Je wajua kwamba Allah kwenye Quran anasema anahitaji kunusuriwa?

Je wajua kwamba Allah kwenye Quran anasema anahitaji kunusuriwa?

Kwahiyo ukiabudu Mwezi ambao ni mmoja na kuuita Mungu mmoja na kujinyenyekesha kwa huo mwezi mmoja basi wewe ni Muislamu:
Toka Mwamedi awaruhusu kusema uwongo mnapo itetea dini basi kuongopa ndio silaha yenu:
 
Yesu alitumwa kwa Wana wa Israeli* linapatikana katika Injili ya Mathayo 15:24, ambapo Yesu anasema wazi:

"Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli." (Mathayo 15:24)

Naomba andiko kwamba katumwa kwa watu wote
Jina Israel unajua lilitoka wapi na nini maana yake ? Au unadhani jina Israel ni kabila au ukoo ....siri ya jina la Israel ni wateule hivyo yesu alitumwa kwa wateule siyo waisrael wote ni wateule kumbuka hivyo wateule ni wale ambao watamtii mungu wa kweli katika kweli na haki yote.
 
Kwa upande wangu nimeshangaa sana kuona Mungu Allah anahitaji wanadamu wamnusuru. Kwa yeyote anayejua naomba msaada wa kuielewa hii Aya,

47:7
Enyi mlioamini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu.

Allah ana matatizo gani ambayo anahitaji wanadamu wamnusuru?
Kwenye mambo gani anahitaji tumnusuru! Tuelekezane wakuu namna ya kumnusuru Allah.

NI DHAIFU NDO MAANA WENYEWE HUMPAMBANIA SANA.
 
maandiko katika Qur’an yanayoeleza wazi kwamba Mtume Muhammad (ﷺ) alitumwa kwa watu wote, si kwa Waarabu pekee.

Qur'an Surah Saba (34:28):
"Na hatukukupeleka ila kwa watu wote, uwe mbashiri na mwonyaji..."
(Qur'an 34:28)

Qur'an Surah Al-Anbiya (21:107):
"Wama arsalnaaka illa rahmatan lil’aalamin"
"Na hatukukupeleka ila kuwa rehema kwa walimwengu wote."

Qur'an Surah Al-A’raf (7:158):
"...Mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu nyote..."


Maandiko haya yanaonesha wazi kwamba Mtume Muhammad (ﷺ) alitumwa kwa ulimwengu mzima, tofauti na Mitume wengine waliotumwa kwa mataifa yao tu.

Huyu ndio katumwa kwa watu wote

Hakuna kona kona
Nikweli mtume mudi boy alitumwa kwa watu wote ila tatizo ni aliye mtuma ni SHETANI SIYO MUNGU .tatizo lipo hapo
 
Kwa kuwa hutaki tujadiliane ok poa.....ila hata hiyo Aya umeweka ya mfano kwamba Mungu anamswalia Muhammad, huko ni kumkosea Mungu. Mungu hawezi kumtakia Rehema mwanadamu, Rehema anazo yeye Kisha amtakie mtume Rehema, anamtakia kutoka kwa nani?

Mimi nikisema nakutakia wewe kheri ni kwamba nakutakia kutoka kwa Mungu. Sasa Mungu naye anamtakia mtume Rehema kutoka kwake mwenyewe?

Ni sawa mwanao anahitaji pesa ya matumizi Kisha mimi na wewe tumuombee pesa kwako. Inakuingia akilini hiyo? Yaani wewe umuombee pesa mwanao kutoka kwako mwenyewe. It's funny 😂.
Hicho kituko kiko hata kwa wakristo...nao wanasemaga tunambariki mungu au mungu ubarikiwe...tena unamsikia anaye sema hivyo anadai ana roho mtakatifu je hiyo siyo kufuru mwanadamu anaweza kumpa baraka mungu ?
 
Kwanza naomba ambao tunajadiliana tuwe na subira nitajibu hoja ya mtu mmoja mmoja maana nimekuta notification kama zote

Bwana hamis77 sasa ngoja nikupe shule

Nilikuuliza unaelewa nini kuhusu Uislamu,matokeo yake ukaleta porojo tu hapa

Uislamu ni :


Maana ya Uislamu:

Uislamu ni dini inayomaanisha “kujisalimu (kujisalimisha) kwa Mwenyezi Mungu kwa unyenyekevu, kwa utiifu na kwa amani.”

