Je, wajua Vyama vya Siasa TZ ni Public Parties? Maamuzi yake lazima yazingatie Public Interest na siyo kufuata ujinga na ubinafsi wa viongozi insane!

Wanadai democrasia nchini wakati udicteta umetamalaki kwenye vyama vyao,si ajabu viongozi na wanachama wao wanaojitambua kuvikimbia vyama hivi.
 
Hii ni dalili njema ya ACT kuacha ujinga na kutanguliza mbele maslahi ya taifa.
P
 
Naunga mkono hoja, Hongera sana Mhe. Halima Mdee kwa kukataa ujinga na kutanguliza mbele maslahi ya taifa.
Mungu atawabariki sana na hakuna yoyote wa kuwafanya chochote!.
P
 
Mkuu fundimchundo , nimeguswa na bandiko lako hili, mimi ni realist, ma realists wote, hata kama hau support kilichofanyika, lakini when kumetokea kitu kilichotokea, and there is nothing anyone can do to change the situation, ma realists wote tunakubali matokeo, katika muktadha wa appreciating the situation and suggest the best way forward out of the situation.

Vyama vya siasa sio mali ya watu, viongozi, ni mali ya umma, hivyo maamuzi yoyote yatafanywa kwa kutanguliza maslahi ya umma.
Kwenye hili, maslahi ya umma ni kwa wapinzani hao wachache waliopata fursa ya kuingia Bungeni, waingie waka salvage what is left of opposition in Tanzania.

P
 
Mkuu Drifter, kwanza asante kwa mchango wako, very objective, kiukweli tangu nimepandisha uzi huu, wewe ndio mtu wa kwanza kunielewa, kwasababu, kiukweli kabisa, hii jf ya sasa, tuna watu wachache sana, wenye kuweza kusoma bandiko na kisha kujiuliza what is the motive behind.

Chama cha Mapinduzi ni chama cha ukweli na haki, kiliasisiwa na Mwalimu Nyerere, mpenda haki na mtenda haki. Baada ya Mwalimu, CCM ilipitia mageuzi na kuishiwa kuhodhiwa na wenye fedha, hivyo kuzalisha kada kubwa ya makada wa CCM ambao ni makada maslahi, na kwenye uchaguzi, wanakuwa wako tayari kutumia mbinu zozote kushinda uchaguzi. JPM alipoingia, amekuja kuibadili CCM kuirudisha ile CCM ya Nyerere. Sasa ndani ya makada wa CCM, kuna makada wa aina mbili, kuna "CCM Die Hard", hawa ndio wanaotaka kuhakikisha CCM inaupondaponda upinzani na kushinda kwa asilimia 99.9% kwa kutumia mbinu zozote.

Tupo sisi makada "Modern CCM" ambao kutokana na good track ya kazi nzuri ya JPM, CCM innashinda kwa mshindi mzuri safi na clear victory, kushinda kwa haki bila kufanya figisu figisu zozote.

Kwa vile Bunge letu ni Bunge la vyama vingi, mimi naamini kuna baadhi ya wana CCM very genuine, hakupenda kuona baadhi ya wapinzani wakishindwa akiwemo mtu kama Zitto!. Lakini kutokana na wapinzani kukataliwa na wananchi, ili Bunge lichangamke, zile kamati 2 za oversight committee, PAC na LAAC, lazima ziongozwe na wabunge wa upinzania ambao ni vichwa vya ukweli, kwenye hao wabunge wote sijaona watu wa kalibre hiyo ndio maana kila siku, tunamuomba Mwenyekiti wetu, JPM, katika zile nafasi zake 10, awateua wapinzani 4, Zitto, JJ Mnyika, Mbatia na kale kabinti Queen Sendiga.

Ili CCM itawale vizuri inahitaji Upinzani makini, ndio maana kila uchao, naibalasa Chadema humu na ACT Zanzibar, waache ujinga wa kususa. Ili kusasa kwa akili ni kususa kama kwa kususa huko utaachieve something, lakini kususa tuu for the sake of kususa, huku you won't achieve anything huu ni ujinga!.

