Je wajua kwamba Allah kwenye Quran anasema anahitaji kunusuriwa?

Kumbe hujalala ,safi, nilikuwa nachambua hapa QURANI ,

Tuendelee , unasema lahaja hazibadilishi maana, basi kwa nini Qur’an ya Hafs na Warsh zinatofautiana katika baadhi ya aya hata kwa matamshi, herufi na wakati mwingine maana ya sentensi?

Kwa mfano, katika Sura 2:184, Qur’an ya Warsh inasema "fa man tatawwa'a khayran" (anayefanya wema kwa hiari),

ilhali Hafs inasema "fa man tatawwa'a khayran fahuwa khayrun lahu" (anayefanya wema kwa hiari ni bora kwake).

Tofauti iko wazi na hiyo si lahaja tu, ni tofauti ya muundo wa maana.

Halafu unadai tafsir ina stages, na kweli, lakini hicho ndicho kinazua tatizo kubwa zaidi kwa nini Qur’an inayodaiwa kuwa Haina shaka ,Nyepesi kueleweka inahitaji masahaba, tabiin, hadith, na ijma kuielewa? Hapo ndipo tofauti na Biblia ilipo.

Biblia inaeleweka hata na mtu wa kawaida, kwa msaada wa Roho Mtakatifu bila ya kupitia tabaka la wasomi wa dini au lugha ya Kiarabu ya kale.

Na kuhusu Halifa Uthman kuirudisha Qur’an kwenye lahaja ya Quraish hiyo ni ushahidi kuwa kulikuwa na mgongano mkubwa wa usomaji.

Uthman mwenyewe alituma maagizo ya kuchoma nakala nyingine zote jambo ambalo linaonyesha hofu ya kupotea kwa maana au mchanganyiko wa maandiko.

Huo ni ushahidi wa wazi kuwa Qur’an haikutunzwa kwa mfumo wa muujiza kama mnavyodai,na kudanganywa watu kama mlivyodanganywa.

Kama kweli Qur’an ni neno la Allah lisilobadilika, kwanini lihitaji kurekebishwa na kuchujwa na kuchomwa moto na mwanadamu?

Nimeona pia unadai Qur’an ipo original πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

je, unaweza kuionesha hiyo copy ya original? Je, ipo wapi hiyo Qur’an ya wakati wa Muhammad?

Nakala za kale za Quran zinajulikana Mzee baba , kuna ya Sanaa (Yemen) na Topkapi (Istanbul), lakini hata hizo zina tofauti zao. Sasa, Qur’an ipi ni hiyo β€œoriginal” unayodai mnayo?πŸ˜‚πŸ˜‚


Umeisoma Qur’an ya Sanaa ya karne ya 7? Unaijua tofauti yake na ya Cairo edition ya 1924?


Ni nani aliyetoa ruhusa kwa Uthman kuchoma Qur’an zingine? Ni Allah au nani?


Kama Qur’an ni rahisi kueleweka, kwa nini iwe ngumu mpaka ihitaji tabaka la wanachuoni?

Je, unaweza kuthibitisha kwa maandishi kuwa lahaja zote hazikubadilisha maana, au unategemea β€œimani tu”?

Karibu tuchambue pamoja kwa hoja, si kwa hisia.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ulitaka ashuke aje aanze kueneza yeye mwemyew kwa njia gani au apigane yeye na wanaadam ?? post yako haina ata mashiko nawee
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ et macho...wapi imesemwa anaumwa macho... hii dini kama mnaipenda si mje tu wazee mnazunguka sana
 
k
kumbe ulikua na mengi ya moyon unataka uyatoe πŸ˜‚πŸ˜‚ haya si bado tuko na uislam na ukijichanganya kuchoma moto Quran na kumtukana hadharan Allah cha moto utakiona πŸ˜‚ siumeona wenzangu wa ulaya
 
Kama kawaida yenu kuchop vimstari bila kusoma full context.
 
Nitajibu yale ambayo ni ya msingi,ila yale yenye mtazamo wa kuleta ligi zisizo na maana ntakuachia mwenyewe

HIyo ayah ni hii:

2:184 - (Mfunge) siku maalumu za kuhisabika. Na atakaye kuwa miongoni mwenu mgonjwa au yumo safarini basi atimize hisabu katika siku nyengine. Na wale wasio weza, watoe fidiya kwa kumlisha masikini. Na atakaye fanya wema kwa kujitolea, basi ni bora kwake. Na mkifunga ni bora kwenu, kama mnajua.

