Mkuu hizo sifa unazompa chui/leopard nadhani unamfananisha na duma/cheeter, chui hukamatwa kwa urahisi sana hata na mbwa wa kufugwa, 2011 kuna chui alijilengesha hapa kwenye mifugo yangu ndan ya fence usiku, aliuawa kirahisi tena na mbwa mmoja. Mbugani pia chui akihisi makazi yake yapo karibu na pride ya simba anahama, hana uwezo kabisa hata wa kupambana na ndama la simba Au Simba Mgonjwa.
Mkuu ninachoandika nakijua duma na chui ni wanyama tofauti kabisa, duma ni predator dhaifu ukilinganisha kati yake na chui na simba, kwaulicho kisema katafute tafiti za TAWIRI kuhusu wanyama pori wenye conflict kubwa na binadamu mmoja wao chui anaongoza sana kwa kuua hasa mbwa na mbuzi na kondoo, kwa kesi yako kua mbwa alimuu chui sikatai nataka unijuze mazingira yake je mlimtega chui? Je chui alikua mwenye hali gani mgonjwa au mzee? Chui katika ubora wake mbwa hawezi pata nafasi ya kuishi mkuu, katika bandiki langu hapo juu nimeeleza kwa kiasi maisha ya chui , chui anaishi solitary hivyi nafasi ya simba mmoja akutane na chui 20 haipo, lkn kama umewakusanya chui 20 na simna mmoja wapigane simba hatoweza tena dk 1 hamalizi,ni sawa na tyson apogane na akina cheka 20 kwa wakati mmoja....Note muhimu ujue kwanini wanyama pori wanakuja vamia/winda kwenye makazi ya watu, itakusadia kupata mwanga kwanini mbwa wako aliweza muua chui.
Kuhusu suala la chui kuhama pakiwa na pride ya simba ni kweli, kwakua chui mmoja hawezi pambana na simba hata mmoja sasa pride ya simba inamaa ni simba zaidi ya mmoja ndio kabisa since chui ni solitary and territorial
Naomba ni ni declare interest mm ni wildlife expert. 15 year experience..kama una swali unaweza niuliza na ntakujibu kadiri ya nijuavyo