Neno "Islam" linatokana na neno la Kiarabu "Salaama", ambalo lina mizizi ya maana ya amani, usalama, na kujitoa kwa Mwenyezi Mungu.

Kwa hiyo, Muislamu ni mtu anayejisalimisha kwa Mwenyezi Mungu kwa moyo wa unyenyekevu, anamtii na kuishi kwa amani na viumbe wote.

Uislamu ni dini ya:

  • Tauhidi (kumwamini Mungu mmoja)
  • Uadilifu
  • Huruma
  • Amani


Natumaini umeelewa sasa expert wangu
Nguzo ya neno dini ya kweli ya Mungu ni HAKI ..huruma nje ya haki ni uovu tu amani nje ya haki ni uovu tu na kumwamini mungu nje ya haki ni uovu na unafiki tu
 
Hao USA wengi ni Wayahudi kama hukulijua na ndio maana kama mnataka muifute Israel, mtangulie kufuta USA na baadhi ya mataifa ya Ulaya, la sivyo mtakua mnachezea kipigo muda wote kama ilivyotokea juzi.
Tumekubaliana Mungu hahitaji kupiganiwa lkn hayo madege yanayo waua kobaz yanampigania nani?
 
Kwanza sio dhumuni langu kwamba nikitoa majibu nataka mtu haelewe mara moja,huenda kuna mazingira yakafanya iwe hivyo

Tafsir ni tofauti na lugha halisi iliyokuja na qur'an,kwahiyo kwenye tafsir tegemea uwepo au matumizi ya maneno mbali mbali lkn kubwa yote yanatufikisha katika lengo moja

Mfano inasema Allah anamswalia Mtume,hapa si sahihi kwasababu haiwezekani Allah akamswalia Mtume ila humtakia rehema mja wake,huo ni mfano tu

Turudi kwenye swali lako,Allah hapa anakusudia kwamba kama watu hawakutakuwa tayar kufuata maagizo yake au amri zake,basi hana haja nao kwakuwa yeye sio mhitaji useme kwamba ataathirika kwa chochote,ila anaweza leta watu wengine ambao ambao watamnusuru/kumsaidia/kufuata maamrisho yake na hukumu zake
Hapo kwenye Allah kumswalia mtume ,kwanini utoe neno kumswalia uweke neno kumtakia rehema,unamaanisha kwenye kiarabu hakuna neno kumtakia rehema badala yake inabidi litumike neno kumswalia?? Au kwenye tafsiri ya hakuna neno kumtakia rehema badala yake lipo hilo kumsalia pekee??
Umeshinda wewe,are you happy now?

Amini unachoamini expert wangu

Asante
Na siku nyingine ukome kuikosoa quran kwamba kilichoandikwa sicho ila unachokitaka wewe ndicho
 
Unataka kusema JF nzima hakuna wasomi wa Quran?
Siyo wasomi wa Quran, bali wenye elimu ya 'fiq'hi', yaani tafsiri sahihi na maana ya misemo iliyomo humo. Kusoma tu tuko wengi tunaoweza kusoma na hata kufasiri aya kwa kiswahili kama zilivyotafsiriwa 'word by word', lakini ukumbuke kile ni kiarabu cha karne ya nane na ni kiarabu cha kabila la Quraish la Mtume (SAW). Hii ni sawa na lugha ya kiswahili cha Muyaka bin Haji (sijui umewahi kuona mashairi yake?) ambayo iko tafauti na ile tunayozungumza sasa na ndiyo mana kuna watu wanasoma literature (fasihi) ili kuweza kufanya tafsiri sahihi.

Hata waarabu ni wachache ndiyo wanaoweza kukupa maana halisi ya aya zilizoandikwa kwenye msahafu.
 
Kama Uislamu ni amani, kwa nini Qur'an inasema:
"Pigeni vita wale wasioamini..."
Surah At-Tawba 9:29
"Piganeni na wale wasioamini katika Mwenyezi Mungu wala Siku ya Mwisho..."
Jipange expert wangu!