Hapa utaona atakaye fanya kwa kujitolea na kwako atakaye fanya kwa hiari, lakini je msingi wa hiyo aya haujaeleweka?

Utaona kwamba umeeleweka,hii ni tofauti na biblia ambayo haina rejea,sasa kama qur'an tu ina original yake lkn kuna maneno kidogo yanatofautiana vipi kuhusu biblia ambayo haina rejea kabisa?

Na tofauti ya hayo maneno kidogo ni kutokana na tafsir,na tafsiri sio qur'an bali hiyo inaitwa tafsir ya qur'an,maana yake ni kwamba qur'an yenyewe haina shida wala shaka

Ni tofauti na biblia ambayo leo kama kuna upotoshaji huwezi kuurekebisha au kuuona,ndio mnapata maneno kama Ayubu alimpiga Mungu mwereka au mtama

Lakini ukiacha tofauti ndogo ya neno moja au mawili ambayo yanatokana tafsir,bado huwezi kuta qur'an ina migongano kama biblia, kama kuna aya zina migongano naomba uzilete hapa

Ila mimi nakuwekea migongano ya biblia hapa;


1. Nasaba ya Yesu
- Mathayo 1:1-16 na Luka 3:23-38 zote zinaorodhesha nasaba ya Yesu, lakini majina mengi yanatofautiana, hasa kati ya Daudi hadi Yosefu.
- Mathayo: Yesu kupitia Mwana wa Daudi, Solomoni
- Luka: Yesu kupitia Mwana wa Daudi, Nathani

---

2. Idadi ya watu waliouawa na Daudi

  • 2 Samweli 24:1: Daudi aliwaagiza watu wahesabu Israeli – Mungu alikasirika.
  • 1 Mambo ya Nyakati 21:1: Shetani ndiye aliyemsukuma Daudi kufanya hivyo.

Mmoja anasema Mungu, mwingine anasema Shetani.

---

3. Tarehe ya kusulubiwa kwa Yesu

  • Marko 15:25: Yesu alisulubiwa saa tatu asubuhi.
  • Yohana 19:14-16: Yesu bado alikuwa hajasalibishwa saa sita (noon).

---

4. Je, Mungu hujaribu?

  • Yakobo 1:13: β€œMungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye hamjaribu mtu yeyote.”
  • Mwanzo 22:1: β€œBaada ya hayo Mungu alimjaribu Ibrahimu…”

---

5. Watu wangapi waliona kaburi la Yesu?
Mathayo 28:1
: Maria Magdalena na Maria mwingine.
- Yohana 20:1: Maria Magdalena peke yake.

1. Sheria ya Musa: Imebatilika au bado?

- Mathayo 5:17-18
Yesu alisema: β€œSikuja kuitangua torati bali kuitimiliza... hata nukta moja haitapita...”

- Wagalatia 3:13
β€œKristo alitukomboa na laana ya torati...”

- Warumi 6:14
β€œKwa maana hamko chini ya sheria, bali chini ya neema.”

Mkanganyiko:
Je, sheria bado inatumika au ilifutwa?

---

2. Imani au matendo huokoa?

- Warumi 3:28
β€œMwanadamu huhesabiwa haki kwa imani pasipo matendo ya sheria.”

- Yakobo 2:24
β€œMwaona ya kuwa mtu huhesabiwa haki kwa matendo, wala si kwa imani peke yake.”

---

3. Hakuna mtu mwema?

- Warumi 3:10
β€œHakuna mwenye haki, hata mmoja.”

- Luka 1:6
Zekaria na Elizabeti walikuwa waadilifu mbele za Mungu...

---

4. Je, Mungu huonekana?

- Yohana 1:18
β€œHakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wowote.”

- Kutoka 33:11
β€œBwana alikuwa akizungumza na Musa uso kwa uso...”

---

5. Yesu alijua kila kitu?

- Yohana 16:30
Wanafunzi walimwambia Yesu: β€œUnajua mambo yote...”

