Je, Wajua Waraka wa TEC Sio Neno la Mungu? Ili Kuepuka Kuchanganya Dini na Siasa, Kuna Haja Waumini Tuambiwe Ukweli Waraka wa TEC Sio Neno la Mungu?

Soma Kitabu Cha Wafalme wa Kwanza Sura ya 18 na 19 kuhusu Nabii Elia na Mfalme Ahabu. Kama huamini Utakatifu wa Biblia basi soma tu kama Story ya Kawaida utaelewa Nafasi ya Watumishi wa Mungu kwamba ni maiki ya Mungu kuzungumza na Taifa lake.
 
Soma Kitabu Cha Wafalme wa Kwanza Sura ya 18 na 19 kuhusu Nabii Elia na Mfalme Ahabu. Kama huamini Utakatifu wa Biblia basi soma tu kama Story ya Kawaida utaelewa Nafasi ya Watumishi wa Mungu kwamba ni maiki ya Mungu kuzungumza na Taifa lake.
Pia kumbuka kuwa mamlaka yoyote ya kidunia hubarikiwa na Mungu pia. Ukimuona rais anaapa kashika kitabu cha dini jua kuwa anabeba mzigo mzito lakini kazi yake ina kibali kwa Mungu.

Ukiona serikali imeamua kupuuza huo waraka ujue kwamba ni kwa faida ya watanzania milioni sitini na ushee ambao ndio hao hao wenye sauti ya wengi inayojulikana kwa Mungu.
 
Unabii wa maaskofu unaheshimiwa na sisi wakatoliki lakini unahojika pia. Kama miongoni mwao wanayo maslahi makubwa ya utafutaji mali na wanajificha kwenye sera za uzawa maana yake serikali inayotazama mbali inayo haki ya kuendelea na mipango yake.

Baadhi ya wapakwa mafuta hawa walishachafuliwa na hulka za kifisadi tangu awamu ya nne, na baadhi yao ni matajiri wakubwa wenye uhusiano na wafanya biashara mafisadi hivyo na sisi wakatoliki tuwe macho katika maamuzi yetu pia.

Tatizo baadhi yetu ni watiifu mno kwa kanisa, hatuna tabia ya kuhoji na kutafakari kwa kina.
 
Paskali pitia hii comment huenda ubongo wako ukafunguka


Ndagha....
 
Mungu ni KWELI na neno lake ni ukweli.
Kama waraka una ukweli basi ni neno la Mungu, kama uongo siyo.
Huyo ni njaa inamtesa, sijui alikwama wapi kama 1990 tayari alikuwa na degree viwanja pale Ubungo nadhani ilikuwa ni pori unajikatia mpk Manzese darajani maanake sahivi alitakiwa awe na mali nyingi sn sijui ni uzinzi na starehe vilimponza sahivi ndiyo kajibana channel 10 apate namna ya kuishi
 
Tatizo kibogoyo ni sawa na simba aliyekula nyama ya mtu........................
 
Sio kujibu kwa ufasaha, hataweza kujibu kabisa
 
Mungu hamtumii Kila mtu kufanya maamuzi sahihi. Historia zinaonesha Wafalme wengi na watawala wamewahi kuuingiza umma kwenye matatizo kwa kukaidi sauti za Mitume na Manabii. Hao Watanzania milioni 60 na shee unaosema wewe ni wangapi wamekubali maamuzi ya Serikali kama sio wale tunwalioko serikalini na vibaraka?
 
Kiapo cha rais ni duniani na mbinguni kumbuka hilo.Hao manabii wetu na wao ni wachafu vile vile na ushahidi ulishawekwa hadharani na mwingine hatuwezi kuuweka humu jukwaani.

Uwekezaji wa DPW ni suala la kisayansi ni suala la kitaalam ambalo serikali kwa kuamua kulifanya ina lengo la kupandisha ubora wa maisha hata wa hao manabii unaowaongelea.

Hili sio suala la kisiasa ambalo kila mtu anao uwezo na maarifa ya kuliongelea kwa kina,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…