Usihofu expert wangu utapata majibu pasina shaka yoyote ile,na katika Uislamu hatukariri chochote ila ni elimu ndio msingi mkubwa wa dini yetu

Kwanza ifahamike waislamu hawakupigana vita yoyote pasina sababu,dini yenye ni ya amani na huo ndio ukweli

Na Mitume wote walikataliwa katika miji yao waliyokulia au kuzaliwa,na Mtume Muhammad swalla aallahu alaih wa sallamu naye alikataliwa na watu wake pia

Kwahiyo wote ambao waliingia katika Uislamu waliteswa sana na kunyanyaswa sana,hivyo hakukuwa na namna nao wapigane na wazushi na hatimaye amani ipate kutulia

Aya ya Qur’an inayoruhusu Waislamu kujilinda dhidi ya wanaowapiga ni kama ifuatavyo:

Surah Al-Hajj (22:39):
"Wameruhusiwa kupigana wale wanaopigwa vita, kwa sababu wameonewa. Na hakika Mwenyezi Mungu anao uwezo wa kuwasaidia."

Maana: Waislamu waliruhusiwa kupigana si kwa kushambulia, bali kwa kujilinda dhidi ya uonevu na dhulma. Aya hii ilikuwa ya kwanza kuruhusu kupigana baada ya muda mrefu wa kuvumilia mateso huko Makka.

Qur’an haifundishi kupigana kiholela, bali inasisitiza:
  • Kujilinda dhidi ya dhulma,
  • Kuepusha fitna (vurugu),
  • Na kutafuta amani pindi adui akitaka amani (Qur’an 8:61).


Kaa kwa kutulia Bey atajibu hoja zote
 
Kwa upande wangu nimeshangaa sana kuona Mungu Allah anahitaji wanadamu wamnusuru. Kwa yeyote anayejua naomba msaada wa kuielewa hii Aya,

47:7
Enyi mlioamini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu.

Allah ana matatizo gani ambayo anahitaji wanadamu wamnusuru?
Kwenye mambo gani anahitaji tumnusuru! Tuelekezane wakuu namna ya kumnusuru Allah.
Anusurike dhidi ya Jahanum itakapokua haijajaa
 
.Je, wauaji wa kigaidi kama ISIS nao walikuwa wakijisalimisha kwa Mungu kwa amani?

Kama mtu akijisalimisha kwa mamlaka ya polisi kama huko Buza au Segerea, je naye ni Muislamu kwa sababu "amejisalimisha"?
Nilikwambia ujipange lakini unaniangusha sana...sasa wewe mwenyewe umekiri kuwa ISIS ni wauaji wa kigaidi,halafu unawatumia kama hoja ya kuonyesha amani ya Uislamu

Umeandika kabisa ukiwa serious? Jipange!!!

Unaleta porojo nyingine kuhusu polisi,sijui buza au segerea, expert wangu jipange unapojadiliana na Bey

Kaa kwa kutulia expert wangu
 
Jipange expert wangu!

Usihofu expert wangu utapata majibu pasina shaka yoyote ile,na katika Uislamu hatukariri chochote ila ni elimu ndio msingi mkubwa wa dini yetu

Kwanza ifahamike waislamu hawakupigana vita yoyote pasina sababu,dini yenye ni ya amani na huo ndio ukweli

Na Mitume wote walikataliwa katika miji yao waliyokulia au kuzaliwa,na Mtume Muhammad swalla aallahu alaih wa sallamu naye alikataliwa na watu wake pia

Kwahiyo wote ambao waliingia katika Uislamu waliteswa sana na kunyanyaswa sana,hivyo hakukuwa na namna nao wapigane na wazushi na hatimaye amani ipate kutulia

Aya ya Qur’an inayoruhusu Waislamu kujilinda dhidi ya wanaowapiga ni kama ifuatavyo:

Surah Al-Hajj (22:39):
"Wameruhusiwa kupigana wale wanaopigwa vita, kwa sababu wameonewa. Na hakika Mwenyezi Mungu anao uwezo wa kuwasaidia."

Maana:
Waislamu waliruhusiwa kupigana si kwa kushambulia, bali kwa kujilinda dhidi ya uonevu na dhulma. Aya hii ilikuwa ya kwanza kuruhusu kupigana baada ya muda mrefu wa kuvumilia mateso huko Makka.

Qur’an haifundishi kupigana kiholela, bali inasisitiza:

  • Kujilinda dhidi ya dhulma,
  • Kuepusha fitna (vurugu),
  • Na kutafuta amani pindi adui akitaka amani (Qur’an 8:61).


