Je wajua kwamba Allah kwenye Quran anasema anahitaji kunusuriwa?

Je wajua kwamba Allah kwenye Quran anasema anahitaji kunusuriwa?

Chizi kivipi mkuu! Kutaka kujua Aya za Quran tukufu ya Allah na mtume wake Muhammad ni uchizi!? Acha kutukana Imani za watu mzeebaba
Kobaz hawataki hata kushauriwa wala kutumia akili za kdg kufikiri nje ya mavutabu yaliyoletwa kwenye majahazi, ukiwaambia wanakwita kafir wakati wao kwa 100% ndio hasa hasa wenyewe!!
 
Ungetuliza akili na kutaka kuelewa ungeelewa wala usingeona kama nachekesha.
Jamaa hapo juu niliyemjibu alisema maana ya hiyo aya ni kumtakia Rehema mtume. Ndo nikuhoji, Allah anamtakia Rehema mtume kutoka kwa nani? Yeye ndo mwenye hizo Rehema Kisha anamtakia mtume Rehema inaingia akilini hiyo? Yaani wewe una pesa kisha unamuombea mtu pesa kutoka kwako, sio kichekesho hicho?
Your grasp of things seems inaccurate and inconsistent with the name you claim to bear Mr. Clever.

Kwani nini maana ya rehma kwa muktadha wa hiyo aya? Maana yake ni Allah kumsifu mtume wake mbele ya malaika Wake.

Kusanya ufahamu wako ili uelewe vyema kwa kila kinachoandikwa. Kwa sababu si kila kinachoandikwa kinakuhusu, vingine vina wenyewe. Ikiwa kama mahali hujapaelewa ni vyema kuuliza kuliko kukosoa kwa kutaka kuonekana mjuaji kumbe unadhihirisha una ufahamu mzito kwa namna gani!
 
Ertugrul Bey nakusihii kasome Tena dini yako ,ni wazi huijui na kama unaijua basi umefundishwa uongo mwingi

Unapokuja kujadili na Mimi ,kwanza jipange ,

Hii hoja kwamba mitume wote walikuwa Waislamu kwa sababu walijinyenyekeza kwa Mungu mmoja ni dhaifu na ya kulazimisha, ni hoja ambayo hata kina Mazinge walishaiacha ,nimeshangaa wewe Bado umekaririshwa .

Hakuna ushahidi wowote wa kihistoria wala wa maandiko unaothibitisha kuwa dini ya Uislamu, kwa jina, mfumo na mafundisho yake (kama Shahada, Swala mara tano, Saumu Ramadhani, Hija, n.k), ilikuwepo kabla ya Muhammad katika karne ya 7 A.D. Wala hakuna maandiko ya Biblia yanayomwita Ibrahim, Musa au Yesu kuwa Waislamu. Hawa wote walikuwa Wayahudi, waliomwabudu Mungu kwa mujibu wa agano la kale, na Yesu akafundisha Agano Jipya.

Kujinyenyekeza kwa Mungu mmoja si kigezo cha kumfanya mtu kuwa Muislamu. Kama ni hivyo, basi hata Wakristo na Wayahudi wote ni Waislamu, jambo ambalo halikubaliki kiimani wala kihistoria. Yesu hakuwahi kufundisha Shahada ya Kiislamu, hakuswali kwa rakaa tano, wala hakufunga Ramadhani.

Hata Qur’an inasema wazi katika Surah Al-Ma’idah 5:3 kwamba

“Leo nimekukamilishieni dini yenu...”,

ikimaanisha kwamba Uislamu haukuwa umekamilika kabla ya Muhammad.

Kwa hiyo, kusema mitume wote walikuwa Waislamu ni tafsiri ya kulazimisha isiyo na msingi wa kweli. Ni sawa na kumpachika mtu uraia wa nchi ambayo haikuwepo wakati wake.
Expert wangu relux sawa, unazungumzia tu kunyenyekea lakini huzungumzii kufuata maamrisho yake na kuacha makatazo yake

Anyway tusitumie neno Uislamu maana naona linakutoa ufahamu unachanganyikiwa kabisa

Tuseme hivi utaratibu wa Mwenyezi Mungu toka awali ni mmoja,ni kushuhudiwa kwamba hapana apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mungu mmoja

Watu wajitenge na ushirikina kwa kuabudia miungu mingine au hata kumpa Mungu sifa ambazo hana kama kuwapa washirika katika Ufalme,kama vile utatu ambao mnampa

Hii ndio dini ya kweli kwa Mwenyezi Mungu Mmoja,kwahiyo acha kuanzia sasa kumshirikisha Mwenyezi Mungu ili uwe na mwisho mwema
 
Ok nakuelewa,
Kwani ni wapi mi nimetoa tafsiri yangu binafsi? Mi nimeleta mada kwa kusoma Quran yenu ambayo ipo kwa kiswahili. Sijaongeza chochote wala kupunguza,
Uelewa wako ni mdogo! Hili suala tangu awali nilishakujibu.

Wewe hujaleta tafsiri kwa lugha ya kiswahili! Wewe umeleta tarjuma.

Tarjuma ni kuhamisha Qur'an kutoka kwenye lugja ya kiarabu kupeleka kwenye lugha isiyo ya kiarabu.

Mfano:

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ

Tarjuma ya Kiswahili:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehma mwenye kurehemu.

Tafsiri yake ni nini? Maana ya hiyo aya ni nini?

Tafsiri yake ni, kwa jina la Mwenyezi Mungu mwenye kuneemesha wema na waovu duniani na mwenye kuneemesha wema pekee siku ya malipo.

Wewe hukuleta tafsiri, wewe ulileta tarjuma.
Kama ni watu tu ambao walikuta Quran tayari ipo na wakaamua tu kutafsiri kwa maoni yao, why tuwaamini bila kuhoji? Tafsiri ilibidi itolewe na mtume mwenyewe ila kama wanatoa watu ambao hata hawakuwa na ukaribu na mtume ni wazi kwamba wametafsiri kwa matakwa YaoYao
Uelewa wako ni mdogo zaidi.
Wapi nilipoandika kuwa wanatafsiri Qur'an wao wenyewe?

Nimekuambia elimu ya kiislamu ina sanad, ulimwengu mzima ndiyo ipo hivyo hivyo!

Na mlolongo wa mapokeo ya dini ynapokelewa kama yalivyotoka kwa Mtume kwenda kwa maswahaba, kwenda kwa wanafunzi wa maswahaba waliyotapakaa mpaka kufika kwetu.

Na kwa mlolongo huo nikakuambia Qur'an inatafsiriwa kwa nyenzo 3.
1)Qur'an bi Qur'an
2)Qur'an kwa sunna za Bw. Mtume
3) Qur'an kwa kupitia maswahaba ambao ni wanafunzi wa Mtume

Wapi nilipoandika Qur'an inatafsiriwa kwa uelewa wao?

Mbali na ufahamu wako mdogo, au najadiliana na mtu ambaye amelewa?
 
Your grasp of things seems inaccurate and inconsistent with the name you claim to bear Mr. Clever.

Kwani nini maana ya rehma kwa muktadha wa hiyo aya? Maana yake ni Allah kumsifu mtume wake mbele ya malaika Wake.

Kusanya ufahamu wako ili uelewe vyema kwa kila kinachoandikwa. Kwa sababu si kila kinachoandikwa kinakuhusu, vingine vina wenyewe. Ikiwa kama mahali hujapaelewa ni vyema kuuliza kuliko kukosoa kwa kutaka kuonekana mjuaji kumbe unadhihirisha una ufahamu mzito kwa namna gani!
Ok twende polepole ndugu,
Rehema ni nini?
 