- Marko 13:32
Yesu alisema: β€œLakini juu ya siku ile au saa ile hakuna ajuaye, wala malaika... wala Mwana, ila Baba peke yake.”


Hapo unaona kabisa biblia imeenda chaka kimaana na taarifa tofauti


Ngoja nibreak down tena upate kuelewa nilimaanisha nini niliposema kwamba kuna stage nne za kutafsir qur'an

Sio kwamba unazipitia zote hizo laa! Bali kuna tafsir ambayo qur'an yenyewe inatoa ufafanuzi wa aya fulani

Pili anayetafsir atapata rejea kutoka kwenye hadith sahihi za Mtume,je Mtume swala aallahu alaih wasallamu alifafanua vipi jambo fulani

Anayetafsir qur'an atafanya rejea kwa Masahaba ambao walikuwa na Mtume na wakaelewa vizur aya hiyo

Kisha anaweza fanya rejea kwa tabiin ambao waliwakuta masahaba

Halafu kuna ijmaa ya wanazuoni wa kiislamu

Kwahiyo huyu mfasiri wa qur'an pamoja na kusoma fani ya kutafsir qur'an bado kama kuna sehemu itakuwa na mushkeli basi atapitia kati ya taratibu hizo

Hili sio jambo la ajabu,lau Biblia original ingekuwepo nanyi mngekutana na hali kama hizi


Sasa tuje je,tuna copy original ya qur'an?

Ndiyo hii misahafu ambayo tunayo leo ndio copy ya qur'an ile ile isipokuwa tu wakati qur'an inashuka haikuwa na harakaa [ nikimaanisha fatha,kasra na dhuma]

Na kwa wenye lugha yao hawahitaji hizo harakaa kwasababu wanajua vizur lugha yao

Jipange!
 
Kama umeanza kukimbia maswali mengine ni wazi hii mada inaenda kukushinda Tena vibaya sana ,biblia Haina migongano ila uelewa wako mdogo tu

Ndio maana nilisema dakika moja mbele ukibanwa utasema biblia Ina shida ,ila ukibanwa vizuri unaitumia kuthibitisha uislamu ulikuwepo kabla πŸ˜‚πŸ˜‚

Umeona jinsi ilivyovigumu kuutetea uislamu??

Ukisema Qur’an haijawahi kuguswa au kubadilika hata herufi, hiyo ni kauli ya imani si ya kihistoria.

Ukweli ni kwamba Qur’an inayosomwa leo duniani kote ni toleo la Cairo la mwaka 1924, lililochaguliwa na kamati ya Al-Azhar chini ya mfalme Fuad wa Misri na wahuni wachache.

Toleo hilo liliandaliwa kisiasa kwa nia ya kufuta machafuko ya usomaji yaliyokuwepo baina ya qira’at mbalimbali kama Hafs, Warsh, Qalun, na wengineo. Kwa hiyo, si sahihi kusema Qur’an leo ni ile ile ya Uthman au ya Muhammad.

Hata Saudia, Mekka, na Madina maeneo matakatifu ya Kiislamu wanatumia Mushaf wa Cairo, wala hawana β€œoriginal Qur’an” ya Uthman hadi leo.πŸ˜‚πŸ˜‚

Kwa msingi huo, hoja ya kwamba Qur’an haijabadilika haina uthibitisho wa kihistoria. Hakuna hata nakala moja ya Qur’an kutoka karne ya 7 iliyo kamili iliyoandikwa wakati wa Uthman au Muhammad. Kinachojulikana kama "Mushaf wa Uthman" kwenye makumbusho ya Tashkent au Istanbul ni vipande visivyo kamili, vimeandikwa kwa maandishi ya awali yasiyo na nukta wala alama za sauti.

Tafiti za kitaaluma, kama zile za Dr. Gerd Puin na Dan Brubaker, zimeonyesha tofauti nyingi katika maandiko ya kale zikihusisha kufutwa kwa maneno, kurekebishwa kwa aya, na hata kuongezwa au kupunguzwa kwa herufi kwa mkono wa binadamu.

