasishangae siku watakapozinduka na alaa, kumbe mtu mwenyewe ndiye huyu? Kweli umdhaniye siye, ndiye.
Mimi si Chadema lakini nimewaunga mkono kwa mengi hadi baadhi ya wenzetu humu kunituhumu kuwa mwana Chadema. Ukweli ni kwamba naamini kwa dhati kuwa adui mkubwa wa taifa hili ni CCM na siku Watanzania watakapolitambua hili kwa ujumla wao watakuwa wamekata minyororo ya utumwa kwa hili zimwi.
Ninavyofahamu Lwakatare awali alikuwa mbunge kutoka kutoka chama cha CUF na Chadema ilimpa hifadhi kama ilivyowapa wahamiaji wengi tu kama Dr. Slaa pamoja na Lowassa. Hili swala la Chadema kufa au hatma yake kuwa mikononi mwa mtu kwa kuwa tu ametimuliwa humo ni utabiri wa kijinga.
Hata hivyo ukweli mchungu ni kwamba hatma ya wana Chadema iko mikononi mwa hilo zimwi, CCM. Wanaweza wakawaua wana Chadema, wanaweza wakawateka, kuwatesa na hata kuwamiminia risasi, wanaweza wakawafunga gerezani, wanaweza wakawanunua kwa nguvu wana Chadema, naam yote hayo wanaweza.
Lakini ambacho hawawezi na katu hawataweza ni kulazimisha wapendwe, hawataweza kufuta upinzani...siku hadi siku wataendelea kuchukiwa zaidi na zaidi kwa dhulma na maovu dhidi ya Watanzania. Najua kwa uovu wao wanaamini kuwa watakuwa viongozi milele, hiyo ni ndoto waliyo nayo wadhulumu siku zote.
anatafuta ukuu wa wilaya kwa hooks and crooks na hapati. mimi namshauri ajiunge na chadema tumpe jimbo.Pasco umekuja kua mpuuzi mmoja wa ajabu.