Je, wajua Vyama vya Siasa TZ ni Public Parties? Maamuzi yake lazima yazingatie Public Interest na siyo kufuata ujinga na ubinafsi wa viongozi insane!

Chama umesema ni cha umma, hapo hapo unasema wasitangulize maslahi ya chama bali maslahi ya umma. Ni wazi kuna nyaya zimeanza kupiga short.
Ukitaka kuzungumzia maslahi mapana ya nchi, ungewashauri walioiba kura wajiuzulu kwani hakuna kazi ngumu kama kuongoza watu ambao hawakuwahi kukuchagua.
 
usiwatukane wapinzani! Mbona nyie wawili mnafanana kwa misemo yenu, mvivu anawezaje kumkanya mvivu mwenzake kwa uvivu!
Mkuu elvischirwa , tofautisha facts and fallacy, kama mtu ni mjinga, anafanya ujinga, kumuita ni mjinga na kumwambia anachofanya ni ujinga, sio kumtukana bali ni kumwambia ukweli!.
P
 
Bado naisisitiza hoja hii,
kabla ya kususa, pima matokeo, unasusa ili kupata nini?. Kama unasusa tuu ili kususa lakini kwa kususa huku you'll gain nothing, then kususa huko hakuna faida yeyote!.

CHADEMA pelekeni majina ya wabunge wenu 19 wa viti maalum, pimeni pros na cons za kususa muone nini kina faida zaidi, hata kama sio kwa Chadema as chama, then waachieni fursa za ajira wanawake wenu 19, tena nashauri priority iwe ni kwa wale waliogombea majimboni.

ACT Wazalendo, pelekeni jina la Maalim Seif, akateuliwe Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na kumuwezesha Dr. Mwinyi kuwateulia wawakilishi 5 na kuunda GNU!. Maalim Seif at 77 years, uchaguzi umekwisha, uchaguzi mwingine ni 2025, kipindi cha miaka 5 mingine kwa mtu mwenye umri wa miaka 77, anayeishi kwa depression ya kudhulumiwa ni kirefu sana kwa umri huo. Hata kama ni kweli alidhulumiwa, but for sake of his age, samehe saba mara sabini, peleka jina kwa Dr. Mwinyi, awe Makamu wa Kwanza wa Rais, angalau 2025 itafika kwa amani, lakini akisusa, something is telling me kuwa 2025....(naomba nisimalizie maana mimi sio ...)
 
Mkuu elvischirwa , tofautisha facts and fallacy, kama mtu ni mjinga, anafanya ujinga, kumuita ni mjinga na kumwambia anachofanya ni ujinga, sio kumtukana bali ni kumwambia ukweli!.
P
Si kila jambo tunatumia facts na tukitumia facts kila jambo viongozi wetu hawataweza kutuongoza, tutawafurumusha. Nilipokuwa mdogo niliumia nikiona baba tunapokula anachukua nyama zilizonona (fact) lakini sikuthubutu kumuuliza, nilivumilia. Nitakuona jasiri siku ukimuambia mwenyekiti wako anatudanganya kwa jambo fulani, ni wazi mengi aliyoahidi miaka mitano iliyopita hajayatimiza (fact) na hataweza kuyatimiza milele na milele (fact). Miaka kumi iliyopita Kigoma waliahidiwa itakuwa kama Dubai, Kigoma mpaka leo ni ileile ya barabara moja Kigoma kwenda Ujiji, stesheni ya treni ni ilele na bandari ni ileile na meli ni ileile Liemba ya mjerumani! (fact).
Ulisema tabia ya mwanamke sawa na mtoto nikakuuliza unatatizo gani na mama yako? Ninaamini alikuwa na tabia nzuri na alikunyonyesha na kukusafisha kwa wakati na muonekano wako wa sasa unajieleza.
Staha ni msingi mkubwa sana kwa waafrika kuliko ukweli (fact), ukikosea sikupi za uso nitatumia neno lenye staha nawe utanielewa vizuri.
 
Hivi wasipoleta majina ya viti maalum kuna shida gani?au kuna athari gani? Naomba kuelimishwa maana naoma kuna nguvu kubwa inatumika .
 
Hahaha ni ujinga na upumbavu kuanza kufikiria kugwana mali ya wizi na mwizi.

Ukimuonea wivu mwizi kwa mali za wizi nawe utaingiwa na pepo la kuiba, hivyo ni bora kuwaacha majambazi wa ccm wendelee kula walivyoiba.