Kaa kwa kutulia Bey atajibu hoja zote
Ndugu Uislamu sio dini ya amani huo ni UPOTOSHAJI ,umetoa maelezo ya uongo ,

hoja yako kwamba Waislamu hawakupigana bila sababu ni upotoshaji mkubwa ,labda unadhani hatuujui uislamu ,binafsi nimezaliwa kwenye uislamu,nimesoma uislamu,kwahiyo naongea ninachokijua,kwa sababu historia na Qur’an yenyewe zinaonyesha kwamba si kila vita ilikuwa ya kujilinda kama unavyosema ,

Kwa mfano, vita ya Khaybar, Banu Qurayza, na vita zingine nyingi zilikuwa ni za kushambulia na kueneza Uislamu kwa nguvu jambo linalopingana moja kwa moja na dhana ya AMANI unayosema hapa ..

Tukirudi kwenye Qur’an, kuna Aya nyingi ambazo hazihusu kujilinda bali zinachochea mashambulizi ya wazi. Mfano nitakupa Aya kadhaa hapa👇👇

Surah At-Tawbah 9:29
"Piganeni na wale wasioamini katika Mwenyezi Mungu... mpaka walipe kodi kwa unyenyekevu nao wakiwa wanyonge."


Hii ni amri ya wazi ya kushambulia wasiokuwa Waislamu na kuwafanya kuwa chini ya utawala wa Kiislamu kwa kulipa Jizya si kwa kujilinda, bali kwa kutawala.

Surah Muhammad 47:4
"Basi mnapokutana na wale waliokufuru wapigeni shingoni mwao..."

Hii pia si hoja ya kujilinda, bali ni amri ya vita dhidi ya wasiokuwa Waislamu kwa sababu tu ya imani yao.

Hata mtume wenu Muhammad alikiri kwamba ametumwa kwa upanga.

Tafsiri za hadithi maarufu zinaeleza

Sahih al-Bukhari (Hadith 2948)
"Nimeamrishwa nipigane na watu mpaka washuhudie kwamba hakuna mungu ila Allah..."
Hii inapingana na hoja yako ya kwamba vita zilikuwa kwa kujilinda tu.

Viongozi wengi wa Kiislamu baada ya Muhammad waliendeleza utawala wa upanga: Mashambulizi dhidi ya Uajemi, Byzantine, India, Afrika Kaskazini haya yote hayakuwa kujilinda, bali ni kueneza Uislamu kwa nguvu. Hilo linaelezwa hata na wanazuoni wa Kiislamu kama Ibn Khaldun aliyekiri kuwa jihadi ni njia halali ya kueneza dini kwa mujibu wa Sharia.

Na kuhusu hoja kwamba “Mitume wote walikataliwa,” ni kweli walikumbana na upinzani, lakini hakuna kati yao aliyepiga vita kwa ajili ya kueneza ujumbe wake kama Muhammad alivyoagiza.

Yesu alisema

“Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi...” (Mathayo 5:44)

Yesu alikataa kutumia upanga (Mathayo 26:52), tofauti na Muhammad ambaye alisema:
"Nimekuja kwa upanga." (Ibn Sa’d, Kitab al-Tabaqat al-Kabir)

Kwa hiyo si kweli kwamba Uislamu ni dini ya amani .

Uislamu unaruhusu mapigano ya kimwili kwa sababu ya dini jambo linalotofautiana na mafundisho ya injili ya upendo, msamaha, na kuvumilia mateso.
 
Nilikwambia ujipange lakini unaniangusha sana...sasa wewe mwenyewe umekiri kuwa ISIS ni wauaji wa kigaidi,halafu unawatumia kama hoja ya kuonyesha amani ya Uislamu

Umeandika kabisa ukiwa serious? Jipange!!!

Unaleta porojo nyingine kuhusu polisi,sijui buza au segerea, expert wangu jipange unapojadiliana na Bey

Kaa kwa kutulia expert wangu
Muda wa porojo haupo ndugu, jikite kwenye hoja na mada

Sikutumia ISIS kama kipimo cha Uislamu mzima, bali nilisema wazi kuwa vitendo vyao vinaendana moja kwa moja na baadhi ya Aya na Hadith za Kiislamu. Wao hawatungi sheria, wanatekeleza zilizoandikwa. Mfano:

Qur’an 9:5
"Waue washirikina popote mnapowakuta..."

Qur’an 8:12
"Nitatie hofu katika nyoyo za waliokufuru, wapigeni juu ya shingo..."

Sahih Muslim 1:33
"Nimeamrishwa nipigane na watu mpaka washuhudie kuwa hakuna mungu ila Allah..."

Sasa swali ni Je, ISIS walitunga aya hizi au wanazitekeleza?

