Je, wajua nini hutokea katika Ulimwengu wa Roho wawili wanapoungana katika NDOA Takatifu?

Immanuel haikuwa Jina la Mtu mkuu Wala haikuwa Tafsiri yake kuwa Ni mtu mmoja..

Sasa kwa concepts hiyo Naomba Tafsiri ya Hili andiko ambalo pia limetumia Immanuel...

Isaya 8:8
[8]naye atapita, atapita kwa kasi na kuingia Yuda; atafurika na kupita katikati, atafika hata shingoni; na kule kuyanyosha mabawa yake kutaujaza upana wa nchi yako, Ee Imanueli.


Biblia yaoo inasema Usiongeze neno mbona unaongeza maneno kwenye 1 Yohana 4 ?

Kuhusu yesu Kuwa Mungu tulishafunga Huu mjadala siku nyingi maana hukunijibu hoja zangu kwenye Ile nyuzi yako ya Uungu wa Yesu...

Na Yesu anakiri Yeye ni Mtu..

Yohana 8:40
Lakini sasa mnatafuta kuniua mimi mtu ambaye nimewaambia iliyo kweli, niliyoisikia kwa Mungu. Ibrahimu hakufanya hivyo.
Je Mungu aweza kuwa Mtu ?

Hesabu 23:19 :
Mungu si mtu,
hata aseme uongo; wala si binadamu, hata abadili akasema jambo na kulitimiza; Je! Ananena wala hatalitimiza? Au anavyoongea na hatalifanya?"

Mungu si Mtu wala Mwanadamu...
lakini yesu vyote amekiri Kuwa navyo Yesu amekiri kuwa Yeye ni Mtu na pia amekiri kuwa ni Mwana wa Adam (Mwanadamu)
sasa Mkuu kwenye hiki tulifunge au tuendelee
 
(Mathayo 1:23) Tazama Bikra atachukua mimba, naye utamwita Jina lake Immanuel imerudiwa tena kitabu Cha Mathayo kudhihirisha kuwa Immanuel ndiye Yesu sawasawa na Kitabu Cha Isaya.

Ndomana nasema, wewe unaongozwa na Roho ya mpinga kristo sababu, huamini juu ya Mungu kuja katika form ya mwanadamu,

Yaani Mungu pamoja na wanadamu.

Huna Roho wa Mungu, lazima uanguke kwenye kukufuru.
 
Usiyejazwa Roho mtakatifu huwezi Fungua code za Nabii Isaya.

Imerudiwa tena katika Mathayo 1:20 na kuendelea ikielezea Kuzaliwa Kwa Yesu.

Unahitaji kufundishwa, kumjua Yesu ni nani, wahitaji ufunuo wa Roho mtakatifu.
 
Swali la Nyongeza Je Unabii huo ulitimia?
Umekuja kwenye point nzuri sana japo sio swali nililouliza..

Sasa check hapa..

Mathayo 1:21,
Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.

Kwahyo unataka kusema Malaika Gabriel aliyepeleka Ujumbe kwa kina Maria na yusuph kuhusu jina la mtoto na Malaika aliyempa utabiri isaya walipata ujumbe tofauti?

Au malaika Gabriel hakusoma Utabiri wa Isaya badala ya kupeleka jina la Immanuel akapeleka jina la Yesu...
Maana hata kimaana majina haya ni tofauti

Sasa hapo Hilo fungu ulilotoa Ni most contradictory Theology ambayo kwa level yako ni ngumu kulijibu..
Isaya vs Mathayo 1:23...

Viko Contradicted na uhalisia ulivyokuwa ...

Lets say niseme kwamba..

Nitabiri kwamba Mwaka 2025 Rais atakayeshinda Tanzania ataitwa Juma..
Then ukafika mwaka 2025 akashinda Hassan..

Unatka niamini kwamba Hassan na Juma ni kitu kimoja kwa sababu wote ni waislam....au ni jina moja ...
Go and learn bro...

Kingine umehamisha mada ya swali nililokupa ni kutoka Isaya 8:8 ambalo na lenyewe lina jina La Immanuel..
Na haian muktadha wa Huyo yesu unalizungunziaje..
Kbla sijazungumzia kuhusu Hiyo unayoita bikra atachukua mimba..
Wakati kisarufi haimaanishi hivyo
 
Usiyejazwa Roho mtakatifu huwezi Fungua code za Nabii Isaya.