Sema utakavyo vyama vya wananchi vimekataa kula haram.

Wameiba wanakula vya wizi na wanajipongeza, basi tumewaacha mle, hamtaki kukubali kwamba hatutaki.
 
Mkuu Nguruvi3 , kwanza mtu kuwa kada wa chama chochote, hakuondoi haki yake kutoa mawazo yake kama Mtanzania mwingine yoyote, hivyo kwenye hili la Chadema kususia viti maalum, tusinyoosheane vidole kuwa linawagusa CCM sana kuliko wapinzani, linawagusa Watanzania wote regardless vyama vyao.

Vyama vya siasa Tanzania ni public parties vya wananchi na sio private parties vya wanachama, japo vinaanzishwa privately na wanachama na kuongozwa na wanachama, but the moment vinaanza kupokea ruzuku ya serikali, they automatically turn into public parties, because they receive taxpayers money, and hence the taxpayers have an interest and they deserve to serve the interest of the public and not of its its members, hivyo maamuzi yote ya chama, lazima yazingatie na kutanguliza mbele public interest, maslahi ya taifa kwanza.

Jee uamuzi huu wa Chadema kususia viti maalum umezingatia public interest?. Una maslahi kwa Chadema?. And in so doing, what do they expects to achieve?.


P
 
Duh...!.
P
 
Uzi mreeefu afu pumba.. your submission is mostly not in tune with "public interest"..

Unajitahidi kutetea kikundi kidogo haramu cha wakoloni kilichokataliwa na umma kwny sanduku la kura, kikapoka madaraka kwa kutumia kura feki against "Public interest"..
Shame!
 
Paskali "hivi unashindwaje Kuomba kazi direct kwa Mukulu "mpaka unatumia njia ndefu ndefu ya kuandika vitu visivyokupa Crédit humu? Angalia sasa unasahaulika kuteuliwa!!

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
Naendelezea hapahapa~~chochote chenye public interest kina mawazo na maamuzi yanayotoka kwa watu kwa ajili ya watu,mwenyekiti wa ccm ndiye anejigeuza kuwa mwenyekiti wa Tanzania,yeye ndiye anayeamua nini kiwe for public interest na kipi kisiwe,alipomtimua mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali baada ya mkaguzi huyo kusimamia public interest wewe Pascal Mayalla hukumgombeza magufuli au kumkumbusha kuwa pesa iliyopotea ni ya umma,na mkaguzi ndiye jicho la umma,unamshangilia mwizi halafu unaongea habari za public interest,fool
Duh...!.
P
 
Sijasoma hii makala kwa sababu huyu bwana waga ana tabia ya kuandika misaafu mingi lkn isiyo na substance yoyote na lengo ikiwa zaidi kujipendekeza kwa mtawala.

Kwa kuwa sijui ulicho andika zaidi lkn kwa kuangalia heading naona tena kama hauna hoja ila ni muendelezo uleule wa kujaribu kujipendekeza kwa Magufuli.

Tunajua mnakipigia debe chama chenu ili kuweze kupata unafuu wa kutawala baada ya kukosa "The legitimate mandate" kufuatia kuhujumu uchaguzi uliopita.

Tunachukua fursa hii kuwahimiza Chadema kutothubutu kupeleka majina ya wabunge wa viti maalum ndio serikali ikose ufadhilii wa shilingi trilioni mbili plus kwani Magufuli aliishasema upinzani ndio unakwamisha maendeleo ndio sasa tuone hayo maendeleo atayaletaje kwa hii dhuluma aliyofanya.

Let them go to hell with their worthless development.
 
Mkuu Capt Tamar ,
Asante,
Ubarikiwe
Japo sina uhakika, kwavile siwezi kusoma mabandiko ya watu wote humu, lakini humu JF, mimi ni miongoni mwa tuliomuongelea sana CAG, Ofisi ya CAG na Ripoti za CAG!.
Nakutakia Jumapili Njema
P
 
Agreed 100%.....ebu angalia Chadema, ACT, na chama cha wala wali na nyama (cha Mh. Rungwe).....yaani ni upuuzi mtupu kwa kweli. Kama kweli wapinzani wanataka kushindana na CCM, yabidi kuvunja vyama vyao na kuungana kisha waje na viongozi wa ukweli na great thinkers si hawa wabangaizaji tuliowazoea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…