Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Watu wengi wanachukulia kuwa Iran na Israel ni maadui wakati wote, na wengine kwa kutoelewa wanadhani uhasama wa Israel na Iran umechangiwa na utofauti wa imani za kidini. Kama unafikiria hivyo, umepotea kabisa.
Kabla ya mwaka 1979, Iran ilikuwa mnunuzi mkubwa wa silaha toka Israel (Before the Iranian Revolution in 1979, Iran under the Shah Mohammad Reza Pahlavi was an ally and major buyer of Israeli weapons.)
Wakati wa vita kati ya Iran na Iraq, Israel ilikuwa upande wa Iran, na ndiyo iliisaidia sana Iran kwenye upande wa silaha (Israel supported Iran during the Iran–Iraq War).
Nov 1979, wairan wenye msimamo mkali walipowateka wamarekani, na marekani kuiwekea vikwazo Iran, Israel iliendelea kushirikiana na Iran kwa kuiuzia Iran silaha ambazo Iran ilinyimwa na Marekani, kiasi cha Marekani kuudhiwa na kitendo hicho cha Israel (Iran Unable to get military equipment from the Carter administration, the Iranians reached out through back channels to the Israeli government and negotiated a preliminary covert arms deal between the two countries. In early 1980, the first military equipment sale by Israel to the Iranian government of Ayatollah Khomeini occurred).
Ili Israel isigundulike kuwa inaiuzia silaha Iran, Israel ilitengeneza kampuni US ili kuhakikisha inaisaidia Iran kupata silaha bora (Israeli intelligence ran a front company of 50 employees on John Street in the Wall Street area.[29] The office was used to direct the covert purchases of American military equipment to resell to Iran.[28] In March 1982, there was a leak to The New York Times about Israel's covert weapon sales to Iran.[30][31] Fearing the company's operations might have been compromised, the covert Israeli weapons purchasing operation was moved to London in 1983).
Ikumbukwe kuwa Iran ilikuwa nchi ya pili kulitambua Taifa la Israel baada ya Uturuki.
Kuna wakati kulikuwa na urafiki mkubwa kati ya mataifa haya, kiasi hata cha wananchi wake kuuziana kuku na mayai.
Urafiki wa kale kati ya mataifa haya, mpaka leo, umeifanya Iran kuwa ni nchi pekee ya Mashariki ya kati yenye wayahudi wengi.
MAONI
Mataifa haya yakirudi nyuma, yakaangalia kilichowatenganisha, yakashughulikia hayo, na kisha kurudi kwenye mahusiano yao ya kale, kuna mambo mema mengi kwa pande zote yatatokea:
1) ugaidi unaweza kufutika au kupungua sana Middke East.
2) uchumi wa Iran utapaa sana .
3) Mataifa haya mawili kwa kiasi kikubwa yatasimamia usalama wa mashariki ya kati nzima.
Hakuna lisilowezekana, wagombanao ndio wapatanao. Kauli ya Iran kuwa haitafanya shambulio dhidi ya Israel baada ya shambulio la jana, ni hatua nzuri, isichukuliwe kama.ni udhaifu au unyonge. Ni vema Israel nayo ikanyosha mkono wa heri wa namna hiyo hiyo, na kutoa kauli kuwa haitaishambulia Iran. Likitokea hilo, kauli moja tu ya Iran kuwataka Hamas, Hezbollah na Houthi kutoishambulia Israel, itaifanya Israel kusimamisha vita, na kisha kuyavunja makundi haya kwa njia ya amani. Bila msaada wa Iran, makundi haya hayatakuwepo.
Misri ilipoitambua Setikali ya Israel na kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia, mara moja, Israel ililirudisha eneo la lililoliteka wakati wa vita, eneo la Sinai, kwa Misri. Hivyo hakuna kinachoshindikana katika ama kuwapa Wapalestina nchi au kuwafanya wapalestina, Waarabu, Wayahudi kuwa Taifa moja lenye kuheshimu jamii zote. Yakitokea hayo itakuwa ni heri kwa Dunia, na pigo kubwa kwa wanaopenda uhasama badala ya amani na urafiki. Ifahamike kuwa uhasama kati ya Iran na Israel, umesababisha uhasama hata kwa mataifa mengine nje ya Mashariki ya kati.