Ok twende polepole ndugu,
Rehema ni nini?
Rehema ni nini kwa muktadha upi?

Kwa kiislamu neno linachambuliwa kilugha na kiistilahi.

Rehema ni nini kilugha? Au Rehema ni nini kiistilahi?
 
Uelewa wako ni mdogo! Hili suala tangu awali nilishakujibu.

Wewe hujaleta tafsiri kwa lugha ya kiswahili! Wewe umeleta tarjuma.

Tarjuma ni kuhamisha Qur'an kutoka kwenye lugja ya kiarabu kupeleka kwenye lugha isiyo ya kiarabu.

Mfano:

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ

Tarjuma ya Kiswahili:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehma mwenye kurehemu.

Tafsiri yake ni nini? Maana ya hiyo aya ni nini?

Tafsiri yake ni, kwa jina la Mwenyezi Mungu mwenye kuneemesha wema na waovu duniani na mwenye kuneemesha wema pekee siku ya malipo.

Wewe hukuleta tafsiri, wewe ulileta tarjuma.

Uelewa wako ni mdogo zaidi.
Wapi nilipoandika kuwa wanatafsiri Qur'an wao wenyewe?

Nimekuambia elimu ya kiislamu ina sanad, ulimwengu mzima ndiyo ipo hivyo hivyo!

Na mlolongo wa mapokeo ya dini ynapokelewa kama yalivyotoka kwa Mtume kwenda kwa maswahaba, kwenda kwa wanafunzi wa maswahaba waliyotapakaa mpaka kufika kwetu.

Na kwa mlolongo huo nikakuambia Qur'an inatafsiriwa kwa nyenzo 3.
1)Qur'an bi Qur'an
2)Qur'an kwa sunna za Bw. Mtume
3) Qur'an kwa kupitia maswahaba ambao ni wanafunzi wa Mtume

Wapi nilipoandika Qur'an inatafsiriwa kwa uelewa wao?

Mbali na ufahamu wako mdogo, au najadiliana na mtu ambaye amelewa?
Mzeebaba unaweza kujadili kwa amani au huwezi?
Weka uelewa wako wa jinsi umeelewa hii mada ili tujadiliane kulingana na maelezo yako. Kama huwezi kuleta uelewa wako leta maoni ya hao unaowaamini ili tuendelee na mada. Naona umekazania uelewa wangu mdogo, ndo nipo hapa kuukuza uwe makubwa kwa hiyo tuvumiliane.
NB. Inawezekana umetoa maoni yako kuhusu unavyoielewa hii Aya, naomba nikumbushe.
 
Wewe si muislamu na hujaisoma hii dini!

Sisi ni waislamu na tumeisoma hii dini!

Ajabu wewe ambaye si muislamu na hujaisoma hii dini unaona mtazamo wako upo sahihi juu ya masuala ya elimu yahusiyo dini ya uislam.

Jipime wewe mwenyewe, tukufafanuaje?
 
Mimi nazungumza kulingana na nilivyoelewa, wewe ndo muislam mwenye kuzifata hizo Aya, utakachokifanya ni kunielekeza kulingana na Imani yenu ilivyo.

Kinachobaki ni mimi kuamini maelezo yako au kubaki na jinsi nilivyoelewa.
Na wala sitataka Aya ieleweke na wengine kulingana na maoni yangu.

Sasa, nadhani maoni yangu umeyaona, nipe maelezo ya Imani yako unayoyaamini
 
Ndugu Uislamu sio dini ya amani huo ni UPOTOSHAJI ,umetoa maelezo ya uongo ,

hoja yako kwamba Waislamu hawakupigana bila sababu ni upotoshaji mkubwa ,labda unadhani hatuujui uislamu ,binafsi nimezaliwa kwenye uislamu,nimesoma uislamu,kwahiyo naongea ninachokijua,kwa sababu historia na Qur’an yenyewe zinaonyesha kwamba si kila vita ilikuwa ya kujilinda kama unavyosema ,

Kwa mfano, vita ya Khaybar, Banu Qurayza, na vita zingine nyingi zilikuwa ni za kushambulia na kueneza Uislamu kwa nguvu jambo linalopingana moja kwa moja na dhana ya AMANI unayosema hapa ..

Tukirudi kwenye Qur’an, kuna Aya nyingi ambazo hazihusu kujilinda bali zinachochea mashambulizi ya wazi. Mfano nitakupa Aya kadhaa hapa👇👇

Surah At-Tawbah 9:29
"Piganeni na wale wasioamini katika Mwenyezi Mungu... mpaka walipe kodi kwa unyenyekevu nao wakiwa wanyonge."

Hii ni amri ya wazi ya kushambulia wasiokuwa Waislamu na kuwafanya kuwa chini ya utawala wa Kiislamu kwa kulipa Jizya si kwa kujilinda, bali kwa kutawala.

Surah Muhammad 47:4
"Basi mnapokutana na wale waliokufuru wapigeni shingoni mwao..."

Hii pia si hoja ya kujilinda, bali ni amri ya vita dhidi ya wasiokuwa Waislamu kwa sababu tu ya imani yao.

Hata mtume wenu Muhammad alikiri kwamba ametumwa kwa upanga.

Tafsiri za hadithi maarufu zinaeleza

Sahih al-Bukhari (Hadith 2948)
"Nimeamrishwa nipigane na watu mpaka washuhudie kwamba hakuna mungu ila Allah..."
Hii inapingana na hoja yako ya kwamba vita zilikuwa kwa kujilinda tu.

Viongozi wengi wa Kiislamu baada ya Muhammad waliendeleza utawala wa upanga: Mashambulizi dhidi ya Uajemi, Byzantine, India, Afrika Kaskazini haya yote hayakuwa kujilinda, bali ni kueneza Uislamu kwa nguvu. Hilo linaelezwa hata na wanazuoni wa Kiislamu kama Ibn Khaldun aliyekiri kuwa jihadi ni njia halali ya kueneza dini kwa mujibu wa Sharia.

Na kuhusu hoja kwamba “Mitume wote walikataliwa,” ni kweli walikumbana na upinzani, lakini hakuna kati yao aliyepiga vita kwa ajili ya kueneza ujumbe wake kama Muhammad alivyoagiza.

Yesu alisema

“Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi...” (Mathayo 5:44)

Yesu alikataa kutumia upanga (Mathayo 26:52), tofauti na Muhammad ambaye alisema:
"Nimekuja kwa upanga." (Ibn Sa’d, Kitab al-Tabaqat al-Kabir)

Kwa hiyo si kweli kwamba Uislamu ni dini ya amani .

