Expert wangu chill twende taratibu
Ngoja kwanza nikwambie asili kwanini watu wanaabudu masanamu
Iko hivi asili ya watu kuabudu masanamu imetokana na watu kuwapenda huenda watu wao wa zamani,wakaamua kuwajengea masanamu,awali si kwa lengo la kuwaabudu,lakini kadri muda unavyoenda kizazi kipya ambacho hakijui ufahamu kwanini hayo masanamu yalikuwepo ndio huanza kuyaabudu
Kwa taarifa yako tu, washirikina wa Makka by that time walikuwa wana miungu 365,kwa maana kila siku fulani ina Mungu wake
Kwahiyo hao miungu wao uliowataja wakawanasibisha kwamba ni mabinti wa Allah kitu ambacho si kweli
Tukija kwenye ibada ya kuzunguka al kaaba,kwanza lile sio jiwe jeusi bali ni kama mfano wa chumba ambacho kimefunikwa na pazia jeusi,ingawa katika moja ya kona kipande kidogo cha jiwe ambacho legend inasema kilikuwa cheupe kutoka peponi ila kimekuwa cheusi kutokana na kushikwa kwa wanadamu,kutokana na madhambi yao
Kwahiyo washirikina,kabla ya Mtume Muhammad swalla aallahu alayhi wa sallamu,walikuwa wanafanya ibada za kishirikina,ila awali kabisa ilikuwa ni nyumba ambayo wenye kumuamini Allah walikuwa wanafanya ibada baaada ya kujengwa kwa mara ya pili na nabii Ibrahim
Baada ya ujio wa Muhammad swalla aallahu alaihy wa sallamu ndio ikarudishwa kwenye ibada sahihi,ambapo mpaka leo waislamu wanatekeleza ibada zao