Karibu tena.
P
 
Wanabodi, kiukweli kabisa jf inasaidia sana. Bandiko hili limesaidia sana, na matokeo ya bandiko hili ni haya
Huu sasa ndio uamuzi wa busara, sio kususa tuu bila mpango.
Asiyekubali kushindwa sio mshindani, if you can't get what you want, just take what you get!, and if you can't beat them, join them!.
Hatimaye ACT Wazalendo sasa wamekubali matokeo, sio tuu watapokea kidogo walichopata, bali pia wata wa join them kwenye kuunda SUK.
Hongera sana ACT, hizi ndio siasa za kweli.
P
 
Huu sasa ndio uamuzi wa busara, sio kususa tuu bila mpango.
Asiyekubali kushindwa sio mshindani, if you can't get what you want, just take what you get!, and if you can't beat them, join them!.
Hatimaye ACT Wazalendo sasa wamekubali matokeo, sio tuu watapokea kidogo walichopata, bali pia wata wa join them kwenye kuunda SUK.
Wana jf, tujifunze kuukubali ukweli jinsi ulivyo, hakuna mkate mgumu mbele ya chai!. Maalim Seif at 77, has everything to gain and nothing to lose.
Hongera Dr. Mwinyi kwa uteuzi huu.
Hongera Maalim Seif kwa kuitanguliza mbele Zanzibar.
Hongera sana ACT Wazalendo for doing the right thing na sasa hizi ndio siasa za kweli za maendeleo, na sio kususa susa bila manufaa yoyote.
P
 
Hizi sasa ndio siasa za ukweli. Sio zile siasa za kususa susa. Wakati Chadema wanaendelea kushupaza shingo, wenzao, wamepiga bao la kisigino.
Naendelea kusisitiza, "if you can't get what you want, then what you get". Yaani usipopata kile kikubwa unachokitaka, pokea hata kidogo ulicho patina!.
Na kwenye mapambano ya kupigania kitu, "if you can't beat them, join them". ACT Wazalendo wameipambania Zanzibar kwa kupigana na CCM, they couldn't beat them, now they have joined them.

Hongera sana ACT Wazalendo kwa kujitambua, hongera sana rais wa Zanzibar, Dr. Hussein Mwinyi kwa kuwa muungwana kama baba yako.
Mungu Ibariki Zanzibar
Mungu Ibariki Tanzania..
P
 
Mjinga ni wewe usiejua hata ccm ni public party na sii mali ya magufuli, timu ya watu wasiozidi 30 walimfukuza membe kisa alitaka kugombea urais ili hali watanzania walimtaka ni ujinga na upumbavu mkubwa
 
Sii wengi wanatambua wale wabunge 19 wa Chadema, wametokana na kuufuata ushauri huu. Hivyo ninawatetea mpaka mwisho!.
P
 
Chadema sasa imekitambua, keshokutwa Jumatano itatangaza kumtambua rasmi rais Samia na kuyatambua matokeo ya uchaguzi Mkuu wa 2020 ambapo waliuita uchafuzi.
Update
Hatimaye Chadema wameacha kushupaza shingo na wamekubali matokeo!, kwa kuufuata ushauri wa bandiko hili CHADEMA kubalini matokeo na m-survive, or shupazeni shingo. You go to hell 6ft under Hao Makamanda 19 ni mashujaa, kuendelea Ubunge wao

Nimepokea taarifa, hii kutokea twitwani Kisha nikasoma na bandiko hili humu JF Tundu Lissu: CHADEMA tumeanza kupokea Ruzuku

Chadema wameufuata ushauri wa bandiko hili, waneacha ujinga wa kujifanya hawayatambui matokeo ya uchaguzi wa 2020!, sasa wameacha kushupaza shingo, wameyatambua matokeo kimya kimya!, wamewasamehe mashujaa hawa kimya kimya msamaha ambao utatangazwa rasmi siku ya Jumatano tarehe 8 Machi na Mwenyekiti wa Chadema, mbele ya Rais Samia!.

Iliwa kusemwa kuwa hakuna mkate mgumu wowote mbele ya chai!, tayari Chadema imeisha anza kupokea ruzuku hivyo sasa ita survive!. Na ile kesi ya kina Halima Mdee na wale 19 iliyopo mahakamani itafutwa!.

Hongera sana Chadema, for doing the right thing!, mtabarikiwa, viongozi wenu watabarikiwa, chama chenu kitabarikiwa na Tanzania Itabarikiwa!.
Mungu ibariki Chadema
Mungu ibariki CCM kwa kukubali reconciliation
Mungu ibariki Tanzania
Paskali
 
Walikutukana sana ulipokuwa ukiwambia humu ila sasa hivi wanaona aibu sana.


Aliewaroga chadema ana dhambi sana
 
Asante sana kwa taarifa hii, ushauri wangu ni atangaze chochote na alalakike vyovyote kuhusu hizi figisu figisu za uchaguzi wa serikali za mitaa, ila hala hala ,Chadema wasifanye kosa 2019 kususia uchaguzi wa serikali za mitaa,hivyo uchaguzi wa 2020 waliambulia jimbo moja tuu la ngama,wakasusia kuutambua uchaguzi,wakauita ni uchafuzi, baada ya maridhiano wakautambua na kuyatambua matokeo。

Kufanya kosa sii kosa,kosa kurudia kosa, Chadema wasirudie makosa,wasijitoe kwa kususia uchaguzi wa seikali za mitaa!。
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…