Je, wajua Wazaliwa wa Pwani huwaona wazaliwa wa Bara kama washamba tu?

We're the smartest generation nyie someni sisi talents kibao tunajitambua hatuna ujinga sana someni sana maana despite na anavyokazana kusoma ila bado elimu haimisaidii[emoji28][emoji28][emoji28]zaidi ya kuajiriwa
[emoji23][emoji23][emoji23] Mna talent gani sasa? Ya kufunga kikoi au kupanda mnazi?
 
Habari ndo hiyo!
 
Kwenye huu uzi tuweke na trending stories za ajabu from Pwani na Bara ndiyo utaona wapi wanatisha kwa mambo ya hovyo.
Kuna lecturer wangu (RIP) alisoma Israel, alituambia kule wanaamini bora Muafrika asiyeenda shule unaweza mwambia kitu akaelewa kuliko alieenda shule.
 
Uzi umenifurahisha sana [emoji16][emoji16]
 
ALLAAH Aliyetukuka Anasema:
“Enyi watu! Hakika Sisi Tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na Tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa ALLAAH ni huyo aliye mcha Mungu zaidi katika nyinyi” (al-Hujuraat 49: 13).

Na Mtume wa ALLAAH (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
“Hakuna ubora wa Mwarabu kwa asiyekuwa Mwarabu, wala mweupe juu ya mweusi ... isipokuwa kwa taqwa (ucha Mungu)”.
 
..Aliwahi sema Dully Skyes kuwa Fid Q ni mtoto wa mjini lakini ni mjini Mwanza, mimi (Dully) ni mtoto wa mjini lakini ni mjini Dar es Salaam tena Kariakoo....kwa hiyo kuna mtoto wa mjini na mtoto wa mjini Dar es salaam hawawezi kuwa sawa!
 
Washamba nyie angalia mwenyewe talent zote then fananisha na huko kwenu mmetuzidi kuoza meno tu
Hahaha, nani aliyeoza meno sasa? [emoji23] ninyi hamna akili zaidi ya kutawaza na kufunga kikoi
 
Wazaliwa wa Bara huwaona wazaliwa wa Pwani, wakuja, lihoya!
[emoji23]nilienda Nyamongo nikaitwa LIHOYA! Kutuliza nikaambiwa Sisi tunapenda kuita watu oyaah!

Makavu tu naulizwa wewe umetokea wapi, mwingine akadakia huyo ni lihoya!
Mkuu nipo Nyamongo hapa Nyangoto, hatari sana
 
Silaha ya mtu dhaifu ni kubagua wengine, atabagua wengine kwa rangi ilimradi yeye ndio aonekane bora zaidi. Akishindwa kwenye rangi atahamia kwenye kabila, dini nk
 
Mie nakiri mshamba ila yupo mzee wa kizaramo ananimegea eneo huko shamba Mbezi kila baada ya miezi mitatu ananiitia miguu ishirini tunaenda kumalizana serikali za mitaa na wanasheria juu.

Nimeshachukua 40×40 huku wanae wapo kwenye nyumba yao ya urithi nasikia Mburahati huko kwenye maji machafu na msongamano wakija kustuka mshamba mimi nakula upepo murua kwenye ardhi iliyokuwa yao.
 
Wapi weyeee....wabara ndio wameinvest na kutawala hiyo pwani. Wewe nenda kafunge kikoi ukatawaze kisha upeleke pesa ya minazi kwa Mangi [emoji23][emoji23][emoji23]
Hata uinvest ushamba ni mzigo
 
Ustaarabu na maendeleo siku zote huanzia pwani na kuelekea bara, ila Tanzania imekuwa tofauti kidogo,Ustaarabu umeshamiri pwani ila maendeleo kidogo, kuna maendeleo makubwa bara ila wanazidiwa Ustaarabu na pwani.
 
Sio maeneo waarabu walioyokaa.
Duniani kote maendeleo huanzia pwani kisha kusambaa bara, nenda bara lolote au nchi yoyote hali huwa hivyo na hiyo husababishwa na muingiliano mkubwa wa watu kutoka sehemu mbalimbali.
Huu ni ukweli maeneo ambayo waarabu walikaa ustaarabu uliingia mapema Sana tofauti na maeneo Kama shinyanga
 
Huu Uzi haupo sawa kabisa.

Sifa zote za wasukuma walizonazo mjini ukifika kwao huku wanaonekana si chochote si lolote na ni wavivu.
Maeneo kama shinyanga mpaka kwa wanyantuzu huku Dutwa, Lalago mpaka Itilima

Nimeenda mbeya Nako hivyo hivyo kwa wenyeji wa Mbeya mjini ambao ni Wasafwa.

Hata Tabora kwa wanyamwezi,
Kigoma kwa Waha na
ndugu zao wamanyema
Wafipa kule sumbawanga
Wapimbwe kule mpanda

Hadi wameru kule Arusha.

Hivyo ni kawaida kwa wenyeji kudharaulika
Kwa sababu wageni huja na mitaji, fursa kupata kazi pamoja na connection.

Yaani ukifika mjini bariadi mkoa wa simiyu hakuna anayedharaulika kushinda msukuma, Tena anayedharaulika zaidi ni msukuma kutoka Shinyanga na huko Geita.
Ila Mnyantuzu akigundua wewe ni mswahili utaona shobo zake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…