Habari wana JF! Katika pita pita yangu nimekutana na mambo yafuatayo hapa chini nikaona ni vizuri tujuzane, kama kuna anayeweza kutuongezea, pia siyo mbaya: Je wajua;
1.Tar 4/4, 6/6, 8/8, 10/10 &12/12 zinaangukia siku moja kwa mwaka wowote?
2.Fisi hujifungua kupitia kisimi?
3.Mstari wa Equator hupitia nchi 13 ambazo ni: Ecuador,Colombia, Brazil, Sao Tome & Principe, Gabon, Republic of the Congo,Democratic Republic of the Congo, Uganda, Kenya, Somalia, Maldives, Indonesia na Kiribati.
4.Chuo kikuu cha Al – Azhar kilichoko Cairo nchini Misri ndicho chuo kikuu cha zamani zaidi duniani, kilianzishwa mwaka 969 AD.
5.Pesa ya noti haikutengenezwa kwa karatasi bali kwa pamba?
6.Ulimi wa Kinyonga ni mrefu kuliko mwili wake?
7.Binadamu hutengeneza wastani wa nusu lita ya ushuzi kwa siku?