Hata viongozi wa ISIS wamesema,

"Tunaleta Khilafa kwa kufuata Qur’an na Sunnah za Muhammad."

Hii haimaanishi kila Muislamu ni gaidi lakini inamaanisha maandiko yao yanaruhusu au hata kuamuru vitendo vya kimabavu dhidi ya wasioamini, na mtu yeyote anayetaka kuchukua maandiko hayo kwa usomaji wa moja kwa moja (literal interpretation) ataishia kama ISIS.

Hata wewe ukiyatumia maandiko vizuri ya Quran na hadithi lazima uwe GAIDI
 
Nafikiri, tunakimbia kujibu anachoomba ufafanuzi...

JF ya sasa' ni changamoto, Mtoa thread kaomba apate ufafanuzi ili aondoe doubt iliyopo akili mwake...

Mjibuni ili nasi tupate maarifa na uelewa zaidi
Hahitaji ufafanuzi bali ni ujinga ndo alokua nao na kuukashifu Uislamu
 
Kwa nini Qur'an inaruhusu vita (jihad) kwa masharti, kama kweli Uislamu ni wa amani tu?
Surah Al-Baqarah 2:216
"Imewafaradh kenu kupigana, ijapokuwa mnakichukia kitu hicho..."
Sababu ya kupigana nilishaijibu tayar katika ile hoja ya kupigana vita na wazushi

Hapo hao wanaochukia ni wanafiki,kuna watu ambao walijifanya ni waislamu lakini kumbe ni wanafiki wakubwa na hawana imani ya kweli juu ya uislamu,kwahiyo hawa walipoambiwa wapigane na wazushi walikuwa wanachukia sana,sasa walipewa mtihani mkubwa sana kupima imani yao,na wengi wao walitoa sababu kadha wa kadha ya kutokwenda vitani
 
Ikiwa kujisalimisha kwa Mungu ni sifa kuu ya Uislamu, kwa nini Shetani hakuitwa Muislamu alipokubali uumbaji wa Mungu lakini akakataa tu kusujudu kwa Adam?
Surah Al-Baqarah 2:34
"Na tulipowaambia Malaika: Msujudieni Adam, walimsuju
dia isipokuwa Iblis..."
Expert wangu kwani katika hoja zangu niliwahi sema ukikubali uumbaji wa Mungu ndio kujisalimisha au ndio kuitwa muislamu?

Iblis alileta kiburi kwa kukataa agizo la Allah la kumtaka amsujudie Adam alayhi salamu sijida ya heshima sio ya ibada,maana kusujudu ni kwa ajili ya Allah peke yake

Kwahiyo kitendo cha kukataa kwasababu yeye alijiona bora kwakuwa ameumbwa kwa miale ya moto na sisi kwa udongo kukamponza

Akahukumiwa kuingia motoni

Nitajibu hoja za awali kabla ya hizi mpya ambazo unazileta baada ya mimi kujibu,kwahiyo kuwa na subira,Bey atajibu hoja zote
 
Hapo kwenye Allah kumswalia mtume ,kwanini utoe neno kumswalia uweke neno kumtakia rehema,unamaanisha kwenye kiarabu hakuna neno kumtakia rehema badala yake inabidi litumike neno kumswalia?? Au kwenye tafsiri ya hakuna neno kumtakia rehema badala yake lipo hilo kumsalia pekee??

Na siku nyingine ukome kuikosoa quran kwamba kilichoandikwa sicho ila unachokitaka wewe ndicho
Nitakurudia ndugu yangu katika imani,ila kabla sijakurudia

Tafakari jambo hili,je inakuwaje Allah amswalie mja wake?, Kama Allah anamswalia Muhammad swala aallahu alaih wasallamu na Mtume atamswalia nani?

Usikurupuke kama wasio waislamu sawa ndugu yangu,next time tumia lugha nzuri,unamwambia mwanaume mwenzio akome?


Kwa kuongezea kidogo ndugu yangu katika imani,sikusema ile ayah haipo au sio sahihi ila nilisema inaposema Allah ana mswalia Mtume basi inamaanisha anamtakia rehma

Nikupe mfano kidogo wa neno moja lakini linakuwa na maana mbili,mfano Swala inamaanisha ni dua au tendo la ibada ambalo linafunguliwa na Takbira tulhiram na kufungwa na taslimah,fungua ufahamu wako,usikurupuke kama makafiri


Ngoja nidili kwanza na wasio waislamu.
 
Back
Top Bottom