Uislamu unaruhusu mapigano ya kimwili kwa sababu ya dini jambo linalotofautiana na mafundisho ya injili ya upendo, msamaha, na kuvumilia mateso.
Kuzaliwa katika uislamu sio hoja,kuna waislamu wengi wana majina ya kiislamu lkn hawajui uislamu wao

Mmoja wapo ni wewe,lau ungeujua Uislamu usingekuwa kafiri abadani kwakuwa unajua kabisa yeyote anayemshirikisha Allah ni motoni,kwahiyo huna unachokijua katika Uislamu

Uuslamu ni dini ya amani sana ila makafiri wametengeneza propaganda nyingi sana juu ya hoja hii matokeo yake wote nyie mmeingia kwenye mfumo na kuimba wimbo ule ule

Mtume Muhammad swalla aallahu alaih wasallamu,kabla ya kupigana vita yoyote ile kwanza alifanya mazungumzo mengi sana juu ya kutafuta suluhu na kuepuka vita

Ukichukulia kwanza wengi ambao walikuwa ni washirikina walikuwa ndugu na wale ambao wameukubali Uislamu,kwahiyo zilifanyika juhudi nyingi sana,pale zilipo shindikana ndio vita vikachukua nafasi

Mfano mzuri ni mkataba wa Udaibiyah,hawa Mtume na wafuasi wake walikuwa wanaenda kuhiji Makka pasina silaha zozote zile,walienda kwa amani,sasa washirikina wa Makka waliposikia Muhammad anaongozana na msafara mkubwa kwenda Makka,basi wakataka kuwazuia wasiingie Makka au walitaka vita

Lakini Muhammad swalla aallahu alaih wasallamu alisema wanaenda kwa amani,ndio mkataba ukafungwa,lkn mkataba huu haukuwa na maslahi yoyote na waislamu

Moja wapo ya vipengele ni kwamba,mshirikina akienda Madina basi arudishwe Makka kwa watu wake,lakini muislamu akienda Makka asirudishwe

Kufupisha story kuna vipengele vingi sana viliwapa favor washirikina na kuwabana waislamu

Ikafikia kipindi masahaba wakataka kupigana vita,lakni Mtume akakubali akakubali mkataba wa upande mmoja lengo ni kuepusha vita

Kuna masahaba wa Mtume walienda kwenye kabila moja kwa amani kabisa kuutangaza uislamu,lkn wale masahaba 70 wote waliuwawa,je kwa hali hiyo ungetegemea waislamu wachukue hatua gani kama sio kulipiza kisasi

Vita nyingine hazikuwa vita hasa bali ni mbinu za kivita kuwazunguka maadui,kuna makabila ambayo yalileta uasi kwenye dola ya kiislamu,waislamu walichofanya ni kwenye kuwazingira kwa masiku kadhaa mpaka wakaomba poo

Kwahiyo hizo zinazo itwa vita kwa asilimia kubwa zilikuwa ni kuzuia au kuweka mambo sawa baada ya waasi kutaka kupima nguvu ya waislamu

Na kwa taarifa yako,kihistoria waarabu walikuwa wako proud sana na historia yao ya vita hata kabla ya Uislamu kuenea kwa wingi,mtu anaweza kuhadithia ushindi wa vita flani ambazo babu zake walishinda miaka kadhaa huko nyuma,kwahiyo matokeo historia ya bara arabu imejaa visa vingi vya mambo ya vita na watu kwa bahati mbaya wakahusisha vita hizo na Uislamu

Waislamu walieneza dini yao kwa amani ikiwemo kupewa hoja ambazo ziliwaingia kwenye nyoyo zao na wenyewe kwa hiari yao wakaingia katika Uislamu

Mfano mzuri baada ya waislamu kuiteka Hagia Sofia,watu waliachwa huru kuabudu dini zao wakiwemo wakristo,ikafikia kipindi watu waliwapenda zaidi waislamu kuliko hata Waroma,kwakuwa katika Uislamu kuna haki

Uislamu unatufundisha kutenda haki hata ikiwa dhidi ya ndugu yako mwenyewe

Angalia aya zifuatazo:

Katika Uislamu, kutenda haki ni jambo kuu sana. Qur’an inaagiza waislamu watende haki hata kama ni dhidi yao wenyewe au ndugu zao. Hizi ni aya muhimu kuhusu haki (uadilifu):

---

1. Surat An-Nisa (4:135):
"Enyi mlioamini! Kuweni wasimamizi wa haki, mkitoa ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, ijapokuwa ni kinyume na nafsi zenu au wazazi wawili au jamaa wa karibu..."

Aya hii inasisitiza kuwa haki haipaswi kupindishwa kwa upendeleo wa familia au maslahi binafsi.

---

2. Surat Al-Ma’idah (5:8):
"Enyi mlioamini! Kuweni wasimamizi wa Mwenyezi Mungu kwa ushuhuda wa haki. Wala chuki ya watu isiwakupelekeeni kutokutenda haki. Tendeni haki; hiyo ndiyo karibu na uchamungu..."

Hata kama mnamchukia mtu, bado ni wajibu kutenda haki.

---

3. Surat An-Nahl (16:90):
"Hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha uadilifu, ihsani, na kuwapa jamaa..."

Aya hii hutajwa sana katika khutuba za Ijumaa, ikisisitiza kwamba uadilifu ni msingi wa amri za Mwenyezi Mungu.

---

Hitimisho:
Katika Uislamu, uadilifu ni msingi wa imani. Muislamu anatakiwa kuwa na mizani ya haki daima, bila upendeleo wala uonevu – iwe kwa ndugu, marafiki au maadui.

Je,ukristo unasemaje kuhusu Upanga:

1. Mathayo 10:34
"Msidhani ya kuwa nimekuja kuleta amani duniani; la, sikukuja kuleta amani, bali upanga."

2. Luka 22:36
"Basi akawaambia, lakini sasa, yeye aliye na mfuko, na auchukue, na vivyo hivyo mkoba; na yeye asiye na upanga, na auze joho lake, akanunue upanga."

Jipange expert wangu!
 
Muda wa porojo haupo ndugu, jikite kwenye hoja na mada

Sikutumia ISIS kama kipimo cha Uislamu mzima, bali nilisema wazi kuwa vitendo vyao vinaendana moja kwa moja na baadhi ya Aya na Hadith za Kiislamu. Wao hawatungi sheria, wanatekeleza zilizoandikwa. Mfano:

Qur’an 9:5
"Waue washirikina popote mnapowakuta..."

Qur’an 8:12
"Nitatie hofu katika nyoyo za waliokufuru, wapigeni juu ya shingo..."

Sahih Muslim 1:33
"Nimeamrishwa nipigane na watu mpaka washuhudie kuwa hakuna mungu ila Allah..."

Sasa swali ni Je, ISIS walitunga aya hizi au wanazitekeleza?

Hata viongozi wa ISIS wamesema,

"Tunaleta Khilafa kwa kufuata Qur’an na Sunnah za Muhammad."

Hii haimaanishi kila Muislamu ni gaidi lakini inamaanisha maandiko yao yanaruhusu au hata kuamuru vitendo vya kimabavu dhidi ya wasioamini, na mtu yeyote anayetaka kuchukua maandiko hayo kwa usomaji wa moja kwa moja (literal interpretation) ataishia kama ISIS.

Hata wewe ukiyatumia maandiko vizuri ya Quran na hadithi lazima uwe GAIDI
Aya hizo ulizo zitaja hazija agiza tu watu wapigane vita bila sababu,bali vita vilipiganwa katika kuondoa dhuluma,kuweka uadilifu katika jamii,na kusimamisha haki

Uislamu upo kwa maslahi ya jamii nzima,pale panapokuwa na uonevu wa namna yoyote basi hatua zilihitajika kuweka mambo sawa

Waislamu walipigana na wale ambao walistahili kupigwa

Vile vile madhara waliyofanyiwa waislamu na wazushi wanatakiwa warudishe madhara yale yale kama waliyofanyiwa

Vile vile Mwenyezi Mungu hapendi wale wanao anzisha vita

Tusome aya zifuatazo:

Katika Qur’an, kuna aya zinazoruhusu Waislamu kujilinda dhidi ya dhulma, lakini pia zinasisitiza kujizuia, kusamehe, au kulipa kwa uadilifu. Hapa ni baadhi ya aya husika:

1. Surat Al-Baqarah (2:190)
“Piganeni katika njia ya Mwenyezi Mungu na wale wanaowapiga, lakini msianze uadui. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wanaoanzisha vita.”

