a sinner saved by Christ
JF-Expert Member
- Feb 19, 2017
- 611
- 993
Kabla ya hizo dini hao watu waliishije?Amezungumzia ustarabu wa nchi za kiislaam na nchi za kikristo na ushaidi kaweka ila bado ligi ni mbichi.
Mimi siamini kama nchi hii kuna sehemu pana maji ya kutosha lakini watu hawanawi maji,huu mfano wako ni illogical kwa sababu huwezi ukaniaminisha hapa kwamba ilikuwaje mpaka hao unaoita workmates zako wajue ulinawia maji ulipoenda haja.Mi ni mkristo ila situmii tishu/karatasi kujisafisha chooni, natumia maji. Kuna wafanyakazi wenzangu wa dini yangu walinishangaa na kuniona ni mchafu/mshika kinyesi wakati wa kujisafisha chooni na walinionea kinyaa wakidhani nina mabaki ya kinyesi kwenye vidole vyangu vya mkono
Hii ligi ngumu hii watatifuana watu hapa mpaka kieleweke kwamba Ismail sio mzaliwa wa kwanzaHizi dini kuu zote mbili, Wakristo na Waislamu, ni watoto wa baba mmoja Nabii Ibrahim, Waislamu ni uzao wa mzaliwa wa kwanza, Ismail, na Wakristo wa ni uzao mzaliwa wa pili, Isaka.
Tafadhali sana. Siyo matumizi ya maji kama wanavyofanya huko uswazi. Unakuta choo kina ndoo kubwa imejazwa maji na kopo kwa pembeni, eti maji ya kutawazia. Kla mtu anashika hilo hilo kopo na kuliloweka kwenye maji, na mbaya zaidi hawaweki sabuni. Bora nitumie toilet paper kuliko nitumia maji ya aina hiyo.Use water coz ur arse is worth it!
Jamaa kafunga kamba pengine.Mimi siamini kama nchi hii kuna sehemu pana maji ya kutosha lakini watu hawanawi maji,huu mfano wako ni illogical kwa sababu huwezi ukaniaminisha hapa kwamba ilikuwaje mpaka hao unaoita workmates zako wajue ulinawia maji ulipoenda haja.
Maswali ni mengi uliwaaga unaenda choo?ok sawa uliwaaga lakini pia uliporudi ukawaambia ulinawia maji?what for,yaani kabisa ”amenawia maji ana kinyesi mkononi huyo” yaani kabisa haya ndiyo yalikuwa maneno ya wafanyakazi wenzako?andika vitu vyenye kuleta maana bro.
Ndiyo shida inapokuja pale unapoamua kuugeuza utaratibu wako binafsi na famili kuwa ni wa dini kisa tu wewe ni wa dini hiyo.Wanabodi,
Kama kawa kila nipatapo fursa, huja na kwa maslahi ya taifa.
Mimi kama mwandishi wa habari, ni muelimishaji umma, ukiona jambo zuri la jamii fulani, waelimishe na wengine wafuate.
Hii ni mada ya swali Je Wajua Kwenye Usafi wa Mwili, kuna uwezekano Waislamu ni Wasafi Zaidi ya Wakristo?. Waislamu Hujiswafi kwa Maji, Wakristo kwa Karatasi!, Huku Sio Kujipaka?.
Jambo la leo ni usafi binafsi wa mwili, baada ya kupunguza uzito, wenzetu Waislamu na nchi za Kiislamu, wanatumia maji kujiswafi, lakini Wakristo na nchi za Kikisto wanatumia karatasi laini, toilet paper, kujiswafi kwa kujifuta baada ya ile shughuli, hapa nauliza ni kujifuta au pia kujipaka?.
Hizi dini kuu zote mbili, Wakristo na Waislamu, ni watoto wa baba mmoja Nabii Ibrahim, Waislamu ni uzao wa mzaliwa wa kwanza, Ismail, na Wakristo wa ni uzao mzaliwa wa pili, Isaka. Sheria ya Mungu wa dini zote mbili ni sheria moja ya Musa iliyoshushwa kwenye torati.
