Je, Wajua Waraka wa TEC Sio Neno la Mungu? Ili Kuepuka Kuchanganya Dini na Siasa, Kuna Haja Waumini Tuambiwe Ukweli Waraka wa TEC Sio Neno la Mungu?

Je, Wajua Waraka wa TEC Sio Neno la Mungu? Ili Kuepuka Kuchanganya Dini na Siasa, Kuna Haja Waumini Tuambiwe Ukweli Waraka wa TEC Sio Neno la Mungu?

Soma Kitabu Cha Wafalme wa Kwanza Sura ya 18 na 19 kuhusu Nabii Elia na Mfalme Ahabu. Kama huamini Utakatifu wa Biblia basi soma tu kama Story ya Kawaida utaelewa Nafasi ya Watumishi wa Mungu kwamba ni maiki ya Mungu kuzungumza na Taifa lake.
 
Soma Kitabu Cha Wafalme wa Kwanza Sura ya 18 na 19 kuhusu Nabii Elia na Mfalme Ahabu. Kama huamini Utakatifu wa Biblia basi soma tu kama Story ya Kawaida utaelewa Nafasi ya Watumishi wa Mungu kwamba ni maiki ya Mungu kuzungumza na Taifa lake.
Pia kumbuka kuwa mamlaka yoyote ya kidunia hubarikiwa na Mungu pia. Ukimuona rais anaapa kashika kitabu cha dini jua kuwa anabeba mzigo mzito lakini kazi yake ina kibali kwa Mungu.

Ukiona serikali imeamua kupuuza huo waraka ujue kwamba ni kwa faida ya watanzania milioni sitini na ushee ambao ndio hao hao wenye sauti ya wengi inayojulikana kwa Mungu.
 
Ahsante Bro! huyu ni mkatoliki magumashi tu!
Yohanne Mbatizaji alimkemea Herode kwa kumwoa herodia mke wa nduguye--
Matokeo yake fitna ikawepo na yohane mbatizaji akakatwa kichwa.
Wengi waliteswa na kuuawa kwa kuwa wakweli akina Daniel, Jeremia, Paulo na Sira, Na yule nabii aliyemwonya yule tajiri aliyekuja kunyakua shamba la Naboth (shamba la Urithi) nk.
Shadrack abednego na Meshack waliotupwa kwenye tanuru la moto walipokataa kuabudu lisanamu la mfalme!
Maaskofu wetu ukiona wamefikia kutoa barua ya kichungaji jua wako tayari kwa lolote.
Askofu wa Karagwe Rweyongeza kawaambia waumini wake wazi wazi nyie mchague vizuri viongozi wenu. Siye tumezoea kufa/kuuawa kwa sababu ya kweli ndiyo maana mavazi yetu ni mekundu.

Ule waraka ni barua ya kichungaji kama nyingine zilizotolewa, Alipigwa nazo mkapa, Kikwete, Magufuli na sasa huyu.
Askofu ana vyeo 3: Mchungaji, Mfalme na Nabii.
Barua ya kichungaji ni Unabii- Tunatakiwa kuufuata!!
Unabii wa maaskofu unaheshimiwa na sisi wakatoliki lakini unahojika pia. Kama miongoni mwao wanayo maslahi makubwa ya utafutaji mali na wanajificha kwenye sera za uzawa maana yake serikali inayotazama mbali inayo haki ya kuendelea na mipango yake.

Baadhi ya wapakwa mafuta hawa walishachafuliwa na hulka za kifisadi tangu awamu ya nne, na baadhi yao ni matajiri wakubwa wenye uhusiano na wafanya biashara mafisadi hivyo na sisi wakatoliki tuwe macho katika maamuzi yetu pia.

Tatizo baadhi yetu ni watiifu mno kwa kanisa, hatuna tabia ya kuhoji na kutafakari kwa kina.
 
Pasco

kuchanganya dini na siasa ni dhana potofu. Rais na Wabunge wanaapa kwa kushika Biblia na Quran Tukufu.

Bunge linaanza kwa sala ya kutambua uwepo wa Mungu ambalo ni jambo la dini.

Mgeni rasmi wa Baraza la Eid siyo sheikh mkuu ni Rais wa Nchi

Mgeni rasmi wa maadhamisho ya miaka kama yale ya miaka 60 KKkT siyo Askofu mkuu ni Rais

Mvua isoponyesha tunakwenda uwanja wa Taifa viongozi wa dini, siyo RC au DC kuombea Nchi

Tunapozozana kwa Katiba au vyama vya siasa tunakwenda uwanja wa Taifa kuombea amani
Anayeongoza sala na maombi ni viongozi wa dini, siyo Waziri Mkuu au Mkuu wa Mkoa

Orodha inaendelea....

Viongozi wa dini wanaotenda hayo hapo juu wakizungumzia mambo yanayohusiana na hayo hapo juu inakuwa kuchanganya dini na siasa. Yaani kuchanganya siasa na dini ni sawa, lakini dini na siasa si sawa.!!

Kwa wale wanaosoma, mifumo ya utawala wa Dunia imejengwa katika Template ya mifumo ya Tawala za dini.
Yaani dini ndiyo imetengeneza 'structures' za siasa za Dunia ya leo, kwahiyo dini ni siasa kwanza.

Pili, kuna tatizo kubwa sana kwa Watanzania na limjitokeza wakati huu wa tatizo la Bandari
Kuna ' messenger ' halafu ' Message' . Watu wanamshambulia messenger badala ya message

Bila kujali Waraka ni wa kidini, una nguvu gani au la, soma 'contents' kisha uzijibu kwa kukukubaliana nazo au kutokubaliana nazo kwa kuangalia 'MKATABA' kama reference.

