Je, wajua kuwa hatma ya CHADEMA ipo mikononi kwa Lwakatare? Baada ya CHADEMA kumwaga ugali, Lwaka akiamua kumwaga mboga, CHADEMA kwishney!

 
Misukule michache naona ndio imeunga mkono bandiko hili,ila za uso bwana njaa kazipata kisawasawa!
Huyu jamaa ashafanywa toilet paper ya lumumba,shame!
 
Makamanda wameshindwa kuelewa alichoandika Pasikali au ni ndio kuweweseka? Nilitegemea mngejibu kwa hoja za msingi!
 
Lets keep watching tukisubiria Lwakatare ataamua nini, ila amini usiamini, hatima ya Chadema, iko mikononi mwa Mhe. Lwakatare!, kubali, kataa!.

Paskali
P.
Bwana P,
Umejitahidi kuokoteza kwenye ghala lako, yaelekea bado hujaamini kuwa umefilisika.
Ninachokiona ni labda tu kwa porojo hizo, utafanikiwa kuivutia CCM ili ikupende zaidi ya wagombea wenzio, kama Comrade Mwigulu alivyowahi kujifaragua kwa kutoa tuhuma za ugaidi, ambazo mwishowe alishindwa kuzithibitisha hata hapa duniani, kwa huyohuyo Mh Lwakatare.
Wewe na hata hao CCM wenzio yafaa mngekubali ukweli tu kuwa, hamna uwezo wa kuitisha CHADEMA na kama hauna kingine cha kufanya, ungejipumzikia tu badala ya kuhnjahanja.
 
porojo
 

Pasco Mayalla ni mnafiki wa kutupwa yaani. He's not bold man. Ni mtu wa kukaa karibu na kuchaka mara zote. Mambo yakimuendea safi anajisifia ujasiri, yakimuendea mrama anakimbilia kichakani kujificha.
 
Unachekesha kweli,,hiyo mboga mnayozungumzia kama ina sura ya jinai maana yake ni kwamba inamhusu yeye moja kwa moja.Kwahiyo akimwaga mboga kama mnavyosema yeye ndo mhanga nambari mmoja,,ni sawasawa na mtu kukata tawi ulilokalia,je inawezekana?
 
Wewe upo nyuma keyboard unajidanganya kuwa chadema imekufa hao wabunge mliowanunua bado siyo ccm moyoni msipowapa vyeo watawatesa sana hakuna aliyeondoka chadema zaidi ya kununuliwa na ccm, chadema haifi utakufa wewe chadema ipo milele na milele
 
Wewe upo nyuma keyboard unajidanganya kuwa chadema imekufa hao wabunge mliowanunua bado siyo ccm moyoni msipowapa vyeo watawatesa sana hakuna aliyeondoka chadema zaidi ya kununuliwa na ccm, chadema haifi utakufa wewe chadema ipo milele na milele
Waanzilishi wa Chadema Mzee Bob Makani, Mzee Victor Kimesera na wengineo walifariki sembuse mimi? Subiri Mzee Mtei afariki uone kama Chadema itabaki! Mark my word fella!
 
Wengi mnajua mapungufu ya sasa ya ccm mbona imewatupa kinana membe January makamba kapilimba kange lugole hadithi mpya ni ya kenya Congo Zambia Malawi Ghana yanakuja kutokea Tanzania ccm inakuwa chama cha upinzani
 
Misukule michache naona ndio imeunga mkono bandiko hili,ila za uso bwana njaa kazipata kisawasawa!
Huyu jamaa ashafanywa toilet paper ya lumumba,shame!
Leo ndiyo paskal mayala kajua kuwa idadi kubwa ya watanzania hawaitaki ccm ingawa wanekuwa wakilazimisha kupendwa kwa kuwanunua wapinzani kwa pesa za walipa kodi Hii itampa fundisho sahihi
 
Makala ya Paskali imenisaidia kuelewa sababu za Nchi Jirani na sisi kudharau elimu ya Tanzania.
Mwandishi wa ''topic"' hii amesoma, tena amesoma Sheria, katika Chuo Kikuu maarufu kuliko vyote, Udsm, lakini bado anaamini kuwa Siasa za Tanzania ni Siasa za Majina ya watu.
Msomi wa Tanzania anaamini katika u-Rwakatare na u-Mbowe!
Anaamini kuwa kura alizopata Lowasa katika uchaguzi uliopita, zilitoka kwa watu walioweka matumaini yao katika majina ya akina Rwakatare na akina Mbowe!
Hii ni aibu kubwa sana kwa elimu inayotolewa katika shule na Vyuo Vikuu katika JMT.
Bahati nzuri ni kwamba Mwenyekiti wa CCM Taifa hakubaliani na Paskali.
Mwenyekiti wa CCM Taifa anajua fika kuwa Chadema na Vyama vingineo vya Upinzani wa Kweli vinawakilisha maoni na mawazo ya Watanzania.
Na kwa kulijua hilo, anahakikisha kuwa Jeshi la Polisi linawazuia Wapinzani kutowasiliana na umma wa Tanzania, lakini Jashi la Polisi na CCM wanakwama kutokana na maendeleo yaliyofikiwa katika sayansi na teknolijia.
Mungu ibariki Afrika.
Mungu ibariki Tanzania
 
Hawa ni watu wanaotumika kama "lead" kuanzisha mjadala ili mkakati wenyewe ukianza tuwe tushaandaliwa kiakili.
Ukiona huyu kasema hivi jua katumwa.Kuna mkakati nyuma yake.
Chadema muwe makini na huyo Rwakatare.Huenda keshatafutwa tayari.
 
Cadema ya slaaa na hii ni mbingu na Ardhi boss

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…