Kwenye sheria hiyo, Mungu alielekeza namna ya kujiswafi, kabla hujaenda mbele zake na kuelekeza kabisa, lazima unawe kwa maji tiririka!.
Ukristo ulipoingia, wakabadili baadhi ya mambo, ikiwemo kutumia karatasi laini kujiswafi baada ya ile shughuli. Katika pita pita yangu nchi nyingi za Kiislamu, kwenye public toilets zao, kuna maji tiririka, lakini kwenye nchi za Kikristo, kuna TP!.
Sisi Tanzania kwasababu nchi yetu haina dini, public toilets zetu zina both, maji tiririka na TP. Ukisafiri kutokea Dar kwenda Dubai, Doha, Muscat, UAE, kote huko kwenye public toilets zao, utakuta maji tiririka, na TP. Ukienda SA, London, Paris, New York, kwenye public toilets zao, kuna TP only hakuna bomba lolote la maji!.
Japo TP inasafisha, kwa vile ni kavu, inasafisha kwa kupaka, huwezi kulinganisha na maji tiririka ambayo yanasafisha kabisa compared to TP.
Kwa vile sheria ya usafi wa mwili imeelekezwa kidini, na ni Waislamu wanaitekeleza kama Mungu alivyoelekeza, hivyo kuna uwezekano kwenye usafi wa mwili, tukubali tukatae, Waislamu ni wasafi zaidi kuliko Wakristo, na kwa kulijua hilo na umuhimu wa usafi, wanawake wa kisasa wenye kujijali, wanatembea na wipes, na nyumba nyingi za kisasa wanatumia maji tiririka.
Kwa wenzetu Waislamu, wale hata wale wenzetu wao, wakiwa kwenye hali fulani ile, huwa hawafungi na hawaruhusiwi kwenda kuswali Masjid au Msikitini, lakini sikuwahi kusikia hili kwa Wakristu, hivyo wenzetu wale, hata wakiwa kwenye ile hali, wanatinga tuu ibadani mbele za Mungu!, hivyo inawezekana kwenye usafi binafsi, wanawake wa Kiislamu ni wasafi kuliko wanawake wa kikristo?.
Tena usikute usafi huu kwa Waislamu sio usafi tuu wa mwili, ni mpaka moyo na roho, ndio maana wanawake wa Kiislamu wanaweza kuvumilia na kustahimili uke wenza, na ingefanywa survey ya ni wanawake gani akiwa mama wa kambo, anatesa watoto wa aliyemtangulia, a wicked stepmother, mngeshangazwa na matokeo.
Kuna vitu vingi wazungu wametupotosha sisi Wakristo ikiwemo hoja ya mke mmoja, sio mpango wa Mungu, ndio maana nilimpongeza yule Blaza wangu na kumshauri "Pongezi Rais Magufuli Kuwa Mkweli Daima. Tuanzishe Church of Africa, Tuoe Wake Wengi, Tuzae Watoto Wengi?"
Nani aliwaambia wazungu na nchi za Kikristo TP tuu inatosha?.
Nimepandisha bandiko hili kufuatia mimi ni mpenda kula kula vyakula locals kila ninaposafiri, Uliwahi kula vyakula gani kutoka sehemu mbalimbali Duniani ukafaidi? sasa sometimes, tumbo linachafuka ukiwa safarini, inakubidi ujiswafi kwa maji tiririka, tumbo linapokutibuka, ukakuta hakuna maji ni TP pekee ni shughuli, hivyo nimekereka sana na hili!. Hawa wazungu vipi?.
WHO wanapaswa watoe muongozo na maelekezo, public washrooms zote lazima ziwe na maji tiririka na TP, ili wale wa kunawa, wawe huru wanawe na wale wa kujipaka, waendelee kujipaka!.
Paskali
Rejea za mleta mada kuhusu Waislamu na Wakristo
- Waislamu mliofanikiwa kwa Elimu ya Shule za Mission badala ya Madrasa kuweni na Shukrani kwa Wakristo waliowafikisha hapo mlipo
- Japo Wakristo na Waislamu ni Watoto wa Baba Mmoja, Nabii Ibrahim na Mungu ni Mmoja, Kati ya Ismail na Isaka ni nani aliyetolewa Sadaka ya Kuchinja?
