Je, wajua Tanzania inaongoza kwa nguvu za kijeshi Afrika Mashariki na kati?

Je, wajua Tanzania inaongoza kwa nguvu za kijeshi Afrika Mashariki na kati?

MTV MBONGO

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2016
Posts
1,281
Reaction score
1,251
Mwingereza alipotawala nchi za Afrika Mashariki aligawa nguvu za kijeshi kama ifuatavyo:

1. TANZANIA ikawa ngome ya jeshi la ardhi na hivyo ikaongoza kuwa na vifaa vingi vya ardhini mf. vifaru, magari mbalimbali ya kivita na mizinga.

2. KENYA ikawa ngome ya jeshi la maji na hivyo ikaongoza kuwa na meli na boti nyingi za kivita.

3. UGANDA ikawa ngome ya jeshi la anga na hivyo ikaongoza kuwa na ndegevita.
ktk vita kati ya TZ na UG tulifanikiwa kutungua ndege nyingi za UG na hivyo wakapungukiwa ndege nyingi.

Kwa kuwa jeshi la ardhi kwa nchi nyingi maskini ndiyo dili kwani vifaa vyake vingi vina unafuu ktk kununua na kuvitunza. Pia Kenya imedhoofika sana na AL-SHAABAB ktk vita wanavyopambana.

Jeshi letu tangu vita vya UGANDA limekuwa na nafasi kubwa ya kujijenga na kujiimarisha kwa msaada wa pekee kutoka CHINA na hata nchi za ULAYA NA MAREKANI na ndiyo maana mwaka jana pale uwanja wa Taifa ilizinduliwa ndege ya kisasa ya kivita ambayo Afrika nzima tunayo TZ na SOUTH AFRICA pekee.

Ndiyo maana tunaombwa sana kulinda amani nje ya nchi kama DARFUR, CONGO DRC na LEBANON.

VIVA JWTZ
 
Nguvu za kijeshi za wapi? Wamepigana na taifa gani mpaka wajiite wana nguvu za kijeshi ukanda huu wa maziwa makuu? Vibaka tu wa amboni wamewashindwa
mkuu hujui historia ya TZ? tuliwashinda Waganda na Idd Amin Dada. tuna majeshi kulinda amani kama nilivyosema kwenye uzi, au hujausoma wote?
 
Nguvu hiyo ina manufaa gan kwa usalama wa raia??huon watu wsnakufa kias gani??
 
Back
Top Bottom