DINOSARIA WA TANZANIA; MNYAMA MKUBWA WA NCHI KAVU
Miezi ya karibuni kumekuwa na harakati mbalimbali za watu kudai kurejeshwa kwa mabaki ya ‘mjusi’ toka nchini Ujerumani. Ukweli ni kwamba Dinosaria aliishi au waliishi katika eneo la Afrika Mashariki miaka milioni 154 hadi 142 iliyopita.
Ila ugunduzi wa mabaki yake yalipatikana mwaka 1912 katika kijiji cha Tandeguru, kata ya Mipingo katika mkoa wa Lindi, Baada ya ugunduzi huo ‘Mabaki’ ya Dinosaria wetu ‘yalitoroshwa’ na kwenda kuhifadhiwa huko katika makumbusho kubwa ya Humbolt huko Ujerumani.
Dinosaria ni mnyama mkubwa aliyeishi kipindi kinachofahamika kihistoria kama Nyakati za Jurasiki ‘Jurassic period’, anatokea katika genus ya Giraffatitan. Alikuwa na uzito wa tani 89( Kama malori manne ya mchanga). Alikula majani ya juu ya miti mirefu kwani alikuwa ana urefu wa mita 20.
Miguu yake ya mbele ni mirefu zaidi ya nyuma, pia shingo yake ilikuwa na urefu wa kutosha. Mnyama huyo ni uthibitisho mwingine kuwa ‘Africa is Cradle of All Civilisations’. Hii ni kwa kuwa fuvu la mtu wa kale zaidi liligunguliwa huko Olduvai Gorge, Arusha baadaye zana za kale za mawe ziligunduliwa huko isimila katika kijiji cha Ugwachanya mkoani Iringa.
Kwa sasa Makumbusho ya Humbolt ni maarufu sana Ulaya kwa sababu ya uwepo wa Dinosaria wetu. Tuna kila sababu ya kudai kwa nguvu zote ili masalia hayo yarejeshwe hapa kwa kumbukumbu ya vizazi vijavyo na kuwa kivutio kingine cha utalii hapa Tanzania. Hiyo tu haitoshi ila tunapaswa kujiandaa kwa kuwa na wataalamu na vifaa vya kuhifadhi masalia hayo.
Mwishoni tujiulize hivi ni watanzania wangapi huamasika kufika katika makumbusho za nchi hii?
Wenu katika Historia.
Francis Daudi
Bangalore University, India...