Je, wajua kwamba kunguni wanasumbuwa Ulaya na Marekani? Kama na wewe unasumbuliwa na kunguni hii ndio sumu kiboko yao

Je, wajua kwamba kunguni wanasumbuwa Ulaya na Marekani? Kama na wewe unasumbuliwa na kunguni hii ndio sumu kiboko yao

Dr Matola PhD

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2010
Posts
60,050
Reaction score
104,466
Kunguni ni wadudu wadogo wa familia ya Cimicidae Wadudu hawa huishi kwa kufyonza damu ya wanyama wenye damu moto (mamalia na ndege). Spishi hii huishi mara nyingi katika vitanda vya watu na masofa majumbani kwetu.

Watu wengi kwakutokuelewa wanadhani na wanaamini kunguni uwapata watu wachafu kitu ambacho hakina ukweli wowote.

Nakumbuka mwaka 1997 nilikuwa Slough UK katika misele yangu kitaa nilikuta mzungu ametupa kitanda kipya nje bed and mattress nilishangaa sana najuwa Uingereza kutupa vitu ni kawaida lakini kile kilikuwa ni almost brand new, nilitaka kukichukuwa kile kitanda nikaambiwa kina kunguni nilicheka sana sikuelewa maana yake nikasepa, nimekuta mkasa wa kunguni Italy, pia South Africa ndio wakumwaga wanawaita nakumba kwa kizulu na kixosa, sijawahi kufika Marekani lakini nimeambiwa na rafiki zangu huko napo kunguni wanatesa kama kawa.

Watanzania wengi jambo la kusema nyumbani kwake amevamiwa na kunguni anaona ni jambo la fedhea na aibu basi uendelea kutaabika nao na kuishi bila furaha na wengine uhama vyumba.

Sasa baada ya kuona hili tatizo ni serious leo nitawapa dawa ya kuwatekeza kunguni kwa 100% katika kategory mbili, note nimefanya research ya hawa viumbe kwa zaidi ya miaka 10 hatupigi ramli hapa.

Category A hii ni kwa watakaomudu gharama maana bei zake zimechangamka kidogo kwwnye maduka ya dawa za mifugo.

1) Nuvan 500 EC 1litre = 55,000/=
2) Ultracya 1 litre = 25,000/=
1 litre = 1000 mililitres (mls)

Mchanganyiko:


200 mls Nuvan + 100 mls Ultracya Kwenye 15 litres of water.

Tumia mchanganyiko huu wa dawa na ukiisha changanya tena na uendelee kutumia mpaka utakapomaliza kutumia nyumba yote!

Chemical itakayobaki unaweza kutumia huo mchanganyiko kuflashi vyooni kuua wadudu! Ikibaki tunza mbali na watoto!!

Vaa gloves na ufunike pua ama kwa mask au kitambaa cha aina ya taulo taulo ili usivute hewa yake while handling it!

Spray kwenye godoro pande zote mpaka lilowe na uanike nje! Usilalie mpaka likauke kabisa

Spray asubuhi ili uanike mchana kutwa! Ukiweza anika juu ya bati!
Spray kwenye chaga zote zilowe na kitanda chote kilowe kisha anika nje

Spray kwenye kuta zote, milango na fremu, madirisha na fremu, na chini
Spray kwenye sofas au coaches pande zote zilowe na uanike nje! Usikalie mpaka yakauke kabisa!
Vikorokoro visivyotumika vyumbani vitolewe!

Nguo zinazotundikwa vyumbani zifuliwe na kupigwa pasi!
At least kwa kufanya haya utaweza kuwadhibiti!!

Category B hii kwa wenye uwezo mdogo lakini ni ya uhakika mia kwa mia, nunuwa mafuta ya taa liter moja au zaidi inategemea na mahitaji yako, sabuni ya unga Omo nasisita Omo na chumvi ya unga pakti moja, changanya huo mchanganyiko jaza kwe chomo cha kuweza kusplay au tobowa chupa ya maji kwenye kizibo ili ujaze dawa humo.

Ubarikiwe!

