Je, wajua? - Special Thread

Inategemea na jasho la mwanaume gani, kibega mbeba magunia kariakoo anasiku mbili hajaoga, anakunywa piwa na wanzuki ndo fanta yake.
 
Kwa fangasi za miguu paka Ina tu, utapona kabisa, mimi nilipona na hiyo kitu paka wacha majani yakaukie humu then OSHA
 
Je wajua Madini/Mawe ya Tanzanite yanapatikana nchini Tanzania tu
 
1:Mtu akiwa analia halafu chozi la kwanza kudondoka likatokea jicho la kulia basi kilio kile ni cha furaha na likitokea jicho la kushoto linaasharia ni majonzi

2:Tunavalishana Pete za ndoa kwenye kidole cha kushoto kwa sababu hiki kidole ni pekee kilichoonganishwa moja kwa moja na mshipa wa vena unao peleka damu kwenye moyo moja kwa moja

3. Duniani tupo billion 7 hivyo ukisema ukutane na kila mtu kwa kila sekunde moja basi utachukua miaka 32 kukutana na sisi wote

4:Utafiti umeonyesha kuwa binadam wengi tunakuwa na furaha kila inapofika 7:26 pm (saa moja jioni) kila Jumamosi

5:Kumbe mende akikugusa labda hata kwa bahati mbaya basi ni lazima akimbilie mahali salama na akifika anafanya kama kujisafisha

6:Kila mwaka kwa wastani wanakufa watu 7,000 kutokana na madhara ya miandiko ya ki daktari ambayo inapelekea kuchambuliwa na kueleweka vibaya mfano na wauza madawa wanatafsiri vibaya na wkakupa dawa nyingine tofauti na iliyoandikwa

7:Ukiingia Google ukawa search hizi namba "241543903" basi utakutana na picha za watu mbalimbali wame piga wamejifungia kwenye friji

8: Asilimia 96 ya watu hawajui kama Osama bin Laden alishawahi kuwa agent wa CIA miaka ya 1980

9:Watu wanaocheza vido games wanakuwa wepesi wa kufanya maamuzi hata katika maisha yao ya kila siku ya kawaida

10:Asilimia 95 ya watu hawaipendi Sauti yao wenyewe iliyorokediwa kwenye video

11:Bill Gates alishawahi kumwambia mwalimu wake kuwa lazima atakuwa millionea akifikisha miaka 30.. Akawa billionea akiwa na miaka 31

12: Mabadiliko ya haraka ya kihisia kutoka kwenye furaha ukaingia kwenye y huzuni ni kiashiria kwamba kuna mtu unamkosa sana

13:Uwezo wa mwanamke kusoma hisia za mtu ni mara kumi ya uwezo alionao mwanaume

14: Asilimia 75 ya watu hujaribu kurudi kitandani asubuhi Ili wamalize tu ndoto zao mbazo hazikukamilika

15:Utafiti uliofanyika kwa watu wazima 3000 unasema kulala upande wa kushoto wa kitandani una kufanya uwe na mitazamo chanya zaidi

16:Viatu virefu wanavovaa dada zetu vilitengenezwa kwa ajili ya wanaume hasa wanaouza nyama buchani na lengo ilikuwa kuzuia kugusana na damu iliyopo chini

17:Kwa wastani unaweza kujiangalia kwenye kioo mara tano na kiasi kikubwa ukajiona unavutia tofauti na uhalisia kumbe hata huvutii sana sasa ile ni kazi ya part fulani katika ubongo. Asante ubongo

18:kwa utafiti wa wanawake wa Uingereza umeonyesha kwa siku wanawake hujitathimi juu ya muonekano wake si chini ya mara tisa
Na ni asilimia 4 tu ya wanawake ndo wanaridhika na muonekano walionao

19:111111111 mara 111111111=12345678987654321

20:Ukilia unatoa homoni ya stress na ndo maana ukimaliza tu kulia unaanza kuhisi kama unajiskia vizuri hivi

21:Rangi halisi ya pundamilia ni nyeusi ile nyeupe ndo mkanda tu iliyojizungusha

22:HATA UJITAHIDI KWA NAMNA GANI HUWEZI KUKUMBUKA JINSI NDOTO ULIYOOTA ILIVYOANZA SANA SANA UTAKUMBUKA KATIKATI NA ILIVYOISHIA

23:kama mabinti mapacha wakiolewa na wanaume wawili mapacha basi Watoto watakaozaliwa na kila couple watafanana kila kitu