Bila kujali upande mtu anaouchukua, muhimu ni kujibu iwe 'for or against'.
Watanzania hatujui debate au kujenga hoja, tunaongea tu bila ufahamu wa mada.

Ikiwa mtu anadhani kuna kitu kizuri au kibaya kinaambatana na MKATABA wa Bandari, jambo la kwanza atueleze kwanini anadhani mkataba ni Mzuri au ni Mbaya halafu ajenge hoja yake anayokusudia , si kutueleza conclusion bila analysis
Paskali pitia hii comment huenda ubongo wako ukafunguka


Ndagha....
 
Mungu ni KWELI na neno lake ni ukweli.
Kama waraka una ukweli basi ni neno la Mungu, kama uongo siyo.
Huyo ni njaa inamtesa, sijui alikwama wapi kama 1990 tayari alikuwa na degree viwanja pale Ubungo nadhani ilikuwa ni pori unajikatia mpk Manzese darajani maanake sahivi alitakiwa awe na mali nyingi sn sijui ni uzinzi na starehe vilimponza sahivi ndiyo kajibana channel 10 apate namna ya kuishi
 
unamshambulia bure mwenzako, hebusoma hii kutoka kwa Kalidinali Pengo

Kadinali Pengo ameyasema hayo wakati akiadhimisha ibada ya Jumapili ya matawi huko Bagamoyo katika tamasha la vijana.


“Katika wiki chache zilizopita watu wamekuja kwangu wakaniuliza unaionaje ile barua ya Maaskofu kuhusu Kwaresma mwaka huu? Ninazungumzia hilo na wala mtu asiende aka-quote kitu kingine ndio maana nataka kusema wazi kabisa:-
“Barua ile ijapokuwa hata jina langu mnaliona limeandikwa pale kwamba na mimi ni mmoja wa waandishi au watamkaji…mimi nimeipokea, baadhi yenu mmeshaipokea.
” Kwahiyo sioni namna gani mimi naweza kuwa mwandishi au mhubiri kwenu wa ile barua ambayo imetungwa labda na maaskofu…naamini na baadhi ya maaskofu lakini mimi mwenyewe hata nilikuwa sijaiona, hata nilikuwa sijaambiwa kuna kitu cha namna hiyo kinakuja.
“Tuelewane vizuri, ninaposema hivi sitaki kusema ile barua ni mbaya. Moja tu ni kwamba barua nzima imechanganya vitu viwili; Mwalimu angekuwepo angepiga kelele Maaskofu msichanganye Dini na Siasa.
“Angepiga kelele sana kuhusu waraka huu katika nyakati zake. Na hilo nawambia sina hofu, muende mkamwambie mtu yeyote nimesema hivi. Ndio wala msione aibu, najua labda hata wengine mmekunja nyuso, kunjeni tu lakini huo ndio msimamo wangu.
“Zipo sehemu katika waraka huo zinazochanganya Dini na Siasa na si kazi ya maaskofu ni kazi yenu wanasiasa mkiwa ni wa CHADEMA, mkiwa ni wa CCM lakini haiwezi kuwa kazi yangu mimi.
“Siwezi kwanza nikaanza kuchambua na ku-criticize Serikali katika mambo yaliyo yake; sikupewa mamlaka hayo. Na kwanini niwe padri mpaka nikubali kuwa Askofu na huku kumbe wito wangu ni siasa?
Tatizo kibogoyo ni sawa na simba aliyekula nyama ya mtu........................
 
Wakati mwingine kunyamaza pia ni busara, hata kama una uhuru wa kutoa maoni. Hii njia uliyoichagua, itakushushia heshima yako kwa kiwango cha ajabu.

Na ushahidi mdogo tu ni hayo maswali uliyoulizwa na wajumbe! Sidhani kama baadhi yae unaweza kuyajibu kwa ufasaha.
Sio kujibu kwa ufasaha, hataweza kujibu kabisa
 
Pia kumbuka kuwa mamlaka yoyote ya kidunia hubarikiwa na Mungu pia. Ukimuona rais anaapa kashika kitabu cha dini jua kuwa anabeba mzigo mzito lakini kazi yake ina kibali kwa Mungu.

Ukiona serikali imeamua kupuuza huo waraka ujue kwamba ni kwa faida ya watanzania milioni sitini na ushee ambao ndio hao hao wenye sauti ya wengi inayojulikana kwa Mungu.
Mungu hamtumii Kila mtu kufanya maamuzi sahihi. Historia zinaonesha Wafalme wengi na watawala wamewahi kuuingiza umma kwenye matatizo kwa kukaidi sauti za Mitume na Manabii. Hao Watanzania milioni 60 na shee unaosema wewe ni wangapi wamekubali maamuzi ya Serikali kama sio wale tunwalioko serikalini na vibaraka?
 
Mungu hamtumii Kila mtu kufanya maamuzi sahihi. Historia zinaonesha Wafalme wengi na watawala wamewahi kuuingiza umma kwenye matatizo kwa kukaidi sauti za Mitume na Manabii. Hao Watanzania milioni 60 na shee unaosema wewe ni wangapi wamekubali maamuzi ya Serikali kama sio wale tunwalioko serikalini na vibaraka?
Kiapo cha rais ni duniani na mbinguni kumbuka hilo.Hao manabii wetu na wao ni wachafu vile vile na ushahidi ulishawekwa hadharani na mwingine hatuwezi kuuweka humu jukwaani.

Uwekezaji wa DPW ni suala la kisayansi ni suala la kitaalam ambalo serikali kwa kuamua kulifanya ina lengo la kupandisha ubora wa maisha hata wa hao manabii unaowaongelea.

Hili sio suala la kisiasa ambalo kila mtu anao uwezo na maarifa ya kuliongelea kwa kina,
 
Back
Top Bottom