Je, wajua? - Special Thread

Je, wajua? - Special Thread

Ajabu la 21. TANZANIA ndiyo nchi pekee yenye uhaba wa SUKARI
Kweli mkuu? Au umejifungia kwako na hii habari!!!, juzi tu tumehabarishwa kuwa Cameron nayo ina uhaba mkubwa wa sukari, update taarifa zako.
 
Je wajua....
ubongo wa binadamu unaanza kufanya kazi pindi anapozaliwa na unafanya kazi masaa 24(none stop)...
huacha(stop) kufanya kazi pale tu anapofanya mtihani au anapopenda(fall in love).
 
Je, wajua kwamba kuna mambo haya yanayokuzunguka?

1. Je, wajua kwamba binadamu pamoja na akili zake zote, pamoja na mbwembwe zake nyingi, bado hana uwezo wa kufikisha ulimi kwenye kiwiko cha mkono wake?

2. Je, wajua kwamba kama piza zinazoliwa kwenye bara la Amerika kwa siku zingepangwa zingeweza kuchukua eneo lenye ukubwa wa hekta 18?

3. Je, wajua kwamba kila binadamu ana alama tofauti kabisa na za kipekee katika ulimi wake (tongue-prints) kama zilivyo za vidole?

4. Je, wajua kuwa mnyama aina ya mamba huwa hana uwezo wa kutoa ulimi wake nje kutokana na maumbile yake?

5. Je, wajua kuwa farasi na panya ndio wanyama pekee wasiotapika?

6. Je, wajua kuwa jicho la mbuni ni kubwa kuliko ubongo wake?

7. Je, wajua kuwa licha ya binadamu kuwa na uwezo wa kubana pumzi zake, bado hawezi kujiua kwa njia hiyo?

8. Je, wajua kwamba kwa wastani kichwa cha mwanadamu hubeba nywele zipatazo 100,000 na kila unywele unakua kwa wastani wa sentimita 12.5 kwa mwaka?

9. Je, wajua kuwa siafu ndio viumbe pekee wasiolala maisha yao yote?

10. Je, wajua kwamba mwanadamu ambaye anaweza kuishi kwa wastani wa miaka kati ya 50-60, anaweza kuzalisha kiasi cha mate kinachofikia galoni 10,000?

Je, wajua kuwa mwili wa mwanadamu una kiwango cha mafuta chenye kuweza kuzalisha miche saba ya sabuni?

11. Je, wajua kuwa katika ngozi ya mwanadamu mmoja pekee kuna idadi kubwa ya viumbe hai kuliko idadi ya wanadamu wote walioko katika ulimwengu mzima?

12. Je, wajua kuwa kama mdomo wako ukiwa mkavu kabisa huwezi kutofautisha ladha mbalimbali?

13. Je, wajua kuwa ubongo wa mwanadamu hutumia zaidi ya asilimia 25 ya oksijeni yote inayotumiwa na mwanadamu?

14. Je, wajua kuwa kila dakika moja inayopita, kuna seli kati ya alfu 30 hadi 40 zilizokufa zinazodondoka toka katika mwili wa mwanadamu?

15. Je, wajua kuwa ubongo wa mwanadamu umeumbwa kwa maji kwa kiwango cha asilimia 80?

16. Je, wajua kuwa kati ya viumbe wote duniani, ni mwanadamu pekee ambaye anaweza kulala kwa kutumia mgongo wake?

17. Je, wajua kuwa ukubwa wa jicho la mwanadamu daima ni ule ule toka anapozaliwa hadi anapozeeka? Pua na masikio hukua kwa kadiri mwanadamu anavyozidi kukua.

18. Je, wajua kuwa paka ana uwezo wa kubadili sauti yake na kufanya milio zaidi ya 100 tofauti tofauti wakati mbwa ana uwezo wa kufanya hivyo na kutoa sauti kumi tu?

