Je wajua kwa nchi zilizoendelea, kukopa na kununua kwa fedha taslim gharama ni sawa?

Je wajua kwa nchi zilizoendelea, kukopa na kununua kwa fedha taslim gharama ni sawa?

OLS

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2019
Posts
457
Reaction score
773
Bongo imekuja huduma ya kukopa simu kwa sasa ambapo simu hizo zinalipwa kwa siku. Hili suala la kulipa kwa siku lenyewe kwanza ni mtihani lakini pia gharama ya simu inaongezeka mara dufu. Hivyo anayekopa hakuna kitu anaepuka, maana kama unalipa 2100 kwa siku ujumlishe na hela ya kifurushi maana yake kwa siku mtu anatumia Tsh 5000, ambayo hii kwa mwezi inaweza kufika hadi Tsh150,000. Mtu anayeweza kutumia hela hiyo kwa mwezi tayari yuko uchumi wa kati kibongobongo kwa hiyo hiyo sio namna ya kumsaidia masikini nchini.

Kwa wenzetu gharama ya kununua simu ni sawa na gharama ya kukopa. Mathalan angalia hii Iphone 17. Ukiingia kwenye website ya iphone kama fanya kama uko Marekani bei ya iphone 17 pro ni $1,099 ila ukikopa utalipa $45.79 kwa mwezi kwa muda wa miezi 24. Ambapo ukizidisha hiyo 45.79 kwa 24 utakuwa umelipa jumla ya $1098.96. Gharama inarudi kule kule sawa na kununua kwa fedha taslimu.
1758872318125.png


Aidha kwa google pixel na simu nyingine utaratibu ni hivyo hivyo... swali ni je Tanzania tuna nia ya kuongeza watumiaji wa simu kwa gharama kubwa kiasi hiki.
1758872575511.png
 
Kwa Tanzania sababu zinaweza kuwa nyingi ila kubwa ni;
1. Nadhani hakuna regulations juu ya mambo ya namna hii, nani anamfunga papa kengele?
2. Uaminifu kwa mkopaji, baadhi ya wanaokopa sio waaminifu, hakuna sheria za kuwabana hivyo wakopeshaji ni kama wanacheza kamari.
 
Umesema anatumia tsh 5000 kwa siku…hiyo 350000 umeipataje sasa ukizidisha kwa idadi ya siku za mwezi? Au kuna mabadikiko ya idadi ya siku ktk mwezi mmoja?
 
Kama bongo siyo sawa, wenyewe usawa watautoa wapi? Inabidi uelewe maana ya neno kukopa kwanza ndipo ujue uhalisia, neno kukopa maana yake ni biashara ya toa kidogo pata kikubwa, utakua umenielewa nadhani.
 
Back
Top Bottom