2. Surat Al-Baqarah (2:194)
“... Basi anaye kudhuru, mdhuru sawa na alivyo kudhuru...”

3. Surat Ash-Shura (42:40)
“Na kisasi cha uovu ni uovu kama huo. Lakini anayesamehe na kusuluhisha, basi thawabu yake iko kwa Mwenyezi Mungu...”

4. Surat Al-Hajj (22:39)
“Wameruhusiwa kupigana wale wanaodhulumiwa, na hakika Mwenyezi Mungu anao uwezo wa kuwasaidia.”

Aya hizi zinaweka mizani ya uadilifu: Waislamu wanaruhusiwa kujilinda dhidi ya mashambulizi, lakini hawapaswi kuvuka mipaka, na kusamehe kunapendekezwa zaidi.

Sasa tuje tuangalie njia za kupigana vita, Vita ambazo waislamu walikuwa wanapigana zilikuwa kwa wale tu wenye kushika silaha,lakini haikuruhusiwa kuwapiga wazee,wanawake na watoto

Vile vile haikupaswa kuharibu mazao,majumba ya ibada

Lakini je ISIS wanafanya hivyo? Utakuta hao ni magaidi wanapigana kwa kivuli cha Uislamu lakini nyuma yake ni wahalifu kama wahalifu wengine

jipange expert wangu

Kesho inshaAllah tutaendelea na mjadala

Asante
 
Ok nitakujibu kadri nilivyojaaliwa ,

Kwanza Qur’an 9:5 inasema wazi kuwa "waue washirikina popote muwakutapo," siyo kwa kujilinda bali kushambulia kwa msingi wa imani.,

Nadhani huujui uislamu vizuri ,labda kama hizo Aya huzijui

Qur’an 9:29 pia inaagiza kupigana na wasiomuamini Allah hadi walipe jizya kwa unyenyekevu. Hii ni vita ya kulazimisha utawala wa kidini, si kujilinda.

Unaposema vita vya Kiislamu havikuhusisha raia, historia ya Banu Qurayza inathibitisha vinginevyo. Wanaume zaidi ya 600 waliuawa na wanawake na watoto kuchukuliwa utumwani. Pia baada ya Muhammad kufa, makabila yaliyokataa mamlaka ya Kiislamu yalishambuliwa kwenye vita vya Ridda. Haya si mashambulizi ya kujilinda, bali ya kulazimisha utii wa kisiasa na kidini.

Vilevile, kabla ya vita vya Badri, Muhammad mwenyewe alivamia misafara ya Waquraysh akilenga kuvuruga uchumi wao.

Hii inaonesha kuwa Uislamu ulianza kupanuka kwa silaha, si tu kwa hoja au mazungumzo ya amani.

Kwa suala la ISIS, kusema hawana uhusiano na Uislamu si sahihi. Wanatumia aya zile zile za Qur’an kuhusu kupigana, jizya na kushambulia wasio Waislamu. Ikiwa wana misingi ya kisheria na kijihadi kutoka kwenye Qur’an na hadith, si sahihi kuwatafutia uhalali wa nje wa kuwa si Waislamu.

Hoja ya kulipiza madhara kama ulivyofanyiwa pia inakinzana na mafundisho ya Yesu Kristo, aliyefundisha kumpenda adui na kusamehe. Ukristo una mwelekeo wa msamaha, si kulipiza kisasi.

Uislamu unapendekeza kisasi kama haki lakini Kristo alisema tusilipize.

Na kuhusu Uislamu kuwa dini ya amani, historia haithibitishi hilo. Kuanzia Hispania hadi India, kutoka Afrika Kaskazini hadi Balkans, Uislamu ulienea kwa vita vya silaha. Hii si chuki, bali ni historia halisi. Tuwe wa kweli kwa kusoma maandiko na historia kwa pamoja.

Ni wazi Bado huujui uislamu
 
Kuzaliwa katika uislamu sio hoja,kuna waislamu wengi wana majina ya kiislamu lkn hawajui uislamu wao

Mmoja wapo ni wewe,lau ungeujua Uislamu usingekuwa kafiri abadani kwakuwa unajua kabisa yeyote anayemshirikisha Allah ni motoni,kwahiyo huna unachokijua katika Uislamu

Uuslamu ni dini ya amani sana ila makafiri wametengeneza propaganda nyingi sana juu ya hoja hii matokeo yake wote nyie mmeingia kwenye mfumo na kuimba wimbo ule ule

Mtume Muhammad swalla aallahu alaih wasallamu,kabla ya kupigana vita yoyote ile kwanza alifanya mazungumzo mengi sana juu ya kutafuta suluhu na kuepuka vita

Ukichukulia kwanza wengi ambao walikuwa ni washirikina walikuwa ndugu na wale ambao wameukubali Uislamu,kwahiyo zilifanyika juhudi nyingi sana,pale zilipo shindikana ndio vita vikachukua nafasi

Mfano mzuri ni mkataba wa Udaibiyah,hawa Mtume na wafuasi wake walikuwa wanaenda kuhiji Makka pasina silaha zozote zile,walienda kwa amani,sasa washirikina wa Makka waliposikia Muhammad anaongozana na msafara mkubwa kwenda Makka,basi wakataka kuwazuia wasiingie Makka au walitaka vita

Lakini Muhammad swalla aallahu alaih wasallamu alisema wanaenda kwa amani,ndio mkataba ukafungwa,lkn mkataba huu haukuwa na maslahi yoyote na waislamu

Moja wapo ya vipengele ni kwamba,mshirikina akienda Madina basi arudishwe Makka kwa watu wake,lakini muislamu akienda Makka asirudishwe

Kufupisha story kuna vipengele vingi sana viliwapa favor washirikina na kuwabana waislamu

Ikafikia kipindi masahaba wakataka kupigana vita,lakni Mtume akakubali akakubali mkataba wa upande mmoja lengo ni kuepusha vita

Kuna masahaba wa Mtume walienda kwenye kabila moja kwa amani kabisa kuutangaza uislamu,lkn wale masahaba 70 wote waliuwawa,je kwa hali hiyo ungetegemea waislamu wachukue hatua gani kama sio kulipiza kisasi

Vita nyingine hazikuwa vita hasa bali ni mbinu za kivita kuwazunguka maadui,kuna makabila ambayo yalileta uasi kwenye dola ya kiislamu,waislamu walichofanya ni kwenye kuwazingira kwa masiku kadhaa mpaka wakaomba poo

Kwahiyo hizo zinazo itwa vita kwa asilimia kubwa zilikuwa ni kuzuia au kuweka mambo sawa baada ya waasi kutaka kupima nguvu ya waislamu

Na kwa taarifa yako,kihistoria waarabu walikuwa wako proud sana na historia yao ya vita hata kabla ya Uislamu kuenea kwa wingi,mtu anaweza kuhadithia ushindi wa vita flani ambazo babu zake walishinda miaka kadhaa huko nyuma,kwahiyo matokeo historia ya bara arabu imejaa visa vingi vya mambo ya vita na watu kwa bahati mbaya wakahusisha vita hizo na Uislamu

Waislamu walieneza dini yao kwa amani ikiwemo kupewa hoja ambazo ziliwaingia kwenye nyoyo zao na wenyewe kwa hiari yao wakaingia katika Uislamu

Mfano mzuri baada ya waislamu kuiteka Hagia Sofia,watu waliachwa huru kuabudu dini zao wakiwemo wakristo,ikafikia kipindi watu waliwapenda zaidi waislamu kuliko hata Waroma,kwakuwa katika Uislamu kuna haki

Uislamu unatufundisha kutenda haki hata ikiwa dhidi ya ndugu yako mwenyewe

Angalia aya zifuatazo:

Katika Uislamu, kutenda haki ni jambo kuu sana. Qur’an inaagiza waislamu watende haki hata kama ni dhidi yao wenyewe au ndugu zao. Hizi ni aya muhimu kuhusu haki (uadilifu):

---

1. Surat An-Nisa (4:135):
"Enyi mlioamini! Kuweni wasimamizi wa haki, mkitoa ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, ijapokuwa ni kinyume na nafsi zenu au wazazi wawili au jamaa wa karibu..."

