Je wajua kwamba Allah kwenye Quran anasema anahitaji kunusuriwa?

Je wajua kwamba Allah kwenye Quran anasema anahitaji kunusuriwa?

Mkuu mi nataka kujua tu hiyo tafsiri ya kumnusuru imetoka wapi? na je ni kweli hiyo aya imetaja kunusuriwa??
Aya ndo ipo hivo, unaona ajabu eee! NAMI pia nimeshangaa kama ambavyo na wewe huamini kwamba Aya ipo hivo. Fungua Quran usome, au huna?
 
Wanajaribu kutetea hoja isiyoteteeka, kuna mmoja hapo anasema kuheshimu Quran na kumtii Mungu ndo kumnusuru. Ajabu kweli hii
Sio ajabu tatizo wewe una majibu yako kichwani,yakienda kinyume na wewe unapinga

Wakati mwingine ni kukubaliana kwa kutokukubalina simpo
 
Huwa napenda sana majadiliano ya busara na hekima,nisichopenda ni matusi na kuvunjiania heshima

Sijaona baya kwako,wala hatubishani ila ninapoona hakuna muelekeo wa kusikilizana naona bora nikae kimya
We ni mtu makini sana, unaonekana unapenda Amani. Sasa unajadiliana na mimi ambaye nimeonyesha kutaka kujua bila kuingiza maneno ya matusi, kwa nini usinisaidie kujua ukweli wa hii Aya?
 
Nyie fanyeni mzaha na maneno ya Mwenyezi Mungu hapa duniani, lakini nawaambia kila mmoja wenu atayajutia haya maupuuzi anayoyafanya pale tu roho itakapoachana na mwili.
Endeleeni kutiana moyo hapa duniani na endeleeni na mizaha na mambo ya Mwenyezi Mungu, lakini jua fika kuwa kaburini utaingia peke yako na kuulizwa utaulizwa peke yako, hautakuwa na msaada wala kutiana moyo kama mnavyofanya hapa duniani.

Haya niliyo waambia hapa ipo siku mtayakumbuka, hopefully it will be too late
Takbiiirrrr....
 
Sio ajabu tatizo wewe una majibu yako kichwani,yakienda kinyume na wewe unapinga

Wakati mwingine ni kukubaliana kwa kutokukubalina simpo
Sasa ndugu hata kuna baadhi ya wakristo walikuwa wabishi na wameslimu. Maana yake ni kwamba mpe mtu ukweli hata kama unahisi ana kitu chake kichwani huwezi jua anaweza kubadilika. Mi nafikiri kama unajua nieleweshe tu.
 
Nyie fanyeni mzaha na maneno ya Mwenyezi Mungu hapa duniani, lakini nawaambia kila mmoja wenu atayajutia haya maupuuzi anayoyafanya pale tu roho itakapoachana na mwili.
Endeleeni kutiana moyo hapa duniani na endeleeni na mizaha na mambo ya Mwenyezi Mungu, lakini jua fika kuwa kaburini utaingia peke yako na kuulizwa utaulizwa peke yako, hautakuwa na msaada wala kutiana moyo kama mnavyofanya hapa duniani.

Haya niliyo waambia hapa ipo siku mtayakumbuka, hopefully it will be too late
Acha vitisho we mzee, zama kwenye mada kama hujui kitu Kaa kimya.
 
We ni mtu makini sana, unaonekana unapenda Amani. Sasa unajadiliana na mimi ambaye nimeonyesha kutaka kujua bila kuingiza maneno ya matusi, kwa nini usinisaidie kujua ukweli wa hii Aya?
Majibu kutoka kwa Engneeer

أَقْدَامَكُمْ"
"Mkiimsaidia Mwenyezi Mungu, Atakusaidieni na kukazilia nyinyi miguuni mwenu."

### Maelezo ya kina:
1. Maana ya kuwa "kumsaidia Mwenyezi Mungu":
Kuendeleza Dini Yake: Kwa kufuata amri Zake, kudai haki, kusimamisha uadilifu, na kujitolea kwa njia Yake (k.v. kupigana jihad kwa sababu ya kuilinda dini).
Kumtii Mwenyezi Mungu: Kuishi kwa mujibu wa Qur'an na Sunnah, kuepusha uasi, na kushiriki katika mambo yanayokuza Uislamu.

2. Ahadi ya Mwenyezi Mungu ya kusaidia:
Usaidizi wa kimwili na kiroho: Mwenyezi Mungu Atawaondoa maadui wenu na kukupa uthabiti katika vita au shida.
Thabiti katika msimamo wako: Atakufanya uwe imara katika mafundisho ya Kiislamu bila kutetereka.