Wakati unazungumzia tafsir na namna Qur’an inavyopaswa kueleweka kwa misingi ya hadith, masahaba, na tabiin, unathibitisha kuwa Qur’an haiwezi kujieleza yenyewe moja kwa moja, bali inategemea muktadha wa kihistoria na mitazamo ya wanadamu. Ikiwa Qur’an haikuandikwa kwa ufasaha wa kimaandishi wenye alama zote za kisarufi hadi karne kadhaa baadaye, na ikiwa wasomaji wake wanahitaji miongozo ya wanazuoni, basi tayari tunakubali kuwa kuna uwezekano wa tafsiri kupotoshwa au kutegemea mitazamo ya watu fulani. Na tafsir si Qur’an lakini tafsir ndizo zinazoelekeza namna ya kuiamini Qur’an.

Hili linaweka hatari kubwa ya uelewa kutegemea mapokeo na si maandiko yenyewe.

Waislamu wengi leo wanaambiwa kuwa Qur’an ni β€œcopy-paste” ya ile ya mbinguni, haijabadilika, na haijaguswa. Lakini wakifungua macho, wataona kuwa hadi leo kuna migogoro baina ya wanazuoni wa Kiislamu wenyewe juu ya namna Qur’an inapaswa kusomwa. Sheikh Mohammed Hijab, Yasir Qadhi na wanazuoni wengine wamewahi kukiri hadharani kuwa β€œkuna mashimo kwenye simulizi ya Qur’an ambayo hatuwezi kuyasema hadharani.” Hili ni pengo kubwa, na linawaumiza wale wanaotafuta ukweli badala ya mapokeo. Kwanini simulizi la Qur’an linahitaji kufichwa ikiwa ni la kweli?

Tofauti na Qur’an, Biblia ni maandiko ya kihistoria yaliyoandikwa na watu waliomshuhudia Yesu au waliokaribia enzi hizo. Ndiyo maana kuna tofauti kwenye simulizi, kwa sababu ni simulizi halisi za watu tofauti si toleo la kisiasa lililoandaliwa na kamati ya kifalme.

Biblia haiogopi kuwa na majina tofauti ya mababu wa Yesu, au mtazamo tofauti wa tukio hiyo inaonesha uhuru wa kihistoria, si mpangilio wa kimamlaka. Qur’an ya Cairo ilichaguliwa kwa kufuta matoleo mengine yote na ni toleo hilo moja ndilo linapewa mamlaka duniani kote leo.

Je, kama kweli Qur’an ni sahihi, kwanini matoleo mengine yalifutwa?

Kusema kwamba Qur’an haijaguswa ni kukwepa ukweli. Historia inathibitisha kuwa Qur’an iliandikwa miaka mingi baada ya Muhammad, ilikusanywa kwa vipande, haikuwa na harakaa wala nukta, na matoleo yake yalifutwa kisiasa ili kuipa mamlaka toleo moja tu. Hili linaficha ukweli kwa Waislamu wa kawaida – wanaoamini kile walichoambiwa, si kile historia inathibitisha. Ukweli hauogopi uchunguzi. Kama Qur’an ni ya kweli, basi ikabiliwe na historia, maandiko ya kale, na maswali ya msingi – bila kutumia vitisho, matusi au ukanushaji wa kihisia.

Nikuulize Tena, Je, Qur’an ya leo ni ile ile aliyoisoma Muhammad?

Ikiwa jibu lako linategemea toleo la Cairo la mwaka 1924, basi tayari ushahidi unaelekea kwenye ukweli tofauti na simulizi ya kidini unayotetea. Ukweli hauhitaji kujitetea unasimama
peke yake.
 
Expert wangu ni dhahir kwamba unachoamini wewe ndio sahihi,sasa kwenye mazingira kama haya huwa siwezi kuendelea kubishana,na siwezi kukufanya uamini maelezo yangu

Kama tutajadili vipengele vingine karibu,lau kama kwenye kipengele hichi ndio turufu yako ilipokaa,tuishie hapa!

Asante.
 
Kwahiyo nikubadilishie mada ?

Au tujadili utume wa Muhammad? Hivi mnathibitishaje utume wa Muhammad? Mnathibitishaje kuwa Muhammad ni kizazi cha Ishamael?
 