Imerudiwa tena katika Mathayo 1:20 na kuendelea ikielezea Kuzaliwa Kwa Yesu.

Unahitaji kufundishwa, kumjua Yesu ni nani, wahitaji ufunuo wa Roho mtakatifu.
Hahaha Nakubaliana na wewe kabisa imerudiwa ila haikutimia wala utabiri haukufanyiwa kazi vipi kuhusu hilo?
 
Mkuu,
Anajitahidi sana kutetea ila anakosa utulivu wa kujibu anachoulizwa.

Lakini ana kitu serikali imuendeleze🤣🤣
 
Ndo nakwambia, unahitaji ufunuo wa Roho mtakatifu kumjua Yesu ni nani!!

Messiah alitabiriwa kuwa ni mwana wa Daudi, na atokaye katika ukoo huo kabila la Yuda ni Yusuph ambaye KIMWILI alitambilika kama baba wa Mwili wa Yesu, na ndicho waaminicho Wayahudi Hadi Leo wasiookoka.

Bt kiuhalisia, baba wa Mwili wa Yesu ni Yesu mwenyewe, sababu Roho mtakatifu ndiye huyo huyo Roho wa Yesu,

Hizo inazoziita contradictions ndo chenga, Mungu aliwapiga WANADAMU,

Mungu akavaa mwili, akazaliwa na hawakumtambua.

Bado nitakuelewesha Polepole na kukuombea uelewe Yesu ni Mungu.
 
Bado huelewi,

Kwa kuwa Baba wa KIMWILI wa Yesu Si Yusuph, ndipo UKWELI unasimama kuwa Yesu ni Mungu aliyekuja katika mwili.

Got it?
 
Hahaha Anajitahidi kujibu nje ya Mada maana anaulizwa kingine anajustify kingine 😅😅
Ninaposema wewe ni mpinga kristo, HOJA yangu inasimama pale kuwa,

Wewe unaamini kuwa Baba wa Yesu KIMWILI ni Yusuph ilhali BIBLIA imeweka wazi kuwa Baba wa Yesu ni Yesu mwenyewe, Kwakuwa Roho mtakatifu, ndiye ROHO wa YESU.

Kuelewa Hilo ni Mungu akufunulie!!
 
Hicho ukichoandika mkuu umekisoma na wewe au umetuandikia sisi tusome...Maana kwa mtu mwenye Utimamu hawezi andika hivyo...

Yaani Yesu baba yake Ni Yesu 😅😅..
Na kingine kama ulikuwa Hujui basi leo jua kuwa Hata maryam Pia ni ukoo wa Daudi..

Na kuna vingi vya kuzungumza kuhusu Ukoo huu Japo Una poteza mnyororo Halisi kuwa Na ukweli kwamba yesu ni wa Ukoo wa Daud..
 
Umeona kama hapa alipojibu..
Hakuna mahali nimesema naamini kuhusu Baba wa Yesu....
Kingine Kasome mkuu Bado sana..

Kujiita Rabbon umekosea sana kwani kwa kukuona sasa hivi unapaswa kuwa mwanafunzi ...

Yaani uanze kwanza kufundishwa au kama mtoto unastahili kwanza maziwa kabla ya kula chakula kigumu..
Kama anavyosema Paulo katika

Waebrania 5:12
"Kwa maana, iwapasapo kuwa waalimu, (maana wakati mwingi umepita), mnahitaji kufundishwa na mtu mafundisho ya kwanza ya maneno ya Mungu; nanyi mmekuwa mnahitaji maziwa wala si chakula kigumu."

HIcho chakula
unachokula kwa sasa ni kigumu kuliko Umri wako kwahyo jitahidi kunywa maziwa kwNza...
 
Usipooa hutakiwi 1. kununua kahaba, 3. usijichue, 3. Wala usiwe shoga.