3. Muktadha wa kisiasa na kihistoria:
- Aya hii iliteremsha wakati wa vita kwa mujibu wa watafsiri kama Ibn Kathir, ikilenga Waislamu waliojipanga kujihami dhidi ya maadui wao. Inasisitiza umuhimu wa kujitolea kwa Mwenyezi Mungu kwa matokeo mazuri duniani na Akhera.

4. Matumizi ya kisasa:
Kwa mtu binafsi: Kujitoa kwa Mwenyezi Mungu kwa vitendo (k.v. kusali, kutoa sadaka, kufundisha Uislamu) kunaleta baraka na uthabiti.
Kwa jamii: Umoja na uadilifu katika mambo ya kidini na kijamii husababisha msaada wa Mwenyezi Mungu.

### Mithali ya Qur'an:
Aya hii inafanana na Sura Al-Imran (3:160): *"Mwenyezi Mungu Akitaka kukusaidia, hakuna anayeweza kukushinda.

haya majibu kutoka kwa ndugu yangu nilikujibu lkn hukuridhika,naona umerudia swala hilo hilo,nasema tena haya ndio majibu,lau huridhiki,basi tuangalie hoja nyengine expert wangu
 
Qur'an sio kitabu cha kukichambua kwa matamanio yako

Ss tunaenda na ushahidi hatufuati dini kibubusa

Mm naielewa vzr dini yangu na hakuna mkristo yyte wa kunichallenge imani yangu labda muislamu mwenzangu tena anofuata misingi sahihi aniongezee elimu
Wacha uongo wewe jibu haya maswali
1)shetani ibilisi yule aliye laaniwa laana ya milele ni dini gani?
2)je Muhammad kabla ya kufika miaka 40 alikuwa dini gani au kafiri.
3)je Muhammad alisilimu au akusilimu ?
4)muongozo wa mwisho wa Mungu ni kitabu cha injili je Muhamad kabla ya kupewa utume na kitabu, alifuata muongozo upi ulio mwezesha kufikia daraja ya kupewa utume au alikuwa KAFIRI NA UKAFIRI UKAMFIKISHA DARAJA YA UTUME 🙄 ? Kama utatumia akili wote walio kuwa mitume walifuata muongozo wa kitabu vya nyuma yao sasa je Muhammad alikuwa ni mnasala na kwa huo kufikia daraja ya kupewa utume ? Kama siyo je muhamadi alifuata kitabu gani ikiwa akufuata injili ? Je utume wa Muhammadi msingi wake ulikuwa ni kitabu gani kabla ya kuupata? Utume na kupewa msahafu ?
 
Hay
Surah Al-Hijr (15:9):
"إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا الذِّكْرَ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ"

"Hakika Sisi ndio tulioteremsha Ukumbusho (Qur'an), na hakika Sisi ndio tutakaoilinda.

ELEWA HAPO
ALLAH ndio anailinda Quran na uislamu kwa ujumla kwa namna ambayo yeye anataka

Hivyo ALLAH anapambana mwenyewe, kuilinda dini na watu ni asbab
Hayo maneno sisi ndo tulio teremsha koroan ,Alha nalimaaninishaa yeye na nani au yeye na khaaba?
 
Majibu kutoka kwa Engneeer

أَقْدَامَكُمْ"
"Mkiimsaidia Mwenyezi Mungu, Atakusaidieni na kukazilia nyinyi miguuni mwenu."

### Maelezo ya kina:
1. Maana ya kuwa "kumsaidia Mwenyezi Mungu":
Kuendeleza Dini Yake: Kwa kufuata amri Zake, kudai haki, kusimamisha uadilifu, na kujitolea kwa njia Yake (k.v. kupigana jihad kwa sababu ya kuilinda dini).
Kumtii Mwenyezi Mungu: Kuishi kwa mujibu wa Qur'an na Sunnah, kuepusha uasi, na kushiriki katika mambo yanayokuza Uislamu.

2. Ahadi ya Mwenyezi Mungu ya kusaidia:
Usaidizi wa kimwili na kiroho: Mwenyezi Mungu Atawaondoa maadui wenu na kukupa uthabiti katika vita au shida.
Thabiti katika msimamo wako: Atakufanya uwe imara katika mafundisho ya Kiislamu bila kutetereka.

3. Muktadha wa kisiasa na kihistoria:
- Aya hii iliteremsha wakati wa vita kwa mujibu wa watafsiri kama Ibn Kathir, ikilenga Waislamu waliojipanga kujihami dhidi ya maadui wao. Inasisitiza umuhimu wa kujitolea kwa Mwenyezi Mungu kwa matokeo mazuri duniani na Akhera.

4. Matumizi ya kisasa:
Kwa mtu binafsi: Kujitoa kwa Mwenyezi Mungu kwa vitendo (k.v. kusali, kutoa sadaka, kufundisha Uislamu) kunaleta baraka na uthabiti.
Kwa jamii: Umoja na uadilifu katika mambo ya kidini na kijamii husababisha msaada wa Mwenyezi Mungu.