---

2. Surat Al-Ma’idah (5:8):
"Enyi mlioamini! Kuweni wasimamizi wa Mwenyezi Mungu kwa ushuhuda wa haki. Wala chuki ya watu isiwakupelekeeni kutokutenda haki. Tendeni haki; hiyo ndiyo karibu na uchamungu..."

---

3. Surat An-Nahl (16:90):
"Hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha uadilifu, ihsani, na kuwapa jamaa..."

---

Hitimisho:
Katika Uislamu, uadilifu ni msingi wa imani. Muislamu anatakiwa kuwa na mizani ya haki daima, bila upendeleo wala uonevu – iwe kwa ndugu, marafiki au maadui.

Je,ukristo unasemaje kuhusu Upanga:

1. Mathayo 10:34
"Msidhani ya kuwa nimekuja kuleta amani duniani; la, sikukuja kuleta amani, bali upanga."

2. Luka 22:36
"Basi akawaambia, lakini sasa, yeye aliye na mfuko, na auchukue, na vivyo hivyo mkoba; na yeye asiye na upanga, na auze joho lake, akanunue upanga."

Jipange expert wangu!
Ndugu yangu unachanganya propaganda na ukweli uliopo, naimani na nitakuombea utoke kwenye uislamu umpokee Yesu kama Bwana na mwokozi wa MAISHA yako.

Kwanza si kila anayeitwa Muislamu anakuwa na uelewa wa kweli, na wala si sahihi kusema eti mtu akijua Qur’an hawezi kuwa kafiri.

Hata wasomi wa Kiislamu kama Ali Dashti, Ibn Warraq na Tarek Fatah waliichunguza Qur’an kwa kina na wakaiacha kwa hoja.,hao ni baadhi ,wewe kwa maelezo yako Bado maamuma

Hii inathibitisha kuwa uelewa wa Uislamu unaweza kabisa kumpeleka mtu kuachana na uislamu.

Kuhusu amani ya Uislamu, si kila simulizi ni sahihi. Mikataba kama wa Hudaibiyah ulifanywa si kwa sababu ya mapenzi ya amani, bali kwa sababu ya udhaifu wa kijeshi.,kasome historia vizuri ,

Baada ya miaka miwili, mkataba huo ulivunjwa na Muhammad mwenyewe, kisha akashambulia Makka,sijui kama Unajua hili jambo,Hii inaonyesha kwamba mazungumzo yalitumika tu kama mbinu ya kujipanga kivita si kwa misingi ya amani ya kweli.

Vita vya Waislamu si vya kujilinda tu. Waislamu waliua masahaba 70 waliotumwa kwa kabila kwa madai ya ulinganiaji, lakini hiyo haifanyi kisasi kuwa haki. Yesu alifundisha kusamehe, si kulipiza. Haki ya kweli si kulipa madhara bali kuzuia chuki izae tena.

Kuhusu mbinu za kivita, historia inaonyesha kuwa Uislamu ulienezwa kwa nguvu,Soma historia mbona ipo wazi, kutoka Arabia hadi Hispania, India, na Afrika. Hakuna uthibitisho wa watu kuingia kwa wingi kwenye Uislamu kwa hoja tu bila hofu au shinikizo. Hakuna ushahidi wa kihistoria kwamba watu waliwapenda Waarabu kuliko Wamishenari ,

Aya unazotaja kuhusu haki (An-Nisa 4:135, Al-Ma’ida 5:8, An-Nahl 16:90) ni nzuri kwa maandishi lakini historia ya Uislamu haijaonyesha uadilifu huo kwa wale wasiokuwa Waislamu.

Wasio waislamu walitakiwa kulipa jizya, na walidhalilishwa kwa mfumo wa daraja la chini katika jamii za Kiislamu. Uislamu unasema msiwe na chuki lakini Qur’an hiyo hiyo inaruhusu kupigana na washirikina hata kama hawakuanzisha vita (Q 9:5, Q 9:29).,Au huzijui hizi Aya ?

Kuhusu Mathayo 10:34 na Luka 22:36, unakosea kwa kuzinukuu bila muktadha. ,Kwanza huoni aibu kupotosha hizo Aya ??

Yesu alisema hivyo kwa mfano wa mgawanyiko wa kiroho, si mapanga ya damu. Hakuna mahali Yesu alianzisha jeshi, alivamia mji, au kuua mtu yeyote kwa sababu ya imani tofauti.,kama una ushahidi huo nipe.

Hii ndiyo tofauti kuu kati ya Kristo na Muhammad mmoja alitoa uhai wake, mwingine alitoa uhai wa wengine.

Ukweli hauhitaji kupakwa rangi ya propaganda. Historia na maandiko yanazungumza wazi. Uislamu unaweza kuwa na mafundisho mazuri ya maandiko baadhi ili kuhadaa watu , lakini historia yake imejaa mapambano ya kisiasa, upanuzi kwa nguvu, na utawala wa kiimla kwa jina la dini.

Hata Leo nchi za kiislamu,Wakristo wanauliwa ,hakuna uhuru wa dini nyingine

Lakini tunadanganywa Uislamu ni dini ya amani 😂😂
 
Nitaendelea kukujibu kadri ninavyoweza ,maana ni wazi waislamu hamtaki kutoka nje ya box ,hamtaki Kuhoji Imani yenu kuona kwanini imekuwa hivi na sio vile ,

Jitahidi kusoma historia ,AKIOLOJIA na maandiko kabla ya kuja uislamu,uzuri hata Quran imewaambia msome kwa wale waliopewa kitabu kabla yenu

Kaka, kusema kuwa kukubali uumbaji wa Mungu ni sawa na kuwa Muislamu si hoja inayojitosheleza. Maana kila mwanadamu anayekubali kuwa kuna Muumba hajawa Muislamu moja kwa moja. Wakristo, Wayahudi, na hata dini za jadi pia wanakubali kuwa Mungu yupo na ndiye Muumba, lakini hawaitwi Waislamu.

Kuwa Muislamu ni zaidi ya kukubali uumbaji ni kukubali mafundisho ya Muhammad na Qur’an kuwa ndiyo njia sahihi ya kumfikia Mungu, jambo ambalo si kila mtu anakubaliana nalo.