24:KUNA WAKATI UNAHISI UME MMISS MTU FULANI UKWELI NI KUWA HAUJAMMISS YEYE BALI NI MEMORIES

25:75% ya mawazo yetu ni tafakar za kurudisha kumbukumbu na kutengeneza kwa Ubunifu wa hali ya juu namna tunavotaka maisha yawe mazuri

26:watu wenye tabia ya kuisaidia wengine mara kwa mara huwa na furaha na ina ongezeka jinsi wanavyozeeka

27:ASILIMIA 90 YA BINADAMU WANAFIKIRIA KUFANYA MAAMUZI MAGUMU JUU YA JAMBO FULANI KIPINDI WAKIWA WANAOGA

28:asilimia 90 ya unawowasamehe bado unawahitaji kuwa sehemu ya maisha yako

29:mamalia anayekuwa haraka ni nyangumi na anayekuwa taratibu kupita wote ni BINADAMU

30:WANAUME WANAOWABUSU WAKE ZAO KILA ASUBUHI WANA FAIDA YA KUISHI MIAKA 5 ZAIDI MBELE

31:WANAWAKE WANA JIKUTA WANAVUTIWA NA WEWE ENDAPO TU WAKIGUNDUA KUNA WANAWAKE WENZAO ZAIDI YA WAWILI WANAKUANGALIA WEWE BILA YA WEWE KUWAONA WAKIKUANGALIA

32:mimba ya jack chain HAIKUWA miezi 9 ilikuwa 12

33:ng'ombe ana uwezo wa Kutoa maziwa mengi akikamuliwa kipindi anasikiliza nyimbo tulivu

34:KUMBE MBU AKISHAKUNYONYA DAMU HAKUACHI MPAKA AKUKOJOLEE JAPO KIDOGO
 
ukibaka bikira na ukibaka nungaembe utafungwa miaka 30? sio fair kabisa
 
mkuu umetisha sanaa,,kula likes 1000
 
Kisa cha kutokuoga nini....je wajua..??
 
Kisa cha kutokuoga nini....je wajua..??
Naam, Najua.

Ni kwasababu Halle Berry alicheza ile Filamu akiwa kama mtu alierukwa na akili, muathirika wa madawa ya kulevya.

Kwahiyo ikabidi afanye hivyo ili aendane na mazingira ya Filamu aliyoicheza, awe mchafu.

Watu wanaojali kazi zao hao.

Ndani ya miezi mitatu alikuwa akijisafisha sehemu zake za siri tu.

Mfano kama ile Filamu ya Curtis Jackson, ya kuitwa All things fall apart, alieigiza kama muhanga wa Saratani, ikabidi apunguze mwili wake (ajikondeshe) ili aendane na mazingira ya Filamu aliyoicheza.

Na kweli Curtis Jackson, alifanikisha kupunguza mwili wake (kujikondesha) kwa kiasi kikubwa, na kuonekana amedhoofika kama mgonjwa kweli wa Saratani.

Wenzetu wanajali sana kazi zao
 
Je wajua uzi huu wa Kiongozi mandella umeshafikisha miaka miwili tayari na bado unaendelea kutembea
 
Wakuu na waimba mapambio mnajua nani hasa aliasisi mchakato huu wa kumkata mfanyakazi 9% ya mshahara wake kama kodi ya PAYE? Angalia na kusikiliza hii video alafu utafakari kimyakimya kama analala nao "mbere" kama unavyoaminishwa
 

Attachments

1. Nchi ya Gambia ina chuo kikuu kimoja tu (The University of Gambia).

2. Equatorial Guinea ni nchi pekee Afrika ambayo lugha yake ya Taifa ni Kispaniola (Spanish). Hakuna nchi nyingine Afrika inayozungumza Kispaniola.

3. Afrika kusini ndiyo nchi inayotembelewa na wageni wengi zaidi kuliko nchi zote za Afrika.

4. Nigeria ndio nchi yenye matajiri wengi weusi kuliko nchi nyingine za Afrika (richest Black people).

5. Samuel Eto’o ndiye mchezaji anayelipwa ghali zaidi kuliko wachezaji wengine kutoka Afrika. Analipwa Euro 350,000 kwa wiki (sawa na shilingi milioni 980,000/=). Kwa lugha rahisi ni kwamba mshahara wa Et'oo wa wiki 7 unalingana na pesa zote alizoiba Rugemalira kupitia Escrow na kugawia kina Tibaijuka na Ngeleja.

