Je, wajua nusu Hekta unaweza kuvuna gunia hamsini za mahindi?

Je, wajua nusu Hekta unaweza kuvuna gunia hamsini za mahindi?

Ekari moja ni kama 4000m² na hapa mtu akipata sana gunia 26 sasa hiyo nusu hecta ni ndoto za alinacha kupata gunia 50
Humu watu wanaweka nyuzi za kijinga ili washambuliwe na watu wengi. Mwisho wa siku aongeze points za humu JF.. Watu kama hawa dawa yao ni kuwasusia nyuzi tu. Am out.
 
Kwa hesabu za mezani inawezekana, hata kilimo cha matikiti ukipiga hesabu mezani kinatajirisha sana
 
Kama sahizi ukiwasha moto mashambani mahindi yanawaka yote.. Mvua hamna hizo gunia unazipataje?

Pesa sio rahisi kihivyo
 
Huu wizi mchana kweupee...
Kilicho niumiza zaidi ni kuona unatumia majina kamili ya babu yake mtu wangu wa karibu ambaye ni marehemu.
Najiuliza kafufuka kazaliwa Tena akiwa tapeli?
 
Huu wizi mchana kweupee...
Kilichonoumiza zaidi ni kuona unatumia majina kamili ya babu yake mtu wangu wa karibu ambaye ni marehemu.
Najiuliza kafufuka kazaliwa Tena akiwa tapeli?
Hakuna utapeli ongea vizuri na wataalamu wa kilimo.
 
Mkuu utake ladhi tafadhari au kama umeamua kuingia na utapeli huo ili ukawalaghai wasukuma nakuambia tu kuwa zama zimebadilika mkuu.

Mwaka 2021 tulibishana na maafisa kilimo waliletwa na mgodi wa dhahabu wa.....................kwa lengo la kuwapa elimu wakazi wa vijiji vinavyozunguka mgodi huo.

Walinadi kuwa hekali moja ikitunzwa vizuri basi uhakika wa kupata gunia 35 si wa kuuliza. Nikawaambia mimi iwapo heka1 itatoa gunia 15+ tu nitawalipa kila mmoja wenu 200k walikuwa watatu.

Shamba likaandaliwa kila kitu mbolea ya samadi ya kutosha na mbolea za ruzuku hizi zote wakaleta tukapanda kwa vipimo kama walivyodaai wao{ hili lilikuwa kosa la kwanza waliyabana}

Palizi,mbolea za ruzuku kwa wakati hadi na booster tulipiga. Finaly gunia7 na debe5 wakasingizia haliya hewa haikuwa rafiki!

Nikawaambia ukanda huu heka huwa hatoboi gunia13 hapo umekanyaga hapa na pale na ukitoa hizo unakuwa mfano mkubwa kata nzima.

Hivyo mkuu yatosha kumuhamasisha mkeo humu kila mwaka watu tuko field na sio maneno ya kwenye kanga.

Mwaka huu nikifanikiwa kabisa basi heka itatoa debe1 la mahindi !! Hali ni mbaya leo nimeruhusu sehemu kidogo kama robo wachungie ng'ombe tu angalau
 
Hekar inatoa had gunia 45 anae bisha aje pm msimu bado nakupa shamba mbegu mbolea juu yako mi nakupa mautundu aka maujuz
 
Hizi bangi muwe mnavuta mkiwa mmeshiba tena muwe mmechambua
Mwanzo nilidhani anamaanisha Nusu Hekta, ambayo ni sawa na ekari moja na kidogo, hiyo inawezekana bila shaka. Lakini kwenye comment amekuja kufafanua kwamba alimaanisha nusu ekari, hapo ndiyo amejidhihirisha kwamba hajawahi kufanya kazi ya kilimo hapa Tanzania.
 
Back
Top Bottom