### Mithali ya Qur'an:
Aya hii inafanana na Sura Al-Imran (3:160): *"Mwenyezi Mungu Akitaka kukusaidia, hakuna anayeweza kukushinda.

haya majibu kutoka kwa ndugu yangu nilikujibu lkn hukuridhika,naona umerudia swala hilo hilo,nasema tena haya ndio majibu,lau huridhiki,basi tuangalie hoja nyengine expert wangu
SAWA, hapo nimesoma ila bado nahitaji unielekeze zaidi. Kwa nini unataka ukitoa maelezo mara moja yaeleweke kirahisi.
Swali linalokuja hapo ni kwamba,
Mungu anasema anataka kunusuriwa halafu hilo neno kunusuriwa mnalitoa mnaweka kusaidiwa. SAWA, twende hivo, Mungu anataka msaada wa kueneza dini yake. Kisha baadae mnasema Mungu hana haja na usaidizi wa mwanadamu. Hapo huoni kwamba yanahitajika maelezo mazuri zaidi ili mtu aelewe?
 
Wacha uongo wewe jibu haya maswali
1)shetani ibilisi yule aliye laaniwa laana ya milele ni dini gani?
2)je Muhammad kabla ya miaka 40 alikuwa dini gani au kafiri.
3)je Muhammad alisilimu au akusilimu ?
4)muongozo wa mwisho wa Mungu ni kitabu cha injili je Muhamad kabla ya kuoewa utume na kitabu alifuata muongozo upi ulio mwezesha kufikia daraja ya kuoewa utume au alikuwa KAFIRI NA NQ KUFIKIA UKAMFIKISHA DARAJA YA UTUME 🙄 ? Kama utatumia akili wote walio kuwa mitume walifuata muongozo wa kitabu vya nyuma yao sasa je Muhammad alikuwa ni mnasala na kwa huo kufikia daraja ya kupewa utume ? Kama siyo je muhamadi alifuata kitabu gani ikiwa akufuata injili ? Je utume wa Muhammadi msingi wake ulikuwa ni kitabu gani kabla ya kuupata? Utume na kupewa msahafu ?
Mtu akishakuja na anachokiamini ni ngumu kukuamini kma yule anokaribia kutapeliwa

{ وَعِبَادُ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلَّذِینَ یَمۡشُونَ عَلَى ٱلۡأَرۡضِ هَوۡنࣰا وَإِذَا خَاطَبَهُمُ ٱلۡجَـٰهِلُونَ قَالُوا۟ سَلَـٰمࣰا }
[Surah Al-Furqān: 63]

Na waja wa Arrahman Mwingi wa Rehema ni wale wanao tembea ulimwenguni kwa staha, na wajinga wakiwasemeza hujibu: Salama!

Kwaheri
 
Kumbe hawa watafsiri wa kiswahili ndo wamezingua sasa au sio mkuu!
Yap, nitafsiri tu ya kiswahili imebadili....
Unajua kuna maneno ambayo hayana neno kwa neno (kutoka lugha moja kwenda nyingine)
Hata ukitafsiri Kiingereza kuja kiswahili kuna maneno mengi sana ya kiingereza ila hayana neno moja la kiswahili lenye maana sawa..
 
Bora we kidogo umeeleweka kuliko wengine wao ni kujaribu kuitetea vile vile ilivyo.
 
SAWA, hapo nimesoma ila bado nahitaji unielekeze zaidi. Kwa nini unataka ukitoa maelezo mara moja yaeleweke kirahisi.
Swali linalokuja hapo ni kwamba,
Mungu anasema anataka kunusuriwa halafu hilo neno kunusuriwa mnalitoa mnaweka kusaidiwa. SAWA, twende hivo, Mungu anataka msaada wa kueneza dini yake. Kisha baadae mnasema Mungu hana haja na usaidizi wa mwanadamu. Hapo huoni kwamba yanahitajika maelezo mazuri zaidi ili mtu aelewe?
Kwanza sio dhumuni langu kwamba nikitoa majibu nataka mtu haelewe mara moja,huenda kuna mazingira yakafanya iwe hivyo

Tafsir ni tofauti na lugha halisi iliyokuja na qur'an,kwahiyo kwenye tafsir tegemea uwepo au matumizi ya maneno mbali mbali lkn kubwa yote yanatufikisha katika lengo moja

Mfano inasema Allah anamswalia Mtume,hapa si sahihi kwasababu haiwezekani Allah akamswalia Mtume ila humtakia rehema mja wake,huo ni mfano tu

