Uchaguzi 2020 Je, wajua kuwa Mfumo wa Serikali ya Majimbo unatumika kwenye Nchi zenye kukosa Umoja wa Kitaifa?

Hamu na nia ya maendeleo ya mikoa ya Tanzania haina tofauti na haipishani sana. Huyo RC au DC anayeletwa huko mkoani au wilayani ni Mtanzania wa kawaida na anayajua mahitaji ya mkoa husika, kama hayajui basi asaidiwe na RCC au DCC yake. Mfumo huu wa akina Lissu na Amsterdam ni mtego wa kurudisha UKABILA na UTENGANO Tanzania.
 

Kura za bonus???😂😂!! Vijana mna nini???
 
Hiki ndiyo kituko cha mwaka sasa...
Yaani ujui kua ata Federal system ndiyo inafanya D by D kwa ufasaha.....daah Ahsante Lissu kwakweli
 
Mkuu anasema kuchagua Upinzani ni majuto...
Yaani watu wamenyimwa Maendeleo kisa chaguo lao ni opposition... Very primitive
 
Post yako ni sawa na tone la maji katika bahari
 
Hivi ndivyo vichwa vinavyochambua siasa uchwara za uchumi na majimbo.Mwalimu aliwahi kusema kuna wanaotaka Zanzibar ijitenge, wakifanikiwa wajue Unguja na Pemba haitakuwa moja. Na bara nayo haitakuwa moja. Sasa watu hao wameanza kujidhihirisha dhahiri. Bara na Visiwani.
 
Hata ivyo wewe mleta uzi ni shabiki ndaki ndaki wa CCM kwa hiyo hata ukiandika madudu gani , zaidi unakuwa Umeandika uhalo ,utopolo kwa sababu , akili yako imefungwa na uchama, otherwise ufungue akili yako na kuanza kuingiza vitu vipya , hapo utaonekana wa maana zaidi,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kifaurongo ninakushukuru sana kwa kumleta Kafulila. Ameongea vizuri na ameongeza nyama kwenye haya tunayoyajadili.

CHADEMA hawana Sababu yoyote ya kuwa na serikali ya majimbo zaidi ya kutaka kumuenzi muasisi wao.
 
Kuwa CCM au chama kingine sio hoja. Kudharau post yangu kwasababu ya uchama. Wewe jadili hoja zangu uone Kama Zina uzito au laa?
 
Hapo ndipo uasi utakapoanzia. Kwa jinsi ulivyoeleza, Kilimanjaro wanaona serikali ya kitaifa inawachelewesha wao wanamambo wanataka.

Swali

Waliwezaje kufikia hayo maendeleo waliyonayo sasa wakiwa chini ya serikali hii hii?

Angalizo
Mkoa wa Kilimnjaro (ambako nako ni asili yangu) uliwahi kumtuma chifu Mareale kwenda UN kudai uhuru wake.
Mkoa huo ndio anaotoka muasisi wa CHADEMA
Mkoa huo ndio anatoka mwenyekiti mwenye nguvu kuliko wote waliopata kutokea CHADEMA
Mkoa huo na jirani yake yaani Arusha ndiko sehemu CHADEMA inanguvu kuliko maeneo mengi ya nchi.

Nyie wengine na kina Lissu mmelishwa tuu matango pori. Vigogo wenyewe Wana lao la ndani kwenye kutaka serikali ya majimbo.

Ikitokea leo hii kukawa na serikali ya majimbo, Jimbo la kwanza litakalotaka kujitenga, nahofia litakuwa ni Jimbo la kaskazini.

I stand to be corrected
 
Kilimanjaro wana Rasilimali gani kuizidi Singida? Au Shinyanga?

Je Kilimanjaro ina Rasilimali kuizidi Songea au Mtwara?

Ukweli ni kwamba watu wa Kilimanjaro wamekuwa na Spirit ya kupenda kwao na wanaamini maendeleo yanaanzia na wewe binafsi. Sasa wakiendelea wengine tutaenda kujifunza kwao badala ya kwenda Ulaya
 
Nakuelewa sana tena sana lakini salama hii itaendelea kudumu Kama hakutakuwa na mfumo wa majimbo.

Kujifunza hata sasa kunaendelea. Mfano ni suala la usafi wa mji
 
Mfumo wa majimbo utaleta ushindani kati ya jimbo na jimbo.

Kama serikali ya jimbo fulani itazembea kwenye kuibua vyanzo vya mapato, basi watakuwa nyuma kimaendeleo.

Na pia itapunguza mzigo kwa serikali kuu. Yenyewe itaangalia mambo makubwa haswa ya mambo ya ulinzi na ushirikiano wa kimataifa hivyo kuongeza ufanisi kwa masuala makubwa makubwa.
 
Tunayo majimbo ya uchaguzi (constituency) huo ushindani ufanyike huko Kati ya jimbo na jimho
 
Tunayo majimbo ya uchaguzi (constituency) huo ushindani ufanyike huko Kati ya jimbo na jimho

Majimbo hayo hata yakibuni vyanzo vya mapato, sehemu kubwa inaenda serikali kuu.
Majimbo yawe na nguvu ya kukusanya mapato na kuendeleza jimbo husika. Sehemu fulani ya mapato hayo ndio iende serikali kuu.
 
Kwa nini unalisha watu uongo? Nigeria tangu vita vya Biafra vilipo malizika na wakaanzisha mfumo wa Federation mwaka 1970 hadi leo hii hatujawahi kusikia kuna jimbo huko linataka kujitenga.

Kabla ya hapo Nigeria ilikuwa na Unitary System of Government kama tuliyo nayo leo na ndio ilikuwa chachu iliyochochea ukabila na kupelekea wauwane wenyewe kwa wenyewe kabla ya kuachana na huo mfumo na kuanzisha majimbo ambayo imewapa ahueni hadi leo hii.
 
Majimbo hayo hata yakibuni vyanzo vya mapato, sehemu kubwa inaenda serikali kuu.
Majimbo yawe na nguvu ya kukusanya mapato na kuendeleza jimbo husika. Sehemu fulani ya mapato hayo ndio iende serikali kuu.
Unafikiri hayo mapato yakienda serikali kuj yanaenda kufanya Nini? Hebu tuanzie hapo
 
If you are being paid something to write on if, please justify the payment by writing something that has been researched and noble. Do not write crap and you expect as to be baloney.
If you look at those countries that are using federal type of governance, kindly note that RSA,Zambia, Kenya, Nigeria, Angola, Germany, Australia, USA, Brazil, Argentina, Canada to mention just afew have seen governance ro be entrenched at the grassroots level to the gubernatorial positions where all through are elective positions where their loyalties are on the people that they represent. Not political apoointments which play in but rather elective and that is what we need.
 
Historia ya Nigeria ni tofauti sana na sisi. Huko uasi ulikuwa juu sana ukisababishwa na udini, ukabila na uwepo wa rasilimali. Kila mtu akivutia kwake. Ili kuepusha vurugu ndio ikaamuliwa basi wapewe madaraka flani ili roho zao zitulie
My original post is in Swahili, I would expect u to comment in the same order. Anyway, since ur role model insinuated that we r uncaple of communicating in English, I will respond in English just for nothing else but to prove him wrong
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…