Kwa wale ambao hata kukata kucha zao wenyewe hawawezi mpaka wakatwe kucha na muuza urembo, basi unaweza kuwasiliana nami atakuja kijana mtaalam wa wadudu kuja kukutokomezea hawa wadudu wasumbufu kwenye machimbo yao yote.

Hii ni gurentee never fail, no more tears.
 
1. Lipia Tangazo.

2. Ahsante sana kwa Elimu.

3. Naomba kuongezea mojawapo ya njia nyingine isiyo rasmi lakini inafanya kazi vizuri sana ni kuhama nyuma au sehemu unayokaa kwa kuitelekeza kisha urejee baada ya siku 20.
 
Naomba unitajie Viambata vilivyomo kwenye hiyo Dawa Ya Kunguni (Nuvan 500 EC) Tafadhali
 
Maji ya moto unaweza kudeki ndani na kuloweka nguo.

Hizo sumu hapo juu ni bomu la nyuklia kwa kunguni never fail.
Why not? Secondary tumeloweka hadi godoro kwenye maji ya moto. Tatizo hizo dawa zinaua kunguni hai na kuacha mayai yao which later yatahatch na tatizo linarudi palepale. But maji moto yanaua both kunguni na mayai yao.
 
Maji ya moto unaweza kudeki ndani na kuloweka nguo.

Hizo sumu hapo juu ni bomu la nyuklia kwa kunguni never fail.
Hizo zinaua kunguni ila sijajua kuhusu mayai yake

Yale mayai ni msala kwanza hayahitaji kuatamiwa ili yatotoke, sijajua yana hidden incubator ndani yake au namna gani
 
Hizo zinaua kunguni ila sijajua kuhusu mayai yake

Yale mayai ni msala kwanza hayahitaji kuatamiwa ili yatotoke, sijajua yana hidden incubator ndani yake au namna gani
Kila kitu kina elimu yake mkuu, hakuna sumu itakayouwa uwa kunguni yai lisalimike, kinachotokea ni watu kutojuwa exactly machimbo ya hawa jamaa.

Wapo wanaohisi mpaka kunguni ni ushirikina.
 
Write your reply, dawa ya kunguni ni maji ya moto kama yakunyonyolea kuku.

Why not? Secondary tumeloweka hadi godoro kwenye maji ya moto. Tatizo hizo dawa zinaua kunguni hai na kuacha mayai yao which later yatahatch na tatizo linarudi palepale. But maji moto yanaua both kunguni na mayai yao.
Hakuna aliyewakataza kutumia maji ya moto, sijakurupuka kuandika nilichoandika, nina reseach ya kutosha kuhusu hawa wadudu.
 
hata mwezi nenda urudi afu ulale uone mziki wake..
hawa jamaa wanakuwaga wembamba km kiwembe kwa njaa lakini hawafi.ni mdudu sugu sijapata kuona.
aisee walinitafuna siku ya kufungua shule na nilivyokuwa mgum kuwahisi ila hiyo siku waliniweza. Nilikoma kuwahi shule , nikikumbuka hiyo huwa naishia kucheka tu.
 
Kuna wakati Niko A-level bwenini kwetu kulikuwa na kunguni kibao, Hakuna kulala hata mchana.

Tuka-organize Mimi na mwenzangu wa Decker ya chini, tukanunua Rungu spray tukapiga kwenye kitanda. Kunguni tuakangaa wakaisha chumba kizima.
 
1. Lipia Tangazo.

2. Ahsante sana kwa Elimu.

3. Naomba kuongezea mojawapo ya njia nyingine isiyo rasmi lakini inafanya kazi vizuri sana ni kuhama nyuma au sehemu unayokaa kwa kuitelekeza kisha urejee baada ya siku 20.
🤣🤣🤣
 
Hao wadudu wanakosesha Sana raha, niliaibika siku moja demu kaja gheto halafu alikuwa white, walimshambulia balaa, natoka job night shift namkuta kalala chini nikamuuliza kulikon akanambia humu mwako Kuna mifugo mingi Sana fanya utaratibu wa kuwaangamiza, nikampa pole tu
 
Sawa Sawa
Chap Mafuta Ya Taa, Omo, Chumvi
Naiona Imekaa Sawa Sawa
 
Back
Top Bottom