Karibu

Kwanza Waislamu ni watu wa haki,penye haki inasemwa haki,katika wakristo ambao huanzisha mijadala wewe ni mmoja kati ya watu ambao mnaleta challenge nzuri

Hujatumia matusi wala lugha mbaya,kongole kwako expert wangu

Pili,lengo la mjadala si kutafuta ushindi bali kubadilishana uelewa na kupeana challenge,tukiwa nalo hili in mind tutaenda sawa

Twende kazi, Muhammad ni uzao wa Ismai alayhi salaam,huyu alikuwa mtoto wa nabii Ibrahim

Ibrahim alikuwa na watoto wawili,na Ismail alikuwa hijaz/arabia


Muhammad swala aallahu alaih wassalamu,anatoka kwenye ukoo wa Ban Hashim kwenye kabila quraish,ambalo kwa mujibu wa historia linahusiana na kizazi cha Ismail
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ulitaka ashuke aje aanze kueneza yeye mwemyew kwa njia gani au apigane yeye na wanaadam ?? post yako haina ata mashiko nawee
Kwa hiyo hii reply yako ndo ina mashiko?
Mungu hahitaji kushuka mwenyewe na hahitaji wanadamu wamsaidie. Yeye ni kama alivyoumba vitu vingine, neno ni moja tu, "KUWA" na vitu vinatokea. Kwa hiyo ni kusema KUWA Kisha dini inakuwa kubwa Duniani kote. Umeelewa we kobazi!
 
Kuna kitu hujaelewa we kiazi πŸ˜‚... Sasa ukisema kuwa kila kitu kiwe na kina kuwa lengo la kupewa mtihan ni upi??? Itajulikanaje wanaopenda Dini na wasiopenda?? we kiazi sjui unaelewa πŸ˜‚ Sasa unataka kila kitu kiwe hashindwi kufanya kila mtu aanguke amsujudie saiv lkn ni kipimo anapima kila mtu kwsbb kila mmoja kapewa Freewill Brother kiazi
 
Sa we jamaa tulia m nkuulze , Lengo la kuletwa wewe Duniani ni lipi , kwann we clever( stupid,dumb) umeumbwa ??? Nijibu kupitia Dini yako sjui md ukristo au usukuma sijui we nijibu
 
Basi poa, twende polepole, kwa we jamaa unahisi Mungu anahitaji msaada wenu makobazi ili dini yake ienee? Basi Mungu wenu ni dhaifu.
 
Basi poa, twende polepole, kwa we jamaa unahisi Mungu anahitaji msaada wenu makobazi ili dini yake ienee? Basi Mungu wenu ni dhai

Hapana haitaji msaada , Ana uwezo wa kufanya kila mtu awe muislam kama walivo malaika sjui unaelewa , Malaika hawana cha muovu wala nn wao tayar ni kuabudu mwanzo mwisho .... Ila kwa sisi binadam Hii choice tumepewa au Freewill ya ww kuchagua uwe muovu au mwema huo ni mtihani. unapewa mtihan au tuseme majaribio ili ujulikane mwema nani na muovu nani

kwaiy Kumnusuru Allah ni mtihani/jaribio Je utamnusuru au utaamua ufanye ya kwako, Maake ata kumnusuru ni Ibada na tumeletwa kwajili ya ibada.

kwaiyo jibu summarized ni kwamba...Allah haitaji msaada wetu ana uwezo kwsbb kafanya pia malaika wamuabudu wote ila sisi ni kwasbb tumepewa freewill kwaiy tunajaribiwa je tutamnusuru???? apo kiazi umenielewa kichwa yako.
 
Ok ndugu, sasa tujadiliane kiheshima. Mtihani mwanadamu anapewa ili iweje?
 
Ok ndugu, sasa tujadiliane kiheshima. Mtihani mwanadamu anapewa ili iweje?
Mwanadam kwasisi waislam kwanz kaumbwa kwajili ya Kuabudu kwaiyo anapewa mitihani kupimwa je ni mfanya ibada kisawasawa?? au Wewe nd yule una bus lako limepata ajali kwa maana umepewa mtihani then unakimbilia kwa waganga na wakat ulimuomba huyo mungu akupe hilo Bus apo umeelewa
 
Mbona sioni jibu hapo, nimeuliza mtihani mwanadamu anapewa ili iweje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…