Wanabodi,
Kama kawa kila nipatapo fursa, huja na kwa maslahi ya taifa.
Mimi kama mwandishi wa habari, ni muelimishaji umma, ukiona jambo zuri la jamii fulani, waelimishe na wengine wafuate.
Hii ni mada ya swali Je Wajua Kwenye Usafi wa Mwili, kuna uwezekano Waislamu ni Wasafi Zaidi ya Wakristo?. Waislamu Hujiswafi kwa Maji, Wakristo kwa Karatasi!, Huku Sio Kujipaka?.
Jambo la leo ni usafi binafsi wa mwili, baada ya kupunguza uzito, wenzetu Waislamu na nchi za Kiislamu, wanatumia maji kujiswafi, lakini Wakristo na nchi za Kikisto wanatumia karatasi laini, toilet paper, kujiswafi kwa kujifuta baada ya ile shughuli, hapa nauliza ni kujifuta au pia kujipaka?.
Hizi dini kuu zote mbili, Wakristo na Waislamu, ni watoto wa baba mmoja Nabii Ibrahim, Waislamu ni uzao wa mzaliwa wa kwanza, Ismail, na Wakristo wa ni uzao mzaliwa wa pili, Isaka. Sheria ya Mungu wa dini zote mbili ni sheria moja ya Musa iliyoshushwa kwenye torati.
Kwenye sheria hiyo, Mungu alielekeza namna ya kujiswafi, kabla hujaenda mbele zake na kuelekeza kabisa, lazima unawe kwa maji tiririka!.
Ukristo ulipoingia, wakabadili baadhi ya mambo, ikiwemo kutumia karatasi laini kujiswafi baada ya ile shughuli. Katika pita pita yangu nchi nyingi za Kiislamu, kwenye public toilets zao, kuna maji tiririka, lakini kwenye nchi za Kikristo, kuna TP!.
Sisi Tanzania kwasababu nchi yetu haina dini, public toilets zetu zina both, maji tiririka na TP. Ukisafiri kutokea Dar kwenda Dubai, Doha, Muscat, UAE, kote huko kwenye public toilets zao, utakuta maji tiririka, na TP. Ukienda SA, London, Paris, New York, kwenye public toilets zao, kuna TP only hakuna bomba lolote la maji!.
Japo TP inasafisha, kwa vile ni kavu, inasafisha kwa kupaka, huwezi kulinganisha na maji tiririka ambayo yanasafisha kabisa compared to TP.
Kwa vile sheria ya usafi wa mwili imeelekezwa kidini, na ni Waislamu wanaitekeleza kama Mungu alivyoelekeza, hivyo kuna uwezekano kwenye usafi wa mwili, tukubali tukatae, Waislamu ni wasafi zaidi kuliko Wakristo, na kwa kulijua hilo na umuhimu wa usafi, wanawake wa kisasa wenye kujijali, wanatembea na wipes, na nyumba nyingi za kisasa wanatumia maji tiririka.
Kwa wenzetu Waislamu, wale hata wale wenzetu wao, wakiwa kwenye hali fulani ile, huwa hawafungi na hawaruhusiwi kwenda kuswali Masjid au Msikitini, lakini sikuwahi kusikia hili kwa Wakristu, hivyo wenzetu wale, hata wakiwa kwenye ile hali, wanatinga tuu ibadani mbele za Mungu!, hivyo inawezekana kwenye usafi binafsi, wanawake wa Kiislamu ni wasafi kuliko wanawake wa kikristo?.
Tena usikute usafi huu kwa Waislamu sio usafi tuu wa mwili, ni mpaka moyo na roho, ndio maana wanawake wa Kiislamu wanaweza kuvumilia na kustahimili uke wenza, na ingefanywa survey ya ni wanawake gani akiwa mama wa kambo, anatesa watoto wa aliyemtangulia, a wicked stepmother, mngeshangazwa na matokeo.
Kuna vitu vingi wazungu wametupotosha sisi Wakristo ikiwemo hoja ya mke mmoja, sio mpango wa Mungu, ndio maana nilimpongeza yule Blaza wangu na kumshauri
"Pongezi Rais Magufuli Kuwa Mkweli Daima. Tuanzishe Church of Africa, Tuoe Wake Wengi, Tuzae Watoto Wengi?"
Nani aliwaambia wazungu na nchi za Kikristo TP tuu inatosha?.
Nimepandisha bandiko hili kufuatia mimi ni mpenda kula kula vyakula locals kila ninaposafiri,
Uliwahi kula vyakula gani kutoka sehemu mbalimbali Duniani ukafaidi? sasa sometimes, tumbo linachafuka ukiwa safarini, inakubidi ujiswafi kwa maji tiririka, tumbo linapokutibuka, ukakuta hakuna maji ni TP pekee ni shughuli, hivyo nimekereka sana na hili!. Hawa wazungu vipi?.
WHO wanapaswa watoe muongozo na maelekezo, public washrooms zote lazima ziwe na maji tiririka na TP, ili wale wa kunawa, wawe huru wanawe na wale wa kujipaka, waendelee kujipaka!.
Paskali
Rejea za mleta mada kuhusu Waislamu na Wakristo