4. Uwe towashi, mwili wako uwe Sadaka Kwa Mungu.

Kama huwezi kuwa kati ya hao hapo juu, oa haraka mke mmoja tu.
get to your senses, kuoa na kununua dada poa hakuna tofauti
ni yale yale tu unatoa pesa huku ikibadilishwa jina

yule analipia rejareja, huyu analipia jumla,
mbaya zaidi, unalipia jumla kisha unatoa fedha zingine kumhudumia
 
Tizama Ufunuo wa unabii WA YESU kumhusisha na Immanuel. Katika Isaiah na Mathayo:

(ISAIAH 7:14)

Kwa hivyo, BWANA mwenyewe atawapa Ishara, Tazama bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita Jina lake IMMANUEL.

(ISAIAH 9:6-7).

6: Maana Kwa ajili yetu mtoto amezaliwa,

tumepewa mtoto mwanamume,

Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake, naye ataitwa JINA lake,

Mshauri wa AJABU, Mungu mwenye nguvu,

Baba wa Milele, Mfalme wa Amani .

7: Maongeo ya enzi yake na Amani, Hayatakuwa na mwisho kamwe,

Katika KITI Cha enzi Cha Daudi, na ufalme wake, kuthibitisha na kuutegemeza Kwa HUKUMU na Kwa HAKI,

Tangu sasa na hata milele, WIVU wa BWANA wa majeshi ndio utakaotenda hayo.

(MATHAYO 1: 1,) Kitabu Cha ukoo wa Ukoo wa Yesu Kristo, mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimu........

(MATHAYO 1: 18-23).

18: Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi, Mariam mama yake, alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana,alionekana ana mimba Kwa uweza wa Roho mtakatifu.

19: Naye Yusufu, mumewe Kwa vile alivyokuwa mtu wa HAKI, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha Kwa Siri,

20: Basi Alipokuwa akifikiri hayo, tazama, Malaika wa BWANA alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu mwana wa Daudi, usihofu kumchukia Mariam mkeo, maana mimba yake ni Kwa uweza wa Roho mtakatifu.

21: Naye atazaa mwana , nawe utamwita Jina lake Yesu, maana Yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.

22:Haya yote yamekuwa, Ili litimie neno lililonenwa na BWANA Kwa ujumbe wa Nabii akisema,

23:Tazama bikira atachukua mimba, naye atazaa mwana,

Nao watamwita Jina lake IMMANUEL .

Soma hapa Kwa makini nikueleweshe!!!
 
Sijajua mantiki ya hayo mafungu yako...
mafungu nayajua na nimeyafundisha saana miaka mingi ilopita kwa lugha zote Kihebrania,Kigiriki na kiswahili..
So naomba mantiki ya Mafungu hayo kwNza
 
Sijajua mantiki ya hayo mafungu yako...
mafungu nayajua na nimeyafundisha saana miaka mingi ilopita kwa lugha zote Kihebrania,Kigiriki na kiswahili..
So naomba mantiki ya Mafungu hayo kwNza
Kufundisha Si kuelewa,

Soma tena na tena Ili ujue sifa za, IMMANUEL katika (Isaya 9:6-7) Si mtu, ni Mungu.

Ndiye huyo huyo Aliyefunuliwa na Malaika Gabriel katika (Mathayo 1:18-23).

Huyu Yesu aliyeandikwa hapo ndiye IMMANUEL/YESU ambaye ni MUNGU KATIKA mwili wa mwanadamu.

Jibu hapo, baba wa KIMWILI wa Yesu ni nani, sawasawa na nilichokuonyesha katika maandiko?
 
Nimekuuliza swali jepesi kuhusu Isaya 8:8 nayo imetaja kuhusu Immanuel umeshindwa kulijibu...
Hakuna sehemu malaika Gabriel ametaja jina la Immanuel...
Malaika Gabriel ametaja jina La Yesu peke yake..

Mkuu hii ni comment ya Mwisho kwako unaonyesha you have biblical Incompetent...Rudi darasani au jichimbie Soma ..
Vinginevyo usikariri unachoambiwa kwenye Sunday school kuja kukileta mbele za watu...
 

Illusion tu, amka ndugu, wazugu waliwaletea ustaarabu wao mkaiga leo mnajifanya mnaujua kuliko wazungu wenyewe! Na walishaacha hili somo. Eti we unamjua Yesu kuliko waliounda habari hiyo, amka hujachelewa toka kwenye hypnosis mzee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…