Je wajua mpiganaji masumbwi wa enzi hizo wa kuitwa Sugar Ray aliota kuwa iwapo atambana na mpinzani wake Jimmy Doyle, atamuua ulingoni kitu ambacho Sugar Ray kilimuogopesha mno na kuamua kusitisha kupambana na mpinzani wake Jimmy Doyle.
Jambo ambalo watu wa karibu wa Sugar Ray ikiwemo mchungaji wake, walimshauri Sugar Ray aendelee na pambano ile ni ndoto tu, na si kuwa itatokea kile alichokiota, Sugar Ray baadae aliupokea ushauri na kukubali kuendelea na pambano siku ya tarehe iliopangwa.
Basi huwezi amini siku ya siku(siku ya pambano illipofika) Sugar Ray ilipofika raundi ya sita alipeleka ngumi nzito iliopelekea mpinzani wake Jimmy Doyle kwenda chini(kuanguka) bila kunyanyuka, pamoja na juhudi zote za ziada zilizofanyika kumuwahisha Mwanamasumbwi Jimmy Doyle kuwahishwa Hospitalini hazikusaidia na kusababisha Mwanamasumbwi huyo kupoteza maisha akiwa Hospitalini