Kuhusu Iblis kukataa kumsujudia Adam kwa sababu ya kiburi, hiyo hadithi imo ndani ya Qur’an na inafanana na simulizi za kale za Kiyahudi (Midrash). Lakini hata hivyo, inaibua maswali mengi fikirishi ,

Kama kusujudu ni kwa Allah peke yake, kwa nini Allah mwenyewe aagize viumbe wamsujudie kiumbe mwingine, hata kama ni kwa “heshima”?

Hii inazua mkanganyiko kuhusu maadili ya kiungu kwani Mungu angeagiza jambo linalochanganya ibada na heshima?

Na kama Iblis alihukumiwa kwa sababu ya kukataa agizo hilo, je, adhabu hiyo ni kwa sababu ya uasi au kwa sababu alitumia akili kufikiri tofauti? Hii inafanya mtu ajiulize je, imani ya kweli inahitaji kufuata kila agizo bila kuuliza, au inahitaji kuelewa kiini cha agizo hilo?

Kwa hiyo, hoja ya kwamba kujisalimisha kwa uumbaji ni sawa na kuwa Muislamu, au kwamba Iblis alikosea kwa kukataa “sujudu ya heshima,” si hoja yenye nguvu ya kiakili wala ya kiroho. Ukweli unapatikana si kwa kufuata simulizi, bali kwa kumjua Mungu aliye Hai, ambaye alijifunua kwa ulimwengu kupitia Yesu Kristo.
Huwa unapenda sana kutilia mkazo wa kufuata historia na maandiko ya huko zamani,waandishi wengi ni makafir kama wewe,ambao waliandika kwa lengo la kuuchafua Uislamu na waislamu,na ambao rejea zao ndio zinawapotosha wengi sana ukiwemo na wewe,halafu unakuja hapa kifua mbele kana kwamba unayosema ni sahihi

Sisi tunazijua hizo propaganda zao na hatuwezi kuzichukua kama rejea za kupata maarifa,hizo ni kwa ajili yenu

Huwa nafurajishwa sana mkristo anapojifanya anatumia hoja za akili wakati yeye mwenyewe ameshindwa kutumia hoja ya akili katika dini yake

Mfano,kuamini kwamba Mungu alijibadilisha katika umbo la kibina damu ili aje ateswe na kuwakomboa wanadamu katika dhambi, huu ni upuuzi wa hali ya juu sana,kama umeshindwa kutumia akili hapa,je utaweza kutumia akili sehemu nyingine?

Kama unaamini Mungu kazaliwa na mwanamke na akakaa tumboni miezi tisa,akaja kuwa fundi selemala na baadae kuwaambia watu kuwa yeye ni Mungu,mtu anayeamini haya ana uwezo gani wa kutumia akili yake?

Anyway twende kazi, nakufundisha ujue tofauti ya jambo la kiibada na jamba ambalo sio kiibada

Ibada ni matendo au maneno mazuri ambayo anayapenda Mwenyezi Mungu,na haya yana malipo kutoka kwake

Kwahiyo Kusujudu kama ibada ni kwa ajili ya Allah tu

Wakati Allah anataka kumuumba mwanaadamu aliwaambia Malaika kwamba nataka kumuumba hiki kiumbe,wao Malaika wakasema "unataka kumuumba kiumbe kingine ambacho kitakuja kumwaga damu na ufisadi"

Allah akasema "mimi nayajua msiyoyajua nyinyi"

Baada ya uumbwaji wa adamu, Allah subhaanahu wa Taala akawauliza malaika wataje majina ya vitu vyote,wao wakashindwa

Alipoulizwa Adamu akataja majina ya vitu vyote,ndio hapo Allah akaagiza Malaika na Iblis wamsujidie Adam sijida ya heshima

Sasa Iblis alikaidi amri ya Mola wake,ndio akahukumiwa motoni kwasababu ya kuonyesha kiburi mbele ya Allah

Na hata pale Iblis alipo wahadaa Adam na Hawa kule bustanini, Adam aliomba msamaha kwa Mola wake na akasamehewa lakini Iblis hakuomba msamaha,hii inaonyesha ni tabia yake ya kiburi

Na Allah ndio mwenye kujua yote,alijua hiki kiumbe ni kikaidi na hakitobadilika

Unasema ulikuwa Muislamu,unajivua nguo mwenyewe,lau ungekuwa usingeuliza swala hili

Na hii sijida ya heshima hata wazazi wake nabii Yusuphu waliifanya kwa Yusuphu pale walipo mkuta Yusuphu akiwa na mamlaka nchini Misri

Baada ya uumbwaji wa adamu, Allah subhaanahu wa Taala akawauliza malaika wataje majina ya vitu vyote,wao wakashinda

Alipoulizwa Adamu akataja majina ya vitu vyote,ndio hapo Allah akaagiza Malaika na Iblis wamsujidie Adam sijida ya heshima

Sasa Iblis alikaidi amri ya Mola wake,ndio akahukumiwa motoni kwasababu ya kuonyesha kiburi mbele ya Allah

Na hata pale Iblis alipo wahadaa Adam na Hawa kule bustanini, Adam aliomba msamaha kwa Mola wake na akasamehewa lakini Iblis hakuomba msamaha,hii inaonyesha ni tabia yake ya kiburi

Na Allah ndio mwenye kujua yote,alijua hiki kiumbe ni kikaidi na hakitobadilika

Unasema ulikuwa Muislamu,unajivua nguo mwenyewe,lau ungekuwa usingeuliza swala hili

Na hii sijida ya heshima hata wazazi wake nabii Yusuphu waliifanya kwa Yusuphu pale walipo mkuta Yusuphu akiwa na mamlaka nchini Misri

jipange expert wangu
Ndugu yangu, kabla ya kujenga hoja kwa jazba na kejeli, ni muhimu kukubali ukweli wa kihistoria, Uislamu ni dini mpya ukilinganisha na dini ya Uyahudi na Ukristo. Uislamu ulianza karne ya 7 (baada ya Kristo), wakati tayari Biblia ilikuwa imekamilika, Wayahudi walikuwa na Torati na Wakristo walikuwa wameenea sehemu kubwa ya dunia.

Hii ina maana kwamba Uislamu uliingia katika dunia ambayo tayari ilikuwa na historia ndefu ya dini, maandiko, na mitazamo kuhusu Mungu., Uislamu umekuja umekuta Kuna vitabu vingi vya historia ,hata hiyo Quran yako imekopi visa vingi sana kutoka vitabu vya apokrifa,ukitaka ushahidi nitakupa utashangaa sana ,

Huwezi kuja baadae halafu ukatae kila kitu kilichokutangulia kana kwamba hakina msingi, halafu ujiite peke yako mwenye “ukweli wa mwisho”., ndugu Uislamu ni dini mpya

Sasa waliandikaje historia ya kuchafua uislamu wakati haukuwepo ,Nina vitabu vya historia Hadi vya 95AD ,kuja Hadi 500AD hapo hakuna kitu kinaitwa UISLAMU,

Zaidi ya hapo, hata wanazuoni wa Kiislamu wenyewe hawapingi kila kitu kilichoandikwa kabla ya Uislamu.

Kwa mfano, wanahistoria wa Kiislamu kama Ibn Ishaq, Ibn Hisham, Al-Tabari, na Ibn Kathir wameandika wazi kabisa kuhusu maisha ya Muhammad na pia wamekiri uwepo wa maandiko ya kale kama Taurati na Injili.

Wengine kama Al-Bukhari na Muslim walikusanya Hadith ambazo zinaonyesha uhusiano wa karibu wa Uislamu na dini zilizokuwepo kabla, hasa Uyahudi na Ukristo. Kwa hiyo si sahihi kusema kila aliyeandika historia ya dini ni kafiri mwenye nia ya kuchafua Uislamu, hasa mnapotegemea hao hao wanazuoni kwenye maelezo ya historia ya dini yenu.