Turudi kwenye swali lako,Allah hapa anakusudia kwamba kama watu hawakutakuwa tayar kufuata maagizo yake au amri zake,basi hana haja nao kwakuwa yeye sio mhitaji useme kwamba ataathirika kwa chochote,ila anaweza leta watu wengine ambao ambao watamnusuru/kumsaidia/kufuata maamrisho yake na hukumu zake
 
Mtu akishakuja na anachokiamini ni ngumu kukuamini kma yule anokaribia kutapeliwa

{ وَعِبَادُ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلَّذِینَ یَمۡشُونَ عَلَى ٱلۡأَرۡضِ هَوۡنࣰا وَإِذَا خَاطَبَهُمُ ٱلۡجَـٰهِلُونَ قَالُوا۟ سَلَـٰمࣰا }
[Surah Al-Furqān: 63]

Na waja wa Arrahman Mwingi wa Rehema ni wale wanao tembea ulimwenguni kwa staha, na wajinga wakiwasemeza hujibu: Salama!

Kwaheri
Mimi furaha yangu ni kuwaona mnakimbia hivyo hivyo 😁😁😁
 
Kitu ambacho siku zote kipo wazi ni kwamba,pamoja na wasio waislamu kuanzisha nyuzi za kuhoji Uislamu

Hoja hujibiwa na majibu ya kueleweka hupatikana,kwasababu Uislamu umenyooka,kinachobakia ni ushindani wa kipuuzi tu

Sasa hoji kuhusu Ukristo,hupati.majibu ya kueleweka ambayo akili itakinai,sana sana wanajificha kwenye kivuli cha Roho mtakatifu ambaye ni Malaika

Ukiwabana sana watasema ni nafsi tatu ndani ya moja,kwa maana nyingine Mungu ni Malaika,halafu Mungu katika umbile la binadamu na Mungu mwenyewe khaaa!!

Karibuni katika Uislamu tuwasilimishe,huku ni Mungu mmoja tu ambaye ndio muweza wa kila kitu,hakuzaa wala kuzaliwa na hakuna anayefanana naye hata mmoja kwa sifa zake na mwonekano wake

Lakini Mungu akiwa ndani ya Yesu alikula,alilala,na hata mkisema alikula kwasababu anaishi katika mwili, sasa mbona Malaika hubadilika katika umbile la wanadamu na hawali

Mfano walipoenda kuangamiza Sodoma na Gomora,walipitia kwa Ibrahim alayhi salamu,na wakatayarishiwa nyama safi ya kondoo au mbuzi

Je kama Malaika wanakaza hawali kwanini Mungu akiwa ndani ya Kristo asikaze kwa Uwezo wake angali viumbe vyake tu Malaika hawali

Wakijibu kwa hoja naomba mnishtue
Swali zuri sana expert wangu

Kwanza nikurekebishe kidogo expert wangu,Qur'an haijasema kwamba Pombe ilikuwa halali,kama una udhibitisho naomba uweke ubaoni hapa

Pili kwanza tujue kwanini inasemwa binadamu wote wamezaliwa katika asili ya Uislamu ukiwemo wewe let the caged bird sings

Wote tumezaliwa katika asili ya kuumbwa chini ya Mwenyezi Mungu mmoja tu,na wote tuna asili moja ambayo ni unyenyekevu kwa Mungu mmoja

Ila kinachotokea ni huyu kiumbe au mwanadamu kubadilishwa na wazazi wake ima awe mkristo,mbudda au mmajusi

Ndio maana inasemwa Adamu na umati zote zolizo pita walikuwa waislamu

Sasa kwa asili vitu vyote ni halali mpaka viharamishwe na Mwenyezi Mungu

Kwa asili watu walikuwa wanakunywa pombe,mpaka pale alipokuja Mtume wa Mwisho Muhammad swalla aallahu alaihyi wa sallammu ndio Mwenyezi Mungu akaharamisha pombe

Kwahiyo ukisoma kwa mtazamo wa kuelewa hoja utakuwa umenielewa
Hio pepo ya waarabu unaitafuta kwa tabu sana
Nakujibu kwa hekima bila kukukejeli mkuu,Mungu (Allah) anazungumza kwa lugha ya picha tu.ni kama akisema ukimpa chakula maskini "umenipa mimi",ukitenda haki kwa wanyonge na binadamu wenzako bila kujali matabaka yao bas ni kama wema huo umemfanyia Mungu...hii haina maana kwamba Mungu anahitaji chochote kwetu sisi wanadamu..yeye amekamilika na anajitosheleza kwa kila namna hahitaj chochote katika viumbe alivyoviumba.nadhan nimekujibu kwa hekima Clever505
Hizi tunaita ni hekima za abunuasi 😂

Mtajinasibisha nao lakin kamwe hamtakua kama wao
 
Back
Top Bottom