- Je, wajua Wakristo huwasindikiza Waislamu Kufunga Ramadhan? Leo ni Jumatano ya Majivu, Wakristo tutafunga siku 40, vipi Waislamu Mtatusindikiza?
- Mwarobaini wa Kweli wa Mahakama ya Kadhi ni Huu, Wakristo, Waislamu, Kuukubali Bila Matatizo!.
Kwa hiyo ulijisaidia na kujitawaza mbele ya masela?? Wewe lazima utakuwa una kasoro siyo bure. Yaani unatunga uongo kwa gharama ya kujidharirisha na wala hata haujali.Mi ni mkristo ila situmii tishu/karatasi kujisafisha chooni, natumia maji. Kuna wafanyakazi wenzangu wa dini yangu walinishangaa na kuniona ni mchafu/mshika kinyesi wakati wa kujisafisha chooni na walinionea kinyaa wakidhani nina mabaki ya kinyesi kwenye vidole vyangu vya mkono
Usafi mpaka uelekezwe na maandiko? Mbona hizi dini zinawachanganya sana? Kutumia karatasi au maji ni uamuzi wa mtu/familia au jamii. Toilet paper zimetengenezwa kwa ajili hiyo. Maji nayo yakitumiwa kwa njia ya usafi yanafaa na siyo wanavyoweka ndoo ya maji chooni ikiwa na kopo na kila mtu anatumia. Huko ni kujipaka uchafu.Kuna fundisho lolote la kwenye injili linalotaka wanaomwamini Yesu wawe wana jitawaza kwa makaratasi? Hio ya ya wakristo wote umeipata wapi, au ni katekisimu ndio imeagiza?
Kipindi hiki jiandaeni, watu wanakuja na kila aina ya vituko wakilenga kumfurahisha mkuu wa nchi. Kuna mwingine sasa hivi anajiita Abubakar, na ameagiza akifa azikwe kwa taratibu za kidini ya akina Abubakar.Sidhani kama ni wewe Paschal Mayala, the great thinker. Au kuna mtu ka hack account yako? Tunategemea utuletee nini kifanyike Dar tupate maji ya kutosha. Kinyume chake 'Great thinker' unakuja na hoja ya takutumia maji mengi kusafishia vinyeo. Grow up Paschal, you can do better than this.
Ah,kumbe huyu ni Msukuma?Hapa ndo unamkumbuka muendazake na Ile kauli ya kwamba "mayalla kwa kikwetu ni njaa", kwamba watu walikuwa hawakati gogo kabla ya Kuja ukristo na uislamu ili wafundishwe jinsi ya kujisafisha.
Mbona una panic, Mimi siamini suala hili la maji au hapana lina udini. Mtoa mada katumia neno wakristo na waislamu japo yeye ni mkristo. Mimi siamini kwenye hili sasa labda mwenzetu ana ushuhuda na anachosema. Ndio maana nimeuliza kwa nia safi tu kwani vyoo makanisani havina maji? maana kama udini nategemea jibu hakuna maji basi kama vina maji mtoa mada inabidi arekibishe tu kutotumia maji halishikamani na dini. Mwenzangu ume panic kama umetukanwa.Kwa akili za kawaida unadhani inawezekana visiwe na maji?nikisema havina utaamini eti?
Yaani engineer anayejenga bar aweke system ya maji lakini anayejenga Kanisa asiweke hii inaingia akilini?mbona mnakuwa na dharau sana nyie,mna nini cha ziada dunia hii?
Hata waliojenga airport Ethiopia na Nairobi ni ma Engineer pia lakini hakuna maji chooni, unasemaje hilo.Kwa akili za kawaida unadhani inawezekana visiwe na maji?nikisema havina utaamini eti?
Yaani engineer anayejenga bar aweke system ya maji lakini anayejenga Kanisa asiweke hii inaingia akilini?mbona mnakuwa na dharau sana nyie,mna nini cha ziada dunia hii?