Ertugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 14,705
- 30,041
Katika wakristo ambao kidogo wanaweza kujitahidi kufanya mjadala nawe upo kwa kiasi fulaniKwanza inaonekana dini yako huijui , CHATGPT itakupoteza, halafu kabla hujamzushia Yesu na manabii wengine kuwa walikuwa dini ya waislamu,twende taratibu ,nimeona hapo unatumia Biblia kutaka kupotosha ,Vema ...., kabla sijaingia kwenye majibu ya hoja zako, nataka nikuulize swali moja rahisi
Je, unaamini Biblia kama Neno la Mungu?
Kama jibu lako ni ndio,maana umetumia hapo kupotosha , basi tutatumia Biblia kama msingi wa kuelewa Yesu ni nani, alifundisha nini, na kama kweli alikuwa Muislamu au la.
Sasa tuje kwenye hoja zako
Kwanza Uislamu si jina la imani ya mitume wote, bali ni dini iliyoanza karne ya 7 A.D.,ni dini iliyokuja na Muhammad,kabla ya hapo hakuna na hakukuwahi kuwepo dini au imani ya Uislamu,kama unabisha leta ushahidi wa kihistoria,kiakolojia au kimaandiko ..
Ni kweli mitume waliomtangulia Muhammad walimwabudu Mungu mmoja Tena aitwaye YWHW.
Lakini hilo halimaanishi kwamba walikuwa Waislamu, kwa maana ya kufuata dini ya Uislamu kama tunavyoifahamu leo.
Biblia haijawahi kumuita Abrahamu, Musa au Yesu kuwa "Waislamu" kwa jina hilo,kama una Aya au maandiko yaweke hapa
Dini ya Uislamu ulikuja na Muhammad, hivo huwezi kuwaita waliomtangulia kwa jina ambalo halikuwepo wakati wao.
Huo ni upotoshaji wa kihistoria.
Yesu hakuwahi kufuata Uislamu, bali alifuata sheria za Kiyahudi na kumtaja Mungu kama Baba., hii ni kwa Mujibu wa maandiko ambayo yapo kabla ya Muhammad kuja na uislamu
Nimeona umenukuu Yohana 20:17 “Ninapanda kwa Baba yangu na Baba yenu, kwa Mungu wangu na Mungu wenu.”
Ndugu yangu, hapa Yesu anaonesha uhusiano wa karibu sana kati yake na Mungu anamuita Baba, kitu ambacho Uislamu unakikataa kabisa.
Qur’an inasema:
"Hapana mtoto wa Mungu..." (Surah Al-Ikhlas 112:3)
Uislamu unamkataa Mungu kuwa Baba wa mtu yeyote. Lakini Yesu alifundisha mara kwa mara kumuita Mungu Baba,Umeona ulivyojichanganya ,unatumia Biblia kutaka kupotosha
Mathayo 6:9: Yesu anasema “Baba yetu uliye mbinguni...”
Yohana 14:9 Yesu anasema “Aliyeniona mimi amemwona Baba.”
Kwa hiyo, Yesu alikuwa na mafundisho tofauti na ya Kiislamu aliyokuja nayo nabii wa uongo Muhammad kuhusu asili ya Mungu.
Yesu pia alifundisha kwamba yeye ni zaidi ya nabii alidai Uungu.,Yesu sio nabii tu, Kwanza tofautisha Yesu na tapeli Issa wa Quran ,
Katika Yohana 10:30, Yesu alisema:
“Mimi na Baba tu umoja.”
Wayahudi walipoisikia hiyo, walitaka kumpiga kwa mawe kwa sababu alijifanya sawa na Mungu. (Yohana 10:33)
Je, nabii wa kawaida au Muislamu angeweza kusema hivyo? NAJUA HUWEZI KUJIBU HILI
Pia Yohana 1:1,14 inasema
“Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwa kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu... Neno akafanyika mwili...”
Huu ni ushahidi wa wazi kwamba Yesu ni Mungu aliyefanyika mwili jambo ambalo Uislamu hulikataa kabisa.
Kuhusu Marko 12:29 Yesu alithibitisha Mungu ni mmoja, lakini si kwamba yeye hakuwa Mungu.
Umoja wa Mungu (Tauhidi) haupingani na Utatu Mtakatifu.
Katika Ukristo, Mungu ni mmoja, aliye katika nafsi tatu: Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.
Hii ni tofauti na “Tauhidi” ya Kiislamu inayomkana Yesu kuwa Mungu.
Yesu kufundisha Mungu mmoja haimaanishi yeye hakuwa Mungu – bali alikuwa sehemu ya huo Umoja mmoja wa Kimungu (Divine Unity).
.Yesu hakuwahi kufuata nguzo za Uislamu kama Shahada, Swala ya Kiislamu, Saumu ya Ramadhan, Zaka ya Kiislamu, wala Hija.,kama una ushahidi wowote weka hapa
Hizi nguzo tano za Kiislamu zilikuja baada ya Yesu, na hazikuwahi kufundishwa naye.
Yesu alifundisha kutubu dhambi, kupenda adui, msamaha na msalaba. Hakuwahi kufundisha kupigana vita kwa jina la dini.
Ertugrul Bey naomba uje ujibu hoja sio kukimbia hoja ,
Nitarudi kujibu comment hii,uwe na subira mimi sio moderator kwamba nakuwa online mda wote,nashughulishwa na mambo mengine,baadae!