Umekuja na hoja ya kudharau Ukristo eti kwa sababu Mungu alikuja kwa mfano wa mwanadamu, ni vyema tukubaliane kwamba hoja hiyo haipingwi kwa akili bali kwa mtazamo wa kidini wa Kiislamu.,dini ambayo ni mpya kabisa ,

Kama kweli Mungu ni mwenye uwezo wote, basi hawezi kushindwa kuchukua umbile la mwanadamu kwa lengo la kuwaokoa viumbe wake. Huo ni wema na upendo, si udhaifu. Na kama unakubali kuwa Malaika walisujudu Adamu kwa amri ya Allah, na wazazi wa Yusufu walimsujudia Yusufu kwa heshima, basi huwezi kuwalaumu wanaomsujudia Yesu aliyezaliwa kwa muujiza, akaponya, akafufua wafu, na akafufuka mwenyewe kutoka kwa wafu. Hilo ni tukio ambalo halijawahi kutokea kwa mwingine yeyote katika historia.

Kwa kweli, hoja zako si mpya. Zimeshaelezwa na kupingwa na Wakristo kwa karne nyingi sasa. Ni vizuri kujifunza na kuchunguza kwa undani kabla ya kupinga kwa matusi au dhihaka. Dini yoyote inayokwepa maswali, inayokataa historia, na inayoogopa hoja huwa ina udhaifu ndani yake.

Mimi nina uhakika wa imani yangu kwa sababu nimechunguza kila upande, nimepima kwa historia, akili na maandiko. Naomba na wewe ufanye hivyo kwa moyo wa kutafuta kweli, si kwa jazba.
 
Hauwezi kuwa serious wewe,yaani uwe na uhakika na imani ambayo inajicontradict severe
 
Naona unarudi kule kule ,kwanza

Niambie ni maandiko yapi ya biblia unayaamini na yapi huyaamini ,halafu nijuze huyaamini kwasababu hayaendani na Quran au kwasababu hayakusaidii kujenga hoja zako?

Kisha tuendelee

Nimeona unapotosha Yesu alifundisha uislamu,kijana acha huu ujinga humu wenzako walishaachana nazo hizo hoja dhaifu

Yesu alimuita Mungu baba ,je Uislamu unakubali Mungu kuitwa baba ?

Je Unajua Yesu na ISSA ni watu wawili tofauti wenye Sifa tofauti kabisa ?
Maandiko ambayo ni ya Injili ya Yesu ni yale ambayo yana mafundisho sahihi,ambayo yanaendana na vitabu vya Mwenyezi Mungu toka kwenye Zaburi,Torati,Injili na Qur'an

Yote yanazungumzia uwepo wa Mungu Mmoja, kuepukana na kumshirikisha Mwenyezi Mungu,na kufuata maamrisho yake na makatazo yake

Mfano Yesu alisema hakuja kutengua mafundisho ya manabii,hapa ndio pale nilipotoa hoja katika majibu yaliyopita kwamba Manabii na Mitume Wote walifundisha kitu kimoja tu,kumwabudu Mungu mmoja wa kweli na kuepukana na ushirikina wa utatu mtakatifu

Vile vile Yesu alisema hakuja hata kutengua nukta moja ya Torati bali amekuja kuikamilisha,hapa ndio nilisema hii dini ni moja kutoka huko zamani,Yesu kaja kuendeleza na Mtume Muhammada swalla aallahu alaih wasallamu kaja kukamilisha

Tusome aya hapa;

Andiko hilo linapatikana katika Injili ya Mathayo 5:17-18:

Mathayo 5:17-18 (Biblia):
"Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua Torati au Manabii; la, sikuja kuitangua bali kuitimiliza. Kwa maana, amin nawaambia, mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, *hata nukta moja wala kitone kimoja cha torati haitaondoka, hata yote yatimie."*

Maana:
Yesu alisisitiza kuwa hakuja kufuta mafundisho ya Musa (Torati) au manabii, bali alikuja kuyatimiza. Nukuu hii inaonyesha kuwa mafundisho ya awali bado yalikuwa na uzito wakati wake.

Nilivyokwambia ujipange ulifikiri natania expert wangu
 
Mi nimemuuliza jamaa hapo juu amesema Allah anaenda jehanamu. Sasa kama na mimi naenda sio mbaya kama Mungu anataka niende huko.....ila Muhammad ni uhakika ana moto wake wa pekee kwa kuharibu ulimwenguni
wewe ni moja kwa moja 'fi nnaar jahannam', usitafute wa kufuatana nao
 
Nilikwambia usitumie CHATGPT nilikuwa namaanisha kubwa ,sababu kwanza inakulemaza ,pili inakupa majibu ambayo ni yale yale ya UPOTOSHAJI wa kila siku ,nilikuwa na maana kubwa tu,

Unachofanya hapo wenzio walishafanya , yaani ni kituko

Una compare Biblia na Quran ,una compare manabii wa kiyahudi na uongo wa Muhammad,kwanza unazalisha maswali mengi sana

Unatakiwa ujue na ni wazi ipo hivo kabla ya Muhammad hakukuwahi kuwepo uislamu au dini ya Uislamu,

Mitume na manabii wote wa kiyahudi historia zao zipo, walikuwa dini ya kiyahudi ,mbali kabisa na uislamu

Ni wazi huna elimu na dini yako ,ndio maana ninapokuhoji unaenda unapachika kwa CHATGPT inakujibu kwa kadiri ya propaganda za Uislamu

Kwanza huoni unajikoroga?

Biblia huiamini, hapo hapo unataka kuitumia justify uislamu,

Hii ni mbinu ishapitwa na wakati ,utakapokuja na akili yako njoo tujadili ,

Ni kweli, kuna tofauti kati ya Uislamu na nguzo za Uislamu, na ni kweli pia kwamba Mitume wote waliwafundisha watu kumtii Mungu Mmoja na kuacha maovu. Lakini hoja ya msingi hapa si kama watu wa kale walimtii Mungu bali ni kama walifuata "Uislamu" kama dini au la.,hiyo ndio hoja yangu , Uislamu kama dini kuwepo kabla ya Muhammad,sio kuungaunga kwa kuokoteza Aya za biblia ambayo dakika moja mbele nikikubana unasema imetiwa mikono ili Hali biblia halisi huna .

Huwezi kusema kwamba Musa, Daudi au Yesu walikuwa Waislamu kwa sababu hawakutamka shahada ya Muhammad, wala hawakufundisha watu kuswali rakaa tano, kufunga Ramadhani, au kwenda Hajj Makka hizo ni sheria mpya, si mwendelezo tu.

