Je, wajua? - Special Thread

Je, wajua? - Special Thread

Acheni unafiki, mjerumani asingemchukua na kwenda kumhifadhi kwake unadhani yangekuwepo hayo mabaki hadi leo hii?
kwahiyo we unaonaje? tuwaachie waendelee kupiga pesa au tukamchukue na sisi tufaidi ch kwetu?

yaani ni sawa na wewe ukamchukue mtoto wa masikini then umsomeshe awe maybe rais halafu hutaki wazazi wake nao wanufaike.....

fikiria nje ya box hakuna unafiki hapo...
tunashukuru kwa kumtunza ila arudi ili na sisi tufaidi asee
 
Madini,gesi,mbuga na hifadhi za wanyama,maziwa,bahari,ardhi yenye rutuba,n.k ... vyote hivi havijakunufaisha, ila hii skeleton ya huyu dinasour ndo itaweza kukunufaisha?
 
usikate tamaa kirahisi namna hiyo mkuu.
na siyo huyo tu maana kuna jumla ya mabaki 12 pamoja na huyo brachiosaur na wote wapo katika makumbusho ya ujerumani
 
DINOSARIA WA TANZANIA; MNYAMA MKUBWA WA NCHI KAVU

Miezi ya karibuni kumekuwa na harakati mbalimbali za watu kudai kurejeshwa kwa mabaki ya ‘mjusi’ toka nchini Ujerumani. Ukweli ni kwamba Dinosaria aliishi au waliishi katika eneo la Afrika Mashariki miaka milioni 154 hadi 142 iliyopita.
b503b0ca766da256d5c14266d02364ba.jpg

Ila ugunduzi wa mabaki yake yalipatikana mwaka 1912 katika kijiji cha Tandeguru, kata ya Mipingo katika mkoa wa Lindi, Baada ya ugunduzi huo ‘Mabaki’ ya Dinosaria wetu ‘yalitoroshwa’ na kwenda kuhifadhiwa huko katika makumbusho kubwa ya Humbolt huko Ujerumani.

Dinosaria ni mnyama mkubwa aliyeishi kipindi kinachofahamika kihistoria kama Nyakati za Jurasiki ‘Jurassic period’, anatokea katika genus ya Giraffatitan. Alikuwa na uzito wa tani 89( Kama malori manne ya mchanga). Alikula majani ya juu ya miti mirefu kwani alikuwa ana urefu wa mita 20.

Miguu yake ya mbele ni mirefu zaidi ya nyuma, pia shingo yake ilikuwa na urefu wa kutosha. Mnyama huyo ni uthibitisho mwingine kuwa ‘Africa is Cradle of All Civilisations’. Hii ni kwa kuwa fuvu la mtu wa kale zaidi liligunguliwa huko Olduvai Gorge, Arusha baadaye zana za kale za mawe ziligunduliwa huko isimila katika kijiji cha Ugwachanya mkoani Iringa.

Kwa sasa Makumbusho ya Humbolt ni maarufu sana Ulaya kwa sababu ya uwepo wa Dinosaria wetu. Tuna kila sababu ya kudai kwa nguvu zote ili masalia hayo yarejeshwe hapa kwa kumbukumbu ya vizazi vijavyo na kuwa kivutio kingine cha utalii hapa Tanzania. Hiyo tu haitoshi ila tunapaswa kujiandaa kwa kuwa na wataalamu na vifaa vya kuhifadhi masalia hayo.

Mwishoni tujiulize hivi ni watanzania wangapi huamasika kufika katika makumbusho za nchi hii?

Wenu katika Historia.
Francis Daudi
Bangalore University, India...
c5d68da656398d432f99f1b0bef941c7.jpg
 
... Kuwa Tanganyika wakati inapata uhuru ilikuwa ni nchi ya kwanza katika Afrika yenye kusafirisha kwa wingi (export) mazao ya shamba. Miaka saba tu baada ya uhuru, baada tu ya tangazwa azimio la Arusha, tukawa omba omba namba moja wa chakula duniani.
 
oky.. basi tatizo hapa ni ccm.
Embu tufanye kuipiga chini tuwape hawa wapinzani alafu tuone na wao watatupeleka wapi
[emoji41] [emoji41] [emoji41] [emoji41] [emoji41] [emoji41]
 
DINOSARIA WA TANZANIA; MNYAMA MKUBWA WA NCHI KAVU

Miezi ya karibuni kumekuwa na harakati mbalimbali za watu kudai kurejeshwa kwa mabaki ya ‘mjusi’ toka nchini Ujerumani. Ukweli ni kwamba Dinosaria aliishi au waliishi katika eneo la Afrika Mashariki miaka milioni 154 hadi 142 iliyopita.
b503b0ca766da256d5c14266d02364ba.jpg

Ila ugunduzi wa mabaki yake yalipatikana mwaka 1912 katika kijiji cha Tandeguru, kata ya Mipingo katika mkoa wa Lindi, Baada ya ugunduzi huo ‘Mabaki’ ya Dinosaria wetu ‘yalitoroshwa’ na kwenda kuhifadhiwa huko katika makumbusho kubwa ya Humbolt huko Ujerumani.

