Je, wajua? - Special Thread

Je, wajua? - Special Thread

Je wajua kwamba uzito wa sisimizi wote waliopo duniani wakiwekwa pamoja ni sawa na uzito wa binadamu wote waliopo duniani?

mmmh hii haina ushahidi kabisa .Na research yake ni ngumu kufanyika .
 
Je wajua Mbwa Mwitu amemzidi binaadam kwa idadi ya meno ambayo idadi ya Mbwa Mwitu ni 42 ukilinganisha na idadi ya meno ya binaadam ambayo ni 32 tu
 
Je wajua kicheche ndiye mnyama mdogo sana, lakini ana maajabu makubwa. Ana uwezo wa kumdaka kuku wa aina yoyote kwa kutumia mkia wake.

Lakini cha ajabu zaid hawezi kuishi bila kufanya mapenzi, ana uwezo wa kufanya mapenzi mara 26 kwa siku pia ni sawa na kukimbia umbali wa Km 360 kwa siku.

Na ndio maana mwanamke malaya sana huitwa kicheche najua hujui ila ndio nawajuza zaidi.

Anadakaje kuku kwa kutumia mkia??
 
Je wajua

Kanali Ally Mahfoudh kutoka Zanzibar, alifukuzwa Zanzibar kwa tuhuma za kumuua Karume lakini nchi ya Msumbiji imempa heshima zote na amezikwa katika makaburi ya mashujaa huko Msumbiji baada ya kuwasaidia katika harakati za Uhuru.
 
Je wajua

Edward Sokoine anabakia kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania pekee kufariki angali akiwa bado na wadhifa wa Uwaziri Mkuu.
 
Je Wajua

Julius Nyerere, Rais wa kwanza wa Tanzania, aliwahi kufichwa maeneo ya Kigamboni na Usalama wa Taifa wakati Jeshi lilipoasi mwaka 1964.

Eneo alilofichwa Nyerere huko Kigamboni mpaka leo limebaki kuwa ni siri.
 
Je wajua

Simba wanaopatikana hifadhi ya Tarangire, ndio Simba pekee wanaopanda juu ya miti duniani.
 
Je wajua Cleopatra aliyekuwa kiongozi Misri ndiye mwanamke mzuri/mrembo kuliko wote duniani pamoja na kuzaa watoto na hatatokea tena kama yeye? Source: soma Biblia takatifu.

Hii nakataa. Biblia niisomayo mimi inaniambia mabinti aliowapata Ayubu baada ya mkasa ule wa jaribu ndiyo walikuwa wazuri kuliko wote waliopata kutokea duniani.

Job 42:15, "Nowhere in all the land were there found women as beautiful as Job's daughters..."
 
Je wajua vipepeo wananusa kwa kutumia miguu yao
 
Je wajua kicheche ndiye mnyama mdogo sana, lakini ana maajabu makubwa. Ana uwezo wa kumdaka kuku wa aina yoyote kwa kutumia mkia wake.

Lakini cha ajabu zaid hawezi kuishi bila kufanya mapenzi, ana uwezo wa kufanya mapenzi mara 26 kwa siku pia ni sawa na kukimbia umbali wa Km 360 kwa siku.

Na ndio maana mwanamke malaya sana huitwa kicheche najua hujui ila ndio nawajuza zaidi.

source?
 
je wajuwa, kiumbe mwenye sumu kuliko kiumbe chochote na kiumbe anae ishi miaka mingi kuliko vyote dunian ni Jellyfish...
 
Kwa wale wanaopenda kucheza na namba naanza kukupa idadi ya sifuri kwa kila namba kuanzia
1. Milion 1,000,000 (SIFURI 6)
2. Bilioni 1,000,000,000 (SIFURI 9)
3. Trilion 1,000,000,000,000 (SIFURI 12)
4. Quadrilion 1,000,000,000,000,000 (SIFURI 15)
5. Quintilion 1,000,000,000,000,000,000 (SIFURI 18)
6. Sextilion 1,000,000,000,000,000,000,000 (SIFURI 21)
7. Septilion 1,000,000,000,000,000,000,000,000 (SIFURI 24)

Namenumber of zerosgroups of (3) zeros
Trillion124 (1,000,000,000,000)
Quadrillion155
Quintillion186
Sextillion217
Septillion248
Octillion279
Nonillion3010
Decillion3311
Undecillion3612
Duodecillion3913
Tredecillion4214
Quatttuor-decillion4515
Quindecillion4816
Sexdecillion5117
Septen-decillion5418
Octodecillion5719
Novemdecillion6020
Vigintillion6321
Centillion303101




HAPO NDIPO NAMBA ZILIPOISHIA KATIKA ULIMWENGU WA SASA WA PESA!!! KAMA KUNA NYINGINE TUWEKE !!!
 
Back
Top Bottom