Kama dini ya kweli ni ile iliyokuwepo tangu zamani, basi Uislamu ulioletwa na Muhammad si wa asili bali wa marekebisho ya baadaye na Biblia haimtaji Muhammad popote kama nabii ajaye. Hivyo, kudai kwamba Uislamu wa sasa ni mwendelezo wa dini ya Mitume wote si sahihi kihistoria wala ki maandiko.,huu ni UPOTOSHAJI mkubwa , Huwa napenda kusema Uislamu ni dini mpya,maana imekuja tayari Kuna dini imezikuta,imekuta Kuna historia, vitabu,teknolojia,n.k

Jitahidi kujadili kama unamfundisha au kumlingania mtu ambaye anatakiwa aingie kwenye uislamu bila propaganda au Taqya ,

Nina maswali matano kwako maana hoja zako ulizojibu kwa CHATGPT zimezalisha maswali mengi sana ambayo mtu anayekusikiliza zaidi unazidi kumfanya atilie mashaka uislamu

Kama Mitume wote walikuwa Waislamu, mbona hawakufundisha watu kusema

"Ash-hadu alla ilaha illa Allah, wa ash-hadu anna Muhammad rasulullah"?

kama Musa au Yesu walikuwa Waislamu, mbona hawakwenda Hajj Makka, hawakufunga Ramadhani, wala kuswali rakaa tano?

Kama Uislamu ni dini ya kale kabisa, mbona jina "Uislamu" na "Waislamu" havijatajwa hata mara moja katika Biblia nzima au vitabu vya kale?

Kama sheria tu ndio tofauti ila msingi ni uleule, kwanini Qur'an inasema

"dini isiyokuwa Uislamu haitakubaliwa"? Mbona haikusema “dini yoyote inayomwabudu Mungu mmoja ni sawa”?

Mbona Yesu hakusema popote kwamba baada yake atakuja Muhammad? Badala yake alisema “Mimi ndimi njia, kweli, na uzima, mtu haendi kwa Baba ila kwa njia ya mimi” (Yohana 14:6)

Najua utaenda kuuliza kwa CHATGPT,litakupa majibu kulingana na propaganda za Uislamu ila utazalisha maswali zaidi, jitahidi kujibu kama unamfundisha au kumlingania mtu anayetakiwa kuingia kwenye dini isiyo na shaka kama uislamu unavyosemwa
Siri moja kubwa ya mtu ambaye hajiamini au anatapatapa ni kutafuta sababu zisizo na msingi na kuzifanya za msingi

Chatgpt hivi inaweza yenyewe kukuletea jambo ambalo wewe hujaligiza,kitendo cha kuagiza hii tekinolojia inipe data fulani kwa wepesi ni kwamba taarifa hizo nazijua na nazifahamu vizur sana,sasa acha hoja za kitoto

Pili hivi mimi umeshaona nakuambia ukristo hau ujui tangu nianze kujadiliana na wewe? Lakini wewe kila mara unasema siujui Uislamu wangu,nisingeujua tungeendelea kujadiliana hapa?

Relux expert wangu hii kama vita ni ya Israel na Iran, ndio kwanza tupo siku ya tatu ili zitimie kumi na mbili bado siku tisa, umelianzisha nitamaliza kama Muiran,kaa kwa kutulia

Twenze kazi, Shahada ya manabii waliopita haikuwa Ashahadu anlaa ilaha illallah wa ashahadu ana Muhammad rasullah,hii ni shahada Ya Allah Mtume wake Muhammad wa kipindi hiki

Mfano kipindi cha Mussa alayhi salamu ilikuwa Ashahadu anlaa ilaha illallah wa ashahadu ana Mussa rasullah,kwa maana Unashuhudia Uwe wa Mungu Mmoja na kukiri Utume wa Mussa,na mitume wengine ilikuwa hivyo

Kwahiyo hiyo hoja yako ya shahada haiondoi kwamba hii dini ni moja

Kwahiyo hata kama katika vitabu vya zamani,halikuandikwa neno Uislamu lakini asili ya mafundisho na nature ya ibada kwa Mungu Mmoja ni ile ile,hapa mwishoni ndio Allah akaamua sasa kuiweza wazi dini yake kwakuwa imekamilika akaitaja rasmi

Na hoja kwamba sijui hakukuwa na swala tano,ramadhani,hija nakadhalika hii yote ni namna Allah alivyoamua kupanga mambo yale,mimi na wewe ni nani wa kuhoji hekima yake?

Vizur sana umehoji mbona Yesu hakubashiri ujio wa Mtume mwingine?

Yesu alibashiri ujio wa mtume mwengine ambaye ni Ahmad/Muhammad haya yapo kwenye biblia na qur'an pia

Tena alisema itabidi mimi niondoke ili huyo ajaye apate kuja,alisema pia mimi hamkuniamini katika habar ya zambi,lakin huyo ajaye atawaambia kweli yote,na atawaambia habar ya hukumu

Sasa kwa bahati mbaya sana,mmeligeuza hilo andiko na kusema ni roho mtakatifu,lakini hapa kwa mtu mwenye akili huru atajiuliza hivi, Yesu hakuwa spirit kwa maana alikuwa na mwili halisi,alifanya miujiza mingi tu,kama Yesu hakuaminiwa je huyo roho ambaye yupo ndani ya nyoyo zetu ndio ataaminiwa?

Swali lingine linakuja je huyo roho mpaka sasa ameweza kuleta hukumu ambazo Yesu alisema na habar ya dhambi na hukumu?

Kama huyo roho yupo kwa kila mtu ni namna gani atafundisha hizo hukumu na dhambi,wakati jamii nzima inatakiwa izijue na ziwe wazi, na kama huyo roho yupo kwa mtu maalumu ambaye atasema habar za hukumu na dhambi mbona mpaka leo hatuja mjua?

Tusome aya zifuatazo hapo,Yesu akitabir ujio wa Muhammad;

Andiko linaloelezwa na baadhi ya wanafunzi wa dini kuwa Yesu alitabiri kuja kwa Mtume mwingine linapatikana katika:

Injili ya Yohana 14:16-17
"Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele. Ndiye Roho wa kweli, ambaye dunia haiwezi kumpokea... lakini ninyi mnamjua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu."

Yohana 15:26
"Lakini ajapo Msaidizi nitakayempeleka kwenu kutoka kwa Baba, yaani Roho wa kweli atokaye kwa Baba, huyo atanishuhudia."

Yohana 16:7, 13
"Lakini nawaambia kweli, yawafaa ninyi niondoke; kwa maana nisipoondoka, yule Msaidizi haji kwenu... naye atakapokuja, huyo atawaongoza kwenye kweli yote."

---

Hoja ya Waislamu:
Waislamu wanaona aya hizi kama ishara ya kuja kwa Mtume Muhammad (SAW), ambaye aliitwa "Amin" na kuleta ujumbe wa haki. Neno la Kigiriki "Parakletos" (Msaidizi, Mfariji) huonekana kufanana na "Ahmad", jina la pili la Mtume Muhammad lililotajwa katika Qur’an (Surat As-Saff 61:6).

---

Qur'an – As-Saff 61:6
"Na Isa bin Maryamu alisema: Enyi wana wa Israil! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu... na mwenye kutoa bishara ya kuja Mtume baada yangu, jina lake ni Ahmad..."

Sasa hiyo sijui roho wa kweli atakaa milele,ni janja janja za watu kuficha ukweli na kujikita au kuweka maandishi yaonekane si Mtume au Nabii anayekuja bali ni roho

Kama watu waliweza kubadilisha maandiko ya kumfanya Yesu kuwa Mungu,je watashindwa kucheza na jambo hili

Wakristo nawahusia hakika siku ya mwisho kuna moto kwa wale ambao wanaabudu miungi mingine pamoja na Mwenyezi Mungu mmoja

Hao waliotangulia mbele ya haki miongoni mwa ndugu zenu wameijua haki lakini kwakuwa wameshakufa hawana namna ya kurekebisha,nyie bado mpo hai basi Mumuamini Mungu Mmoja mpate kusalimika

jipange expert wangu
 
Back
Top Bottom