Pasco
kuchanganya dini na siasa ni dhana potofu. Rais na Wabunge wanaapa kwa kushika Biblia na Quran Tukufu.
Bunge linaanza kwa sala ya kutambua uwepo wa Mungu ambalo ni jambo la dini.
Mgeni rasmi wa Baraza la Eid siyo sheikh mkuu ni Rais wa Nchi
Mgeni rasmi wa maadhamisho ya miaka kama yale ya miaka 60 KKkT siyo Askofu mkuu ni Rais
Mvua isoponyesha tunakwenda uwanja wa Taifa viongozi wa dini, siyo RC au DC kuombea Nchi
Tunapozozana kwa Katiba au vyama vya siasa tunakwenda uwanja wa Taifa kuombea amani
Anayeongoza sala na maombi ni viongozi wa dini, siyo Waziri Mkuu au Mkuu wa Mkoa
Orodha inaendelea....
Viongozi wa dini wanaotenda hayo hapo juu wakizungumzia mambo yanayohusiana na hayo hapo juu inakuwa kuchanganya dini na siasa. Yaani kuchanganya siasa na dini ni sawa, lakini dini na siasa si sawa.!!
Kwa wale wanaosoma, mifumo ya utawala wa Dunia imejengwa katika Template ya mifumo ya Tawala za dini.
Yaani dini ndiyo imetengeneza 'structures' za siasa za Dunia ya leo, kwahiyo dini ni siasa kwanza.
Pili, kuna tatizo kubwa sana kwa Watanzania na limjitokeza wakati huu wa tatizo la Bandari
Kuna ' messenger ' halafu ' Message' . Watu wanamshambulia messenger badala ya message
Bila kujali Waraka ni wa kidini, una nguvu gani au la, soma 'contents' kisha uzijibu kwa kukukubaliana nazo au kutokubaliana nazo kwa kuangalia 'MKATABA' kama reference.
Bila kujali upande mtu anaouchukua, muhimu ni kujibu iwe 'for or against'.
Watanzania hatujui debate au kujenga hoja, tunaongea tu bila ufahamu wa mada.
Ikiwa mtu anadhani kuna kitu kizuri au kibaya kinaambatana na MKATABA wa Bandari, jambo la kwanza atueleze kwanini anadhani mkataba ni Mzuri au ni Mbaya halafu ajenge hoja yake anayokusudia , si kutueleza conclusion bila analysis