19. Je, wajua kuwa visiwa vya Hawaii huvisogelea vile vya Japan kwa umbali wa inchi 4 kila mwaka?

20. Je, unajua kuwa kutengeneza karatasi mpya kutokana na karatasi za zamani zilizoisha matumizi yake kunaweza kusaidia kupunguza matumizi ya nishati kwa asilimia takriban 70 kulinganisha na kutengeneza karatasi hizo kutokana na miti
 
JE, ULIYAJUA HAYA?

Kuna maswali mengi yasiyo na majibu kuhusu maisha na ubinadamu Duniani. Kwa mfano, watafiti bado hawajui hasa ni kwanini wanadamu huota ndoto.

Hakuna anayejua hasa kwanini wanadamu hutoa machozi ya kicheko, furaha, huzuni. Kuna aina nyingi za machozi, lakini machozi ya hisia ni ya kipekee kwa binadamu.Na hata kama muda ni kama sehemu muhimu ya maisha, hakuna mtu anayeweza kuelezea ni lini ulianza au ni lini itakuwa mwisho.

Baadhi huamini wakati ni ulitungwa na binadamu, na wengine wanaamini kwamba wakati ulikuwepo muda mrefu kabla ya wanadamu kutunza kumbukumbu yake.Dunia imekuepo kwa muda mrefu sana. Wanasayansi wamekadiria umri wa dunia kuwa ni miaka bilioni 4.55.

Asilimia 71 ya uso wa dunia imefunikwa na maji, watafiti wanakadiria kuwa ni chini ya 5% ya hiyo imeonekana kwa macho ya binadamu nyingine bado haijawahi kuonwa na binadamu.
 
Ili kupata majibu yako inabidi ujiulize chanzo cha binadamu ni nn
 
JE?, UNAJUA KWAMBA
Wanaume wasio waaminifu wana IQs ndogo sana kulingana na utafiti wa kisayansi.

Nusu ya wanawake wote ambao wanakufa kutokana na mauaji , kuuawa na waume zao wa sasa au wa zamani .

Wanaume hudanganya mara 6 kwa siku, ambayo ni mara mbili zaid ya wanawake

Kama unahisi Laptop yako inajoto , wala usijaribu kuiweka kwenye mapaja yako kama wewe nimwanaume, inaweza kusababisha utasa.

Wanaume hutumia karibu miezi sita kunyoa ndevu katika maisha yao yote.

Kutokana na utafiti uliofanyika inasemekana kuwa wanaume wenye wake wanaovutia wametajwa kuridhishwa zaidi katika ndoa zao,

Mwanaume mwenye umri wa miaka 99 , alimpa talaka mke wake mwenye umri wa miaka 96 , baada ya miaka 77 ya ndoa, kwa sababu aligundua kuwa mkewe alikuwa na mahusiano nje ya ndoa mwaka 1940.

Uvutaji wa Sigara unaweza kusababisha utasa kwa wanaume.

Ifikapo mwaka 2020, China inaweza kuwa na wanaume kati ya milioni 30 na milioni 40 ambao hawawezi kupata wake.

Wanaume ni wakwanza zaidi kusema "nakupenda" kuliko wanawake ,kutokana na utafiti

uliofanyika.

Wanaume hutokwa jasho mara mbili zaid ya wanawake .
Uwezekano wa wanaume kujiua ni mara 3 had 4 zaid ukilinganisha na wanawake...
 
MORE AT..... WAJANJATZ
[emoji15]
 
Duuuu huu uzi inatakiwa kuwa kama mbayu wayu unaposoma baadhi ya comments
 
kama kichwa cha habari kinavyojitosheleza hapo juu
Tanzania ni nchi iliyobarikiwa sana
anaitwa brachiosaur
serikali ya Tanzania imeendelea kudai mabaki hayo yaliyoko nchini ujerumani yarudi nchini ili watanzania pia wafaidi bila mafanikio.
kumbuka ujerumani inajiingizia mapato makubwa kutokana na mabaki ya dinosaur huyo.
aligunduliwa mwaka 1906 huko tendaguru Lindi wakati huo Tanganyika ikiwa chini ya wajeumani.
 
1467517692605.jpg
 
scanning-brachiosaurus.jpg

Researchers using a laser to create a 3D copy of the Berlin Brachiosaurus skeleton.
 
Back
Top Bottom