Dinosaria ni mnyama mkubwa aliyeishi kipindi kinachofahamika kihistoria kama Nyakati za Jurasiki ‘Jurassic period’, anatokea katika genus ya Giraffatitan. Alikuwa na uzito wa tani 89( Kama malori manne ya mchanga). Alikula majani ya juu ya miti mirefu kwani alikuwa ana urefu wa mita 20.

Miguu yake ya mbele ni mirefu zaidi ya nyuma, pia shingo yake ilikuwa na urefu wa kutosha. Mnyama huyo ni uthibitisho mwingine kuwa ‘Africa is Cradle of All Civilisations’. Hii ni kwa kuwa fuvu la mtu wa kale zaidi liligunguliwa huko Olduvai Gorge, Arusha baadaye zana za kale za mawe ziligunduliwa huko isimila katika kijiji cha Ugwachanya mkoani Iringa.

Kwa sasa Makumbusho ya Humbolt ni maarufu sana Ulaya kwa sababu ya uwepo wa Dinosaria wetu. Tuna kila sababu ya kudai kwa nguvu zote ili masalia hayo yarejeshwe hapa kwa kumbukumbu ya vizazi vijavyo na kuwa kivutio kingine cha utalii hapa Tanzania. Hiyo tu haitoshi ila tunapaswa kujiandaa kwa kuwa na wataalamu na vifaa vya kuhifadhi masalia hayo.

Mwishoni tujiulize hivi ni watanzania wangapi huamasika kufika katika makumbusho za nchi hii?

Wenu katika Historia.
Francis Daudi
Bangalore University, India...
c5d68da656398d432f99f1b0bef941c7.jpg

Hapana, hakutoroshwa kama unavyotaka kutuaminisha. Alichukuliwa.

Hivi wakati huo, ardhi hii ilikuwa inaitwaje?

Hivi wakati huo kulikuwa na mtaalamu yupi hapa wa kuweza kufanyia utafiti hayo mabaki?

Hivi kwa wakati huo ulikuwa na maabara ipi hapa ya kuweza kufanyia utafiti hayo mabaki?

Tuwe wa kweli.
 
oky.. basi tatizo hapa ni ccm.
Embu tufanye kuipiga chini tuwape hawa wapinzani alafu tuone na wao watatupeleka wapi

[emoji41] [emoji41] [emoji41] [emoji41] [emoji41] [emoji41]

CCM ilikuwa wala haijulikani kama itakuwepo wakati huo.
 
Habari zenu wadau.

Wote tunaamini kua kuna mambo mengi sana ya kisiasa, elimu, sayansi, geografia, na maarifa mengine mengi tu ambapo kwa namna moja au nyingine mtu unakua hujapata fursa ya kuyashuhudia au kuyasikia kwa muda muafaka. Hii inaweza kua kipindi kilichopita au hata kwa wakati huu ulipo.

Basi kupitia Thread hii ni vyema wadau tukafahamishana haya kwa lengo moja la kuelimishana.

Hivyo niwakaribishe wote wenye nia njema kuwekea wayajuayo, kwani ukijuacho wewe naweza nisikijue na akijuacho mwenzanko unaweza usikijue.

Karibuni.

Je wajua mwanamke ana uwezo mkubwa wa kuvumilia shida kuliko mwanaume
 
Kicheche ni mnyama mdogo sana lakini ana maajabu makubwa. Ana uwezo wa kumdaka kuku wa aina yoyote kwa kutumia mkia wake, lakini cha ajabu zaidi
hawezi kuishi bila kufanya mapenzi, ana uwezo wa kufanya mapenzi mara 26 kwa siku pia ni sawa na kukimbia umbali wa Km 360 kwa siku.
Na ndio maana mtu malaya sana huitwa kicheche.

Najua wajua ila nakujuza zaidi.
 
Back
Top Bottom