Je, wajua? - Special Thread

Je, wajua? - Special Thread

Wakati majirani zetu Zambia wakitaaruki kifo cha rais wao Michael Chilufya Sata ambaye alifariki dunia tar 28 Oct 2014 na kwa sasa Wanatarajia kuuzika mwili huo ktk viwanja vya embassy park ambako viongozi wengine kama Levy Mwanawasa na Fredirick Chiluba walizikwa, tukienda mbali zaidi historia inathibitisha takriba viongozi 11 wafia madarakani swali la kujiuliza kwanini? labda ufahamu na kuorodheshea wachache tu .

1. Rais Malam Bacai Sanha wa Guinea Bissau - Machi 2012

2. Rais Bingu wa Mutharika April 2012 Atimaye majozi yaliwapata waghana kufariki kwa

3. Rais John Atta Mills - Julai 2012,

4.
Waziri mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi - Agosti 2012 na wengine wengi.

Hivi kwanini inatokea inatokea hali kama hii?

Please members just share what you have on such crucial issue.
 
namba 4 ni uongo tena mkubwa chuo cha kwanza kilijegwa 200's ad
 
Kifo si kifo tu, kwa hiyo unataka kusema kuwa maraisi inatakiwa wakiwa madarakani wasife?Kifo ni kifo tu hata kama wangekufa wakati wa kampeni za urais
Umemsahau shujaa na mshupavu, Captain Thomas Sankara wa nchi ya watu waliyotukuka, Burkina Faso
 
Watu wengine bhana. Sasa hao 11 wako wapi wakati hata wa tano hukufikisha kuwataja
 
Nadhani kuna willium wa liberia kuna ayadena wa togo kuna gadafi
 
Kama:
  • Nyimbo za taarabu zinachukua Air time ndefu ya redio kuliko aina nyingine yoyote ya Mziki Tanzaniai!!


  • Watanzania walio wengi hawajishughulishi na siasa katika maeneo yao au nchi yao kwa ujumla ndio maana mbuge au chama kinatawala weee! huku maendeleo kiduchu kufikishwa huko, na wananchi wasiwachukulie hatua, wachaguliwe tena, na tena na tena!!


  • Watanzania ni zaidi ya Milioni 45 lakini ni chini ya 6% ndio wanatumia huduma za mabenki


  • Shia na Sunni ni madhehebu makubwa sana katika uisilamu na tofauti yao kubwa sio Imani bali ni Nguvu kwenye dola za kiisilmu, baada ya Muhammad S.A.W kufariki, kuna kundi walitaka Familia ya Muhammad iendelee kuongoza uisilamu, hao walikuja kua Shia, na kundi lingine lilitaka kiongozi wa waisilamu achaguliwe miongoni mwa waumini, kundi hili lilijiita Sunni ( madhehebu haya yanavisasi mpaka vya kulipuana mabomu)


  • Marekani inaunga mkono sana uchaguzi wa kidemokrasia katika nchi mbali mbali ulimwenguni, mwaka 2006 Hamas ilishinda viti vingi katika bunge la Palestina, lakini Wamarekani hawakuutambua ushindi huo




  • Tanzania hakuna sera ya kueleweka ya Nishati, watu kwa wingi wanatumia mkaa, huku wafanya biashara hiyo wakipambana na serikali (idara ya mali ya asili), matokeo yake bei ya nishati hiyo inapanda kila uchwao.


  • Askari wa barabarani (hasa mijini ) mara nyingi wanakamata dereva wa daladala kwa kosa la kutofunga Mkanda ilihali abiria woote hawajafunga mkanda!!
 
Je wajua mashindano ya kombe la dunia yaliyofanyika nchini Germany mwaka 2006 Switzerland ndio nchi pekee ambayo haikuruhusu goli hata moja hadi wanatoka mashindanoni
 
Wajua kuwa lugha ya kiarabu inaongoza duniani kwa kuwa na waongeaji wengi ikiwa na idadi ya watu milioni 170 ikifuatiwa na Kiingereza watu milioni 130 na Ufaransa watu milioni 115?.
 
Je maana yako ni ipi hasa kudai"lugha ya Kiarabu inaongoza kwa kuwa na wazungumzaji wengi zaidi duniani?".

Je unamaana ya kuwa lugha ya Kiarabu inaongoza kuwa na "native speakers" wengi?

Je unamaana ya kuwa lugha ya Kiarabu inaongoza kwa kwa maana ya kuwa na "total speaker" wengi zaidi?

Je unamaana ya kuwa lugha ya Kiarabu ni "widely spoken?" katika dunia hii tunayoishi?

Kwa majibu yote utakayotoa kuhusu maswali ya msingi hapo juu sidhani kama utakuwa sahihi kudai ligha ya Kiarabu inazungumzwa na watu wengi zaidi.

Lugha ya Mandarin ndio ina "native speakers" wengi zaidi. About 990 million. Inazungumzwa China, Taiwan na sehemu za Singapore.

Lugha ya Kiingereza ndio lugha iko "widely spoken". Karibu kila nchi kwa mabara yote duniani Kiingereza ni lugha official au lugha ya pili kwa matumizi.

Vile vile lugha ya Kiiengereza ndio inaidadi kubwa ya "total speaker". Karibu watu 1.4 billion hadi 1.8 billion.
Tujitahidi kuinua Kiswahili. Ni lugha ambayo inaweza kupata wazungumzaji wengi na kuwa "widely spoken". Mandarin ina waongeaji wengi lakini sio widely spoken. Sehemu chache tu ndio wanazungumza. Nadhani umeona tofauti.
 
takwimu hii iliktolewa star tv..ila kwa kmbukumbu zangu idadi hiyo ni kwa afrika sio dunia nzima
 
Wajua kuwa lugha ya kiarabu inaongoza duniani kwa kuwa na waongeaji wengi ikiwa na idadi ya watu milioni 170 ikifuatiwa na Kiingereza watu milioni 130 na Ufaransa watu milioni 115?.

mh mkuu hebu tutake radhi basi... yaani kiingereza kinazungumzwa na watu milioni 130 tu?! nadhani kwa Afrika pekee idadi ya watu wanaozungumza lugha hiyo inaweza ikakaribia idadi hiyo kama sio kupita kabisa. unaijua lugha inaitwa mandarin? hebu ifuatilie hiyo lugha halafu uje ufute huu uzi.
 
Je wajua? Kitabu kitakatifu kwa wakristo kijulikanacho kama Biblia kina


[*]Herufi 3,566,480,


[*]Maneno 810,677


[*]Mistari 31,175


[*]Sura 1089


[*]Sura ndefu kuliko zote ni Zaburi 119


[*]Sura fupi kuliko zote ni Zaburi 117


[*]Mstari ambao upo katikati ya biblia (ambako kwenda mbele ni sawa na kurudi nyuma) ni Zaburi 118:8


[*]Jina refu kuliko yote katika biblia linapatikana Isaya 8:1


[*]Neno Bwana linapatikana kwenye biblia mara 1855


[*]Misitari katika biblia inayofanana neno kwa neno ni 2Wafalme 19 na Isaya 37


[*]Mstari mfupi kuliko yote ni Yohana 11:35


[*]Je wataka kujua nini juu ya Biblia?
 
Biblia ya aina gani King James, Good News au ipi?
Na imeandikwa kwa lugha gani hiyo Biblia??

Tumsifu Yesu Kristo
 
Kuuliza sio ujinga,hivi kuna tofauti ya biblia na tafsiri ya biblia?
 
Back
Top Bottom