6. Raia kutoka Nigeria anaitwa Nigerian, Raia wa Niger anaitwa Nigerien na raia wa Burkina Faso anaitwa Burkinabe.

7. Nigeria imeshinda vikombe vingi vya soka kuliko Uingereza (England).

8. Ethiopia na Liberia ni nchi pekee Afrika ambazo hazijawahi kutawaliwa. Italia ilipojaribu kuitawala Ethiopia iliishia kupigwa vibaya na ikassurender.

9. Kabila la Limba huko Zambia, mama wa mvulana ndiye anayemtafutia mwanae binti wa kuoa. Mama ndiye anayemuapproach binti, na kulipa mahari kabla hata binti hajamuona kijana mwenyewe. Kinachotakiwa ni binti kumkubali mama tu.. Ukimkubali mama means umemkubali na mwanae. So mwanae utakutana nae kwenye harusi, mambo mengine kabla ya harusi anafanya mama yake.

10. Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ndiye Rais msomi zaidi duniani. Ana degree 7 alizozisomea ktk vyuo vikuu mbalimbali, mbili kati ya hizo ni Masters.

11. Zinedine Zidane aliwahi kurudi nchi yake ya asili Algeria ili aichezee kwenye mashindano ya kimataifa. Alipofika waziri wa michezo wa Algeria, Abdelmalek Sellal akamwambia "tuna wachezaji wengi wazuri kuliko wewe na hawajapata nafasi kwenye kikosi. Labda tungeruhusiwa kucheza zaidi ya 11 uwanjani ungeweza kubatika kupata namba"

12. Robert Mugabe ndiye Rais mzee zaidi duniani. Anashikilia rekodi kwa kuwa na umri wa miaka 91 akifuatiwa na Shimon Peres, Rais wa Israeli mwenye miaka 90.

13. Shelisheli (Seychellois) ndio nchi ya kwanza duniani ambayo raia wake wameelimika kuliko nchi nyingine. Inakadiriwa kuwa asilimia 91.9% ya watu wake wana elimu ya sekondari na kuendelea. (Tanzania wenye elimu ya sekondari na kuendelea ni asilimia 13.5 kwa mujibu wa HakiElimu.)

14. Mauritius ndiyo nchi pekee Afrika inayoingiza fedha nyingi kupitia utalii wa fukwe (Beach Tourism). Mwaka 2013 iliingiza takribali shilingi trilioni 4.5 kupitia utalii wa fukwe. Tanzania tuliingiza shilingi bilioni 1.7 kupitia Utalii wa fukwe mwaka huohuo.

15. Rwanda ndiyo nchi pekee yenye usawa wa kijinsia kuliko nchi zote duniani (Bunge la Rwanda ni 50% wanaume na 50% wanawake).

16. Ethiopia ndio nchi pekee Afrika yenye viwanja vingi vya ndege vyenye hadhi ya kimataifa (International Airports). Ina viwanja vya ndege 23 vyenye hadhi ya kimataifa. (Tanzania tuna viwanja vya ndege vitatu vyenye hadhi ya kimataifa (JNIA-Dar, KIA-Moshi, na Songwe-Mbeya).

17. Uchumi wa Ethiopia unakua kwa kasi kuliko Uchumi wa China. Uchumi wa Ethiopia (GDP) unakua kwa wastani wa 18.7% kwa mwaka, China GDP inakua kwa wastani wa 11.4% kwa mwaka (according to the World bank fact sheet, 2014)

18. Rais wa Eritrea Isaias Afwerki ndiye Rais Maskini kuliko wote Afrika. Analipwa mshahara wa Dola 500 za kimarekani ($ 500) sawa na Shilingi 945,000/=. Hiki ni kiwango kidogo cha mshahara kuliko daktari wa mfunzo nchini Tanzania (Intern Doctor).

19. Angola ina watu wengi wanaoongea Kireno kuliko Ureno kwenyewe. Angola ina watu milioni 22 na wote wanaongea Kireno, lakini Ureno ambao ndio wenye lugha wana watu milioni 10.7 tu.

20. Somalia ilipata mashine yake ya kwanza ya ATM tarehe 7, October, 2014. Kabla ya hapo hakukuwa na ATM yoyote nchini Somalia.
 
This content is 3 years old. Most of the facts now don't count...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…