Mkuu utake ladhi tafadhari au kama umeamua kuingia na utapeli huo ili ukawalaghai wasukuma nakuambia tu kuwa zama zimebadilika mkuu.
Mwaka 2021 tulibishana na maafisa kilimo waliletwa na mgodi wa dhahabu wa.....................kwa lengo la kuwapa elimu wakazi wa vijiji vinavyozunguka mgodi huo.
Walinadi kuwa hekali moja ikitunzwa vizuri basi uhakika wa kupata gunia 35 si wa kuuliza. Nikawaambia mimi iwapo heka1 itatoa gunia 15+ tu nitawalipa kila mmoja wenu 200k walikuwa watatu.
Shamba likaandaliwa kila kitu mbolea ya samadi ya kutosha na mbolea za ruzuku hizi zote wakaleta tukapanda kwa vipimo kama walivyodaai wao{ hili lilikuwa kosa la kwanza waliyabana}
Palizi,mbolea za ruzuku kwa wakati hadi na booster tulipiga. Finaly gunia7 na debe5 wakasingizia haliya hewa haikuwa rafiki!
Nikawaambia ukanda huu heka huwa hatoboi gunia13 hapo umekanyaga hapa na pale na ukitoa hizo unakuwa mfano mkubwa kata nzima.
Hivyo mkuu yatosha kumuhamasisha mkeo humu kila mwaka watu tuko field na sio maneno ya kwenye kanga.
Mwaka huu nikifanikiwa kabisa basi heka itatoa debe1 la mahindi !! Hali ni mbaya leo nimeruhusu sehemu kidogo kama robo wachungie ng'ombe tu angalau